MAELEZO
KUJIBU KERO ZA WAVUVI WADOGO KWA SERIKALI
NA.
|
TAREHE
|
KERO HUSIKA
|
MAELEZO
|
1.
|
2001 - 14
|
Kuhamishwa kutoka maeneo salama ya
maegesho ya vyombo vya uvuvi katika mlango wa Bandari ya Dar Es Salaam na
Mamlaka ya Bandari Dar Es Salaam
|
Wizara inakubaliana na ukweli kuwa
Bandari ya Dar Es Salaam siyo salama, hivyo kuna umuhimu wa wavuvi wadogo
kuhamishwa. Kwa kuzingatia Mkataba wa Kimataifa kuhusu usalama wa Bandari chini ya taasisi ya Kimataifa ijulikanayo
kama “International Maritime Organization- IMO” ambao Tanzania imeridhia,
uhamishaji huu ni muhimu ufanywe kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.
Hata hivyo kwa kuzingatia kwamba eneo la
feri lina watu wengi wenye shughuli mbalimbali zinazowapatia kipato, ni
mtizamo wa Wizara kuwamba uhamishwaji huo uzingatie maandalizi ya maeneo
mbadala yatakayotumiwa na wavuvi husika. Kwa kuwa agizo la uhamishwaji huo
lilikuwa la haraka, Wizara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wavuvi
kuhusu suala hilo hatua zilizochukuliwa ni pamoja na:-
i.
Kufanya mikutano mbalimbali iliyohusisha wavuvi
pamoja na wadau wengine wakiwemo Wizara ya Uchukuzi; Halmashauri za Manispaa
za Temeke, Ilala, na Kinondoni; Mamlaka ya Bandari; na Vyama vya wavuvi
kujadili suala hilo;
ii.
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi iliiandikia
Wizara ya Uchukuzi kusitisha zoezi la kuwaondoa wavuvi hadi pale maeneo
mbadala yatakapopatikana na kuwekewa miundombinu inayofaa kutumiwa na wavuvi
kuegesha vyombo vyao na masoko ya kuuzia samaki katika Halmashauri za Manisapaa
za Temeke na Kinondoni; na
iii.
Wizara iliwasiliana na Wizara ya TAMISEMI kuhusiana
na suala hili ili kuzielekeza Halmashauri za Manispaa za Temeke na Kinondoni
kuliweka kuwa suala la kipaumbele katika mipango yao ya maendeleo.
|
2.
|
2008
- 14
|
Kukosekana
kwa utekelezaji wa Waraka wa Mkurugenzi wa uvuvi uliopiga marufuku matumizi
yaharamu na zisizo kuwa haramu mwaka 2008
|
Waraka tajwa ulikuwa wazi kupiga marufuku
uvuvi wa kutumia zana na vifaa haribifu hususani nyavu aina za Juya au
kokoro, Mtando, “ring net” na matumizi ya mitungi ya gesi ya oksijeni, miwani
na viatu vya kupigia mbizi. Waraka huo ulitolewa kulingana na Kifungu Na. 4
(3) cha Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni za Uvuvi za Mwaka
2005, Kanuni ya 14, 15 na 17 (2) (a) zilizompa Mamlaka Mkurugenzi wa Uvuvi
kutoa nyaraka na maelekezo ya kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Uvuvi.
Ufafanuzi wa Hoja:-
i.
Zana haramu kwa mujibu wa sheria huthibitishwa
kitaalamu kupitia tafiti na kuthibitika kuwa zina madhara kwa rasilimali ya
uvuvi na mazingira yake. Madhara hayo ni pamoja na kuathiri uwingi wa
rasilimali za uvuvi na ubora wa mazingira hivyo kusababisha kutokuwepo uvuvi
endelevu;
ii.
Uharamu wa zana unatokana na jinsi ilivyotengenezwa,
matumizi yake, “material” iliyotumika, mahali inapotumika na athari zake
katika rasilimali za uvuvi na mazingira yake. Aidha, zana halali ikitumika
eneo lisiloruhusiwa inakuwa zana haramu ya uvuvi;
iii.
Uvuvi wa samaki katika maji yote una zana
zinazokubalika Kisheria na hivyo hakuna sababu ya zana mbadala kama
inavyodaiwa katika hoja hii. Hata hivyo, endapo utafiti utabaini zana mpya ya
uvuvi ambayo ni rafiki kwa rasilimali na mazingira, Serikali itahakikisha
kuwa teknolojia husika inasaambazwa kwa wavuvi na kujumuishwa katika sheria;
na
iv.
Tanzania ina maji makuu (Major water bodies) ambayo
inamiliki pamoja na nchi nyingine na hivyo usimamizi wake unazingatia
makubaliano ya pamoja ya Kikanda na Kimataifa (harmonization). Kwa msingi huo, zana nyingi zinazokubalika
kisheria pia zinazingatia suala hili na tunakubaliana na nchi jirani aina ya
zana na mbinu za matumizi yake.
Kwa
kuhitimisha hoja hii, Mheshimiwa Waziri alisisitiza kuwa katika Waraka huo
matumizi ya gesi ya Oksijeni na viatu vya kuogelea vimeruhusiwa kwa wavuvi
wenye leseni za kuvua samaki hai wa mapambo, wavuvi wanaruhusiwa kutumia
miwani na mitungi ya Oksijeni kwa usalama wao, waogeleaji, burudani, utalii
kwenye matumbawe pamoja na utafiti. Aidha, Waziri alisisitiza kuwa anayetaka
kutumia zana apate vibali kutoka Idara ya Maendeleo ya uvuvi na kufuata
Sheria husika. Maamuzi ya Bunge la wakati huo kuhusu Tamko la Serikali la
2008 yaliwekwa kwenye Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009.
Kama
ilivyofafanuliwa hapo juu, Waraka ulilenga kuimarisha usimamizi wa rasilimali
za uvuvi kwa kuzingatia Sheria. Aidha, Sheria haibagui kama inatumika kwa
uvuvi mdogo ama mkubwa bali huangalia uendelevu wa rasilimali na uhifadhi wa
mazingira.
|
3.
|
2000
- 12
|
Juu
ya Waraka wa Mwaka 2008, Wavuvi tulikatazwa kurudi tena Bungeni ili
kukumbusha utekelezaji wa KAULI YA SERIKALI na kero nyingine za maeneo ya
maegesho ya vyombo vya uvuvi, Kodi za zana za uvuvi, kama ilivyo kwa wenzetu
wa kilimo wanavyoruhusuka kwa mujibu wa sheria NG NA. 305 ya tarehe
28/08/2009 inayotaja uvuvi na kilimo
|
Wizara inatambua kupanda kwa gharama za
zana za uvuvi jambo ambalo huathiri usitawi wa shughuli zao. Hata hivyo,
kutokana na juhudi za Wizara na wadau kufuatilia suala hili, Serikali kuanzia
mwaka 2011 iliondoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye injini za
kupachika (outboard engine), vyombo vya uvuvi, Nyuzi za kushonea nyavu, Nyavu
za uvuvi na vifungashio.
|
4.
|
2003
- 14
|
Kucheleweshwa
kwa ufikishaji wa leseni za uvuvi na ukaguzi wa vyombo vya uvuvi baadhi ya
maeneo ya mialo/bandari za uvuvi chini ya SUMATRA na Idara ya Maendeleo ya
Uvuvi
|
Kwa
mujibu wa Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni za Mwaka 2009,
utoaji wa leseni za uvuvi chini ya mita 11 hutolewa na Halmashauri husika na
vyombo vinavyozidi mita 11 hutolewa na Wizara. Leseni hii hutumika kuanzia Januari hadi
Desemba. Aidha, Halmashauri ndizo zinazohusika na usajili wa vyombo vyote
vinavyoruhusiwa kuvua ikiwa moja ya vyanzo vyake vya mapato. Ukaguzi na
utoaji wa Cheti cha Usalama wa Chombo (Seaworthness Certificate) ni jukumu la
Mamlaka ya Usalama wa Vyombo vya Usafiri na Nchi Kavu na kwenye Maji
(SUMATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi.
Ili
kuondoa tatizo la ucheleweshaji wa utoaji wa leseni na usajili wa vyombo vya
uvuvi, Wizara kwa kuanzia imechukua jukumu la kushirikiana na Halmashauri za Manispaa
za Temeke, Ilala na Kinondoni za Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kuanzisha mfumo wa
kutoa leseni za papo kwa papo, kusajili vyombo na kutoa tagi maalum (Smart
License). Zoezi hili litasaidia upatikanaji wa leseni za uvuvi kwa wakati na
kuongeza mapato kwa Halmashauri. Kutokana na mafanikio ya zoezi hili, Wizara
itaendelea kutoa elimu na kuhamasisha Halmashauri nyingine zifuate mfumo huu
ambao unatarajiwa kujumuishwa kwenye
Sheria ya Uvuvi.
|
5.
|
2014
|
Kurudiwa
tena kwa amri ya kututaka tuondoke eneo salama kwa maegesho ya vyombo vya
uvuvi kwa madai ya kuwa uwepo wetu unakaribisha ushirikiano na maharamia wa vyombo
vya majini
|
Wizara
ya uchukuzi imesitisha zoezi la kuhamisha wavuvi hadi pale eneo mbadala litakapopatikana.
Halmashauri za Manispaa za Temeke na Kinondoni kwa kushirikiana na wadau
zinaendelea kutafuta maeneo mbadala
|
6.
|
2010
|
Kutothamini
ushiriki wetu katika usimamizi wa rasilimali za uvuvi na mazingira pale
tulipokamata wavuvi haramu tukiwa baharini
|
Katika
maji yote nchini Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika
ulinzi wa rasilimali za Uvuvi. Serikali ina utaratibu wa kusimamia rasilimali
za uvuvi kwa kushirikisha Vikundi vya Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi (Beach
Management Units – BMUs).
Kwa
mujibu wa Sera ya Uvuvi ya Taifa (1997), moja wapo ya wadau walioainishwa
katika kusimamia rasilimali za uvuvi ni Jamii za Wavuvi, Vikundi mbalimbali
na Mashirika yasiyoya Kiserikali. Katika kutekeleza Sera hii, Sheria ya Uvuvi
Na. 22 ya Mwaka 2003, Kifungu cha 18 (1 na 2) kinatamka wazi wazi ushiriki wa
jamii za wavuvi wakiwemo wavuvi wenyewe kwa kuanzisha kwa hiari Vikundi vya
Usimamiazi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi (Beach Management Units – BMUs).
Aidha,
majukumu yao yameainishwa kikamilifu katika Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009,
ushiriki wa wavuvi katika kusimamia rasilimali za uvuvi kupitia vikundi vyao
(BMUs) umefafanuliwa kwa kina katika Kanuni ya 25(1-3). Katika Halmashauri za
Manispaa za Temeke, Ilala, na Kinondoni kuna jumla ya BMUs ….. na hivyo kufunya idadi ya BMUs kufikia 739 kwa nchi nzima
Kwa
msingi huu, Wizara inatambua na kuthamini umuhimu wa wadau katika ulinzi
shirikishi wa rasilimali za uvuvi na mazingira yake. Hivyo, Wizara imekuwa ikishirikisha jamii
za wavuvi katika masuala mbalimbali kwa mfano mikutano, warsha, semina,
maonesho, upatikanaji wa taarifa za kiintelijensia na kufanya doria. Aidha,
elimu imeendelea kutolewa kuhusu uendelevu wa rasilimali na mazingira ya
uvuvi na hatua za kuchukua iwapo wanakamata wahalifu wanaovunja Sheria ya
uvuvi.
|
7.
|
2012
- 14
|
Tumekuwa
tukilipishwa ushuru wa mauzo ya mazao ya baharini (samaki nk.) bila kuondoa
gharama za uendeshaji/mtaji wa uvuvi. Hali tunapoitolea kauli lakini haina
majibu
|
Utozaji
wa ushuru wa mauzo ya mazao mbalimbali nchini yakiwemo ya uvuvi unafuata
Sheria, Kanuni na taratibu za utozaji wa kodi. Utozaji wa ushuru wa mauzo ya
mazao ya uvuvi ni jukumu la Halmashauri husika kulingana na Sheria husika na
Sheria ndogo (By-Laws) kama chanzo cha mapato cha Halmashauri hizo.
|
8.
|
2000
- 14
|
Kero
ya ulazima wa kurudia usajili na kukata leseni ya uvuvi kila tunapofika
katika Halmashauri nyingine. Ikiwa leseni hiyo ina hadhi moja ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuna tofauti gani na vyombo vya nchi kavu?
Ikiwa fedha zote za leseni huenda katika hazina moja ya nchi
|
Kulingana na Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka
2003 na kanuni zake za 2009 na Sheria ya Ugatuaji wa Madaraka (D by D) ya
mwaka 1982 na Maboresho yake ya Mwaka 1996 na utekelezaji wake kuanza mwaka
1998, wavuvi wadogo wapo chini ya usimamizi wa Halmashauri. Mfumo huu unawezesha
kudhibiti nguvu ya uvuvi katika eneo husika. Aidha, mapato kutokana na leseni
na usajili wa vyombo vya uvuvi na wavuvi ni chanzo cha mapato kwa ajili ya shughuli
za maendeleo ya Halmashauri husika. Vilevile, mapato haya hutumiwa na
Halmashauri katika usimamizi wa rasilimali za uvuvi, mazingira yake na
maendeleo ya Sekta.
|
9.
|
2002
- 15
|
Ubabaishaji
na upotoshaji wa makusudi juu ya uendeshaji wa mradi wa kuendeleza uvuvi kwa
soko la samaki Magogoni/Feri kwa kukosa uendeshaji wenye dhamira ya
kuendeleza uvuvi Tanzania na kuondoa umaskini katika nchi zilizokithiri kwa
umaskini duniani chini ya HIPC na MKUKUTA
Yanayofanywa
na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yatatufanya tusisaidiwe tena na wahisani
waliosaidia uwepo wa soko hili kwa jamii ya sekta ya uvuvi
|
Mfumo
wa uendeshaji wa soko la Feri tangu lilipokabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa
ya Ilala ulikuwa bayana kuwa soko litaendeshwa na Bodi maalumu itakayohusisha
wadau mbalimbali wa sekta. Serikali imekwisha toa maagizo kwa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala ianzishe Bodi hii. Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Kilimo, Mifugo na Maji imetoa maagizo kwa Halmashauri hiyo ilipotembelea soko
hilo tarehe 9/03/2015 kukamilisha suala la uanzishwaji wa Bodi. Wizara
itaendelea kufuatilia utekelezaji wa maagizo haya.
|
10.
|
2015
|
i.
Usitishaji wa mauzo ya zana za uvuvi zilizoagizwa
kutoka nje ya nchi,
ii.
Uteketezaji wa zana za uvuvi kwa watumiaji,
iii.
Usitishaji wa aina ya uvuvi uliokuwa unavuliwa kwa
miaka mingi na jamii
iv.
|
i.
Serikali haijasitisha mauzo ya zana halali za uvuvi
kutoka nje kwani uzalishaji wa ndani wa zana husika huatoshelezaji mahitaji
ii.
Uteketezaji wa zana haramu za uvuvi ni suala la
kisheria na ni mahakama pekee inayotoa maamuzi ya uteketezaji wa zana za
uvuvi zilizokamatwa kwa kuvunja sheria.
iii.
Kulingana na sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003,
aina yoyote ya uvuvi (wa kienyeji au kisasa) ambayo siyo rafiki kwa
rasilimali za uvuvi na mazingira unakatazwa. Lengo ni kuwa na uvuvi endelevu
unaozingatia ikolojia na mazingira.
|
11.
|
2015
|
Ni
juu ya VAT na ushuru, kwenye miaka ya 2008 hapakuwa na ushuru na VAT kwa zana
za kilimo na uvuvi. Lakini hivi sasa leo katika zana za uvuvi tu kuna VAT
katika zana za uvuvi kwa 50% kwa kulipia nyuzi ndoana na mashine za
kuendeshea vyombo vya uvuvi
|
Kuanzia mwaka 2011, Serikali iliondoa kodi
ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye injini za kupachika (outboard engine),
vyombo vya uvuvi, Nyuzi za kushonea nyavu, Nyavu za uvuvi na vifungashio.
|
12.
|
2015
|
Ni
juu ya malipo ya leseni ya ukaguzi na usajili wa vyombo vya uvuvi kwa wavuvi
wadogo kulipishwa kwa thamani
|
Kulingana na
Sheria ya Uvuvi Na, 22 ya mwaka 2003, viwango vya leseni za uvuvi hutozwa
kulingana na thamani ya Dola za Kimarekani kwa wakati husika (equivalent).
Hata hivyo, viwango vya leseni vilivyopo katika sheria ya sasa ni vidogo sana
ukilinganisha na thamani ya mazao ya uvuvi nchini na nje ya nchi. Kwa mfano,
leseni ya uvuvi ni dola 10 kwa mwaka ambayo ni sawa na shilingi 18,000/= kwa
mwaka.
|
MAELEZO YA UWAWANDA KATIKA KUANISHA KERO ZA WAVUVI KATIKA MWAMBAO WA BAHARI YA HINDI NA KUTOA MUELEKEO WA UTATUZI WA KERO.
1. UTANGULIZI:-
MHESHIMIWA MKURUGENZI WA IDARA YA UVUVI
UWAWANDA tunatoa shukrani zetu za dhati kwako binafsi kwa kutujali na
kutukumbuka/kutushirikisha katika Semina na Warsha mbalimbali za Wadau wa Uvuvi.
2. UWAWANDA NI:-
Umoja wa Wavuvi Wadogo Wadogo Dar es Salaam, Ni Umoja wa Kijamii uliosajiliwa
Kisheria Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Kupewa hati ya usajili Na. SO:8061
ya 1995 kwa nia na madhumuni ya kuwajumuisha Wavuvi Wadogo Wadogo wa Mkoa wa
Dar es Salaam na kanda ya mwambao wa bahari ya hindi kuwa pamoja na kufanya
shughuli zao za Uvuvi kwa kufuata Sheria za nchi.
3. MALENGO
- Sehemu kubwa ya Wavuvi Wadogo Wadogo ni Wanachama na Wanatumia umoja huu kwa maendlezi ya Uvuvi endelevu kwa kupata maslahi yao ya kila siku.
- Kuona namna Wizara/Idara ya Uvuvi inavyoweza kuchangia katika kuboresha hali duni ya Wavuvi Wadogo Wadogo.
- Kuwa na Chombo cha kutetea hali ya maslahi ya Wavuvi Wadogo Wadogo.
- Kuelimisha Wanachama ambao ndio walengwa juu ya:
(b) Umuhimu wa kuzingatia Uvuvi halali
(c) Umuhimu wa kuelewa na kuzingatia sheria, taratibu na maadili yanayosimamia shughuli za
Uvuvi
- Kuwasaidia Wavuvi Wadogo Wadogo kuendesha Uvuvi kwa namna ambayo sio tu inawapatia riziki bali pia kuwapunguzia (kuondoa) umaskini.
- Kujumuika na taasisi nyingine katika kutunza mazalio ya samaki na kuhakikisha kuwabahari inakuwa endelevu kwa maisha ya Wavuvi na vizazi vijavyo...
- Umoja wetu kuwa chombo muhimu na daraja (kiunganishi)baina ya serikali na Taasisi nyingine kwa upande mmoja na Wavuvi Wadogo Wadogo (UWAWADA) kwa upande mwingine.
USHIRIKI WA UWAWADA KATIKA MJADALA KUHUSU MITAALA YA
SHUGHULI ZA UVUVI
1. USHIRIKI:-
Wa wavuvi wadogo (UWAWADA) kupewa fursa ya kuchangia katikauundaji wa
mitaala ya shughuli za Uvuvi. Hili tunaomba lizingatiwe.
2. MAHITAJI
Mtaala ulio na faida maana kwa mvuvi ni ile ambao unalenga katika kushughulikia
mahitaji ya mvuv - kwa maana nyingine mtaala ushughulikie mambo yafuatayo;-
i) Kukuza ujuzi wa mvuvi mdogo katika zifuatazo;
a) Ujuzi kuhusu uvuvi kwa ujumla kama vile.
1. USHIRIKI:-
Wa wavuvi wadogo (UWAWADA) kupewa fursa ya kuchangia katikauundaji wa
mitaala ya shughuli za Uvuvi. Hili tunaomba lizingatiwe.
2. MAHITAJI
Mtaala ulio na faida maana kwa mvuvi ni ile ambao unalenga katika kushughulikia
mahitaji ya mvuv - kwa maana nyingine mtaala ushughulikie mambo yafuatayo;-
i) Kukuza ujuzi wa mvuvi mdogo katika zifuatazo;
a) Ujuzi kuhusu uvuvi kwa ujumla kama vile.
- Mbinu nzuri za uvuvi.
- Matumizi ya nyenzo za Uvuvi.
- Ujuzi kuhusu tabia za bahari na namna ya kutumia tabia hizo za bahari.
- Usajili mzuri wa vyombo vya Uvuvi.
b) Ujuzi binafsi wa mvuvi kuvua ukizingatia mambo kama matayarisho muhimu kabla na
wakati wa kuvua. Usalama wa mvuvi awapo baharini n.k
ii) Kuhamasisha na kukuza ujasiriamali miongoni mwa wavuvi.
- Mafunzo kuhusu biashara ya uvuvi na faida zilizopo.
- Mafunzo ya kuandika rasimu za mradi kwa ajili ya kupatia mkopo.
- Mafunzo ya ushirika.
iii) Mafunzo kuhusu utunzwaji wa samaki kwa lengo la kuhifadhi ubora wake.
iv) Mafunzo kuhusu uhifadhi wa bahari na utunzaji wa mazingira ya ufukwe za bahari
v) Mafunzo ya uelewi wa sheria na ujenzi wa utawala bora wa mitandao ya vikundi vya
uvuvi
iv) Mafunzo kuhusu uhifadhi wa bahari na utunzaji wa mazingira ya ufukwe za bahari
v) Mafunzo ya uelewi wa sheria na ujenzi wa utawala bora wa mitandao ya vikundi vya
uvuvi
- kuna mahitaji makubwa ya samaki katika masoko ya ndani na nje ya Tanzania.
- Samaki wa Ukanda wa uchumi na Bahari wataongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.
- Baadhi ya wabia wana nia ya kuendesha uvuvi Tanzania.
Programu na mradi ambayo itaongezea Ajira na mapato ya samaki ni:
1. Programu ya kujenga uwezo katika uvuvi ambao utahusisha kuanzisha na kuimarisha
Ushirika katika uvuvi, kutoa elimu ya Teknmolojia muafaka katika kuvua samaki na
kuwaunganisha na wanunuzi na walaji wa samaki.
2. Programu ya kuimarisha vyombo vya uvuvi kuwa na usjili wa kisasa.
3. UTEKELEZAJI WA MALENGO:
- Kazi kubwa iliyofanywa mpaka sasa ni uhamasishaji wa wavuvi wadogo kujiunga na kutumia umoja wao kwa maendeleo yao. Na sehemu kubwa ya wavuvi wadogo wadogo kwa sasa ni wanachama.
- Umoja wa wavuvi wadogo wadogo kwa muda mrefu sasa umekuwa ndo njia ya mawasiliano baina ya serikali, serikali za mitaa na taasisi kadhaa katika kuwafikia wavuvi wadogo wadogo.
- Tumeshiriki kikamilifu katika jitihada za kuunga mkono TAMKO la serikali (Wizara) la kupambana na uvuvi haramu tukiwa watoaji taarifa kuhusu wahusika wa vitendo hivyo viovu. kwa kuelekeza mbinu wanazotumia na maeneo wanayoendesha uovu wa uvuvi haramu kwa kupiga vita uvuvi wa kokoro na uvuvi wa mabomu.
- Tunahusika kikamilifu katika kuweka mazingira safi ya fukwe hususan maeneo yanayozunguka soko la samaki la Feri.
- Katika vikao vyetu tumekuwa tunakumbushana juu ya umuhimu wa kuzingatia taratibu na maadili ya uvuvi halali.
4. UPUNGUZE/UDHAIFU WA WAVUVI WADOGO:-
- Uelewa mdogo wa wavuvi juu ya sheria, kanuni na maelezo ya Wizara/idara namna nzuri ya kutunza mazingira ya bahari.
- Nyenzo duni za kuendesha shughuli za uvuvi kwa kuzingatia maeneoya uvuvi kwa sasa yako maeneo ya mbali (mengi)
- Mawasiliano duni kati ya Wizara/idara na wavuvi wadogo kwa kupeana taarifa za mara kwa mara.
- Sheria zote za uvuvi zimetungwa kwa lugha ya kingereza kwa hiyo ni vigumu wavuvi wadogo wadogo kuzisoma na kuzielewa.
- Ushindani usio wa mazingira sawa baina ya wavuvi wadogowadogo na wawekezaji wakubwa.
- Nyenzo/vyombo duni za utendajizinazoshughulika katika maeneo am bayo pia yanatumiwa na wawekzaji wenye nyenzo/vyombo vya habari.
- Sheria, taratibu na maelekezo ambayo yanaonekana dhahiri kuwapendeza wawekezaji wakubwa.
- Leseni ya Uvuvi imekuwa ni kikwazo hata kama unayo, umekatia Dar es salaam ukienda kuvua Kilwa au Mafia ukate tena leseni nyingine ya uvuvi.
- Mapato ya malipo ya mwanzo ya samaki asilimia tano saasa imekuwa mzigo mkubwa kwa mvuvi mdogo ukiangalia gharama zilizotumika ali[pokwenda kuvua.
- Zana za uvuvi zinauzwa na wafanya biashara kwa bei ghali sana haziwezi kumsaidia mvuvi mdogo kujikwamua kutoka hapa alipo.
- Soko lisilo na uhakika ambalo pia linafurishwa na wawekezaji wakubwa
- Usumbufu unaotokana na mamlaka za bandari kutojali wala kuwatambua wavuvi wadogo wadogo hata kama wao ndio chanzo cha eneo lote la bandari.
UDHAIFU WA KANUNI NA SHERIA ZA UVUVI ZIIMARISHWE:-
MAPENDEKEZO
Kwakuwa utaratibu tunaoenda nao kwa sasa hauna tija, tunafahamu mvuvi haruhusiwi kuvua samaki mpaka awe na LESENI. Sisi kama UWAWADA tunapendekeza kuwa wavuvi wote wakaguliwe LESENI zao bandarini na wakiuza samaki ikiwa hajakata LESENI samaki wake wakamatwe wauzwe na mamlaka husika kisha akatiwe LESENI papo hapo pamoja na kulipa faini ya kosa lake.
Tunapendekeza kuwa mvuvi yeyote akikutwa amebebazana za kulinda za uvuvi baharini akamatwe na apew adhabu kama itakavyo tajwa kutokana na kosa.
- Kuwa na chupa za Gesi bila kibali maalum
- Kukutwa na baruti
- Bunduki
- Chuma chenye ncha kali
- Mimea yenye sumu
- Kemikali za viwanda
ADHABU
1. Miaka mitatu jela au zaidi
2. Faini milioni mbili na zaidi
3. Chombo pamoja na zana zake vifilisiwe na baadhi kuteketezwa kwa moto
UVUVI WA NYAVU (RING NET)
Uvuvi wa nyavu zijulikanzo kama RING NET unaovuliwa "MCHANA" upigwe marufuku.
Kisheria uvuvi huu wa mchana wavuvi hawafuati sheria walio wekewa na idara ya uvuvi.
- Wanavua kina cha maji mita (7) hadi (10) badala ya mita (50) na zaidi.
- Kuwa uvuvi hu wa mchana wavuvi wote hutumia chupa za Gesi (5).
- Hawaiheshimu mitego ya watu wengine.
- Samaki wa kuvuliwa mwezi mmoja wao wanavua kwa siku mmoja.
- Uvuvi huu wa kuvua wa kuwafukuza samaki una madhara makubwa ya kuwahamisha samaki na kutoweka katika maeneo hayo
Faini milioni tano au kifungo cha miaka mitatu au vyote na mtego na chombo kifilisiwe
na mtego huu utekelezwe.
KOKORO
Mvuvi yeyote atakae kamatwa anavua kokoro kwa kuzingatia kuwa kokoroni uvuvi unao
haribu mazalia ya samaki na kuua samaki wachanga. Adhabu yake iwe miaka iwili jela,
faini milioni tatu,mtego na chombo vifilisiwe na mtego uteketezwe.
NYAVU ZA KUTEGA
Nyavu za kutega zianzie nchi mbili na nusu na kuendelea.
MAKAMPUNI WASHIRIKI WA UVUVI
Makampuni ya uvuvi ndani na nje ya nchi yasipewe kibali hadi wawe na barua ya
utambulisho kutoka Taasisi za uvuvi zilizo karibu nao.
Makampuni yanayo jishughulisha na rasilimali za bahari ikiwa ni pamoja na
na mtego huu utekelezwe.
KOKORO
Mvuvi yeyote atakae kamatwa anavua kokoro kwa kuzingatia kuwa kokoroni uvuvi unao
haribu mazalia ya samaki na kuua samaki wachanga. Adhabu yake iwe miaka iwili jela,
faini milioni tatu,mtego na chombo vifilisiwe na mtego uteketezwe.
NYAVU ZA KUTEGA
Nyavu za kutega zianzie nchi mbili na nusu na kuendelea.
MAKAMPUNI WASHIRIKI WA UVUVI
Makampuni ya uvuvi ndani na nje ya nchi yasipewe kibali hadi wawe na barua ya
utambulisho kutoka Taasisi za uvuvi zilizo karibu nao.
Makampuni yanayo jishughulisha na rasilimali za bahari ikiwa ni pamoja na
- Kuvua samaki
- Kuchakata samaki
- Kufuga Samaki
- Kufuga kaa
- Kufuga kamba n.k
zilizopo karibu nae.
Kufanya hivyo ni kudhibiti ili utendaji uende na sheria alizo pangiwa
UWEPO LESENI YA MUUNGANO
"UWAWADA" unapendekeza uwepo kw aleseni ya muungano kwa sababu wavuvi pande
zote hulazimishwa kukata leseni ya upande mmoja alipo hata kama anayo leseni ya upande
wa pili, vibali hawavitaki pande zote.
MAZINGIRA KWA WAVUVI
Tunapendekeza kuwa wavuvi wapangiwe zone za uvuvi ili kutunza na kuendeleza uwepo
uvuvi endelevu.
Kufunga eneo moja na kuruhusu eneo lingine kwa muda wa miezi sita na atakae kiuka
utaratibu uliowekwa achukuliwe hatua za kisheria ni pamoja na kifungo miezi mitatu faini
laki mbili au vyote pamoja.
WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
Ilione suala hili kisheria kutoa elimu ya uvuvi kw awavuvi kupitia maafisa ugani waliopo
katika maeneo yao ya kazi katika mwalo, vituo vya kushushia samaki na maeneo ya
uvuviya samaki wabichi.
Wizara/idara itie mkazo kwa makampuni na mashirika kuwakopesha wavuvi pembejeo za
uvuvi, kama wanavyo kopeshwa wakulima pembejeo za kilimo, kufanya hivyo itasaidia
kupunguza umaskini uliokithiri kwa jamii ya wavuvi nchini. Suala hili ni muhimu sana
uwepo utaratibu madhubuti wa kukopeshwa.
UHARIBIFU WA MELI ZA MIFUGO
Vyombo hivyo humaga mafuta baharini na kusambaa kwa eneo kubwa, hali hiyo
husababisha viumbe wa bahari kukosa uhuru wa kuishi na hata kupoteza maisha.
MAHITAJI/MAPENDEKEZO
MAHITAJI/MAPENDEKEZO
- Sheria tarajiwa ionekane kuwatambua na kuwalinda wavuvi wadogo wadogo dhidi ya wawekezaji wakubwa.
- Utambuaji wa sheria, taratibu zizingatie maadili yanayomiliki shughuli za uvuvi na tafsiriwa ili zionekana kwa lugha ya kiswahili.
- Ombi Wizara/Idara itoe tamko kuhusu matumizi ya leseni ya uvuvi itambuliwe na itumike maeneo yote ya uvuvi.
- Makato ya asilimia tano ya mauzo ya mvuvi, samaki wake yalipwe baada ya mvuvi kutoa gharama zake zote zilizotumika wakati walipokwenda na kurudi mavuvini
- Msaada wa kielimu na kiufundi juu ya:-
pwani.
- Elimu ya hifadhi wa samaki tangu anakovuliwa mpaka kumfikia mlaji.
- Itolewe elimu ya usindikaji kw akutumia majiko ya moshi/joto.
- Vita dhidi ya uvuvi haramu uimarishwe tena kwa bidii zote.
- Mamlaka ya bandari ifanywe kutambua umuhimu wa wavuvi wadogo wadogo
kuwepo kwetu ufukweni kwa usalama wa vyombo vya mali za wavuvi.
- Wizara isaidie kusimamia miradi yote inayopitia idarani iweze kuwafikia wavuvi
wengi waliopo ukanda huu wa pwani ya bahari ya hindi kwani ndio tegemeo la
wavuvi wadogo wadogo katika kulinda na kupiga hatua ya uvuvi endelevu.
- Itolewe elimu ya usindikaji kw akutumia majiko ya moshi/joto.
- Vita dhidi ya uvuvi haramu uimarishwe tena kwa bidii zote.
- Mamlaka ya bandari ifanywe kutambua umuhimu wa wavuvi wadogo wadogo
kuwepo kwetu ufukweni kwa usalama wa vyombo vya mali za wavuvi.
- Wizara isaidie kusimamia miradi yote inayopitia idarani iweze kuwafikia wavuvi
wengi waliopo ukanda huu wa pwani ya bahari ya hindi kwani ndio tegemeo la
wavuvi wadogo wadogo katika kulinda na kupiga hatua ya uvuvi endelevu.
- Wakati TAFIRI ikiendelea na mtafiti wa mavuvi ya kamba iwaangalie zaidi wavuvi adogo wadogo kwa kuwatengea maeneo maalumu ya uvuvi kwa kuangalia hali zao za kimaisha na majukum waliyonayo. kwa kutegemea kazi zai ni uvuvi tu.
- Wizara/idara iweke mikakati ya kuwasaidia baadhi ya wavuvi wadogo wadogo kuinua uwezo ili hatimaye waweze kuchukua nafasi ya wawekezaji wakati wa wakubwa.
- Sisi wavuvi wadogo wadogo tunapongeza serikali pamoja na kitengo cha utafiti FASIRI kwa kazi nzuri zinazoifanya kujua hali halisi ya samaki wetu na namna gani wavuliwe samaki watakwisha na kutoweka kama yaliyowatokea wenzetu.
MWISHO
Wavuvi wadogo wadogo tuko pamohja na seikali kama tumejizatiti kuendeleza SERA YA
KILIMO KWANZA MAPINDUZI YA KIJANI pamoja na kauli mbiu ya MATOKEO
MAKUBWA SASA KILIMO NI BIASHARA endelevu ianzishwe benki ya wakulima na
wavuvi ndio suluhisho la kujikwamua.
Pamoja na kuvitazama kwa kina vikundi na vyama vya uvuvi vinavyotaka kuvuruga na
kukejeli mafanikio ya idara ya uvuvi katika kusimamia uvuvi endelevu.
NAWASILISHA
RAMADHANI H. MWIGAH
KATIBU MKUU - UWAWADA
MWAKILISHI WA WAVUVI - KANDA YA PWANI
O713 482119/0789482119
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni