Nav bar

Alhamisi, 23 Machi 2023

SERIKALI KUKOPESHA WANAWAKE SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

Serikali kupitia Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (EIB) inatarajia kutoa mkopo wa Sh1.3 trilioni kusaidia wanawake kuboresha biashara na uwekezaji kwenye mnyororo wa thamani katika sekta za mifugo na uvuvi.

Akizungumza kuhusu fursa hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya mifugo na uvuvi Dkt. Daniel Mushi alisema dhumuni la fedha hiyo ni kuwezesha sekta binafsi kuwa kichocheo cha maendeleo, Machi 21, 2023

“Kwa kuanzia walengwa mahsusi ni sekta binafsi hususan kwa biashara zinazoongozwa na wanawake au shughuli zinazoambatana na uchumi wa buluu ikiwemo kilimo cha mwani”alisema Dkt. Mushi.

Aidha Dkt. Mushi alisema sio tu kuwainua wanawake katika uwekezaji bali hata kuzalisha fursa za ajira kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya bahari na mifugo kwa ujumla na kupunguza suala la ukosefu wa ajira nchini.

“Wajasiriamali watumie fursa hii vizuri ili iwe kioo na baadae tuaminike ili fedha zijazo zipitie moja kwa moja kwenye sekta binafsi na fursa hii itakuja tena ikiwa tutakuwa waaminifu kwa kutumia vizuri mikopo hiyo”alisema.

Akizungumza katika mkutano wa kuwajengea uwezo na kujadili fursa za mkopo huo, Mchumi kutoka Wizara ya fedha na Mipango Vidah Malle alisema mkopo huo ni fursa pekee kwa sekta binafsi kukuza uaminifu kwa kutoa matokeo chanya ya fedha watakazozichukua.

“Sina uhakika kama fursa kama hii imewahi kupitia katika sekta binafsi mara nyingi hupitia Taasisi za Serikali kwa hiyo hii ni hatua nzuri na tumeoneshwa kuaminiwa hivyo tujitahidi tutakapopata fedha hizo basi tulete matokeo chanya”alisema Vidah.

Kaimu Mkuu kitengo cha kilimo rejareja NMB, Wogofya Mfalamagole alisema benki yao imejipanga kutoa mikopo hiyo kwa wawekezaji wote kwenye sekta binafsi kwa mujibu wa taratibu walizopangiwa na Serikali kwa riba isiyozidi asilimia 10.

Rose Lyimo ni mwekezaji na Katibu wa Chama cha usindikaji wa maziwa Tanzania (TAMPA) alisema katika jamii kuna wanawake wengi wanaofanya shughuli za uwekezaji na hawana mitaji ya kutosha kupanua biashara hivyo mitaji hiyo itasaidia kuwainua wanawake na kuonyesha uwezo wao

Mkopo huo ambao unatajwa kuwalenga zaidi wanawake utakwenda moja kwa moja kwa sekta binafsi kupitia Benki za NMB, CRDB na KCB

 


Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi akiongea wakati wa kufungua kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika Machi 21, 2023 Jijini Dodoma

Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Vidah Malle akiongea wakati wa  kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika Machi 21, 2023 Jijini Dodoma

Sehemu ya washiriki wa kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika Machi 21, 2023 Jijini Dodoma


Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Daniel Mushi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mara baada ya kufungua kikao cha wadau juu ya uwezeshwaji wa miradi ya uwekezaji kwenye Mifugo na Uvuvi kupitia dirisha la Uwezeshwaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kilichofanyika Machi 21, 2023 Jijini Dodoma


Alhamisi, 16 Machi 2023

VIJANA MTWARA KUFAIDIKA NA PROGRAM YA ATAMIZI

Kiongozi wa vijana wanaoendelea na programu maalum ya Atamizi kwa upande Sekta ya Uvuvi waliopo  kwenye kituo cha Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Mikindani, Mtwara. Bw. Charles Songa akiwaongoza wenzake wakati wa mafunzo kwa vitendo kuhusu ufugaji wa matango bahari ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Programu hiyo (15.03.2022).

Mkufunzi kutoka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kituo cha Mikindani, Mtwara Bw. Shaban Saleh (kulia) akiwafundisha vijana wanaoendelea na programu maalum ya Atamizi kwa upande wa sekta ya Uvuvi fursa zilizopo kwenye ufugaji wa tango bahari wakati wa Mwendelezo wa Programu hiyo  (15.03.2023).

Mkufunzi kutoka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) kituo cha Mikindani, Mtwara Bw. Shaban Saleh (wa pili kutoka kulia) akiielekeza timu ya tathmini kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi inayoongozwa na Bi. Yasinta Magesa (kulia) namna wanavyowawezesha elimu ya Ufugaji wa samaki vijana wanaoshiriki Programu maalum ya Atamizi waliopo kituoni hapo muda mfupi baada ya timu hiyo kuwasili  (15.03 2023)

 

VIJANA WAPATIWA MAFUNZO YA UKUZAJI VIUMBE MAJI KWA VITENDO (ATAMIZI) MAGU MKOANI MWANZA

Meneja wa Shamba la kufugia Samaki la KONGA AGRIBUSINESS FARM, Bw. Steven Satola akitoa maelezo ya utendaji kazi wa shamba hilo ambalo limepokea vijana wahitimu  waliochaguliwa kupata mafunzo ya vituo atamizi vya uvuvi na ukuzaji Viumbe  maj kwa wataalamu wa Uvuvi waliotoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, walipoenda kutembelea na kuona mafunzo hayo yanavyoendelea kwa vijana hao kwenye shamba hilo lililopo Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza, Machi 15,2023.

Wataalamu wa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakiongea na vijana wa mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa Vitendo (Atamizi) waliochaguliwa kwenye Shamba la kufugia Samaki la KONGA AGRIBUSINESS FARM, ili kujua wanajifunza nini na changamoto gani wanazioitia wanapokuwa kwenye mafunzo hayo, shamba hilo lipo katika Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza, Machi 15,2023.

Vijana waliochaguliwa kwenye mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji (Atamizi) wakifanya zoezi la kuhamisha vifanga vya Samaki kwenye bwawa ili waweze kusafisha bwawa hilo ambalo wanafanyia mafunzo ya Ufugaji Samaki katika Shamba la KONGA AGRIBUSINESS FARM Lililopo Wilaya ya Magu,Mkoani Mwanza  mbele ya Wataalamu wa uvuvi kutoka  Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Machi 15,2023.

Vijana wa mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji kwa Vitendo (Atamizi) waliochaguliwa kwenye Shamba la kufugia Samaki la KONGA AGRIBUSINESS FARM, wakiwaelezea wataalamu wa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (hawapo pichani) namna ya vifaranga vya samaki vinavyozalishwa katika Maabara ya Uzalishaji wa Vifaranga vya samaki (Hatchery), Shamba hilo lipo katika Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza,  Machi 15,2023.

 

VIJANA WAPATIWA MAFUNZO YA UFUGAJI WA SAMAKI KWA NJIA YA VITENDO MKOANI MARA

Mkuu wa Kikosi cha 27KJ Makoko mkoani Mara, Lt. Col. Simon Rugaimukamu (kulia) akiwaeleza wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu namna walivyowapokea vijana ambao wamepelekwa kwa ajili ya kupata mafunzo kwa vitendo kuhusu ufugaji wa samaki kwenye vizimba ambapo ameiomba Wizara kukitumia kituo hicho kama shamba darasa ili vijana na wavuvi waweze kujifunza. (15.03.2023)

Afisa Uvuvi Mwandamizi, Bi. Kresensia Mtweve akizungumza na vijana waliopo kwenye kituo cha 27KJ Makoko mkoani Mara (hawapo pichani) kwa ajili ya kupata mafunzo kwa vitendo kuhusu ufugaji wa samaki kwenye vizimba wakati wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu walipotembelea kituo hicho kuona namna mafunzo hayo yanavyoendeshwa ambapo amewasihi vijana hao kutumia elimu waliyofundishwa ili kuleta tija katika ufugaji. (15.03.2023)

Picha ya pamoja ya wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu na vijana wanaopata mafunzo kwa vitendo kwenye kituo cha 27KJ Makoko mkoani Mara mara baada ya kukagua na kunzungumza na vujana hao. (15.03.2023)

Baadhi ya Vizimba vilivyopo kwenye kikosi cha 27KJ Makoko mkoni Mara vinavyotumika kufugia samaki. (15.03.2023)

 

KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI DKT. CHARLES MHINA AFANYA KIKAO NA MSHAURI ELEKEZI KUTOKA FAO, BI, TERESA AMADOR

Mshauri elekezi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Bi. Teresa Amador akiwasilisha taarifa ya majumuisho juu ya Sera na Sheria  za Uvuvi  kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Mhina (kulia) mara baada ya ziara yake Wizarani hapo, Machi 15,2023 Mtumba jijini Dodoma, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi Tanzania Bw. Melkizedeck Koddy

Kaimu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina (kulia) akiongea mara baada ya kupokea taarifa ya tathmini ya Sera na Sheria za Uvuvi kutoka kwa Mshauri elekezi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Bi. Teresa Amador  (katika)  kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi Tanzania Bw. Melkizedeck Koddy, Machi 15,2023 Mtumba jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Uvuvi Tanzania Bw.  Melkizedeck Koddy, (kulia) akichangia hoja wakati wa kikao cha kupokea taarifa kutoka kwa mshauri elekezi Bi. Teresa Amador kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi  mtumba jijini Dodoma,  Machi 14,2023

Kaimu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi , Dkt. Charles Mhina (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshauri Elekezi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Bi. Teresa Amador (wa tatu kutoka kushoto) na watendaji kutoka Sekta ya Uvuvi mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika kwenye ofisi za Wizara hiyo Mtumba Jijini Dodoma, Machi 15,2023

 

WATAALAM KUTOKA SEKTA YA UVUVI WAWATEMBELEA WAFUGAJI WA SAMAKI KWENYE MABWAWA WILAYANI CHAMWINO

Mfugaji kwenye mabwawa Bw. Manoa Samson (kushoto) akielezea namna walivyoanza ufugaji wa samaki na adi walipofikia kwa sasa pamoja na changamoto na mafanikio waliyoyapata na kuhamasisha wafugaji wengine kutokukata tamaa wakati walipotembelewa na watendaji kutoka wizara ya mifugo na uvuvi, Machi 14, 2023 Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma .

Afisa Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (uvuvi) Bw. John Mallya (wa pili kutoka kulia) akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wafugaji wa samaki walipowatembelea wafugaji hao kwenye wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Machi 14,2023

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Mkomanile Mahundi akiwaeleza wafugaji wa samaki kwenye mabwawa aina ya vyakula vya kulisha samaki hao na namna ya kuwalisha wakati walipowatembelea kwenye kijiji cha Handari halmashauri ya wilaya ya chamwino mkoani Dodoma, Machi 14,2023

Mkurugenzi Msaidizi wa Utafiti, mafunzo na Ugani  kutoka wizara ya mifugo na uvuvi (uvuvi) Bw. Anthony Dadu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafugaji wa samaki kwenye mabwawa  na wataalam kutoka sekta ya uvuvi mara baada ya kuwatembelea wafugaji hao na kuona namna wanafanya ufugaji wao na changamoto zinazowakabili kwenye wilaya ya chamwino mkoani Dodoma, Machi 14,2023

 

KIKAO CHA KUIMARISHA USHIRIKIANO BAINA YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MKURUGENZI WA MELI ZA ALBACORA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiongea na Uongozi wa Kampuni ya Meli ya Albacora alipokutana nao kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na Kampuni hiyo hususan kwenye eneo la Uvuvi wa Bahari Kuu. Mhe. Ulega alikutana na Uongozi huo jijini Dar es Salaam Machi 14, 2023. Uongozi wa Kampuni ya Albacora uliongozwa na Mkurugenzi wa Meli, Bw. Imanol Loinaz.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akimuelekeza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA), Dkt. Emmanuel Sweke (kulia) wakati wa kikao kifupi baina ya Waziri huyo na Mkurugenzi wa Meli za Albacora, Bw. Imanol Loinaz (kushoto) kilichofanyika jijini Dar es Salaam Machi 14, 2023. (kushoto) Mkurugenzi wa Meli za Albacora, Bw. Imanol Loinaz.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akimuonesha Mkurugenzi wa Meli za Albacora, Bw. Imanol Loinaz maelezo yaliyopo katika Kitabu cha Ilani ya ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 - 2025 yanayosisitiza kuhusu Uvuvi wa bahari kuu wakati wa kikao chao kifupi kilichofanyika jijini Dar es Salaam Machi 14, 2023.


