JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
RUZUKU KWA WAVUVI
TAARIFA KWA UMMA
|
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi imetenga kiasi cha fedha katika mwaka 2013/2014 kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa jamii za wavuvi. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
anawatangazia wananchi kuwa, Serikali itatoa ruzuku kwa vyama vya
ushirika wa wavuvi, vikundi vya wavuvi na Vikundi vya Usimamizi Shirikishi wa
Rasilimali za Uvuvi (BMUs) vilivyosajiliwa kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014.
Vigezo na masharti yatakayotumika kutoa ruzuku ni kama
ifuatavyo:-
1. Ruzuku
itatolewa kwa vyama vya ushirika vya wavuvi, vikundi vya wavuvi na Vikundi vya
Usimamizi Shirikishi wa Raslimali za
Uvuvi vilivyosajiliwa kisheria, na vyenye
kuzingatia jinsia;
2. Kikundi
kiwe kinafanya kazi za uvuvi kufuatana
na Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na Kanuni za Uvuvi
za mwaka 2009 na kuzingatia miongozo mbalimbali;
3. Kikundi
kiwe na Akaunti ya Benki;
4. Mradi
wowote wa uvuvi utakaowasilishwa na kikundi
lazima ukidhi matakwa ya Sheria ya
Uvuvi
Na. 22 ya mwaka 2003 na Kanuni za Uvuvi za
mwaka 2009 na sheria nyingine
za nchi ikiwemo ya Mazingira ya mwaka 2004;
5. Miradi
itakaofadhiliwa ni pamoja na ununuzi wa boti za uvuvi, injini za kupachika,
nyavu za dagaa na nyavu za samaki wakubwa ndoana (long line);
6. Kikundi
kithibitishe kuwa kina uwezo na kipo tayari kuchangia asilimia arobaini (40%) ya gharama
ya mradi unaoombwa. Serikali itachangia asilimia sitini (60%) ya gharama za zitakazonunuliwa;
7. Maombi
yapitishwe kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa husika kwa ajili ya
kupitia maombi hayo na kuona kama yanakidhi vigezo vilivyowekwa na baada ya
hapo kuwasilishwa Wizarani;
8. Maombi
yaambatane na mchanganuo wa gharama za mradi;
Kwa tangazo hili, vikundi husika vinashauriwa
kujiandaa kwa ajili ya kutumia fursa hii kwa
kushirikiana na Halmashauri zao. Aidha,
Halmashauri zinashauriwa kufuatilia na kuwandaa
walengwa ili hatimaye vipatikane vikundi vyenye
sifa ya kupewa ruzuku.
Tangazo limetolewa na:-
Katibu Mkuu,
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo
na Uvuvi,
Sanduku La Posta 9152,
DAR ES SALAAM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni