Nav bar

Alhamisi, 27 Agosti 2020

TAMATAMAH AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUHUSU MJADALA WA VIWANGO VYA MAZAO YA DAGAA NA MWANI

 Serikali imesema ipo katika mchakato wa kutengeneza viwango vya kitaifa vya ubora na usalama wa mazao ya Mwani na Dagaa ili kuyapa mazao hayo fursa pana ya masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah alipokuwa akifungua mkutano wa Wadau kuhusu mjadala wa viwango vya mazao ya Dagaa na Mwani uliofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 24, 2020.

Dkt. Tamatamah alisema kuwa kutengenezwa na kuanzishwa kwa viwango vya kitaifa vya ubora na usalama wa mazao hayo ya uvuvi kutaimarisha na kukuza soko la kitaifa na kimataifa la bidhaa zinazotokana na mazao hayo ya uvuvi.

“Mazao ya Dagaa na Mwani kwa muda mrefu yamekuwa hayana viwango vya ubora jambo ambalo limekuwa likifanya bidhaa hizo kutokutambulika katika soko la kimataifa ndio maana sasa serikali imeamua kutengeneza viwango vya ubora vya mazao ya uvuvi hasa Daagaa na Mwani ili yaweze kupata masoko yenye uhakika ndani na nje ya nchi,”alisema Dkt. Tamatamah

Alisema kuwa uvuvi wa dagaa pamoja na ukulima wa mwani ni muhimu kwa uchumi wa jamii inayoishi Pwani na taifa kwa ujumla huku akisema kuwa kilimo cha mwani peke yake kinawahusisha takribani wakulima elfu tatu (3000) wengi wao wakiwa ni wanawake.

“Kwa mwaka 2019/2020 kiasi cha tani 1449 za Mwani zilizalishwa  na kati ya hizo, asilimia 10 zilitumika hapa nchini katika kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo sabuni na asilimia 90 zilisafirishwa kwenda nje ya nchi zikiwemo nchi za China, Marekani, Canada, Uingereza, Denmark na Ufaransa,”alifafanua Dkt. Tamatamah.

“Kwa upande wa Zanzibar, uzalishaji wa Mwani umefikia takriban tani 35000 na ndio bidhaa ya pili inayosafirishwa kwa wingi kwenda nje ya nchi,”aliongeza 

Dkt. Tamatamah aliendelea kueleza kuwa kutokana na umuhimu huo ni dhahiri kwamba kuna haja ya kuwepo kwa viwango vya ubora na usalama ili wafanyabiashara waweze kuyafikia masoko mbalimbali  duniani.

“ Kupitia mradi wa SWIOFish ulio chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wameweza kuandaa viwango viwili ambavyo ni TBS/AFDC 23 kwa ajili ya unga wa Dagaa na TBS/ AFDC (5714)  kwa ajili ya Mwani mkavu,”alibainisha Dkt. Tamatamah

Naye Mkulima wa Mwani, Wilayani Bagamoyo, Mzee Machao Ally Jingalao alisema katika mkutano huo kuwa hatua hiyo ya Serikali ya kutengeneza viwango vya ubora kwa ajili ya mazao hayo ya uvuvi ni hatua nzuri ya kuelekea uchumi wa viwanda.

“Naiomba serikali iongeze nguvu katika kuimarisha biashara hii ya mazao ya uvuvi kwani ikisimamiwa vizuri itasaidia sana kuiongezea mapato nchi na kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja,”alisema Jingalao

Meneja wa Kampuni ya Uwekezaji katika zao la Mwani, Mariculture, Roger Valle Morre aliiomba Serikali kulinda wawekezaji katika zao la Mwani dhidi ya watu wanaojiingiza katika biashara hiyo bila kuwa na vibali. 

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akiongea na Wadau wa Sekta ya Uvuvi alipokuwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uvuvi kuhusu Mjadala wa Viwango vya Mazao ya Dagaa na Mwani uliofanyika jijini Dar es Salaam. (24.08.2020)

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Uvuvi muda mfupi baada ya kufungua Mkutano wa Wadau kuhusu mjadala wa viwango vya mazao ya Dagaa na Mwani uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi (WMUV), Ezra Mutagwaba na kushoto ni Mratibu wa Mradi wa SWIOFish, Daniel Nkondola. (24.08.2020)

Mratibu wa Mradi wa SWIOFish, Daniel Nkondola akifafanua jambo katika Mkutano wa Wadau kuhusu mjadala wa viwango vya mazao ya Dagaa na Mwani uliofanyika jijini Dar es Salaam. (24.08.2020)

Mkulima wa zao la Mwani, Kijiji cha Mlingotini, Wilaya ya Bagamoyo, Mzee Machano Ally Jingalao akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kufunguliwa kwa Mkutano wa Wadau kuhusu mjadala wa viwango vya mazao ya Dagaa na Mwani uliofanyika jijini Dar es Salaam. (24.08.2020)

Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi (WMUV), Ezra Mutagwaba (kushoto) akiongea katika Mkutano wa Wadau kuhusu Mjadala wa Viwango vya Mazao ya Dagaa na Mwani uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah na kulia ni Mratibu wa Mradi wa SWIOFish, Daniel Nkondola. (24.08.2020)

Meneja wa Kampuni ya Mwani Mariculture, Roger Valle Morre akifuatilia kwa makini Mjadala kuhusu viwango vya mazao ya Dagaa na Mwani uliofanyika jijini Dar es Salaam. (24.08.2020)





ZIARA YA MAKATIBU WAKUU WILAYANI MAFIA.

 

Kaimu Muhifadhi Mfawidhi, Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Bw. Amin Abdallah (kushoto) akisoma taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya taasisi hiyo kwa Makatibu Wakuu kutoka Wizara nne tofauti walipotembelea taasisi hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah. (22.08.2020)

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akieleza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Bw. Shaib Nnunduma (kushoto) wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu na Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya kilichofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya. (22.08.2020)

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (Kulia) akiongea na Watumishi wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) (hawapo pichani) alipotembelea Taasisi hiyo iliyopo katika eneo la Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia. Kushoto ni Kaimu Muhifadhi Mfawidhi, Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Amin Abdallah. (22.08.2020)

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (Kulia) akiongea na Watumishi wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) (hawapo pichani) alipotembelea Taasisi hiyo iliyopo katika eneo la Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia. Kushoto ni Kaimu Muhifadhi Mfawidhi, Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Amin Abdallah. (22.08.2020)

Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Bw. Shaib Nnunduma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu walipotembelea Ofisi yake. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Injinia Joseph Malongo, wa pili kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli na wa pili kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Alloyce Nzuki. Wengine pichani ni Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Kisiwani Mafia.

Mhifadhi Mshirikishi Jamii, Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Albert Makala (katikati) akieleza jambo mbele ya Makatibu Wakuu katika kikao kilichofanyika kwenye Ofisi za MPRU zilizopo Kisiwani Mafia. Kulia anayemuangalia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Alloyce Nzuki. Wengine pichani ni Watumishi wa MPRU. (22.08.2020)

Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa pili kutoka kulia waliosimama mbele) akiwa na Makatibu wa Wakuu wenzake, kutoka kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Injinia Joseph Malongo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Bw. Gerald Mweli na wa pili kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Alloyce Nzuki wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) walipotembelea ofisi za MPRU. (22.08.2020).

Makatibu wa Wakuu kutoka Wizara nne tofauti wakimsikiliza Mwenyekiti wa Wavuvi wanaoishi katika Kisiwa cha Nyororo kilichopo katika Kisiwa cha Mafia, Bw. Likua Said Mchomoko (kulia aliyevaa Tshirt ya Njano) alipokuwa akitoa maelezo kuhusu shughuli za uvuvi wanazozifanya katika eneo hilo. Wa kwanza kutoka kulia waliosimama ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Injinia Joseph Malongo na wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, anayesimamia Elimu, Bw. Gerald Mweli. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Alloyce Nzuki na wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah. (23.08.2020)





Jumatano, 19 Agosti 2020

KATIBU MKUU SEKTA YA UVUVI DKT. RASHID TAMATAMAH ATEMBELEA VIZIMBA VYA KUFUGIA SAMAKI :KONGWA FARM WILAYA YA MAGU MKOANI MWANZA.(09/08/2020)

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akifafanua jambo kwa mmiliki wa shamba la kufugia samaki linalojulikana kama "Konga Farm" Bi Loycana Mwidunda alipofika kwenye Vizimba vya shamba hilo vilivyopo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza (09.08.2020).


Mmiliki wa Shamba la Kufugia samaki linalojulikana kama "Konga Farm" Bi. Loycana Mwidunda (katikati) akitoa maelezo kuhusu Shamba lake kwa
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazaeli Madala (kulia) wakati wa ziara ya viongozi hao Wilayani Magu (09.08.2020) 

 


 

Waliokaa mbele Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji Dkt. Nazaeli Madala wakiwa kwenye boti kuelekea kwenye vizimba vya kufugia samaki vya Shamba la "Konga Farm" vilivyopo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza (09.08.2020).


PICHA KILELE CHA MAONYESHO YA NANENANE MKOANI ARUSHA TAREHE 09/08/2020

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua ng'ombe bora kwenye kilele cha maadhimisho ya maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020) 

 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akipata maelezo kutoka kwa msambazaji wa madini ya Mifugo kutoka kampuni ya usambazaji wa madini (JOSERA), Bw. Elirehema Laizer alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye kilele tea maadhimisho ya maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020) 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiangalia mashine ya kukatia nyama kwenye banda la SIDO alipotembelea kwenye kilele cha maadhimisho ya maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020) 

 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akiongea na wananchi (hawapo pichani) kwenye maadhimisho ya kilele cha maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020) 


 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. abdallah Ulega akimpongeza Bw. Anthony Fabian Mnyanganyile kwa kutoa elimu kwa wadau na wananchi wote juu ya nyavu haramu na nyavu sahihi kwa uvuvi kwenye kilele cha maadhimisho ya maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020) 



Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua mazao katika moja ya mabanda ya kilimo kwenye kilele cha maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (09/08/2020) 


NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI, MHE. ABDALLAH ULEGA ATEMBELEA GEREZA LA KARANGA KUJIONEA UJENZI WA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI (KILIMANJARO LEATHER INDUSTRIES CO. LTD






Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua ramani ya ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd kilichopo katika eneo la Gereza la Karanga Mkoani Kilimanjaro, ambapo ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 60. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Mhandisi Masoud Omary. (08.08.2020) 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiwa na baadhi ya maafisa kutoka katika wizara hiyo na kukutana na mkuu wa mkoa huo Dkt. Anna Mghwira ambapo wamezungumza mambo mbalimbali ya kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi kabla ya kuelekea katika Gereza la Karanga kujionea ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd. (08.08.2020) 

 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua baadhi ya mitambo itakayofungwa katika kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd kilichopo katika eneo la Gereza la Karanga Mkoani Kilimanjaro na kusisitiza watanzania kununua bidhaa za ngozi zinazozalishwa hapa nchini ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji pamoja na wajasiriamali. (08.08.2020) 


Muonekano wa maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd kilichopo katika Gereza la Karanga Mkoani Kilimanjaro, ambapo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amelipongeza Jeshi la Magereza Mkoa wa Kilimanjaro kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa kwa ajili ya ujenzi huo ambapo baadhi ya wafungwa wamepatiwa pia elimu ya ujenzi katika gereza hilo. (08.08.2020) 

 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua ubora wa matofali yanayotengenezwa na wafungwa wa Gereza la Karanga kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd kilichopo katika eneo la gereza hilo, ambapo ameridhishwa na ubora wa matofali hayo ambayo ni mchanganyiko wa saruji na vumbi la miamba/mawe. (08.08.2020) 


HABARI PICHA ZA MAONYESHO YA NANENANE KWENYE MIKOA YA SIMIYU, LINDI, ARUSHA, MBEYA, DODOMA, TAREHE 08/08/2020











Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) akitoa maelezo kuhusu mradi wa "deep sea" kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) baada ya Waziri Mkuu kufika kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi muda mfupi uliopita kwenye Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (08.08.2020). 

 


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa maelezo kuhusu teknolojia ya uhimilishaji kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) baada ya Waziri Mkuu kufika kwenye mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi muda mfupi uliopita kwenye Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (08.08.2020), Wa pili kutoka kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina. 

 


Kutoka Kulia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah wakipata maelezo namna mradi wa "deep sea" unavyofanya kazi muda mfupi baada Mhe. Waziri Mkuu kufika hapo leo (08.08.2020) kwenye Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 


Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiwakabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah, Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt. Angelo Mwilawa wakipokea zawadi ya kombe baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushika nafasi ya pili kwenye maonesho ya Kilimo (NANE NANE) kwa upande wa Taasisi za Serikali wakati wa kilele cha Maonesho hayo kitaifa Mkoani Simiyu  (08.08.2020) 


Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya Kombe Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Mifugo (TALIRI) Dkt. Eliggy Shirima baada ya taasisi hiyo kushika nafasi ya pili kwa upande wa taasisi zilizo chini ya Wizara wakati wa kilele cha Maonesho ya Kilimo (NANE NANE) kitaifa Mkoani Simiyu  (08.08.2020).

 


Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt. Angelo Mwilawa, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah wakifurahia zawadi ya Kombe walilokabidhiwa baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushika nafasi ya pili kwenye maonesho ya Kilimo (NANE NANE) kwa upande wa Taasisi za Serikali wakati wa kilele cha Maonesho hayo kitaifa Mkoani Simiyu (08.08.2020)


LINDI


Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Melkidezeky Kody akitoa maelezo kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba wakati alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini katika viwanja vya Ngongo - Manispaa ya Lindi. (08.08.2020) 

 



Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na mmoja wa wajasiriamali, Hadija Malibiche (aliyebeba mtoto) wakati alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini katika viwanja vya Ngongo - Manispaa ya Lindi. (08.08.2020) 


ARUSHA


Afisa Mfawidhi kutoka kituo cha Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Nyumba ya Mungu Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Godbless Msuya (kushoto) akitoa maelezo juu ya nyavu zinazoruhusiwa na zisizoruhusiwa kwenye uvuvi kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (08/08/2020) 


Daktari wa Mifugo kutoka Wakala ya Maabara ya Vetenari Tanzania (TVLA), Bw. Rowenya Mushi akitoa maelezo na kuelekeza namna ya kutumia darubini kwa wanafunzi wa shule ya msingi Maromboso waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha. (08/08/2020) 


Afisa Mifugo kutoka Idara ya Uendelezaji wa Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Bw. Francis Ndumbaro akitoa maelezo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (08/08/2020) 

 


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Asimwe Rwiguza akijadili jambo na maafisa kutoka Wizara hiyo kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha (08/08/2020) 

 


MBEYA

Naibu spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Akson akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya maonyesho ya nanenane yaliyofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya tarehe 08.08.2020

 


Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi kabla ya kufunga maadhimisho ya maonyesho ya nanenane ambapo leo ndio ilikua kilele cha madhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale- Mbeya tarehe 08.08.2020. 

 

DODOMA


Mratibu wa Maonesho, banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bezia Rwongezibwa(katika) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi, Kampuni ya Rushu, Mabula Charles (aliyeshika Kombe) ambaye ndiye aliyeibuka Mshindi wa kwanza katika kundi la Paredi- Wafugaji wakubwa, Ngombe wa Nyama. Wengine wanaofurahia ushindi huo ni watumishi wa Wizara na Wafanyakazi wa Kampuni ya Rushu. Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa Mshindi wa Pili katika Kundi la Wizara za sekta ya uchumi- uzalishaji katika kilele cha kusherehekea Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji- Nane Nane iliyofanyika kwenye Viwanja vya Nzuguni, Dodoma Agosti 8, 2020. 

 


 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (kulia) akikabidhi cheti cha Ushindi wa Pili katika kundi la Wizara za sekta ya uchumi-uzalishaji kwa Mratibu wa Maonesho, banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bezia Rwongezibwa (wa kwanza kushoto) katika kilele cha kusherehekea Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji- Nane Nane iliyofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma Agosti 8, 2020. Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Uvuvi Mkuu, Ezra Mutagwaba. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Viumbe maji, Dkt. Imani Kapinga. 


Jumanne, 18 Agosti 2020

HABARI PICHA ZA MAONYESHO YA NANENANE KWENYE MIKOA YA DODOMA NA ARUSHA, TAREHE 07/08/2020

Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya ndani, Mhe. George Simbachawene akiangalia mbegu bora za malisho ya wanyama zinazozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TARILI) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni, Kanda ya Kati, Dodoma Agosti 7, 2020. 


Afisa Mauzo, Kampuni ya Inas, Hussein Juma(kulia) akimkaribisha Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene kuonja vipande vya Nyama   vilivyokaushwa na kutafunwa kama kichangamsha mdomo alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni, Kanda ya Kati, Dodoma Agosti 7, 2020. 

 


Mkuu wa Kitengo cha Uhimilishaji, Kanda ya Kati, Idara ya Uzalishaji na Masoko, Denis Sichwale(Kulia) akitoa maelezo kuhusu Uhimilishaji kwa Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni, Kanda ya Kati, Dodoma Agosti 7, 2020. 

 


 

Mratibu wa Maonesho, banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bezia Rwongezibwa (wa pili kulia) akimkaribisha Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene (kushoto, aliyevaa kaunda suti) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Kanda ya Kati, Dodoma leo Agosti 7, 2020. 


ARUSHA


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mgwira akipata maelezo ya ufugaji wa sungura kutoka kwa mtaalam wa sungura wa kampuni ya SAORE, Bw. Isack John kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (07/08/2020) 

 


Mkufunzi kutoka Wakala ya vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA), Bw. Ijumaa Bakari akitoa maelezo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (07/08/2020) 

 


Msambazaji wa madini ya Mifugo kutoka kampuni ya usambazaji wa madini (JOSERA), Bw.  Elirehema Laizer akitoa elimu ya madini na umuhimu wake kwa Mifugo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (07/08/2020) 


Daktari wa Mifugo kutoka kituo cha Uhimilishaji NAIC, Bw. Elibariki Njiku akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Suye waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (07/08/2020)