Nav bar

Jumamosi, 25 Agosti 2018

UZINDUZI WA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA KASKAZINI KATIKA VIWANJA VYA THEMI - ARUSHA.Mgeni rasmi katika ufunguzi alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli za mbalimbali za maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Themi - Arusha tarehe 05/08/2018

#Nimetembelea mabanda na kujionea shughuli mbalimbali, nawapongeza sana kwa kazi nzuri,
nimefurahishwa na maonesho kutoka Halmashauri na mashamba darasa, Alisema - Mpina

#Vilevile kwa ufugaji bora mnaofanya , nimeona kwenye (paredi) kuna ng'ombe wanaotoa hadi lita 28, hongereni kwa kazi nzurii , Alisema - Waziri

#Kauli mbiu yetu ya leo ni Wekeza katika Kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa maendeleo ya viwanda, tukae tujiulize tunawekeza nini katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na tunachangamoto zipi, Alieleza - Waziri

#Aidha, kati ya ng'ombe mil 30 .5, ng'ombe mil 4 na laki 4 zote zinatoka ukanda wa kaskazini ambapo ni zaidi ya asilimia 10 ya ng'ombe wanatoka ukanda huu, Alieleza - Mpina

#Pia kati ya Kondoo mil. 5.3 kondoo mil 2.7 wanazalishwa Ukanda wa kaskazini, na Kati ya mbuzi Mil 18.8 wanaozalishwa hapa ni mbuzi mil 4.1, Aliongezea kusema - Mpina.

#Kwapande wa uvuvi mna maeneo mengi ya maziwa na mabwawa, kwahiyo mnayo fursa nyingi za
kufuga samaki na kupata vifaranga bora vya samaki. Alisema - Mpina

#Niwahakikishie kituo chenu cha Tanga kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019 tutakiboresha na
kukiimarisha vizuri ili kiweze kuzalisha vifaranga bora vya samaki. Alisisitiza - Mpina

#Halmashauri, Wakuu wa Mikoa na Watendaji wote , Tokomezeni uvuvi haramu kwenye maziwa na
mabwawa yetu, Kwanini tuagize samaki kutoka nje wakati tunaacha rasilkmali zetu zinafanyiwa uvuvi haramu. Alisema - Luhaga

#Ningeomba uzalishaji wa samaki uongezeke kama kuna soko la uhakika kwenye mazao haya inabidi
tuwekeze vyakutosha, hatuzuii kuagiza nje lakini tuagize bidhaa zile tu ambazo hatuwez kuzalisha Nchini. - Mpina

#Wito wangu kwenu wekezeni katika Kilimo, Mifugo, na Uvuvi,pia muanzishe mashamba na mabwa
makubwa ya kufuga samaki.

#Watendaji wangu kutoka Wizarani zungukeni maeneo yote ya wananchi na kuhamasisha ufugaji 
bora.

#Awali ya yote hakikisheni Kanda ya kaskazini kuna kuwa na viwanda vikubwa vya  kuchinjia, kuchakata na kusindika nyama.

#Nataka wakenya waje kununua hapa nyama Watanzania wengi hatunufaiki mifugo mingi inatoroshwa ambapo Mbuzi laki 125 na ng'ombe 37 wametoroshwa kwenda nje ya Nchi.

#Wito wangu kwa Watendaji na Halmashauri zote ni lazma tupate kiwanda kikubwa cha kusindika
nyama, hatuna kiwanda kikubwa cha Usindikaji wa nyama, -

#Nawapongeza Halmashauri kwa kutenga maeneo elf 66, Ni muhimu kuendelea kutenga maeneo ya
mifugo na tutakuja kuyatambua na kuyasajili, Alisema - Mpina

#Majosho hayafanyi kazi yote na mengine hayana miundo mbinu muhimu na machinjio hayafanyi kazi, pia Kituo chetu NAIC - Usa River kitaboreshwa zaidi na mapungufu yatatatuliwa. - Mpina

#Migogoro ya  Wakulima na Wafugaji lazma itatulike, migogoro isiyokuwa na lazima haiitajiki, kila mtu aweze kuheshimu mifugo ya mwenzake, Alisistiza - Mpina

#Ni lazima tujipange na tuhakikishe Halmashauri wametenga maeneo ya mifugo, tutafatilia mimi na
watendaji wangu kuhakikisha maeneo yaliyosemwa yametengwa - Mpina

#Natoa Maelekezo 6 kupitia ugeni wangu:-

1. Ninampa siku 7 Katibu Mkuu Kilimo kunieleza kwanini bei za mahindi na mtama zinazaliwa hapa
mchini na zinauzwa kwa bei kubwa.

2. Nipewe maelezo kwanini Bei ya Uhimilishaji inayotozwa ni kubwa wakati kituo ni cha serikali na
mbengu zimahifadhiwa katika sehemu ya serikali.

3.Taasisi zinazohusika na Udhibiti wa madawa hapa nchini TPRI, TFDA na DVS wafanye tathmini ya utendaji wao wa kazi, kasoro zao kwanini wananchi wanunue dawa ambazo hazina ubora na wakati Taasisi hizo zipo.

4. Natoa miezi 5 Halmashauri kuhakikisha majosho na mabwawa yanakaratibiwa na yanafanya kazi
mwezi wa 1 tarehe 1 nikikagua nikakuta hakuna miundo mbinu muhimu nitafuta ukusanyaji wa kodi
yoyote katika eneo lolote na makusanyo.

5. Pia Kila Halmashauri ziwe na mashamba darasa la malisho  na kuhakikisha wananchi wanajifunza ufugaji wa samaki na Shamba la kuzalisha vifaranga vya samaki, kufikia June 2019 tujiridhishe kila Halmashauri lina bwawa la mfano. - Mpina

6.Mpango wa kudhbiti uvuvi haramu, wizara yangu imejipanga vizuri kushirikiana na watendaji wengine kuhakikisha uvuvi haramu wa kwenye mabwawa, maziwa na mito yote yanakwisha - Waziri.

#Halmshauri wekeni mipango dhabiti ya kupambana na uvuvi haramu katika sehemu zote za
maziwa,mito na mabwawa.

#Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano hakikisha katika viwanja vyetu vya ndege na bandari lazima kuwe na miundo mbinu bora na sehemu za kutunzia samaki na nyama zijengwe. - Mpina

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ambae ni mgeni rasmi kstiks msonesho ya nanenane akiwasili katika viwanja vya Themi- Arusha

Mhe.Waziri akimpongeza mfugaji kwa ufugaji bora wa ng'ombe.

Mhe. Waziri ambaye ni mgeni rasmi akiwapa mikono washiriki wa maonesho ya naenane Mkoani Arusha alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Mhe. Luhaga Mpina akioneshwa madawa mbalimbali ya mifugo kutoka LITA
Ijumaa, 24 Agosti 2018

KATIBU MKUU UVUVI DKT. RASHID ADAM TAMATAMAH AFANYA ZIARA WILAYANI MUSOMA.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya (Uvuvi) Dr. Rashid Tamatama amefanya ziara
Wilayani Musoma Mkoani Mara katika kiwanda cha samaki cha Musoma Fish Processors.

Akiongea na wafanyakazi katika kiwanda hicho, Dkt Tamatama amesema kuwa rasilimali ya uvuvi
imepungua kwa kiwango kikubwa sana kitu ambacho sio kizuri kwa mustakabali wa maisha ya baadaye. Kipato cha mwananchi mmoja mmoja kimepungua kwa kiwango kikubwa na pia kumekuwa na ulaji wa wastani wa samaki ambao ni mdogo sana kwa Watanzania. alisema.

Aidha, Katibu Mkuu Uvuvi Dkt.Tamatama alisisitiza kuwa hakuna malighafi za samaki zinazokuja kiwandani kwa ajili ya uchakataji hivyo kwa kutokuwa na malighafi hizo kunarudisha nyuma nguvu ya kufikia Tanzania ya Viwanda.

Sisi kama Wizara yenye dhamana tumeliona hilo ndio maana tumekuja na operesheni mbalimbali
ambazo zimeonyesha Mafanikio makubwa sana, kwani ukiangalia samaki waliopo viwandani na
wanaoliwa na wananchi huko mtaani ni wakubwa na wana minofu.

Hata hivyo tumepokea wazo lenu chanya la uchakataji na usindikaji wa samaki kutoka kwa Wafugaji wa Samaki wa mabwawa na vizimba. Nimekuja hapa ili tuweze kuzungumza kwa kina kuhusu maombi yenu hayo na ninaahidi kuwa Wizara itafanya utafiti kutambua kiwango cha samaki kinacho fugwa kama kitatosheleza mahitaji ya soko la walaji wa ndani na ziada kuchakatwa viwandani. Tukijiridhisha nina uhakika Wizara haitasita kutoa kibali, ninaamini mtachakata zaidi na kuongeza pato kwa Taifa. alisema.

