Wafugaji Mkoani Mwanza wametakiwa kufuga kisasa ikiwa ni
pamoja na kuwa na mifugo ya kutosha ili kuweza kupata tija na kufikia uchumi wa viwanda.
Akiongea na wadau mbalimbali wa mifugo katika mnada wa
Nyamatara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza hivi karibuni, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Profesa Elisante Ole Gabriel amewataka wafugaji kujifunza mbinu bora za ufugaji ili sekta ya mifugo
iweze kutoa mchango stahiki katika upatikanaji wa Mali ghafi za viwandani.
Aidha Profesa Elisante amewataka wafugaji na wadau wote wa
sekta ya mifugo kufata sheria za nchi katika kutekeleza shughuli zao ili kuepusha migongano baina
yao na mamlaka mbalimbali za nchi.
Hata hivyo profesa Elisante Ole Gabriel amewahakikishia
wafugaji kwamba serikali kupitia Wizara ya mifugo itahakikisha matatizo mengi ya wafugaji yanatatuliwa
kwa wakati ili waweze kufanya kazi zao vizuri.
Pia amesisitiza kuwepo kwa matumizi ya mizani ya kupimia ng’ombe
na sio kuuza kwa kuangalia ukubwa wa ng’ombe kwa macho ambapo itasaidia mfugaji na mnunuzi,
na kuwepo na ushirikiano wa karibu kati ya Wizara, wafugaji na wanunuzi wa
mifugo ili kuweza kufanya kazi zao katika utaratibu unaoeleweka.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi,kitengo cha Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel akiwa katika mnada wa Nyamatara Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza. |
Profesa Elisante Ole Gabriel akiongea na wafugaji katika mnada wa Nyamatara Mkoani Mwanza |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni