Nav bar

Jumamosi, 28 Oktoba 2023

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Saame amewataka wataalamwa Sekta ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha wanachukua  takwimu sahihi wakati wa kukusanyataarifa za kitafiti   ili ziweze kuisaidia Serikali katika kupanga mipango yake.

Waziri  Shaame ameyasema hayo wakati akifunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano  Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha  Oktoba 27, 2023.

"Takwimu sahihi kuhusu taarifa za mifugo na uvuvi zitasaidia kutunga sera,  kunyoosha maono, fikra na miongozo ya ilani ya chama cha mapinduzi kuweza kufikia  malengo ya kuwainua wananchi  kupata mafanikio kwa haraka," alisema

Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inawategemea sana wataam na hivyo watumie vizuri teknolojia walizonazo ili zikaboreshe tasnia nzima ya ufugaji ili kupata maendeleo.

“Wizara na Wadau wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa pamoja lazima tutambue kuwa huu ni wakati mwafaka wa kufanya mapinduzi makubwa katika minyororo ya thamani ya mifugo na samaki ili kukidhi mahitaji ya chakula na lishe bora kwa Wananchi na masoko yanayotuzunguka” Alisema Mhe. Shaame

Aliendelea kwa kuwahimiza Wafugaji na wazalishaji kuwekeza katika teknolojia za kisasa na vitendea kazi sahihi vitakavyoongeza uzalishaji katika kilimo, mifugo na sekta ya Uvuvi na hivyo Wizara, itaendelea kuhakikisha kuwa mazingira bora ya kufuga, kusindika na kufanya biashara ya mifugo na uvuvi yanazidi kuwa bora kwa watengenezaji wa vyakula vya mifugo na samaki.

Aliongeza kuwa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo  inaunga mkono jitihada za vyama vya hiari vya kitaaluma , hivyo TSAP iendelee kujitangaza ili kuongeza mashirikiano na wataalamu walioko Zanzibar ili kuendelea kupata wanachama wengi.

Naye Naibu Katibu Mkuu amewataka wataalam kuweka bidii katika kujiendeleza kutaaluma ili kuongeza ujuzi na ufanisi zaidi katika kazi zao na kuweza kutengeneza mfumo utakaohifadhi taarifa za wataalam wote wa mifugo nchini ili kujua umma uliopo ni asilimia ngapi ya wataalam walioko huko nje.

Pia amewataka wataalam kuwa chachu ya kuhamasisha wafugaji kulima, kuhifadhi malisho na kutengeneza vyanzo mbadala vya maji kwa mwaka mzima ili kupunguza idadi kubwa ya vifo vya wanyama vinavyotokea kipindi cha kiangazi.


Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo  Mhe.  Shamata Saame akiongea na Washiriki (hawapo pichani) wakati akifunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika katika Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha  Oktoba 27, 2023.
Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Dkt.  Daniel Mushi akiongea wakati wa kufunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27, 2023.
Mwenyekiti wa TSAP, Dkt. Jonas Kizima akitoa neno katika Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa  47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lilifanyika katika Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27, 2023.
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Saame (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya Washiriki muda mfupi baada ya  kufunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27, 2023.



 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni