Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2026

VIJANA 3,004 WAOMBA MITAJI SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema jumla ya maombi 3,004 kwa ajili ya kuwawezesha mitaji vijana wanaojishughulisha na sekta za mifugo na uvuvi yamepokelewa na Wizara huku uchambuzi wa waombaji waliokidhi vigezo ukiendelea.  Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo leo Mei 26, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Bunda Mjini Mhe. Ester Amos Bulaya (CCM) aliyehoji ni lini vijana wa Bunda watanufaika na Mradi wa Ufugaji Samaki wa Vizimba kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi? “Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), ilitangaza Machi 4, 2026 fursa ya mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 23.68 kwa ajili ya vijana wanaojihusisha na sekta za mifugo na uvuvi, hadi sasa jumla ya maombi 3,004 yamepokelewa kutoka maeneo mbalimbali nchini, yakiwemo ya vijana kutoka Bunda, huku uchambuzi ukiendelea ili kupata waombaji wal...

DKT. MADELE AWATAKA WATENDAJI SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA UADILIFU

Picha
◾ Awataka Watendaji hao kuja na Mikakati Mudhubuti ya kudhibiti Uvuvi haramu. ◾ Abainisha Mpango wa Wizara kutenga Hekta 196,324.25 kwa ajili ya Malisho. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Magawa Madele, amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Uchumi na Uzalishaji, Madaktari wa Mifugo na Uvuvi wa Mikoa, Maafisa Uvuvi wa Mikoa na Wakuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kufanya kazi kwa weledi, uwajibikaji, uadilifu na uzalendo mkubwa ili kuleta mabadiliko katika Sekta hizo mbili na Taifa kwa ujumla. Akizungumza kwa Niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, leo Mei 25, 2026 Jijini Dodoma katika Kikao kazi kilichojumuisha Wataalam mbalimbali wa Taasisi za Serikali wa Sekta hizo mbili za Mifugo na Uvuvi, Dkt. Madele amesema lengo la Kikao hicho ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji na usimamizi wa vipaumbele vya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027, na kusaidia kutoa mwelekeo na Mikakati ya pamoja ya utekelezaji wa vipaumbele hivyo. "Ni ma...
Picha
WATAALAM 155 WA WANYAMA WAPATIWA USAJILI  Na. Stanley Brayton, WMUV ◾ Vituo 69 kupewa Usajili katika Utoaji Huduma za Afya ya Wanyama. Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) limekamilisha mapitio kwa ajili ya kusajili Wataalam wa Wanyama wenye sifa stahiki, pamoja na Vituo mbalimbali vya kutoa Huduma za Afya ya Wanyama, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Sheria ya Veterinari SURA 319. Akizungumza katika Kikao cha 63 cha Baraza, leo Mei 23 2026 Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), ambaye  ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka amesema Baraza limepitia na kuridhia kuwapa usajili Wataalam wa Wanyama 155 na Vituo vya Utoaji Huduma za Wanyama 69, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo. “usajili huu umefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Veterinari SURA 319, pamoja na Kanuni mbalimbali na miongozo ambayo imeangalia uhalali na vigezo mbalimbali stahiki vya Wataalam” amesema Prof. Kusiluka Aidha, Prof. Kusiluka amewa...

TALIRI YAPONGEZWA KWA KUWEKEZA KWENYE UZALISHAJI WA MALISHO YA MIFUGO

Picha
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Fabian Madele ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa juhudi zake za kuwekeza katika uzalishaji wa malisho na mbegu bora za malisho ya mifugo, hatua aliyosema ni muhimu katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa malisho nchini. Dkt. Madele ametoa pongezi hizo leo Mei 22, 2026 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kituo cha West Kilimanjaro kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo. Akizungumza katika ziara hiyo, Dkt. Madele amesema sekta ya mifugo inaendelea kukabiliwa na changamoto ya upungufu wa malisho kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, hivyo uwekezaji unaofanywa na TALIRI ni hatua muhimu ya kuimarisha ufugaji wenye tija na kuongeza uzalishaji. Aidha, Dkt. Madele amewataka wataalamu wa TALIRI kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu mbinu bora za ufugaji wa kisasa i...

BWAWA LA LITA MILIONI 1.2 LAJENGWA TALIRI KUIMARISHA UZALISHAJI WA MALISHO YA MIFUGO

Picha
Katika jitihada za kuimarisha uzalishaji wa malisho ya mifugo na kuongeza uwezo wa wafugaji kukabiliana na athari za ukame, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Kanda ya Kaskazini imefanikiwa kujenga bwawa lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 1.2 za maji kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji katika eneo la shamba darasa la uzalishaji wa malisho ya mifugo. Mradi huo unatekelezwa kupitia programu ya kuwajengea uwezo wafugaji na kuimarisha mifumo ya ufugaji kwa familia za kifugaji sambamba na kuchangia uendelevu wa usalama wa chakula nchini. Bwawa hilo lina uwezo wa kuhakikisha upatikanaji wa maji ya uhakika kwa shughuli za umwagiliaji katika shamba darasa lenye ukubwa wa ekari moja kwa kipindi cha hadi miezi mitatu bila kujazwa tena. Hatua inatarajiwa kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa malisho hata katika vipindi vya ukame vinavyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi. Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta y...

DKT. BASHIRU ATAKA MKAKATI WA TASNIA YA KUKU UZINDULIWE NANE NANE 2026

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ameiagiza Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Watendaji wake kuhakikisha inakamilisha uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kuendeleza Tasnia ya Kuku nchini na kuuzindua mkakati huo wakati wa Maonesho ya Nane Nane ya Mwaka huu 2026. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo wakati  akifungua rasmi Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Wadau kuhusu Kilimo cha Mikataba, Uwezeshaji wa Fedha kwa Wakulima na Maendeleo ya Vyama vya Wakulima uliofanyika jijini Dodoma leo Mei 22, 2026 ambapo ameeleza kuwa kukamilishwa na kuzinduliwa kwa mkakati huo kutasaidia kuirasimisha tasnia ya kuku ambayo ina mchango mkubwa kwa uchumi na usalama. "Tatizo Kubwa tulilonalo pamoja na sekta hii kuwa kubwa, ni sekta  ambayo haijarasimishwa wala kupewa hadhi inayostahili, ndio maana ndani ya wizara tunaandaa Mkakati wa Kitaifa wa Maendeleo ya sekta ya Kuku, Napenda kuelekeza Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wataalam wenzake nahitaji...

DKT. BASHIRU AAGIZA KUFANYIKA TATHMINI MIUNDOMBINU YA KUFUGIA SAMAKI - NANE NANE

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amemwagiza Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji kufanya tathmini ya miundombinu ya kufugia samaki kutoka kwa Mwekezaji Hawa Fish Farm ili eneo hilo litumike kwa ajili ya Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT Uvuvi). Balozi Dkt. Bashiru ametoa agizo hilo leo Mei 21, 2026 wakati alipotembelea na kukagua Mabwawa ya Kufugia Samaki ya  Mwekezaji Hawa Fish Farm yaliyopo Viwanja vya Nane Nane vya John Malecela jijini Dodoma, ambapo mwekezaji huyo amesema anaondoka na kwenda kuwekeza sehemu nyingine. "Hatuwezi kuendesha shughuli za kiserikali zinazohusu watu bila kuwa karibu nao na kurahisisha mawasiliano, Nataka maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Viumbe maji kwa nini tumechelewa kumpa majibu mwekezaji huyu kutokana na mapendekezo yake?, Pia ifanyike tathmini ya miundombinu  hii kama inafaa kwa shughuli gani? amesema Balozi Dkt. Bashiru. Aidha, Balozi Dkt. Bashiru ameongeza kwa kuitaka idara hiyo kuja na wazo mbadala la...

DKT. MADELE AAGIZA UJENZI WA SOKO LA SAMAKI KIPUMBWI, PANGANI KUKAMILIKA KWA VIWANGO

Picha
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Fabian Madele, amemtaka mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Ujenzi wa Soko la Samaki Kipumbwi kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa huku ukizingatia viwango vya ubora vinavyokidhi mahitaji ya soko la kisasa. Dkt. Madele ametoa maelekezo hayo leo Mei 21, 2026 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa katika eneo la Kipumbwi, Wilaya ya Pangani mkoani Tanga. Mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 30, 2026. Amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya kisasa ya sekta ya uvuvi kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza ajira pamoja na kuinua uchumi wa wananchi wanaotegemea shughuli za uvuvi na biashara ya samaki. Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji, mradi huo umefikia asilimia 52 ya utekelezaji ukiwa na gharama ya jumla ya shilingi bilioni 1.34 hadi kukamilika kwake ukihusisha uj...

DKT. MADELE ASISITIZA TAASISI ZA MIFUGO KUWAPA WAFUGAJI SULUHISHO LA KISASA NA LENYE TIJA

Picha
“Tunayo kazi kubwa ya kuhakikisha wafugaji wanapata majawabu ya changamoto zinazowakabili katika sekta ya mifugo. Matarajio yao makubwa ni kuona wanapata mbari bora za mifugo, mbegu bora za malisho pamoja na huduma bora za afya ya mifugo.” Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Fabian Madele, wakati wa kikao chake na watumishi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kilichofanyika leo Mei 20, 2026 katika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) jijini Tanga. Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na TALIRI, Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (LITA) pamoja na Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA). Katika hotuba yake, Dkt. Madele amesema sekta ya mifugo ina nafasi kubwa katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa, hivyo ni muhimu kwa taasisi zote za wizara kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na mshikamano ili kuhakikisha wafugaji wanapata teknolojia sahihi za ufugaji kwa wakati. Amesema upati...

TALIRI YATAKIWA KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA KWA MAENDELEO YA SEKTA YA MIFUGO

Picha
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Fabian Madele ameielekeza Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kuongeza nguvu katika kufanya tafiti zinazolenga kutatua changamoto halisi za wafugaji ili kuchochea maendeleo ya sekta ya mifugo na kuongeza tija nchini. Dkt. Madele ametoa maelekezo hayo leo Mei 20, 2026 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kituo cha TALIRI Kanda ya Mashariki, ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa utekelezaji wa majukumu ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Katika ziara hiyo, Dkt. Madele amesema tafiti zinazofanywa na TALIRI zinapaswa kuendana na mahitaji ya sasa ya wafugaji pamoja na mabadiliko ya sekta ya mifugo, huku akisisitiza umuhimu wa kutumia tafiti hizo kama nyenzo ya kuongeza uzalishaji, kuboresha afya za mifugo na kuinua uchumi wa wafugaji. Aidha, ameiagiza taasisi hiyo kuongeza kasi ya usambazaji wa teknolojia bora za mifugo zilizoibuliwa na watafiti wake, ikiwemo uendelezaji wa mbari bora...

DKT. BASHIRU AIPONGEZA “INADES” MAADHIMISHO YA SIKU YA PUNDA

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amelipongeza shirika lisilo la Serikali la “INADES” kwa kufanikisha maadhimisho ya kitaifa ya Punda yaliyofanyika Mei 08,2026 mkoani Geita. Balozi Dkt. Bashiru ametoa pongezi hizo Mei 20,2026 mara baada ya kutembelewa ofisini kwake na Mkurugenzi wa shirika hilo Bi. Jacqueline Nicodemus ambaye alifika kwa kwa lengo la kuwasilisha fupi ya utekelezaji wa maadhimisho hayo. “Yapo makundi ya watu yanajifunika kwenye blanketi la kuwahudumia wananchi ila baada ya muda unakuta wapo kwenye mgongano wa kimaslahi baina yao na Serikali hivyo tunapopata wadau mnaotusaidia kweli tunafarijika sana” ameongeza Balozi Dkt. Bashiru. Aidha Balozi Dkt. Bashiru amelitaka shirika hilo kwa kushirikiana na ofisi yake kutafsiri mwongozo wa ustawi wa mnyama huyo kwa lugha ya kiswahili ili iwe rahisi kueleweka na watu wengi zaidi tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo mwongozo huo umeandaliwa kwa lugha ya kiingereza pekee. Kwa upande wake Mkurugenzi wa sh...

DKT. MADELE AITAKA NARCO KUONGEZA UBUNIFU WA UZALISHAJI KIBIASHARA

Picha
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Fabian Madele, ameiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kuongeza ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kibiashara ili kuimarisha mchango wa sekta ya mifugo katika uchumi wa nchi. Dkt. Madele ametoa agizo hilo leo Mei 19, 2026 alipofanya ziara katika Ranchi ya Mzeri Hill iliyopo katika Wilaya za Handeni na Korogwe mkoani Tanga kwa lengo la kukagua shughuli za uzalishaji na maendeleo ya ranchi hiyo. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kusisitiza matumizi ya sayansi na teknolojia katika sekta ya mifugo ili kuyafikia matarajio ya wafugaji pamoja na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya Taifa. Aidha, ameitaka NARCO kuongeza uzalishaji wa malisho ya mifugo ili kuhakikisha upatikanaji wa malisho bora na ya kutosha kwa mifugo katika nyakati zote za mwaka, hatua ambayo itasaidia kuongeza uzalishaji wenye tija na kuh...

DKT. MADELE AITAKA TALIRI KUONGEZA UZALISHAJI WA MALISHO KUKABILIANA NA KIANGAZI

Picha
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Fabian Madele, ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kuongeza juhudi za uzalishaji na uhifadhi wa malisho ya mifugo ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa malisho kipindi cha kiangazi. Dkt. Madele ametoa maelekezo hayo leo Mei 19, 2026 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kituo cha TALIRI Kanda ya Mashariki kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali za utafiti na maendeleo zinazotekelezwa na taasisi hiyo. Amesema upatikanaji wa malisho bora na ya kutosha ni msingi muhimu wa kuongeza tija katika sekta ya mifugo, hivyo ni muhimu TALIRI kuendelea kufanya tafiti na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa za uzalishaji wa malisho ili kuwasaidia wafugaji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. “Ni muhimu kuhakikisha kuwa kunakuwa na mkakati wa kudumu wa uzalishaji na uhifadhi wa malisho ili wafugaji wasiendelee kuathirika kila kipindi cha ukame. Tafiti zinazofanywa hapa...

SERIKALI KUIMARISHA MINADA YA KIMATAIFA YA MIFUGO NCHINI

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha na kuimarisha Minada ya Kimataifa ya Mifugo katika maeneo ya kimkakati nchini, ikiwemo Jimbo la Tarime Vijijini mkoani Mara, kwa lengo la kukuza biashara ya mifugo na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wafugaji na wafanyabiashara. Kauli hiyo imetolewa leo Mei 18, 2026, Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini, Mhe. Mwita Mwikabe Waitara, ambaye alihoji ni lini Serikali itaanzisha Minada ya Kimataifa ya Mifugo katika jimbo hilo. “Serikali inatambua umuhimu wa kuboresha minada hiyo kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya mifugo katika eneo la Tarime Vijijini pamoja na ukaribu wake na mipaka ya nchi jirani, hali inayotoa fursa kubwa za biashara ya mifugo ndani na nje ya nchi.” Alisema Balozi Dkt. Bashiru. Aidha, Dkt. Bashiru aliongeza kuwa  Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara ya m...

SERIKALI KUANDAA MWONGOZO WA KURAHISISHA UWEKEZAJI SEKTA YA UVUVI NCHINI

Picha
Serikali imeanza mchakato wa kuandaa Mwongozo ambao utaainisha fursa mbalimbali ili kurahisisha Uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi kwa lengo la kuongeza tija katika Sekta hiyo. Akizungumza leo May 16, 2026 Jijini Dodoma kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa Kikao kilichojumuisha Wataalam wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, ikiwemo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mkurugenzi Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (DRTE), Bw. Samwel Mdachi amesema kikao kazi hicho ni cha kuandaa Mwongozo wa fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Uvuvi nchini. "lengo kuu la kikao hiki ni kuandaa nyenzo itakayosaidia kutangaza na kuelezea kwa kina fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Uvuvi na uchumi wa Buluu nchini." amesema Ndg. Mdachi Aidha, Ndg. Mdachi amebainisha kuwa Mwongozo huo unatarajiwa kuwa dira muhimu kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, kwa kuwa utaonesha maeneo yenye fursa, aina za uwekezaji zinazo...

SERIKALI, BENKI YA DUNIA ZAJADILI KUIMARISHA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bashiru Ally Kakurwa, amekutana na Mkurugenzi wa Kanda wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Sekta ya Mazingira kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Anna Wellenstein, na kufanya mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo katika kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi nchini. Mazungumzo hayo ni sehemu ya ziara ya ujumbe wa Benki ya Dunia nchini Tanzania iliyoanza leo Mei 11 hadi 13, 2026, ikiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo katika sekta za maji, kilimo na mazingira. Majadiliano hayo yamejikita katika kutathmini utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, ikiwemo Mradi wa Kukuza Usimamizi Endelevu wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Bahari Tanzania (TASFAM), pamoja na kubaini maeneo mapya ya ushirikiano yatakayochangia maendeleo endelevu ya wananchi na ukuaji wa uchumi wa Taifa. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma, Bi. Wellens...

SERIKALI YAKABIDHI MITAJI KWA VIJANA 47 WA BBT- UVUVI KAGERA

Picha
Na. Fausta Njelekela  Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Erasto Sima ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, amesema Serikali itaendelea kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia Sekta ya Uvuvi ili kukabiliana na changamoto ya ajira nchini. Mhe. Sima  amesema hayo Mei 9, 2026 katika hafla ya kukabidhi mitaji kwa njia ya mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana 47 walionufaika na Programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT–Uvuvi) iliyofanyika Katika Mwalo wa Bilolo Kemondo Bukoba.  “Programu hii inalenga kutoa mafunzo kwa vitendo pamoja na mitaji ili kuwawezesha vijana kujiajiri na kuwa wawekezaji katika Sekta ya Uvuvi,” amesema Mhe. Sima Aidha, Mhe. Sima amesema kuwa hafla hiyo ni mwendelezo wa ugawaji wa mitaji uliozinduliwa Machi 7, 2026 katika eneo la FETA Nyegezi mkoani Mwanza, ambapo vijana 55 walikabidhiwa pembejeo mbalimbali za ufugaji wa samaki kwa vizimba. Mhe. Sima amewataka wanufaika hao kutumia fursa waliyopewa kwa uwajibikaji, nidhamu na uadilifu ili kuhakikisha miradi...