Nav bar

Ijumaa, 27 Juni 2025

MASOKO YA NYAMA NJE YA NCHI YAFUNGUKA MIAKA 4 YA RAIS SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema jitihada za serikali ya awamu ya sita za kufungua masoko nje ya nchi zimeongeza mauzo ya nyama kwa upande wa sekta ya Mifugo kutoka Dola za marekani milioni 4.2 mwaka 2020/2021 hadi kufikia Dola za Marekani milioni 61. 4 Mwaka 2025.

Mhe. Dkt. Samia amesema hayo wakati akihutubia na Kuhitimisha shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hafla inayofanyika Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 27, mwaka 2025.

Aidha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan serikali itabeba nusu ya gharama ya chanjo ya ng’ombe,Mbuzi na Kondoo huku gharama zote za chanjo ya Kuku zitabebwa na serikali.

Pia Rais Mhe. Dkt. Samia ametoa rai kwa wabunge kuhimiza wananchi kuwa na matumizi bora ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima kwa kufanya ufugaji wa kisasa.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni