Mpango wa Modenaizesheni ya Sekta ya Mifugo imelenga kuleta mageuzi makubwa yatakayoifanya sekta hii kuwa na mchango chanya hivyo kuchangia zaidi katika pato la taifa, kuyakabili mahitaji ya soko na tija kiuchumi, kijamii na uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo endelevu. Mkakati huu umelenga kuzivuna fursa katika sekta za nyama, maziwa na kuku kwa kuimarisha usimamizi wa mnyororo mzima wa thamani ili kukabiliana na umaskini pamoja na kufanya maboresho katika usalama wa chakula, upatikanaji malisho bora, ubora wa vinasaba kwenye mifugo asilia, kupunguza migogoro baina ya makundi ya wakulima, waf ugaji na hifadhi, uhakika wa maji na virutubisho vinginevyo.
Mkakati unalenga pia kutoa majibu ya changamoto za vinasaba katika mifugo asilia, ufugaji na uthibiti wa magonjwa, uwepo wa masoko ya uhakika, ubora na usalama katika bidhaa za mifugo na uongezaji thamani katika bidhaa za mifugo. Mkakati utakaoratibu mahitaji yote ya kisera, kisheria, kiuchumi na kimkakati hivyo kupelekea ustawi na ubora wa sekta ya mifugo mageuzi kutoka ufugaji wa mazoea kuwa wa kisasa, wenye kuleta tija, kuhifadhi mazingira, kuinua viwango vya lishe kwa maendeleo endelevu ya jamii na taifa kwa ujumla kwa kufanya yafuatayo:-
(i) Kuwawezesha wafugaji kwa kuwapa teknolojia za kisasa,
ujuzi na elimu bora ya ufugaji
(ii) Kuwezesha upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo
(iii) Kuimarisha miundombinu ya masoko ya mifugo na bidhaa za mifugo
(iv) Kuwawezesha wafugaji, jamii za wafugaji na sekta binafsi kuwa na mchango zaidi
(v) Kuimarisha taasisi za kitaifa na serikali za mitaa kuweka ukisasa katika sekta ya mifugo
(vi) Kuboresha mifumo ya kitaasisi na kisera katika uwekezaji ili kuweka mazingira bora ya kuvutia uwekezaji baina ya seri-
kali na sekta binafsi.
Muundo wa Mpango wa Modenization.
Mpango wa modenaizesheni ya Sekta ya Mifugo unalenga kutekeleza Sera ya Taifa ya Mifugo ya mwaka 2006 katika muktadha wa Dira ya Taifa ya miaka mitano, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), Kilimo Kwanza, Mkakati wa Taifa wa Kukuza Uchumi
na kuondoa Umaskini (MKUKUTA),
1. Kipaumbele cha kwanza ni :-
(i) Mkakati wa Kuanzisha maeneo maalumu ya malisho katika Vijiji: Mkakati huu unalenga kuanzisha na kuhifadhi maeneo ya malisho katika vijiji kama ilivyo kwa maeneo ya hifadhi ya misitu ya vijiji.
(ii) Uimarishaji vinasaba assilia (Sus- tained Genetic gains in Tanzania Livestock breed)
(iii) Kuimarisha ufugaji wa ng’ombe wa nyama
(iv) Kuimarisha ufugaji wa kuku
(v) Kuimarisha ufugaji wa ng’ombe wa maziwa
(vi) Kuimarisha masoko ya ndani na nje ya nchi
(vii) Kuimarisha mifumo ya vet erinari ili kuhakikisha afya na
usalama kwa mifugo na binadamu .
(viii) Kuboresha tafiti na huduma za ugani kwa kuimarisha mifumo ya mawasiliano ya kisasa .
(ix) Kujenga jamii za wafugaji zilizo imara .
(x) Kupunguza migogoro ya ardhi na kuhifadhi mazingira (Conflict to coexistence: Livestock & Con- servation)
(xi) Kichocheo katika uwekezaji kwa maendeleo ya sekta ya mifugo .
(xii) Kuhuisha Mpango wa maendeleo wa sekta ya mifugo katika mpango wa taifa wa maendeleo ya sekta ya kilimo na maendeleo vijijini .
(xiii) Masuala mtambuka Uhifadhi na usimamizi wa malisho Kuna msukumo mkubwa wa wa magugu na mimea mingine inayoendelea kuharibu mifumo ya ikolojia hivyo kuathiri malisho asilia. Ongezeko la shughuli za kibinadamu na wingi wa mifugo unaombatana na uharibifu mkubwa wa mazingira na pia harakati za uhifadhi wa ardhi vimepelekea migogoro ya mara kwa mara katika maeneo mengi nchini.
Takribani asilimia 2% ya ardhi inayofaa kwa malisho (hekta milioni 1.28) inamilikiwa na serikali za vijiji katika mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao umetekelezwa na vijiji chini ya asilimia 10% katika wilaya 81 kati ya wilaya 150. Vile vile,aina
23 kati ya aina 30 za magugu vamizi zilizogundulika nchini Tanzania yameathiri zaidi maeneo ya malisho hivyo mifumo imara ya ikilojia ni nguzo muhimu kwa uzalishaji wa mifugo asilia na ile ya kisasa. Kwa kutambua kuwa zaidi ya asilimia 50% ya kaya za Tanzania zinafuga, suala la malisho linasta- hili kupewa kipaumbele kikubwa hivyo jukumu la kwanza na la msingi katika mkakati huu wa modenaizesheni ni kutafuta na kuimarisha malisho bora.
Mkakati huu utazingatia sheria na kanuni zilizopo na zitakazotungwa pia zikisimamiwa ipasavyo.