Nav bar

Jumamosi, 25 Oktoba 2014

SHAMBA LA KUTOTOLESHA VIFARANGA VYA SAMAKI NA WATENGENEZAJI WA CHAKULA CHA SAMAKI EDEN AGRI-AQUA LTD PUGU KINYAMWEZI DAR-ES-SALAAM TANZANIA


Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani mara baada ya kuwasili katika shamba la Eden Agri-Aqua LTD na kupokelewa na mwenyeji wake Bw William Bwemelo katika eneo la Pugu Kinyamwezi nje kidogo ya Jiji la Dar-es-salaam
Waziri Kmani akaribishwa katika Ukumbi wa Mkutano wa shamba la Eden Agri-Aqua LTD
Katibu wa Waziri Bw Eliukana  Mwakipesile, akifatilia jambo wakati wa maelezo ya Mmiliki wa shamba la Eden kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani hayupo pichani


 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani akiangalia utotoleshaji wa vifaranga vya samaki aina ya perege kwenye shamba la Eden Agri-Aqua LTD lililopo nje kidogo mwa Jiji la Dar-es-salam Pugu KinyamweziMmiliki wa shamba la Eden Bw William Bwemelo akimuonyesha Waziri Kamani Mtungo wa hewa ya Oxygen inayotumika kuweka kwenye vyombo vya kusafirishia vifaranga vya samaki wateja wanaponunua
Meneja wa shamba la uzalishaji vifaranga akitoa maelezo kwa Mhe Waziri Kamani
Hali ya hewa imebadilika ghafla mvua imeanza kunyeshaMeneja wa shamba aliendelea kutoa maelezo ya uzalishaji na utunzaji wa vifaranga vya samaki kwa Mhe. Waziri Kamani


Mhe Dkt Titus Kamani Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi alishuhudia mabwawa ya aina mbalimbali ya kulelea samaki wazazi , wakuuzwa kwa ajili ya chakula , wadogo na vifaranga vinavyouzwa kwa wateja wanaohitaji hapa Tanzania
Mhe Waziri alipata nafasi ya kuwapa samaki chakula na kuona jinsi chakula kinachokubalika kinachoelea kinavyoweza kuliwa na samaki hao
Mhe Waziri alipata nafasi ya kuwapa samaki chakula na kuona jinsi chakula kinachokubalika kinachoelea kinavyoweza kuliwa na samaki hao


Eneo linalotumika kukuzia vifaranga vya samaki mara wanapotoka kwenye mashine za kutotolesha

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani akielekea kwenye Jengo linalotumika kwa uzalishaji wa chakula cha samaki ambapo mashine mbalimbali za kuandaa chakula hicho zimefungwa
Hiki ndio chakula cha samaki kilichohakikiwa na wataalam wa samaki, mchanganyiko wake ni bara kwa makuzi ya samaki au viumbe kwenye maji
Meneja uzalishaji wa vyakula vya samaki akitoa maelezo kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugio na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani juu ya utengenezaji wa vyakula hivyo
Waziri Kamani aliuliza maswala kadhaa ya kutaka uhakika wa ubora wa chakula hicho kuanzia mwanzo hadi mwisho

Mhe Dkt Titus Kamani, akikagua chakula malighafi zinazotengeneza mchanganyiko wa chakula cha samaki pembeni ni Mmiliki wa Eden Agri-Aqua akimtazama malighafi hiyo

Bw William Bwemelo akitoa maelezo kwa Waziri Kamani

Mhe Dkt Kamani akiangalia moja ya mashine zinazo tengeneza aina ya chakula cha samaki chenye uwezo wa kuelea juu ya maji, ambacho ndicho kinachopendekezwa na wataalam wa Ufugaji Viumbe kwenye Maji
Mhe Wziri akiangalia kifungashio cha chakula hicho cha samaki
Bi Eva Sessoa kutoka TBC-1 akichukua picha za luninga tayari kwa kuwasilisha Habari juu ya ziara ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani katika shamba la Eden Agri- Aqua LTD
Mhe Waziri Kamani akishika chakula hicho kilicho katika mfumo wa pellets
Mkononi mwa Waziri ameshika chakula cha samaki na anaangalia ubora wake kwa karibu zaidi

Chakula cha samaki kilichotengenezwa kwa mfumo wa pelets kikiwa kimeanikwa kwenye mikeka maalum ili kikauke vizuri

Ijumaa, 24 Oktoba 2014

WAZIRI KAMANI ATEMBELEA SHAMBA LA SAMAKI WA MAPAMBO UKONGA CICHILD FARM WALIO NA SOKO ZURI NJE YA NCHI


Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi  Mhe. Dkt Titus Kamani alipotembelea shamba la samaki wa mapambo aina ya Cichild Farm Ukonga, samaki  wanaopatikana ziwa Tanganyika wenye upekee duniani
Waziri Kamani akionyesha samaki wa aina mbalimbali ambao alipata maelezo yake jinsi ya kuwapata, kuwahifadhi kuwasafirisha na kukaa kwa muda Cichld Farm  Ukonga kabla ya kusafirishwa nje ya nchi

Waziri Kamani akijaribu kumkamata mmoja wa samaki hao na kumuangalia kwa karibu, pembeni mwa Waziri mwenye kofia ni Meneja anayehudumia shammba hilo Bw Yusuf Mohammed
Kifaa aina ya Scoop kinaachotumika kumchota samaki bila kupata madhara
Muangalizi wa shamaba na mtaalam wa kusafirisha samaki kutoka Kigoma mpaka Dar-es-salaam


Mkurugenzi wa shamba la Ukonga Cichld Farm Bibi Sophia Mruma  akimuelezea Mhe Kamani Changamoto na nembo za kusafirisha samaki hao nje ya nchi wengi hupelekwa Marekani
Mhe Waziri Kamani akisisitiza umuhimu wa shamba hilo kuweka nembo, kuwa samaki hao wanatoka Tanzania 
 
Mpiga picha wa TBC - 1 Bi Eva Sessoa ,Mwandishi na Mpiga picha alikuwa mmoja wapo waliotembelea shamba hilo kw aajili ya kuhabarisha Umma mwenye video camera
Mkurugenzi wa shamba la Ukonga Cichild Farm akimshukuru Mhe Kamani kwa kutembelea shama lake


Mhe Waziri Kamani akijibu baadhi ya Changamoto zinazokabili shamba hilo na kuwaelekeza kushirikiana na Wizara kupitia Idara ya Ukuzaji  Viumbe kwenye Maji, ili kutatua changamoto hizo
Mkurugenzi wa Shamba la Ukonga Cichild Farm Bibi Sophia Mruma

Mtaalam wa kudaivu Bw David akielezea changa moto za kudaivu mita 30 chini kutafuta samaki wa mapambo
Mkurugenzi wa shamba la Ukonga Cichild Farm akiagana na Mhe. Waziri Kamani