Katika hatua nyingine, Dkt.Tamatama alisema kuwa amefurahishwa na hatua za uandaaji wa samaki
kuanzia samaki analetwa kiwandani, kuchakatwa, uhifadhi hadi kufikia kwenye hatua ya usambazaji kwenye soko la ndani na nje ya nchi. Kazi kubwa ya Serikali kwa sasa ni kuhakikisha tunashirikiana kupatikana kwa malighafi ya kutosha kuchakatwa kwenye viwanda na pia kuhakikisha tunafikia uchumi wa viwanda kwa kuongeza uwekezaji wa viwanda zaidi vya kuchakata na  kuongeza thamani (value addition) samaki na mazao yake .

Vilevile, Dkt Tamatamah alisisitiza na kutoa wito kwa Wavuvi na Wadau wote kuacha uvuvi haramu ili kuinua uchumi wa viwanda, na samaki wavuliwe wale wanaokidhi vigezo vya Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 na sio kuvua samaki wachanga ambao bado wanahitaji kukua na kufikia umri wa kuzaa. Serikali itaendelea kuwakamata wavuvi wanaotumia zana haramu kuvua samaki kinyume cha Sheria, Kanuni na taratibu na wale wanaofanya biashara ya kuuza samaki wachanga na zana haramu.  Pia, tutaongeza nguvu zaidi na  kasi ya kupambana na uvuvi haramu hivyo ninawasihi wawekezaji wa viwanda vya samaki na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya uvuvi na biashara haramu katika Sekta ya Uvuvi.

Kwa upande mwingine, Menejimenti ya Kiwanda pamoja na baadhi ya wafanyakazi kwenye Kiwanda hicho walieleza kuwa changamoto kubwa zinazowakabili wawekezaji hao ni ugumu wa upatikanaji wa samaki ikiwa ni malighafi muhimu kwao. Hii imesababisha Wafanyakazi wengi kufukuzwa kazi,  kiwanda kimelazimika kupumguza shift za uzalishaji na kuathiri kwa kiwango kikubwa utendaji wa kiwanda,  Hali hii ndiyo sababu  kubwa ya kuomba kibali cha kuchakata samaki aina ya "Sato" kutoka kwa wafugaji samaki nchini. 

Aidha, Dr Tamatamah alieleza kuwa Wizara inatambua uwapo wa changamoto kwenye ufugaji wa samaki hususani  upatikanaji  wa vifaranga bora vya samaki kwa wingi na pia upatikanaji wa chakula bora cha samaki wanaofugwa. Akasisitiza kuwa Wizara kwa kushirikiana na sekta binafsi itahakikisha kwamba vifaranga vya samaki vinapatikana kwa wingi pamoja na chakula kilicho bora.

Naye Vincent Naano Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mjini Mkoani Mara amewaomba waliopo kwenye
sekta ya Uvuvi (agents/mawakala) waje na maandiko ili wawezeshwe kupatiwa Mikopo na TAASISI za kifedha, pia watengeneze mfumo rasmi wa ajira ili watu wanaofanya kazi ziwani wakiingia watambulike.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma Bw Vicent Naano ameshauri wavuvi wadogo  wajiunge kwenye vikundi ili waweze kuwezeshwa kuendesha shughuli zao. Safari hii watakaotumia zana haramu za kuvulia hawatapigwa faini tuu, bali tutawapeleka mahakamani. alisema.


Dkt. Rashid Tamatamah akipewa maelezo juu ya mazao ya samaki yanayosafirishwa nje ya nchi.

Samaki aina ya sangara wakiwa kwenye eneo la uchakataji

Bw. George, Meneja wa kiwanda akitoa maelezo ya kiwanda.

Dkt. Rashid Tamatamah na Mkuu wa Wilaya Mhe. Vicent Naano pamoja na wajumbe wakiingia kiwandani


Alhamisi, 23 Agosti 2018

WAFUGAJI WAKUMBUSHWA KUFUGA KISASA
Wafugaji Mkoani Mwanza wametakiwa kufuga kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na mifugo ya kutosha ili kuweza kupata tija na kufikia uchumi wa viwanda.
                                                                                         
Akiongea na wadau mbalimbali wa mifugo katika mnada wa Nyamatara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza hivi karibuni, Katibu Mkuu Wizara ya  Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka wafugaji kujifunza mbinu bora za ufugaji ili sekta ya mifugo iweze kutoa mchango stahiki katika upatikanaji wa Mali ghafi za viwandani.

Aidha Profesa Elisante amewataka wafugaji na wadau wote wa sekta ya mifugo kufata sheria za nchi katika kutekeleza shughuli zao ili kuepusha migongano baina yao na mamlaka mbalimbali za nchi.

Hata hivyo profesa Elisante Ole Gabriel amewahakikishia wafugaji kwamba serikali kupitia Wizara ya mifugo itahakikisha matatizo mengi ya wafugaji yanatatuliwa kwa wakati ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Pia amesisitiza kuwepo kwa matumizi ya mizani ya kupimia ng’ombe na sio kuuza kwa kuangalia ukubwa wa ng’ombe kwa macho ambapo itasaidia mfugaji na mnunuzi, na kuwepo na ushirikiano wa karibu kati ya Wizara, wafugaji na wanunuzi wa mifugo ili kuweza kufanya kazi zao katika utaratibu unaoeleweka.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi,kitengo cha Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa katika mnada wa Nyamatara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.

Profesa Elisante Ole Gabriel akiongea na wafugaji katika mnada wa Nyamatara Mkoani Mwanza


Jumanne, 21 Agosti 2018

Wizara imejipanga kudhibiti utoroshaji wa mazao ya mifugo na uvuvi- Mhe. Ulega; Simiyu.
Utoroshwaji  wa mazao ya  Mifugo na  Uvuvi kwenda nje ya Nchi bila kibali  pamoja na matumizi ya zana haramu za uvuvi vimetajwa kuwa ni baadhi ya changamoto kubwa zinazokwamisha juhudi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kuwa sekta za Mifugo na Uvuvi  kuchangia mchango mkubwa katika pato la Taifa.

Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nanenane kitaifa, yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi mjini Bariadi.

Ulega alisema Wizara yake inachangia asilimia 30 tu katika uchumi wa Nchi wakati inauwezo mkubwa wa kuwekeza na kuchangia pato la Nchi kwa kiwango kikubwa.

“Mchango wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika pato la Nchi ni mdogo sana ukilinganisha na sekta yenyewe, lakini sababu kubwa zinazokwamisha na kusababisha hayo ni wananchi wenyewe ambao baadhi yao wamekuwa wakitorosha mazao ya mifugo na bahari kwenda nje ya nchi bila kibali “Alisema

Alisema kwa sasa Wizara yake imejiandaa kuhakikisha wanapambana na wale wote wanatorosha mazao ya Mifugo na Uvuvi bila kibali huku wakijikita kutoa elimu na kuzuia matumizi mabaya ya zana haramu ambazo zinasababisha uzalishaji wa mazao ya bahari kupotea.

“Ni aibu sana kuona Wizara kubwa kama yangu  inachangia asilimia 30 tu katika pato la taifa…nitahakikisha tunatatua hilo kwa kufanya msako (operation ) ili kuifanya Wizara kuwa na tija…Alisema

Waziri wa Kilimo Charles Tizeba aliwataka wananchi hasa wakulima wa Mikoa ya Simiyu,  Shinyanga na Mara kuyatumia maonesho ya nanenane katika kujifunza ili yaweze kuleta tija na kubadilisha kilimo, kipato na maisha yao kwa ujumla .

Aidha alisikitishwa sana kuona sekta ya kilimo yenye nguvu kazi kubwa ya wakulima asilimia zaidi ya 70 nayo inachangia kiasi kidogo katika pato la Taifa.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alisema kuwa maonesho hayo ya nane nane ambayo yameanzishwa kwa kanda mpya ya ziwa mashariki inayohusisha Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara yatawapunguzia wakulima kwenda nje ya nchi kujifunza .

Mtaka alisema watajitahidi kuendelea kuyafanya maonyesho hayo kuwa ni ya kimataifa na kwamba kanda hiyo itakuwa ni kitovu kikubwa kwa wakulima na wafugaji  kuja kujifunza kwa vitendo.

Kelvin Emanuel mvuvi kutoka Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu alisema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi inajukumu kubwa la kutoa elimu kwa wananchi juu ya ufugaji wa kisasa na wenye tija badala ya kuwachomea zana zao za Uvuvi  kwani haitasaidia kutokomeza Uvuvi wa kutumia zana haramu.

binafsi naona Wizara inawajibu wa kuelimisha Uvuvi bora,  tena si tu kuelimisha bali kuelimisha na kutoa nyavu vinazotakiwa ili kwa pamoja waweze kuleta tija kwa wavuvi na Taifa kwa ujumla.Waziri wa Kilimo Mhe. Charles Tizeba akiwa kwenye banda la Mifugo na Uvuvi, katika kiwanja cha Nyakabindi Mkoani Simiyu.Waziri wa Kilimo akisema neno wakati akitembelea banda la Mifugo na Uvuvi katika kiwanja cha Nyakabindi Mkoani Simiyu.