SERIKALI, BENKI YA DUNIA ZAJADILI KUIMARISHA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Bashiru Ally Kakurwa, amekutana na Mkurugenzi wa Kanda wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Sekta ya Mazingira kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, Bi. Anna Wellenstein, na kufanya mazungumzo yaliyolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo katika kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi nchini.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya ziara ya ujumbe wa Benki ya Dunia nchini Tanzania iliyoanza leo Mei 11 hadi 13, 2026, ikiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo katika sekta za maji, kilimo na mazingira.

Majadiliano hayo yamejikita katika kutathmini utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Benki ya Dunia, ikiwemo Mradi wa Kukuza Usimamizi Endelevu wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Bahari Tanzania (TASFAM), pamoja na kubaini maeneo mapya ya ushirikiano yatakayochangia maendeleo endelevu ya wananchi na ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma, Bi. Wellenstein aliambatana na viongozi kutoka Benki ya Dunia, akiwemo Mkurugenzi wa Sekta ya Maji, huku Kwa upande wa Serikali, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena, Naibu Katibu Mkuu (Mifugo), Dkt. Fabian Madele, pamoja na watendaji mbalimbali wa Wizara.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa alipokuwa akizungumza na Benki ya Dunia kuhusu kuimarisha wa Sekta za mifugo na uvuvi, ikiwa ni sehemu ya ziara ya ujumbe wa Benki hiyo nchini Tanzania iliyoanza leo Mei 11 hadi 13, 2026.

Mkurugenzi wa Kanda wa Benki ya Dunia kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini anayeshughulikia sekta ya Mazingira Bi. Anna Wellenstein akieleza jinsi Benki ya Dunia ilivyojipanga kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika sekta za Kilimo, Maji na Mazingira wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa leo Mei 11 hadi 13, 2026 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa kwanza kulia) alisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kanda wa Benki ya Dunia katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini anayeshughulikia Sekta ya Mazingira Bi. Anna Wellenstein (watatu kushoto) kuhusu kuimarisha wa Sekta za mifugo na uvuvi, wakati wa mazungumzo leo Mei 11 hadi 13, 2026.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (katikati), Mkurugenzi wa Kanda wa Benki ya Dunia  ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini anayeshughulikia Sekta ya Mazingira Anna Wellenstein (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Agnes Meena wakiwa kwenye Picha ya Pamoja baada ya mazungumzo  leo Mei 11 hadi 13, 2026.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (katikati), Mkurugenzi wa Kanda wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Sekta ya Mazingira katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini Bi. Anna Wellenstein (kushoto, waliokaa) na Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Agnes Meena wakiwa kwenye Picha ya Pamoja baada ya mazungumzo  leo Mei 11 hadi 13, 2026. Wengine kwenye picha hiyo ni wataalam wa wizara na Benki ya Dunia.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO