Na. Stanley Brayton, WMUV
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti amewataka wafugaji kuachana na Ufugaji wa kizamani na kufuga kisasa ili kuongeza tija katika Mifugo.
Akizungumza katika Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo yalioshirikisha nchi tatu ikiwemo Tanzania, Kenya na Namibia, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani, Mhe. Mnyeti, amesema Serikali awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sasa inaendelea na mchakato wa kuhamasisha wafugaji kuachana na Ufugaji wa kizamani na kuingia kwenye Ufugaji wa kisasa wenye tija.
“ni matumaini yangu kuwa wafugaji mtachangamkia fursa hii kwa kutafuta na kununua mbegu bora za mifugo zitakazowaletea tija zaidi kwenye ufugaji wenu kuliko kuendelea na Ufugaji wa kizamani usio na tija.” ameseama Mhe. Mnyeti
Aidha, Mhe. Mnyeti amesema maonesho haya ya mifugo yana lengo la kuhamasisha matumizi ya mbegu bora za mifugo ili kumwezesha mfugaji kuzalisha mazao mengi ya mifugo na kupata faida zaidi, pamoja na kuiwezesha Sekta ya Mifugo kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa Taifa, pamoja na kuwawezesha wafugaji kuleta mabadiriko katika Ufugaji wao wa kisasa.
Vilevile, Mhe. Mnyeti amesema swala la Malisho ya Mifugo imekuwa changamoto na wafugaji wengi wanatembea na rundo kubwa la mifugo kwa ajili ya kutafuta malisho, lakini Ufugaji wa kisasa utasaidia kuwa na Mifugo michache yenye tija ambayo italeta faida kubwa kutokana na uzito na ubora wa mifugo kuliko kuwa na Mifugo mingi yenye uzito mdogo ambayo haina faida yeyote wala tija.
Pia, Mhe. Mnyeti amewataka wafugaji kutafuta mbegu Bora za Malisho na kuzipanda kwa wingi kwa ajili ya Mifugo yao ili Mifugo iweze kupata chakula Cha kutosha kitakachowafanya kuwa Bora zaidi, na amesisitiza wafugaji kuendelea kujitokeza kwenye Benki na Serikali ili waweze kupata mikopo ambayo itawasaidia kukua katika swala la Ufugaji wa Kibiashara.
Halikadhalika, Mhe. Mnyeti amebainisha kuwa Serikali inaendelea kutatua changamoto zinazowakabili Wafugaji na wadau wa Sekta ya Mifugo, ikiwa ni pamoja na kufanya jitihada zake za kuhakikisha wafugaji wanafikiwa na kupata huduma za ushauri wa kitaalam kwa wakati ambapo imeendelea kuajiri maafisa ugani pamoja na kusambaza vitendea kazi kwa maafisa wote, kwani Lengo la Serikali ni kuwa na Afisa ugani katika ngazi ya Kijiji ili kuwawezesha wafugaji kufikiwa na huduma kwa wakati.
Mhe. Mnyeti amekishukuru Chama cha Wafugaji Ng’ombe Kibiashara, Ranchi ya Mbogo pamoja na wadau wengine kwa kuandaa na kufanikisha maonesho hayo ambayo yameambatana na mnada wa mbegu bora za mifugo zenye tija zaidi kwenye uzalishaji wa Mifugo Bora mana wameungana na Serikali katika kuhamasisha Ufugaji wa kisasa.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti (aliyenyoosha mikono juu), akionyesha ishara ya Uzinduzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo baada ya kukata utepe, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho hayo, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti, akihutubia wadau wa Sekta ya Mifugo, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti (wa pili kushoto), akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Namibia nchini Tanzania, Mhe. Lebbius Tobias (wa nne kulia), mara baada ya kuwasili kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani, wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Samwel Mdachi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti (wa kwanza kulia), akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Ndg. Isaac Njenga (wa kwanza kushoto), mara baada ya kuwasili kwenye Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uzalishaji na Masoko Sehemu ya Uzalishaji Mifugo, Dkt. Yeremia Sanka (wa pili kulia), akimuelezea Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti (wa nne kulia), juu ya shughuli zinazofanyika katika Sekta ya Mifugo, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ranchi ya Mbogo, Ndg. Naweed Mulla.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti (anaekunywa Juisi), akionja bidhaa ya Ranchi ya Mbogo (Juisi) inayotokana na mchanganyiko wa Maziwa na Matunda, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani, wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Samwel Mdachi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti (katikati), akitazama mbegu Bora za Mifugo, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani, wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Samwel Mdachi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti (wa tatu kushoto), akikabidhi Cheti cha Usajili kwa Wafugaji wanaofuga ng'ombe za mbegu nchini, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti (waliokaa katikati), akiwa kwenye picha ya Pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, mara baada ya Ufunguzi wa Maonesho ya Kimataifa ya Ufugaji Kibiashara na Mnada wa Mifugo, yaliyofanyika katika Ranchi ya Mbogo, Juni 14, 2025, Chalinze - Pwani.