Nav bar

Ijumaa, 21 Julai 2023

ULEGA AZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA RUTORO WILAYANI MULEBA MKOANI KAGERA KWA AJILI YA KUTATUA MGOGORO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Rutoro (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mawaziri Nane wa Kisekta iliyolenga kutatua mgogoro katika Kijiji hicho cha Rutoro Wilayani Muleba, Mkoani Kagera Julai 20, 2023.

Timu hiyo ya Mawaziri nane iliongozwa na Mwenyekiti, ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabula.
Mawaziri wengine walioshiriki katika ziara hiyo ni Naibu wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Antony Mavunde, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Khamis Hamza Chillo.







KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI AMEFANYA KIKAO NA UONGOZI WA GIZ NCHINI TANZANIA.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 19Julai,2023 jijini Dar es Salaam amekutana na Uongozi wa Shirika la Misaada la ujerumani (GIZ) na kufanya kikao na Uongozi wa GIZ Tanzania pamoja na  Uongozi wa Hifadhi za Bahari na maeneo Tengefu (MPRU), TAFICO pamoja na maafisa wengine wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.


Lengo la Kikao hicho ni kumjulisha Katibu Mkuu kuhusu mradi wa “Transboundary conservation and sustainable management of coastal and marine biodiversity" utakaofadhiliwa na Serikali ya ujerumani kupitia shirika lake la Misaada la (GIZ)  kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya.


 Aidha, Mradi huo wa “Transboundary conservation and sustainable management of coastal and marine biodiversity, utatekelezwa katika maeneo ya Kwale Tanga,Tanzania,pamoja na Kenya.


Vilevile, Mradi huo utakuwa na shughuli nyingi ikiwemo uhifadhi wa mazingira, uchumi na kuongeza uwezo na  maendeleo kwa jamii ya Kitanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (kulia) akimsikiliza kwa Makini Bw.Jens Bruggemann,Kiongozi kutoka shirika la Misaada la Ujerumani (GIZ)  katikati, akielezea namna mradi wa “Transboundary conservation and sustainable management of coastal and marine biodiversity utakavyofanya Kazi nchini Tanzania. Kushoto ni Dkt.Immaculate Sware, Meneja wa MPRU.

Picha ya Pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe na baadhi ya Maafisa walioshiki kikao hicho leo tarebe 19/07/2023 jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza Bw. Jens Bruggemann,Kiongozi wa Shirika la Misaada la uzjrumani GIZ (Hayupo pichani) akieleza maeneo ambayo mradi huo utatekelezwa.

KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI AFUNGUA KIKAO CHA KWANZA CHA "OCEAN INNOVATION HUB" JIJINI DAR ES SALAAM.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe Jana tarehe 18 Julai, 2023 alifungua kikao cha kwanza cha kuanzisha TANZANIA OCEAN INNOVATIO HUB chini ya Marine Park Reserve Unit (MPRU) kwa kushirikiana  na Early Carrier Ocean Professionals (ECOP).


Aidha, lengo la kikao hicho ni kuwafanya vijana wawe sehemu ya wanufaikaji wa fursa za bahari na watatuzi wakuu wa changamoto za matumizi ya bahari. 


Pamoja na mambo mengine, Mhe. Maryvonne Pool, Balozi wa Seychelles nchini Tanzania alishiriki kikamilifu katika kikao hicho cha kwanza pamoja na washiriki wengine 30.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe, akisalimia na Balozi wa Seyshelles  Mhe.Maryvonne Pool, mara baada ya kumaliza kikao cha kwanza cha kuanzisha Tanzania Ocean Innovation Hub kilichofanyika jana tarehe 18July 2023 Jijini Dar es Salaam.

Picha mbalimbali za Washiriki wa kikao cha kwanza cha Tanzania Ocean Innovation Hub Kilichofanyika Jana tarehe 18 July 2023 jijini Dar es Salaam. Lengo la kikao hicho ni kuwafanya Vijana wawe sehemu ya Wanufaikaji wa fursa za Bahari na watatuzi wakuu wa Changamoto za Matumizi ya Bahari.

Picha ya Pamoja ya Katibu Mkuu   Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (wa tatu kutoka kushoto) Wengine ni Dr.Immaculate Sware, Meneja wa MPRU, Balozi Maryvonne Pool, Dr. Leonard Valenzuela-Peres wa UN OCEAN Decade na Dkt. Kimirei, Mkurugenzi Mtendaji wa TAFIRI.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe (Wa Pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya washiriki wa  Semina ya Ocean Innovation Hub Tanzania jana tarehe 18July, 2023 Jijini Dar es salaam.

WADAU WA MAENDELEO WAUNGA MKONO BBT

Taasisi ya Kimataifa ya Heifer imeendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha vitendea kazi vijana wanaofanya shughuli za unenepeshaji wa mifugo katika kituo cha Mabuki kilichopo Wilayani Misungwi, Mkoani Mwanza Julai 18, 2023.


Akiongea na vijana katika hafla fupi ya kupokea vitendea kazi hivyo ikiwemo Lori moja na pikipiki Nne, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega aliwashukuru Wadau hao wa Heifer huku akisema kitendo hicho ni uungaji mkono jitihada za Mhe Rais Samia za kuwawezesha vijana na kina mama kujiajiri na kukuza kipato chao kupitia programu ya BBT Mifugo na Uvuvi.


Alisema kuwa Dkt. Samia anataka kuifanya programu hiyo ya BBT  kuwa ya kielelezo ambapo vijana wengi waweze kujikomboa kwa kujiajiri kupitia shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.


Aliongeza kwa kusema kuwa ni wakati sasa kwa vijana hao kuanza kufanya ubunifu wa kufanya biashara yao hiyo kidigitali kupitia mifumo ya biashara mtandao ili kupunguza kutegemea kuuza mifugo yao kupitia masoko ya kawaida.


Aidha, aliwataka vijana hao wanaopata mafunzo ya unenepeshaji wa mifugo katika kituo hicho cha mabuki kuwa mstari wa mbele katika kufanya mapinduzi ya uchumi kupitia ufugaji wa kisasa ili vijana wenzao wengine waweze kuona na kuamini kwamba inawezekana.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkaazi, Heifer International Tanzania,  Mark Tsoxo alisema wataendelea kufanya kazi na Serikali hasusan katika programu zinazohusu vijana ili kuunga mkono uwezeshaji wa vijana na kina mama kupitia programu ya BBT.


"Hivi sasa tuna  mpango wa kufikia vijana laki moja kupitia programu ya kopa ng'ombe lipa ng'ombe ambayo tunaamini itawezesha vijana wengi kujiajiri", alisema tsoso


Aliongeza kwa kusema kuwa wametoa vitendea kazi hivyo kufuatia ombi la Waziri Ulega ambapo aliwaomba kuona namna ya kuunga mkono programu hiyo ya kielelezo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.



PROF. SHEMDOE AONGOZA KIKAO KAZI CHA KUPITIA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2022/2023

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelekezo wakati Kikao kazi cha kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (15.07.2023)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi (wa pili kutoka kushoto) akizungumza wakati Kikao kazi cha kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (15.07.2023)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Bi. Agnes Meena (wa kwanza kulia) akizungumza wakati Kikao kazi cha kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (15.07.2023)


Wakuu wa Idara na Vitengo wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Manaibu Makatibu Wakuu wakifuatilia wasilisho la utekelezaji wa bajeti lililowasilishwa na Bi. Danietta Tindamanyire. Kikao kimefanyika mkoani Morogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (15.07.2023)

PROF. SHEMDOE AFUNGUA KIKAO KAZI CHA KUPITIA RASIMU YA ANDIKO LA MRADI WA UWEKEZAJI ENDELEVU KATIKA SEKTA YA MIFUGO

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe akichangia mada baada ya wasilisho kutoka kwa wawakilishi kutoka Benki ya Dunia wakati wa Kikao kazi cha kupitia rasimu ya andiko la mradi wa uwekezaji endelevu katika Sekta ya Mifugo nchini Tanzania kutoka Benki ya Dunia kinachofanyika mkoani Mrorogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (14-15.07.2023)


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi, akiuliza swali wakati wa Kikao kazi cha kupitia rasimu ya andiko la mradi wa uwekezaji endelevu katika Sekta ya Mifugo nchini Tanzania kutoka Benki ya Dunia kinachofanyika mkoani Mrorogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (14-15.07.2023)


Afisa Mwandamizi wa Uchumi wa Kilimo kutoka Benki ya Dunia, Bi. Emma Isinika akiwasilisha mada wakati wa Kikao kazi cha kupitia rasimu ya andiko la mradi wa uwekezaji endelevu katika sekta ya mifugo nchini Tanzania kutoka Benki ya Dunia kinachofanyika mkoani Mrorogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (14-15.07.2023)


Mshauri Mwelekezi wa Benki ya Dunia Tanzania kwenye masuala ya Kilimo na Chakula, Bi. Mary Shettu akifafanua jambo wakati wa Kikao kazi cha kupitia rasimu ya andiko la mradi wa uwekezaji endelevu katika Sekta ya Mifugo nchini Tanzania kutoka Benki ya Dunia kinachofanyika mkoani Mrorogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (14-15.07.2023)

Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Sekta ya Mifugo wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa Kikao kazi cha kupitia rasimu ya andiko la mradi wa uwekezaji endelevu katika Sekta ya Mifugo nchini Tanzania kutoka Benki ya Dunia kinachofanyika mkoani Mrorogoro kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morena. (14-15.07.2023)




MAUZO YA NYAMA YAONGEZEKA NJE YA NCHI - ULEGA

 Serikali imesema, kiwango cha usafirishaji nyama hapa nchini kimeongezeka hadi kufikia tani 12,243.79 zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 51.894 ziliuzwa nje ya nchi 2022/23 ikilinganishwa na tani 1,774.20 zilizouzwa nje ya nchi 2020/21 .

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega julai 14,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023) ambao unatarajiwa kufanyika Septemba 5-9 mwaka huu jijini Dar es Salaam huku Rais Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Kwa mujibu wa Ulega ongezeko hilo ni moja ya jitihada zinazofanywa na Rais Samia na wizara yake inaziunga mkono kwa vitendo kupitia Programu ya BBT-LIFE ambapo katika awamu ya kwanza takribani vijana 738 wakiwemo vijana 238 kutoka sekta ya mifugo na vijana 500 kutoka sekta ya uvuvi wamenufaika na mafunzo ya unenepeshaji wa mifugo ,majongoo Bahari na ufugaji wa Samaki kibiashara.

“Tumejipanga kuongeza uzalishaji Kufuatia jitihada za Rais Samia,tumejipanga kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na kuuza ziada ya mazao ya mifugo na uvuvi katika nchi nyingine “amesema Ulega na kuongeza kuwa

“Ujio wa mkutano huo kwa Tanzania ni fursa adhimu ya wadau wetu kukutana na wafanyabiashara mashuhuri na wawekezaji kutoka katika nchi mbalimbali ulimwenguni ,hivyo itasaidia kufungua milango ya uwekezaji na kuongeza mashirikiano ya kibiashara kwa wadau wetu .”

Kwa mujibu wa Ulega mkutano huo pia utatoa fursa za kuona ubunifu na teknolojia mbalimbali ambazo zinazweza kuongeza tia ya uzalishaji wa mazao ya mifugo na uvuvi.

Aidha amesema mkutano huo unatoa fursa kwa wafanyabiashara kufanya maonyesho katika eneo la mkutano kwa lengo la kuonesha shughuli zinazofanyika katika minyororo ya mifumo ya chakula nchini lakini pia kutangaza biashara za wadau ili kupata mitaji na masoko ,hivyo ushiriki wa wadau ni muhimu ili waweze kunufaika na fursa hizo.



Alhamisi, 20 Julai 2023

​PINDA AWATAKA WADAU WA MIFUGO NA UVUVI KUCHANGAMKIA FURSA

Na. Edward Kondela


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amewataka wadau wa sekta za mifugo na uvuvi nchini kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta hizo ili kujikwamua kiuchumi.


Mhe. Pinda amezungumza hayo (12.07.2023) jijini Dodoma wakati wa mkutano wa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kuelekea mkutano mkuu wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) utakaofanyika hapa nchini kuanzia Septemba 4 hadi 8 mwaka huu.


Amesema sekta hizo zimekuwa zikitoa mchango mkubwa katika familia ikihusisha akina mama na vijana na kwamba zikitumika vizuri zinaweza kubadilisha kwa kiasi kikubwa maisha katika ngazi ya familia na kuwataka wadau wa sekta hizo kuangalia fursa zitakazotokana na mkutano huo utakaofanyika Mwezi Septemba ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa mwenyeji wa mkutano huo.


Ameongeza kuwa amefurahishwa na programu maalum ya vituo atamizi ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi inawajengea uwezo vijana katika kuwapatia mafunzo ya ufugaji bora na mitaji ili kuweza kujitegemea katika tasnia ya ufugaji.


Kwa upande wake mgeni rasmi katika mkutano huo Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) ambaye amehamasisha wadau kuendelea kujisajili kwa njia ya mfumo wa kieletroniki ili kushiriki katika mkutano wa AGRF amesema mkutano huo ni fursa kwa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi hapa nchini kubadilishana uzoefu na kufanya biashara pamoja na wadau wa sekta hizo kutoka nchi zingine za Afrika.


Mhe. Ulega amesema mkutano wa leo uliohusisha wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kutoka maeneo mbalimbali nchini unatakiwa kuwa na matokeo chanya kwa kuhakikisha muda uliotumika unakuwa na faida katika mkutano mkuu wa AGRF 2023 ili kukuza sekta hizo kwa kuongeza masoko hususan ya kuuza bidhaa nje ya nchi.


Ameongeza kuwa sekta za mifugo na uvuvi zimekuwa zikiendelea kuchangia katika pato la taifa hivyo jitihada zaidi zinahitajika ili mchango wa sekta hizo uwe imara zaidi na watu wengi kuingia katika sekta za mifugo na uvuvi.


Amesema mkutano wa AGRF 2023 utaleta muonekano tofauti wa namna ya kufanya biashara ya mifugo na uvuvi kwa njia bora zaidi na yenye tija ili kuleta tija na kwamba wafugaji wa Tanzania watakuwa na mengi ya kubadilishana na wenzano kutoka nchi zingine za Afrika.


Naye Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akizungumza kwenye mkutano huo amesema wadau wa sekta ya mifugo na uvuvi watapata fursa ya kujisajili katika mfumo maalum na kujipatia elimu ya kutumia fursa zitakazojitokeza katika mkutano wa AGRF 2023.


Prof. Shemdoe amesema mkutano huo unatoa fursa kwa wadau kupata elimu  katika kupata fursa za namna wanavyoweza kujikita zaidi na kupata manufaa ya mkutano wa Mwezi Septemba mwaka huu.


Wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kutoka maeneo mbalimbali nchini wamehudhuria mkutano uliowakutanisha wadao hao ili kujiandaa na mkutano mkuu ambapo takriban wageni elfu tatu wanatarajiwa kushiriki mkutano huo kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amewataka wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta hizo kuelekea mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) utakaofanyika Mwezi Septemba mwaka huu. Mhe. Pinda amebainisha hayo jijini Dodoma kwenye mkutano wa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi ikiwa ni maandalizi ya mkutano mkuu wa AGRF. (12.07.2023)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi uliofanyika jijini Dodoma, kuelekea mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) utakaofanyika hapa nchini Mwezi Septemba mwaka huu ambapo amesema mkutano wa leo uliohusisha wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kutoka maeneo mbalimbali nchini unatakiwa kuwa na matokeo chanya kwa kuhakikisha muda uliotumika unakuwa na faida katika mkutano mkuu wa AGRF 2023 ili kukuza sekta hizo kwa kuongeza masoko hususan ya kuuza bidhaa nje ya nchi. (12.07.2023)

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na wadau wa sekta za mifugo na uvuvi jijini Dodoma kutoka maeneo mbalimbali nchini juu ya umuhimu wa kujisajili ili kushiriki katika mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF), ambao utafanyika hapa nchini Mwezi Septemba mwaka huu na kuhudhuriwa na wageni takriban Elfu Tatu kutoka nchi mbalimbali. (12.07.2023)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (watano kutoka kushoto), akijisajili kwa njia ya kieletroniki kwenye mfumo maalum kwa ajili ya kushiriki mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) utakaofanyika Tarehe 4 hadi 8 Mwezi Septemba 2023 hapa nchini, wakati wa mkutano wa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi uliofanyika jijini Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo. (12.07.2023)

Picha za baadhi ya washiriki kwenye mkutano wa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi katika mkutano wa maandalizi ya kushiriki mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) utakaofanyika hapa nchini Mwezi Septemba mwaka huu. Mkutano huu wa maandalizi umefanyika jijini Dodoma. (12.07.2023)



SERIKALI YAWEKA NGUVU KATIKA UTAFITI WA RASILIMALI ZA BAHARI NCHINI ILI KUWA NA UVUVI ENDELEVU

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Serikali ya Norway imepokea meli ya utafiti ya Dr. Fridtjof Nansen ambayo inafanya utafiti wa ikolojia ya Bahari na rasilimali za uvuvi zinazopatikana katika Bahari ya Hindi na kusaidia kuimarisha usimamizi wa Rasilimali za Bahari.


Akiongea, katika hafla ya kuipokea rasmi meli hiyo katika Bandari ya Dar es salaam leo 11 Julai 2023, Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Suleiman Makame, amesema utafiti huo unafanyika Tanzania Bara na visiwani (zanzibar) na utatoa taswira ya aina za samaki wanaopatikana  baharini kwa ajili ya kuweka mipango madhubuti ya usimamizi. Utafiti huo, umeanza kufanyika 28 Juni 2023 na utakamilika 28 Julai 2023. 


"Tumekuwa tukifanya uvuvi bila kujua ni aina gani ya samaki na viumbe wengine wa Bahari tulionao, kwa hiyo tutakapokuwa na takwimu sahihi za rasilimali za samaki waliomo baharini tutaweka mkakati wa kudhibiti mazao ya baharini hasa aina za samaki ambao wamekaribia kutoweka." amesema Makame.


Mhe. Makame amesema ni mara ya tatu utafiti kama huu unafanyika katika eneo la bahari nchini Tanzania, kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 1982, mara ya pili ukafanyika mwaka 2018 na sasa unafanywa mara ya tatu na meli ya Dr Fridtjof Nansen.


Amesema baada ya kukamilika kwa utafiti huo Julai 25 mwaka huu Serikali itafahamu aina za samaki waliomo Baharini na tumeambiwa kuna aina mpya za samaki ambao hawajawahi kuonekana lakini kupitia utafiti huu, aina hizo zitawekwa katika rekodi ya dunia.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimerei amesema utafiti unaofanyika ni muhimu katika kupata uhalisia wa kiasi cha samaki waliopo katika maji Baharini. 


"Hadi sasa kiasi cha samaki kinachokadiliwa kuwemo katika maji ya ni tani 100,000 utafiti huu ulifanyika 1982, takwimu za 2018 hazitumiki kwasababu hazikuwa sawa,


 "Tunaamini utafiti unaokwenda kufanyika sasa utatoa majibu sahihi na tutayasilisha Wizarani kwa ajili ya matumizi ya Wizara ikiwemo utungaji wa  Sera ,"amesema Kimerei.


Dkt. Kimerei amesema katika meli hiyo wapo watafiti 25 wakiwamo 13 kutoka Tanzania.


Kwa upande wake Mwakilishi mkazi wa Shirika la FAO Tanzania Dkt. Nyabenyi Tito Tipo amesema, wanatambua umuhimu wa kusaidia ukuaji wa sekta ya uvuvi Tanzania hivyo wataendelea kuishika mkono Serikali na kushirikiana na wadau wengine kuendeleza rasilimali za bahari.


Amesema takwimu zitakazopatikana kwenye utafiti huo zitakuwa hazina ya Tanzania. Meli hiyo ya utafiti imejumuisha watafiti kutoka Kenya, Msumbiji Afrika kusini, Australia na Norway


Tanzania inakusudia kuwa na takwimu za rasilimali zilizopo baharini pamoja na kuweka mkakati wa uvuvi kwa lengo la kudhibiti shughuli za uvuvi na ulinzi wa rasilimali za samaki walio hatarini  kutoweka vilivyo hatarini kutoweka. hii ni baada ya kuruhusu Serikali ya Norway pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Chakula(FAO) kuanza utafiti wa rasilimali zilizopo baharini kwa Tanzania bara na visiwani

Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Mhe. Suleiman Makame akihutubia kwenye hafla ya kupokea meli iliyokuja kwa ajili ya kufanyia Utafiti wa aina mbalimbali ya viumbe wanaopatikana Bahari ya Hindi  ya (Dr. Fridtjof Nansen) katika bandari ya Dar es salaama leo 11 Jully 2023.

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,  Mhe. Suleiman Makame akimsikiliza Captain Tommy Steffensen anayeisimamia meli ya Utafiti ya DR. FRIDTJOF NANSEN, akimuelezea na kumuonyesha sehemu ambayo Captain wa meli anafanya shughuli ya kuiendesha meli hiyo.kwa kutumia vifaa vya kiteknolojia ya kisasa, wakati wa hafla ya kuipokea Meli hiyo iliyofanyika katika Bandari ya Dar es salaam (Port Call Event), 11 Julai 2023.

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Suleiman Makame (watatu kulia) akimsikiliza mhudumu wa kwenye meli ya DR. FRIDTJOF NANSEN ambaye yupo kwenye eneo la Maabara ya samaki (Fish Lab) akimuelezea na kumuonyesha aina mbalimbali za samaki ambazo wanafanyia utafiti kwenye meli hiyo iliyofika nchini kwa ajili ya kufanya utafiti wa Viumbe wa baharini, wakati wa hafla ya kuipokea meli ya utafiti katika Bandari ya Dar es salaam, 11 Julai 2023.

Muonekano wa meli kubwa ya kimataifa ya Dr. Fridtjof Nansen kwa ajili ya kufanya  Utafiti ambao utasaidia Usimamizi wa Rasilimali za Bahari Nchini, imeanza utafiti tarehe 28 Juni 2023 na inatarajia kumaliza Utafiti huo 28 Julai 2023.

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,  Mhe. Suleiman Makame (waliokaa, katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa Idara, wakuu wa Taasisi na Wenyeviti kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya Uvuvi,  mara baada ya hafla ya kupokea meli ya Utafiti katika Bandari ya Dar es salaam,  leo tarehe 11 Julai 2023.

TAASISI ZATAKIWA KUTUMIA VYEMA MAPATO YA NDANI

Na. Edward Kondela


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi ametoa rai kwa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kujijengea uwezo wa kujipatia vyombo vya kazi ili wafanye kazi kwa ufasaha.


Dkt. Mushi amebainisha hayo (10.07.2023) wakati alipokuwa akizindua gari aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 GD STD Manual iliyonunuliwa na Bodi ya Nyama nchini (TMB) kwa thamani ya Shilingi Milioni 99.9.


Akizungumza katika ofisi za bodi hiyo jijini Dodoma amesema ni vyema taasisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa na matumizi mazuri ya fedha kwa kununua vifaa mbalimbali vya kutendea kazi badala ya kufanya matumizi ya fedha yasiyo na tija.


Kwa upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Bw. John Chassama amesema gari hilo wamenunua kwa mapato ya ndani ambapo wamepanga kulipeleka Kanda ya Arusha na kwamba mipango ni kuhakikisha kila kanda inakuwa na gari ili kuboresha utendaji kazi.


Bw. Chassama amesema pamoja na ununuzi wa magari mpango wa bodi ni kuimarisha ofisi za kanda kwa kununua vifaa vingine zikiwemo kompyuta ili kusogeza karibu huduma kwa wadau kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi akizindua gari aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 STD Manual mali ya Bodi ya Nyama nchini (TMB) iliyonunuliwa kwa thamani ya Shilingi Milioni 99.9.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi akiwasha gari ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa gari hilo aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 GD STD Manual mali ya Bodi ya Nyama nchini (TMB) na kuzitaka taasisi zilizo chini ya wizara kuwa na matumizi mazuri ya mapato yao. (10.07.2023)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi akiwasha gari ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa gari hilo aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 GD STD Manual mali ya Bodi ya Nyama nchini (TMB) na kuzitaka taasisi zilizo chini ya wizara kuwa na matumizi mazuri ya mapato yao. (10.07.2023)



MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MAONYESHO YA 47 YA KIMATAIFA YA BIASHARA SABASABA

 

Afisa Utafiti wa Mifugo Mkuu kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt.  Scholastica Doto (kushoto) akielezea kazi zinazofanywa na Wakala  kwa Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gu"lw"ogui (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kitaifa ya biashara sabasaba jijini Dar es salaam Julai 13,2023


Afisa Masoko kutoka kampuni ya SEAWEED, Bi. Sophia Mang'ena (kulia) akionyesha bidhaa walizonazo kwa   Balozi wa Uturuki Nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gu"lw"ogui bidhaa walizonazo ikiwa ni pamoja na pilipili zinazopatikana kwenye kampuni hiyo alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara sabasaba jijini Dar es salaam Julai 13,2023

Mkurugenzi wa Kampuni ya NASHA Aquar Fish Bw. Masumbuko Nzingula (kulia) akieleza fursa za uwekezaji kwenye mnyororo wa thamani wa ufugaji samaki kwa Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoka Keshi la kujenga Taifa (JKT) Makao makuu Dodoma, Kanali Peter Lushika (kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 12,2023

Mkufunzi kutoka Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Bi. Aziza Shekalaghe (kulia) akieleza matumizi ya josho linaloamishika  kwa ajili ya kuongeshea mifugo midogo kama vile mbwa, mbuzi, kondoo, na nguruwe kwa Mkurugenzi wa Idara ya  Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutoka Jeshi la kujenga Taifa (JKT) makao makuu Dodoma,  Kanali Peter Lushika (wa pili kutoka kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 12,2023


Afisa Uvuvi Mwandamizi kutoka Idara ya Uvuvi (DFs) Bi. Neema Respickius (kushoto) akitoa elimu kwa njia  ya machapisho kwa  Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi - Zanzibar Mhe. Suleiman Makame (kulia) wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 11,2023


Sehemu ya wadau wakiangalia kuku kwenye banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati walipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 11, 2023

Afisa Mtafiti Mifugo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Bw. Jovith Kajuna (wa pili kushoto) akitoa elimu ya malisho ya mifugo zikiwemo aina mbalimbali za mikunde pamoja na nyasi  kwa  Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi -Zanzibar Mhe. Suleiman  Makame ( katikati) aliomtembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 11,2023

Afisa Mtafiti Mifugo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Bw. Jovith Kajuna (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya kina kuhusu ufanisi wa mizizi ya nyasi aina Cenchrus ciliaris kwa  Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi -Zanzibar Mhe. Suleiman  Makame  (katikati) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 11,2023

Afisa Mifugo Msaidizi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Reuben Ngailo (kulia) akitoa elimu ya namna ya ulishaji bora wa ng'ombe wa maziwa kwa mdau Bw. Husein Khatibu alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 11,2023.

Mtakwimu Msaidizi kutoka  Mamlaka ya kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) Bw. Venance Nyanda (kulia) akitoa maelezo ya namna wanavyofanya kazi zao kwa Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi - Zanzibar Mhe. Suleiman  Makame (kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya Kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 11,2023.

Afisa Masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) Bw. Hamisi Kihimbi, (kulia) akitoa elimu ya namna ya kupima na kutunza maziwa kwa mdau Bi. Agatha Mmary  wakati alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonesho ya 47 ya  Kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 11,2023

Mdau wa Sekta ya Mifugo, Bw. Paluku Emmanuel (kushoto) akitoa elimu juu ya umuhimu wa  lishe ya Mifugo  kwa Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi - Zanzibar Mhe. Suleiman Makame (katikati) aliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya Kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 11, 2023.

Mtunza Kumbukumbu kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi  (FETA) - Mbegani,  Bi. Lucy Kimea (kulia) akitoa elimu ya namna ya kuzalisha vifaranga vya samaki, ulimaji wa zao la mwani na matumizi ya mwani kwa wadau waliomtembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 11,2023.


Mtaalam kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Bwana Shukuru Guo akitoa elimu kwa mdau wa Mifugo raia wa kigeni alietembelea banda la TVLA kuhusiana na matumizi sahihi ya chanjo za Mifugo zinazozalishwa na Wakala siku ya tarehe 10/07/2023 kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam.


Mtaalam kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Dkt. Jelly Chang'a akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo waliotembelea banda la TVLA kuhusiana na matumizi sahihi ya chanjo za Mifugo zinazozalishwa na Wakala siku ya tarehe 10/07/2023 kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam.


Nahodha kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Bw. Halifa Snapenda  akitoa elimu kwa wadau ya namna ya kufuga samaki kwa njia ya kizimba wakati wa maoneshoya 47  ya Kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 10, 2023


Meneja kutoka Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania  (LITA) Temeke,  Bi. Benadetha Kessy (kushoto)  akitoa elimu ya namna ya kutumia josho kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 10,2023


Fundi Sanifu Mwandamizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Bw. Hiari Chona (kushoto) akitoa elimu kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi juu  ya samaki aliyepotea miaka 65 milioni iliyopita na sasa ameanza kuonekana kwenye Pwani ya bahari ya Hindi mwaka 2003 kwenye maeneo ya Songosongo wakati wa  maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 10,2023.


Mdau wa sekta ya Mifugo Bw. Emmanuel Paluku (kulia) akitoa elimu juu ya umuhimu wa  lishe ya Mifugo  kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 10,2023.


Mdau wa sekta ya Mifugo Bw. Emmanuel Paluku (kulia) akitoa elimu juu ya umuhimu wa  lishe ya Mifugo  kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 10,2023.


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Agape ya mkoani Dar es Salaam waliotembelea banda la TDB wakipata maelezo juu ya matumizi ya mashine ya kukamulia maziwa toka kwa Mtaalamu wa mifugo wa kampuni ya Bajuta kwenye maonesho ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. JK Nyerere jijini Dar es Salaam (10.07.2023)


Mtaalamu wa mifugo toka Kampuni ya Bajuta inayojishughulisha na pembejeo za mifugo Bw. Sifaeli Dalei (kulia) akitoa maelezo ya namna ya matumizi ya mashine ya kukamulia ng'ombe wa maziwa kwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu waliotembelea banda la TDB kwa lengo la kujifunza kwenye maonesho ya Kimataifa ya biashara Sabasaba jijini Dar Es Salaam.(10.07.2023)