 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Meli za Albacora, Bw. Imanol Loinaz (wa pili kushoto) muda mfupi baada ya kumaliza kikao chao kifupi kilichofanyika jijini Dar es Salaam Machi 14, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA), Dkt. Emmanuel Sweke.


PROF. SHEMDOE AMSHUKURU MHE.DKT.SAMIA KWA KUTOA TSH BILIONI 266.7

 

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa jumla ya Tsh. Bilioni 266.7  ikiwa ni gharama ya Ujenzi wa mradi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko Mkoani Lindi.

"Ninamshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia Tsh. Bilioni 266.7  ikiwa ni gharama ya Mradi ya Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi hapa Kilwa Masoko Mkoani Lindi." Alisema Shemdoe.

Aidha, Prof. Shemdoe ameongeza kuwa bandari hiyo ya Uvuvi ikikamilika itakuwa msaada mkubwa sana kwa Watanzania wanaofanya kazi ya uvuvi. Bandari hiyo  itatoa ajira elfu 30 kwa Vijana wa kike na wakiume, itaongeza usafirishaji wa Samaki Nje ya Nchi, itaongeza tija ya Uvuvi Bahari Kuu.

Vilevile, Katibu Mkuu ameainisha faida nyingine kuwa bandari hiyo itapunguza upotevu wa Samaki (Post Harvest), itaondoa changamoto ya uvuvi haramu usioratibiwa na kutolewa taarifa, vilevile itapunguza changamoto ya upungufu wa samaki ndani ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuongeza mchango wa Sekta ya Uvuvi kutoka asilimia 1.71 mwaka 2023 hadi kufikia asilimia 3 mpaka 5 ifikapo 2026.

Pia, Prof. Shemdoe amesema kuwa tayari Mhe. Rais amesharidhia malipo ya awali ya  jumla ya   Tsh. Bilioni 40 na tayari zimeshalipwa kwa Mkandarasi anayejenga bandari hiyo.

Prof. Riziki Shemdoe ameyasema hayo  jana tarehe 13 Machi 2023, alipotembelea eneo la ujenzi wa Bandari  hiyo Kilwa Masoko Mkoani Lindi ambapo mradi huo ni moja ya miradi itakayotembelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo tarehe 16 Machi 2023 kwa lengo la kukagua  miradi inayotekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mkoani Lindi.

Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu amekutana na mkandarasi anayejenga bandari hiyo  kampuni ya  China Harbour Engineering Company Ltd pamoja na Mkandarasi mshauri Elekezi  Dar Al-Handasah Consultants na kuwaelekeza kuwa wafanye kazi kwa bidii ili wamalize ujenzi huo kwa muda uliopangwa.

Kwa upande wake Mkandarasi anayejenga  bandari hiyo pamoja na Mkandarasi Mshauri mwelekezi wamekubali kuwa watafanya kazi usiku  na mchana ili kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.

Awali Prof. Riziki Shemdoe alisema kuwa anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumhamishia Wizarani ya Mifugo na Uvuvi.

"Namshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini na kunipa tena dhamana ya kusimamia Sekta hizi muhimu za Mifugo na Uvuvi, na ninamuahidi Mhe. Rais kuwa nitaendelea kuchapa kazi usiku na mchana ili kuhakikisha Sekta hizi mbili zinasonga mbele na kuchangia mchango mkubwa katika pato la Taifa." Alisema Prof. Shemdoe.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe,(wa nne kutoka kulia) akisikiliza maelezo (Mtoa maelezo hayupo Pichani) nakuangalia ramani ya Bandari ya Uvuvi itakayojengwa Kilwa masoko mkoani Lindi.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe wa nne kutoka kulia akijadiliana jambo na timu ya wahandisi wanaotekeleza mradi huo wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi kilwa masoko mkoani Lindi.


Jumatatu, 13 Machi 2023

SAUTI YETU WIKI HII

 


WIZARA YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA KAMATI

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo na kuwasilisha taarifa ya muundo na majukumu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, taarifa ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Bwawa la kuvuna maji kwa ajili ya kunyweshea mifugo la Matekwe lililopo Nachingwea, Mkoani Lindi, na taarifa ya ujenzi wa bandari ya uvuvi iliyopo Wilayani Kilwa, Mkoani Lindi.


Baada ya kupokea taarifa hiyo mapema leo Machi 12, 2023, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. David Kihenzile  alimuhakikishia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega  kuwa watashirikiana bega kwa bega na Wizara ili kuiwezesha kufikia malengo yake ya kuwahudumia wananchi ili wapate maendeleo  katika shughuli zao za kila siku za ufugaji na uvuvi.


Aidha, kamati hiyo inatarajiwa kufanya ziara Mkoani Lindi hivi karibuni kwa ajili ya kutembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akifafanua jambo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa kwa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kilichofanyika jijini Dodoma Machi 12, 2023. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. David Kihenzile (Mb), akitoa majumuisho baada ya kupokea taarifa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizowasilishwa kwa Kamati hiyo Machi 12, 2023.

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Sera na Mipango, Bw. Mbaraka Stambuli akiwasilisha taarifa ya Wizara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo katika kikao kilichofanyika jijini Dodoma Machi 12, 2023.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (watano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha kuwasilisha taarifa  kwa kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma Machi 12, 2023. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. David Kihenzile (Mb). Wengine ni Wajumbe wa Kamati hiyo na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Alhamisi, 9 Machi 2023

WAZIRI ULEGA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI KOREA

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega(kulia) akimueleza jambo  Balozi wa Tanzania nchini Korea, Balozi Togolani Mavura walipokutana ofisini kwake jijini Dodoma mapema leo Machi 8, 2023.  lengo ni kujadiliana kuhusu fursa za ushirikiano baina ya nchi hizo mbili kwenye kukuza na kuimarisha uchumi wa buluu nchini Tanzania.

Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe. Balozi Togolani Mavura (kushoto) akiongea na  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega walipokutana ofisini kwa Waziri huyo jijini Dodoma Machi 8, 2023.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe. Balozi Togolani Mavura (kulia kwake) muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yao mapema leo Machi 8, 2023. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Bi. Agness Meena. Wengine katika picha ni Wataalam kutoka Wizarani.

Jumamosi, 4 Machi 2023

SEKTA YA MIFUGO SMT NA SMZ ZAIMARISHA USHIRIKIANO

Na Saja Kigumbe


Serikali ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zaimarisha ushirikiano Ili kutatua changamoto kwenye Sekta ya Mifugo  ili kufikia uzalishaji wenye tija wa mifugo.


Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Mhina wakati akifungua kikao cha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) kilichofanyika jijini Dodoma Machi 3, 2023.


‘’Tumekuwa tukishirikiana pia kwenye maeneo ya masoko kuona ni namna gani tunaweza tukaimarisha masoko ya bidhaa za mifugo kwa pande zote mbili.  Kwa hiyo ushirikiano huu unalenga kuondoa vikwazo ambavyo vinaweza kuifanya biashara ya mifugo isikue kwa haraka ,’’ alisema Dkt. Mhina


Dkt. Mhina alisema sehemu zote za Bara na Zanzibar kuna viwanda vya kuzalisha bidhaa za mifugo ikiwemo nyama, ngozi, maziwa na bidhaa nyingine hivyo ushirikiano huo utasaidia kuimarisha sekta hiyo ya mifugo.


Aliongeza kwa kusema kuwa ushirikiano huo umelenga kutatua changamoto kwenye maeneo mbalimbali hususan changamoto  za kikodi kwa kushauri mamlaka husika ziweze kufanya marekebisho ili kuwezesha biashara kufanyika kwa urahisi zaidi kati  ya pande zote mbili  za muungano.


"Lakini ushirikiano huu pia utatuwezesha kutumia fursa za pamoja kama zitakuwepo ikiwemo fursa za kusafirisha bidhaa za nyama kwenda nje ya nchi ili tuweze kuyafikia masoko hayo kwa kiasi kikubwa,’’ alifafanua  Dkt. Mhina.


Aidha, alibainisha kuwa  ushirikiano huo utajikita pia katika maeneo ya utafiti na mafunzo ili waweze  kujifunza kila upande ni namna gani sekta zinafanya ili kuzalisha kwa tija mifugo na bidhaa zake.


‘’Pia tutajifunza ni kwa  namna gani  wafanyabiashara na wafugaji  wa sekta binafsi wanawezeshwa kutumia fursa zilizopo kuzalisha kwa tija na kuongeza mchango wa sekta ya mifugo katika pato la taifa,’’ alibainisha


Kwa upande wake,  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Dkt. Omary Ali Amir  alisema wanatumia ushirikiano huo kujifunza tafiti mbalimbali na pia kujenga uwezo wa wataalam wao kupitia Tanzania bara kwa maana Tanzania bara wako mbele kwenye masuala mbalimbali ikiwemo uzalishaji, Masoko, na Utafiti.


‘’Sekta ya mifugo sio ya muungano, lakini ni sekta ambayo inahitaji ushirikiano, mfano wafugaji wanaposafirisha mifugo kutoka eneo moja kwenda jingine kunakuwa na changamoto za kisera ,kisheria hivyo kupitia ushirikiano huu changamoto nyingi tunaweza kuzimaliza kwa ustawi wa pande zote mbili,’’ alisema Dkt. Omary

Kaimu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Mhina akifungua kikao cha ushirikiano baina ya Serikali ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) upande wa Sekta ya Mifugo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jiji Mtumba Mkoani  Dodoma, Machi 03,2023.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya kilimo, umwagiliaji, maliasili na Mifugo Zanzibar, Dkt. Omary Ali Amir akiongea na wajumbe wakati wa kikao cha ushirikiano baina ya  Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Serikali ya jamhuru ya muungano wa Tanzania (SMT) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jiji Mkoani Dodoma, Machi 03, 2023.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Venance Ntiyalundura akiongea kwenye kikao cha ushirikiano baina ya  Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya jamhuru ya muungano wa Tanzania (SMT) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina (wa tatu kutoka kulia) kufungua kikao hicho  kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jiji Mtumba Mkoani Dodoma Machi 03,2023.

Sehemu ya washiriki wa kikao cha ushirikiano baina ya  Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) Sekta ya mifugo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jiji Mtumba Mkoani Dodoma Machi 03,2023.

Kaimu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Mhina (wa Tano kutoka kulia ) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki  kikao cha ushirikiano baina ya Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwenye Sekta ya mifugo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jiji Mtumba Mkoani  Dodoma, Machi 03,2023.

KIKAO CHA KUJADILI RAASIMU YA MPANGO WA UNYWAJI MAZIWA SHULENI CHAFANYIKA JIJINI DODOMA

 

Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Stephen Michael akisisitiza baadhi ya maeneo ya kuzingatia wakati wa kupitia Rasimu ya Mpango wa Unywaji Maziwa Shuleni alipokuwa anafungua kikao cha kupitia Rasimu ya mpango huo  Machi 2, 2023 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Royal Village Hotel Dodoma, (Kushoto) ni Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya na kulia ni Mwakilishi wa Wadau wa Maziwa Nchini Bw. Joakim Balakana.

Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Dkt. George Msalya (aliyesimama) akitoa neno la utangulizi kuhusu mpango wa unywaji maziwa shuleni kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo),  Bw. Stephen Michael (katikati) kwenye kikao cha kupitia Rasimu ya mpango wa unywaji maziwa shuleni Machi 2, 2023 kwenye Ukumbi wa Royal Village Hotel, Dodoma (Kulia) ni Mwakilishi wa Wadau wa Maziwa Nchini Bw. Joakim Balakana.

Afisa Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko Bw. Edson Kilyenyi akiwasilisha Rasimu ya mpango wa Unywaji maziwa shuleni kwa wajumbe walioshiriki kikao cha kupitia Rasimu hiyo, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Royal Village, Dodoma, Machi 02,2023

Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Stephen Michael (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki  kikao cha kupitia Rasimu ya mpango wa unywaji maziwa shuleni kilichofanyika kwenye  ukumbi wa Hoteli ya Royal Village Dodoma Machi 2, 2023.