MAJIBU
YA SERIKALI KUHUSU HOJA ZILIZOIBULIWA NA WAVUVI KUPITIA GAZETI LA NIPASHE LILILOKUWA NA KICHWA CHA HABARI ‘WAVUVI WATAKA
BEI ELEKEZI SANGARA’ LA TAREHE 22 NOVEMBA, 2018
NA.
|
HOJA
|
MAJIBU
|
1.
|
Kukosekana
kwa bei elekezi ya Sangara
|
Kufuatia
malalamiko ya wavuvi kuhusu bei ya Sangara, Mhe Waziri wa Mifugo na Uvuvi
alishafanyia kazi suala hilo ambapo akiwa Kanda ya Ziwa, alifanya mkutano na
wamiliki wa viwanda na bei elekezi ilitolewa kwamba kwa kila kilo moja ya
Sangara bei itakuwa ni Tsh. 5,500/=. Aidha, wadau wa viwanda pia
walikiri kwa barua kwamba watatekeleza bei elekezi kama ilivyoamriwa.
|
2.
|
Kukandamizwa
na kunyanyaswa kwa wavuvi na wanaosimamia sheria
|
Operesheni zinazoendelea zinatekelezwa kwa mujibu
wa Sheria za Nchi zikiwemo:- Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya Mwaka 2003 pamoja na
Kanuni zake za Mwaka 2009; Sheria ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 1998 na
marekebisho yake ya Mwaka 2007; Sheria ya Mazingira Namba 20 ya Mwaka 2004;
Sheria ya Uhujumu Uchumi (Economic and organized Crime Act Cap 200 Re 2002 as
amended by Act No. 3 of 2016); na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo
Tengefu Namba 29 ya Mwaka 1994. Aidha, kutokana na malalamiko ya kunyanyaswa
wananchi, wizara inashauri waliotendewa ukatili huo walete taarifa rasmi ili
hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
|
3.
|
Nyavu
stahili hazipatikani
|
- Serikali imeendelea kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza
nyavu za kuvulia samaki zinazokubalika kisheria. Mpaka sasa kuna viwanda sita (6) vya
kutengeneza vyavu ambavyo ni pamoja na CFN na Nafaka, (Mwanza), Sunflag
(Arusha), Nyota Venture, Nyamagana Fishing Net na Nashoni Mwita (Dar Es
Salaam). Aidha, kuna maduka manne (4) yanayouza nyavu za kuvulia samaki,
maduka hayo ni pamoja na Imara Fishnet, Kariakoo Fish net, Mbilinyi
Enterprises na Walid Trading yote yapo Dar Es Salaam.
Katika
kuhakikisha kwamba wavuvi wanamudu bei za vifaa vya uvuvi, Serikali inatoa msamaha wa kodi
kwa zana za uvuvi na malighafi zake zikiwemo nyuzi za kushonea nyavu (twines)
na vifungashio. Aidha, Serikali imeendelea kushauri wavuvi kujiunga katika
vikundi ili waweze kukopesheka kwa urahisi
na taasis za fedha kwa ajili ya kupata fedha za kununulia zana za
uvuvi zikiwemo nyavu za kuvulia samaki.
- kwa sasa Serikali inatoa vibali vya kuingiza nyavu nchini ili kuziba
upungufu ulipo. Mpaka sasa jumla ya vibali
31vimeshatolewa toka Julai mpaka Novemba,2018 kwa ajili ya kutatua changamoto
ya upungufu wa nyavu nchini.
|
4.
|
Wavuvi
kutozwa Kodi nyingi kama kodi za TRA, Halmashauri, kodi za samaki, mialo na
kodi za Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu
|
Kodi zote wanazopaswa kulipa wavuvi ziko kwa
mujibu wa sheria za nchi na hivyo wavuvi wanashauriwa kufuata sheria
zilizopo.
|