Afisa Utafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Bw. Hakimu Matola (kushoto) akitoa elimu ya namna ya kukausha samaki aina ya jodari na dagaa kwa kutumia mwanga wa jua kwa mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 09,2023

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka  Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Bw. Mgalula Lyoba (katikati) akitoa maelezo kuhusu samaki aina ya jodari kwa  wadau waliotembelea banda lao wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara sabasaba yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 09,2023


Mdau uvuvi upande wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu(MPRU) na Afisa mauzo kutoka kampuni ya Nyota Venture  Bw. Yahya Makuhana akitoa elimu ya matumizi ya nyavu za uvuvi kwa upande na ziwani na baharini  kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 09,2023


Afisa Utafiti Mifugo kutoka Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani , Bi Grace Masolwa akitoa elimu ya  ufugaji bora kupia machaposho  wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 09, 2023


Mkufunzi kutoka Wakala wa Elimu na mafunzo ya Uvuvi (FETA) Bw.  Mashaka Shabani (kulia) akitoa elimu ya ufugaji wa samaki kwa mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 09,2023.


Afisa Uhusiano kutoka Kampuni ya Ranchi za Taifa Tanzania  (NARCO) Bw. Jumanne Mutalemwa, (kushoto)akitoa elimu ya utaratibu wa upatikanaji wa vitalu, na manufaa ya uwepo wa NARCO Tanzania kwa wadau Bw. Hamis  Makunga alipotembelea  banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya Kimataifa ya biashara  yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam,  Julai 09,2023


Mkufunzi kutoka Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) Bw. Semu Geoffrey (kushoto) akitoa elimu juu ya namna ya kukuza vifaranga vya kuku kwa kutumia kinengunengu au brodder kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 09,2023


Kaimu Meneja masoko kutoka Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw. Nicholai  Chiweka akitoa elimu ya  umuhimu wa usajili wa wadau katika tasnia ya nyama nchini, nyama bora na salama, na  mambo muhimu ya kuzingatia pale mdau anapotaka kuanzisha biashara ya nyama kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya utamaduni, sanaa na michezo Bi. Emma  Lyimo  alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 09,2023


Afisa Mtafiti Mifugo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Bw. Jovith Kajuna (kulia) akitoa elimu ya umuhimu wa jiwe lishe ikiwa ni pamoja na kumsaidia ng'ombe kutoa maziwa mengi, ng'ombe kukua vizuri na kuwezesha upatikanaji bora wa nyama kwa wadau waliomtembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 09,2023


Mwanafunzi kutoka Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Bw. Habibu Ramadhani akitoa elimu juu  ya kilimo cha mwani pamoja na utengenazaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na mwani kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 09,2023


Mtaalam kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Bw. Henry chuma, akitoa elimu ya namna ya kuhakiki ubora wa vyakula vya mifugo kwa  mdau aliyetembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea kufanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam Julai 09, 2023.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba (kushoto) akisaini kitabu cha wageni siku ya tarehe 08/07/2023 alipotembelea banda la Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) lililopo Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam. Waliosimama kulia ni wataalamu kutoka TVLA Dkt. Scholastica Doto pamoja na Bwana Henri Mlundachuma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba (kulia) akipata Maelezo kuhusiana na matumizi sahihi ya chanjo ya Homa ya Mapafu ya Mbuzi (CAPRIVAC-CCPP) kutoka kwa Dkt. Richard Mwakapuja mtaalamu kutoka Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA siku ya tarehe 08/07/2023 alipotembelea banda la TVLA lililopo Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba (kulia) akitoa elimu kwa wadau wa mifugo kuhusiana na virutubisho asilia vyenye sifa ya kuongeza uzalishaji, ustahimilivu, kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na kupunguza matumizi ya madawa ya mifugo  kwa ajili ya kuongeza ukuaji na kiasi cha uzalishaji wa Mifugo na mazao ya Mifugo kama mayai, nyama na maziwa siku ya tarehe 08/07/2023 katika banda la TALIRI lililopo katika eneo la mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam.

Mtaalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) bwana Jovith Kajuna akitoa elimu kwa wadau wa Mifugo kuhusiana na malisho ya Mifugo (nyasi) yenye virutubisho kwa Mifugo na zinazofaa kupandwa kwenye maeneo yao kwa ajili ya ustawi wa Mifugo siku ya tarehe 08/07/2023 banda la TALIRI lililopo Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba Dar es Salaam.

Mtalam kutoka LITA bi Aziza Shekalage atoa elimu kwa mfungaji wa kuku namna ya bora ya kufunga vifanga kwa kutumia njia ya kinengunengu