Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah (kushoto) akitoa maelezo kuhusu
mradi wa "deep sea" kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) baada ya Waziri Mkuu kufika kwenye
mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi muda mfupi uliopita kwenye Viwanja
vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (08.08.2020).
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa maelezo
kuhusu teknolojia ya uhimilishaji kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) baada ya Waziri Mkuu kufika kwenye
mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi muda mfupi uliopita kwenye Viwanja
vya Nyakabindi Mkoani Simiyu (08.08.2020), Wa pili kutoka kulia ni Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina.
Kutoka Kulia Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah wakipata maelezo namna
mradi wa "deep sea" unavyofanya kazi muda mfupi baada Mhe. Waziri
Mkuu kufika hapo leo (08.08.2020) kwenye Viwanja vya Nyakabindi Mkoani
Simiyu.
Waziri wa Kilimo Mhe.
Japhet Hasunga akiwakabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo)
Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt.
Rashid Tamatamah, Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt. Angelo Mwilawa
wakipokea zawadi ya kombe baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushika nafasi ya
pili kwenye maonesho ya Kilimo (NANE NANE) kwa upande wa Taasisi za Serikali
wakati wa kilele cha Maonesho hayo kitaifa Mkoani Simiyu (08.08.2020)
Waziri wa Kilimo Mhe.
Japhet Hasunga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya Kombe Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Utafiti wa masuala ya Mifugo (TALIRI) Dkt. Eliggy Shirima baada ya taasisi
hiyo kushika nafasi ya pili kwa upande wa taasisi zilizo chini ya Wizara wakati
wa kilele cha Maonesho ya Kilimo (NANE NANE) kitaifa Mkoani Simiyu (08.08.2020).
Kutoka kulia ni
Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt. Angelo Mwilawa, Katibu Mkuu Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel, Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah wakifurahia zawadi ya Kombe
walilokabidhiwa baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kushika nafasi ya pili
kwenye maonesho ya Kilimo (NANE NANE) kwa upande wa Taasisi za Serikali wakati
wa kilele cha Maonesho hayo kitaifa Mkoani Simiyu (08.08.2020)
LINDI
Afisa Uvuvi kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Melkidezeky Kody akitoa maelezo kwa Waziri wa Katiba
na Sheria, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba wakati alipotembelea mabanda ya Wizara
ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini katika viwanja
vya Ngongo - Manispaa ya Lindi. (08.08.2020)
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na mmoja wa wajasiriamali, Hadija Malibiche (aliyebeba mtoto) wakati alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini katika viwanja vya Ngongo - Manispaa ya Lindi. (08.08.2020)
ARUSHA
Afisa Mfawidhi kutoka kituo
cha Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Nyumba ya Mungu Mkoa wa Kilimanjaro, Bw.
Godbless Msuya (kushoto) akitoa maelezo juu ya nyavu zinazoruhusiwa na zisizoruhusiwa kwenye
uvuvi kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye
maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha (08/08/2020)
Daktari wa Mifugo kutoka Wakala
ya Maabara ya Vetenari Tanzania (TVLA), Bw. Rowenya Mushi akitoa maelezo na kuelekeza namna
ya kutumia darubini kwa wanafunzi wa shule ya msingi Maromboso waliotembelea
banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane Mkoani Arusha.
(08/08/2020)
Afisa Mifugo
kutoka Idara ya Uendelezaji wa Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Bw.
Francis Ndumbaro akitoa maelezo kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya
Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha
Themi Mkoani Arusha (08/08/2020)
Kaimu Mkurugenzi wa
Idara ya Uendelezaji wa Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Asimwe Rwiguza akijadili jambo na maafisa kutoka
Wizara hiyo kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya
nanenane Mkoani Arusha (08/08/2020)
Naibu spika wa Bunge
la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Akson akihutubia katika kilele cha
maadhimisho ya maonyesho ya nanenane yaliyofanyika kwenye viwanja vya John
Mwakangale mkoani Mbeya tarehe 08.08.2020.
Mkuu wa mkoa wa Iringa
Ally Hapi akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi kabla ya kufunga maadhimisho
ya maonyesho ya nanenane ambapo leo ndio ilikua kilele cha madhimisho hayo
yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale- Mbeya tarehe
08.08.2020.
Mratibu wa Maonesho,
banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bezia Rwongezibwa(katika) akiwa katika picha ya
pamoja na Mkurugenzi, Kampuni ya Rushu, Mabula Charles (aliyeshika Kombe)
ambaye ndiye aliyeibuka Mshindi wa kwanza katika kundi la Paredi- Wafugaji
wakubwa, Ngombe wa Nyama. Wengine wanaofurahia ushindi huo ni watumishi wa
Wizara na Wafanyakazi wa Kampuni ya Rushu. Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa
Mshindi wa Pili katika Kundi la Wizara za sekta ya uchumi- uzalishaji katika
kilele cha kusherehekea Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji- Nane Nane iliyofanyika
kwenye Viwanja vya Nzuguni, Dodoma Agosti 8, 2020.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni