SERIKALI imesema kuwa katika mwaka wa fedha 2021/22 imepanga kuboresha sekta ya mifungo ikiwa ni pamoja na kujenga majosho 129, ili kuongeza thamani ya bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba
Ndaki, aliyasema hayo jana jijini Dodoma, wakati wizara yake ilipokuwa
kiwasilisha bajeti ya sekta ya mifugo kwenye kamati ya kudumu ya bunge ya
kilimo, mifugo na maji.
Alisema, Wizara hiyo imezamilia kufanya
maboresho makubwa katika sekta ya mifugo ili kuongeza thamani ya mazao
yatokanayo na mifugo na kuchangia katika pato la taifa.
Ndaki, alisema moja katika eneo ambalo
watalifanyia kazi ni kujenga majosho 129, mapya pamoja na kukarabati yaliyopo
ili kusaidia wafugaji kupata huduma hizo katika maeneo yao,
“Tutahakikisha kuwa tunajenga majosho
kwa ajili ya kuogeshea mifugo kila eneo lenye mifugo nchini lakini pia
kukarabati majosho yote yalipo ili kuwezesha wafugaji kupata huduma za ugani
katika maeneo yao”alisema
Alisema, pia eneo jingine ambalo
watalifanyia kazi ni kuboresha eneo la malisho kwa ajili ya mifugo ili kuwa na
malisho ya uhakika na kupunguza migogoro baina ya wakulima na wafugaji.
“Katika hili hivi sasa tumepunguza bei
ya kukodisha maeneo ya malisho kwa kukodisha kwa Sh. 3,500 kwa heka kwa mfugaji
atakaye hitaji eneo la malisho”alisema
Vile vile, alisema kuwa katika mwaka
huu wa fedha wamepanga kukusanya mapato katika sekta kiasi cha Sh. bilioni 50.
Awali akiwasirisha bajeti ya sekta ya
mifugo mbele ya katimati hiyo, Katibu Mkuu Wizara mifugo na uvuvi anayesimamia
sekta ya mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel alisema itasaidia kuongeza thamani
ya mifugo.
Alisema, katika mipango ya bajeti ijayo
wamepanga kuhakikisha kuwa wanawekeza katika kuboresha afya ya mifugo,pamoja na
kutafuta masoko ya mazao ya mifugo.
“Katika kipindi hichi tutahakikisha
kuwa tunatafuta masoko katika bidhaa za mazao ya mifugo kama vile nyama, ngozi
, maziwa lakini pia kuongeza fursa nyingine ya matumizi ya vitu kama kwato,
pembe na manyoya”alisema
Aidha, alisema kuwa tayari wamepata
wawekezaji kutoka nchi ya Slovakia, ambao wapenga kuja kuwekeza kiwanda cha
kutengeneza mbolea kwa kutumia manyoya, pembe pamoja na kwato.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wafugaji kutumia fursa ya mitamba ya kisasa iliyopo katika Ranchi za taifa kufanya uhimilishaji ili kupata mifugo iliyobora itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kuongeza pato la taifa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akizungumza wakati wa uwasilishaji wa Taarifa za Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na Makadirio ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 ya Sekta ya Mifugo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyokutana leo Machi 29, 2021 bungeni Dodoma.Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Prof. Elisante Ole Gabriel,
akiwasilisha Taarifa za Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha
2020/21 na Makadirio ya Bajeti ya mwaka 2021/22 ya Sekta ya Mifugo mbele ya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyokutana leo Machi
29,2021 bungeni Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara kwa tiketi ya CCM, Christopher Ole Sendeka, akiwaslisha hoja wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa za Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Kipindi cha Mwaka 2020/21 na Makadirio ya Bajeti ijayo ya 2021/22 ya Sekta ya Mifugo leo Machi 29,2021 bungeni Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatamah akiwasilisha Taarifa za Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/21 na Makadirio ya Bajeti ijayo ya mwaka 2021/22 ya Sekta ya Uvuvi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyokutana leo Machi 29,2021 bungeni Dodoma.
Baadhi ya Viongozi katika Sekta ya Uvuvi wakifuatilia uwasilishwaji wa Taarifa za Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 na Makadirio ya Bajeti ijayo ya 2021/22 ya Sekta ya Uvuvi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyokutana leo Machi 29,2021 bungeni Dodoma.