Nav bar

Ijumaa, 29 Julai 2016

MHE NAIBU WAZIRI ATEMBELEA BOKO FISH FARMING ILIYOPO KIGAMBONI TAREHE 29/06/2016

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha atembelea shamba la BOKO FISHING FARM lililopo Kigamboni Mji mwema.
 
Mfanyakazi wa BOKO FISH FARMING akionesha samaki aina ya KambaleZIARA YA NAIBU WAZIRI NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KAMPUNI YA INTERCHICK MBEZI MAKONDE TAREHE 28/07/2016Mhe.

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Interchick iliyopo mbezi

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha akipewa maelezo jinsi ya kuchanganya chakula cha kuku


Chakula cha kuku
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha akiuliza swali  kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni Bw. Orson Taylor


Alhamisi, 14 Julai 2016

MKUTANO WA MHE CHARLES TIZEBA  WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI NA WAANDISHI WA HABARI 13/7/2016

Na ,GCU (Mifugo na Uvuvi)

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi leo hii amewasimamisha kazi maafisa waandamizi wakuu wa taasisi mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi baada ya kugundua kuwa kulikuwa na ukiukaji mkubwa katika taratibu za uendeshaji wa taasisi zao. Mhe. Waziri ametangaza haya  wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Kilmo 1 jijini Dare es salaam leo hii 13/7/2016 . 

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizemba akiongea na waandishi wa habari kulia kwake ni Katibu Mkuu (U) Dkt. Yohana Budeba

Alisema kwamba hali ya chakula kwa ujumla hapa nchini ni nzuri kwa ujumla  pamoja na kuwa  tathmini ya kiasi cha mazao yanayotakiwa kuvunwa  bado haijafanyika. Alieleza kuwa kumekuwa na ununuzi mkubwa wa chakula kutoka kwa wakulima kabla ya kufanya tathmini ambapo ni kinyume na utaratibu. Ameagiza tathmini hii iwe imekamilika ndani ya wiki mbili.

 

Mhe. Waziri aliendelea kueleza kuwa amebaini kuwa kuna vibali vya kusafirisha mazao nje ya nchi ambavyo vimekuwa vikitolewa na mamlaka ya hifadhi ya chakula kinyume na utaratibu. Aliagiza vibali hivyo visitolewe tena hadi tathmini itakapofanyika, Aidha kutokana na ukiukaji wa taratibu hizo aliagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara  ya usalama wa chakula nchini   Bwana Ombeni Lemweli  ili apishe uchunguzi na Mkurugenzi wa sera na Mipango wa sekta ya Kilimo ameteuliwa  kukaimu nafasi hiyo.

 

Mhe. Waziri aliendelea kueleza kwamba amebaina kuwa kulikuwa na utunzaji mbovu wa nafaka katika maghala yake na hata mahindi yaliyoharibika hayakutolewa kibali cha kuyauza kama chakula cha mifugo kwa visingizio vya kutopata kibali cha TFDA NA TBS  cha kuyauza, lakini baadaye ilibainika kwamba mahindi hayo hayakuwa mabovu aidha imebainika kwamba na kulilkuwa na  ununuzi wa mahindi kiholela bila kuzingatia uwezo wa maghala yaliyopo, hali hii imesababisha hasara kubwa sana kwa Taifa. 

 

Aidha imebainika kwamba walishindwa kutoa takwimu halisi  ya kiasi cha  mahindi kilichoharibika Kutokana na hali hii ameagiza Katibu Mkuu amsimamishe kazi Mtendaji mkuu wa mamlaka hiyo Bwana Charles Walwa na nafasi yake imechukuliwa na Bwana Deusdedt Mpazi ambaye atakaimu nafasi hiyo. Wengine waliosimammishwa kazi ni Mkurugenzi wa uendeshaji  wa huduma Bi Anna  Ngoo na Mkurugenzi wa Masoko Mikalu Mapunda na Meneja wa NFRA Songea Bwana Jeremia Mtafya.

 

Kuhusu zao la pamba Mhe. Waziri alieleza kwamba hadi sasa kuna wanunuzi 12 ambao wamepewa leseni ya kununua Pamba na pamoja na kuwa bei elekezi ya Pamba itakuwa ni Tsh 1000/= kwa kilo ya pamba mbegu, na hii ni baada ya majadiliano na wadau kutofikia muafaka Aliwashauri wakulima wawe wavumilivu wasiuze pamba yao chini ya hiyo bei elekezi. Wakati huo huo Mhe. Waziri aliagiza Halmashauri zinazopata fedha kutokana na mauzo ya pamba zisiwalazimishe wanunuzi kulipa hizo fedha kabla ya kununua kwa kulipa advance, na bodi ya pamba imeagizwa kusimamia hilo. Halamshauri zilishauriwa zisubiri hadi ununuzi ukamilike ndipo wadai fedha zao.

 

Wakati huo huo aliagiza Makao Makuu ya bodi ya pamba yahamishwe kutoka Dar es Salaam kwani Dsm hawalimi pamba na ihamie Mwanza na Vilevile bodi ya chai ihame kutoka DSM na iende Njombe ndani ya wiki mbili na bodi nyingine kama hizo zianze kujitayarisha kufanya hivyo.

 

Kuhusu Uvuvi katika bahari kuu Mhe. Waziri alieleza kwamba Tanzania ina eneo kubwa la kiuchumi katika bahari kuu lakini haina uwezo wa kuitumia  na badala yake tumekuwa tukiwapa wenye uwezo kuvua kiasi wanachotaka kwa leseni ya dola za kimarekani 50,000 kwa muda wote wa leseni na kwa kuvua kiasi wanachotaka wao. Wavuvi hawa wanapovua samaki wa ziada huwa wanawatupa baharini au wanarudi kuja kutuuzia tena hapa sisi wenyewe kinyume na utaratibu.

 

Kutokana na hali hii Mhe. Waziri ameagiza masharti ya leseni yabadilishwe mara moja ili samaki wa ziada wawe wanaletwa hapa nchini. Aidha alishauri uangaliwe uwezekano wa kuvua kwa kushirikiana ili wanachopata tugawane wote.Kwa wale wote walio na leseni aliagiza waendelee kuzitumia hadi hapo zitakapokwisha  na baada ya hapo leseni mpya zitolewe baada ya kubadilisha masharti . Mhe. Waziri aliendelea kueleza kwamba hivi sasa kuna meli takribani 105 ambazo zinavua katika bahari kuu na mamlaka ya Uvuvi katika bahari kuu wanajua hayo hivyo basi waagizwe walete samaki wa ziada hapa nchini.

 

Katika hatua za kuimarisha mamlaka ya Uvuvi katika bahari kuu Mhe. Waziri alimteua Bwana Hosea Gonza Mbilinyi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uvuvi katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu kuanzia leo, Aidha aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo Bwana Rashid Hoza amerudishwa katika kituo chake cha kazi cha awali kuendelea na kazi zake.

 

Mhe. Waziri aliendelea kueleza kwamba Vilevile amebaini kwamba kuna matatizo ya uendeshaji katika vituo vya utafiti vya Uyole Mbeya na Naliendele Huko Mtwara hivyo basi Mkuu wa kituo cha Uyole Dr. Zacharia Malya  anaondolewa na kuhamishiwa Katika kituo cha utafiti cha Seliani Arusha kuendelea na kazi zake za utafiti na Amemteua Dr Anold Msongi anayetoka katika kituo cha utafiti cha  Ilonga  kilichopo Kilosa Morogoro. 

Katibu mkuu wa wizara ya kilimo,mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) Dr.Yohana Budeba aliyesimama mwenye koti jeusi akimkaribisha Mhe.Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe Dr.Charles Tizeba aongee na waandishi wa habari

Ijumaa, 1 Julai 2016

MKUTANO WA MAJADILIANO KUHUSU "SUSTAINABLE FISHERIES PARTNERSHIP AGREEMENT" (SPPA) KATI YA TANZANIA NA NCHI ZINAZOUNDA JUMUIYA YA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA ILIYOFANYIKA MVUVI HOUSE TAREHE 01/07/2016

Katibu Mkuu wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi (U) Dkt. Yohana Budeba akifungua mkutano kuhusu Sustainable Fisheries Partnership Agreement (SFPA) " kati ya Tanzania na nchi zinazounda Jumuiya ya Umoja wa nchi za ulaya". kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uvuvi Bw. Hosea Mbilinyi na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Dkt. Islam Seif kutoka Zanzibar
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uvuvi Bw. Hosea Mbilinyi akitoa maelezo mafupi kuhusu uvuvi na kujadili kuhusu uzoefu kutokaTaasis mbalimbali kuhusu SFA katika nchi zilizojiunga kulia kwake ni Katibu Mkuu (U) Dkt. Yohana Budeba (kushoto) ni Naibu Mkururgenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu Dkt. Omary Amiri
Wakurugenzi na Watumishi  kutoka  WWF, DSFA, ZMA, FETA, MPRU, na TAFIRI wakisikiliza taarifa inayosomwa na Katibu Mkuu (U) Dkt. Yohana Budeba hayupo Pichani
Katibu Mkuu (U) Dkt. Yohana Budeba akisoma taarifa yake kwa Wakurugenzi, Watumishi kutoka Taasis mbalimbali kuhusu SFA katika nchi zilizojiunga