Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji,
maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Saame amewataka wataalamwa Sekta ya Mifugo na
Uvuvi kuhakikisha wanachukua takwimu
sahihi wakati wa kukusanyataarifa za kitafiti
ili ziweze kuisaidia Serikali katika kupanga mipango yake.
Waziri Shaame ameyasema hayo wakati akifunga
Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa
Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika kwenye Ukumbi
wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27,
2023.
"Takwimu sahihi kuhusu taarifa
za mifugo na uvuvi zitasaidia kutunga sera,
kunyoosha maono, fikra na miongozo ya ilani ya chama cha mapinduzi
kuweza kufikia malengo ya kuwainua
wananchi kupata mafanikio kwa
haraka," alisema
Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali
inawategemea sana wataam na hivyo watumie vizuri teknolojia walizonazo ili
zikaboreshe tasnia nzima ya ufugaji ili kupata maendeleo.
“Wizara na Wadau wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi kwa pamoja lazima tutambue kuwa huu ni wakati mwafaka wa kufanya
mapinduzi makubwa katika minyororo ya thamani ya mifugo na samaki ili kukidhi
mahitaji ya chakula na lishe bora kwa Wananchi na masoko yanayotuzunguka”
Alisema Mhe. Shaame
Aliendelea kwa kuwahimiza Wafugaji na
wazalishaji kuwekeza katika teknolojia za kisasa na vitendea kazi sahihi
vitakavyoongeza uzalishaji katika kilimo, mifugo na sekta ya Uvuvi na hivyo
Wizara, itaendelea kuhakikisha kuwa mazingira bora ya kufuga, kusindika na
kufanya biashara ya mifugo na uvuvi yanazidi kuwa bora kwa watengenezaji wa
vyakula vya mifugo na samaki.
Aliongeza kuwa Wizara ya Kilimo,
Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo inaunga
mkono jitihada za vyama vya hiari vya kitaaluma , hivyo TSAP iendelee
kujitangaza ili kuongeza mashirikiano na wataalamu walioko Zanzibar ili
kuendelea kupata wanachama wengi.
Naye Naibu Katibu Mkuu amewataka
wataalam kuweka bidii katika kujiendeleza kutaaluma ili kuongeza ujuzi na
ufanisi zaidi katika kazi zao na kuweza kutengeneza mfumo utakaohifadhi taarifa
za wataalam wote wa mifugo nchini ili kujua umma uliopo ni asilimia ngapi ya
wataalam walioko huko nje.
Pia amewataka wataalam kuwa chachu ya
kuhamasisha wafugaji kulima, kuhifadhi malisho na kutengeneza vyanzo mbadala
vya maji kwa mwaka mzima ili kupunguza idadi kubwa ya vifo vya wanyama
vinavyotokea kipindi cha kiangazi.
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Saame akiongea na Washiriki (hawapo pichani) wakati akifunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika katika Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27, 2023.
Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi akiongea wakati wa kufunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27, 2023.
Mwenyekiti wa TSAP, Dkt. Jonas Kizima akitoa neno katika Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lilifanyika katika Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27, 2023.
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Saame (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya Washiriki muda mfupi baada ya kufunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27, 2023.