Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akisaini Kitabu cha Maomboleza ya
aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kilimanjaro (RAS) Bw.Tixon Tuyangine Nzunda
jana tarehe 21 Juni, 2024 nyumbani kwake Goba, Dar es Salaam.
Jumamosi, 22 Juni 2024
PROF. SHEMDOE ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA ALIYEKUWA KATIBU TAWALA WA MKOA WA KILIMANJARO NDUGU TIXON NZUNDA
Ijumaa, 31 Mei 2024
MRADI WA MAZIWA FAIDA KUBORESHA MIUNDOMBINU MBALIMBALI
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe akishuhudiwa na Balozi Ireland Tanzania
Mhe. Mary O’Neill amezindua miundombinu iliyojengwa kupitia mradi wa maziwa
faida unaotekelezwa na kituo cha TALIRI Tanga kwa udhamini wa ubalozi wa Ireland
chini ya Taasisi ya Teagacs.
Akiongea katika uzinduzi
huo Shemdoe amesema Mradi wa maziwa faida mbali na kuboresha miundombinu
mbalimbali lakini pia umekiwezesha kituo hicho kupata vifaa bora vya maabara
kwa ajili ya kufanyia tafiti mbalimbali za mifugo na malisho bora.
Shemdoe ameendelea kueleza
kuwa lengo la mradi wa maziwa faida ambao umegharimu zaidi ya Bilioni 7 ni
kuboresha mnyororo wa thamani wa maziwa kwa wafugaji ambapo kituo cha TALIRI
Tanga kimekuwa kikiendelea kutoa mafunzo kwa vitendo juu ya ufugaji wenye tija
sambamba na kufanya tafiti mbalimbali za mifugo.
Sambamba na hayo, Shemdoe
ametoa wito kwa jamii kuendelea kuzalisha na kutumia maziwa kwa wingi kwani
tafiti zinaonesha kuwa watanzania tunapaswa kutumia lita 200 za maziwa kwa
mwaka lakini ni kiasi cha lita 50 pekee kinatumika kwa kunywa kwa mwaka kwa
watanzania wote.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) Prof. Erick Komba
akimshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha
mahusiano ya kidemokrasia yaliyopelekea uwepo wa mradi huu muhimu kwa Taifa
wenye kuongeza tija kwa wafugaji amesema TALIRI imejipanga vyema kuhakikisha
mradi wa maziwa faida unaleta manufaa kwa wafugaji na watumiaji wa mazao ya
mifugo.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Kanda ya Mashariki, TALIRI Tanga Dkt. Zabroni Nziku akielezea mafanikio ya
mradi wa maziwa faida amesema Kituo cha TALIRI Tanga kimefanikiwa kutathmini na
kujua aina ya malisho bora, kuendelea kufanya tafiti za kupata ng’ombe bora,
kuanzisha shamba la mfano la malisho, kuwajengea uwezo watafiti, maafisa ugani
na wafugaji ambapo wadau zaidi ya 1000 wamefikiwa na kupatiwa elimu ya ufugaji
bora.
Nae balozi wa Ireland
Tanzania Mhe. Mary O’Neill ameipongeza TALIRI Tanga kwa namna inavyoendesha
mradi huo na kuweza kufikia wadau wengi hususani wafugaji kitendo ambacho
kimeleta mabadiliko makubwa kwa wafugaji hao juu ya ufugaji wenye tija.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa kwanza kulia) jana tarehe 29/05/2024 akiwa na Viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa wa Tanga pamoja na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, amezindua Miondombinu ya majengo na vifaa vya maabara kwenye mradi wa Maziwa Faida Katika Kampasi ya TALIRI mkoani Tanga,
Alhamisi, 30 Mei 2024
MNADA WA MHUNZE KUFANYIWA UTAFITI WA KINA UWEPO WA TOPE MAJI - PROF. MUSHI
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza mchakato wa kufanya Utafiti wa kina juu ya chanzo cha tope maji yatokayo katika ardhi ndani ya mnada wa Mhunze Wilayani Kishapu ikiwa ni njia mojawapo ya kujua athari zinazoweza kujitokeza kutokana na uwepo wa hali hiyo katika eneo la ujenzi ambao unaendelea katika Mnada huo ili kuweza kutafuta suluhisho. Hii ni kufuatia hali hii kuleta taharuki kwa wafugaji na wauzaji wa mifugo kwenye mnada huo.
Akizungumza, leo Mei 29,
2024 Wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga wakati akienda kukagua hali ya eneo la
mnada wa Mhunze, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof.
Daniel Mushi amesema Wizara imeamua kufanya Utafiti wa kina ili kujiridhisha
kama hali ya mnada wa Mhunze ni salama na kukabiliana na uwepo wa tope kwa
ajili ya kuhakikisha usalama wa watu na mifugo kwenye mnada huo.
"Leo tumekuja na
wataalam kutoka Taasisi ya madini Tanzania kwa ajili ya kupima kilichotokea na
kutupa taarifa, ambapo mpaka sasa wameshafanya uchunguzi wa awali na
wametueleza kisayansi ni kitu gani kina sababisha matope haya na kutuhakikishia
kwamba mradi wa ujenzi wa ukuta unaozunguka eneo hili na maboresho mengine
yanaweza kuendelea", amesema Prof. Mushi.
Aidha, Prof. Mushi alisema
Wataalamu watakapofanya uchunguzi wa kina wataeleza namna ya kukabiliana na
suala hili ili yasijitokeze madhara na wataalamu wameihakikishia Wizara kuwa
hakuna madhara yanayoweza kusababisha maafa katika mnada huo wa Mhunze.
Kwa upande wake, Mkuu wa
Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Mkude amesema mbali na utafiti huo lakini pia
yapo marekebisho na maboresho yanayotarajiwa kufanywa kwenye eneo hilo la mnada
na maeneo ya pembezoni ili kujihakikishia usalama wa wananchi na mifugo.
Vilevile Mhe. Mkude
ameishukuru sana Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuja kwa wakati na watafiti ili
kufanya utafiti baada ya kusikia jambo
hili la kufurika kwa tope katika mnada wa Mhunze.
Akitoa ufafanuzi juu ya
suala hilo la kufurika kwa tope katika mnada wa Mhunze, Mjiolojia kutoka
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini Tanzania, Bw. Sudian Chilagwile
amesema, sababu iliyofanya waitwe na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuja kufanya
uchunguzi kwenye eneo la mnada wa Mhunze ni uwepo wa chemchem ya maji tope na udongo uliojaa
matope ukitoka chini ya ardhi.
Bw. Chilagwile, ameweka bayana kuwa wao kama watafiti watafanya kazi ya Utafiti katika eneo hilo la mnada ili kubaini chanzo, japo utafiti wa awali wa kisayansi unaonyesha sababu ya yote ni uwepo wa mvua nyingi ambazo zimeleta athari katika miamba iliyopo aridhini ambayo imesababisha uwepo wa tope hilo, na kubainisha kuwa jambo hili haliwezi kuathiri shughuli za mnada huo kuendelea, ila watatoa ushauri kwa Wizara na wakandarasi juu ya ukarabati wa eneo hilo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Daniel Mushi, akizungumza katika kikao kifupi na Mkuu wa
Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Mkude (hayupo pichani), baada ya kufika Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, kwa ajili ya kujitambulisha na kuelezea nia na
dhumuni la kufika kwake na ujio wake na Timu ya maafisa toka Wizara ya Mifugo
na Uvuvi pamoja na wanajiolojia kwa ajili ya kufanya Utafiti juu ya uwepo wa
tope maji katika mnada wa Mhunze, kikao kimefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Kishapu, leo Mei 29, 2024, Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Prof. Daniel Mushi (katikati), akimuahidi Mkuu wa Wilaya ya
Kishapu, Mhe. Joseph Mkude (kushoto), kushirikiana nae bega kwa bega katika
kutatua changamoto iliyopo na kufuata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa watafiti,
wakati alipofika katika mnada wa Mhunze Wilayani Kishapu kujionea hali ilivyo,
leo Mei 29, 2024, Shinyanga.
Pichani ni sehemu eneo la
mnada wa Mhunze lililo athiriwa na tope maji, Wilayani Kishapu - Shinyanga
VIJANA WATENGEWA BIL. 10.5 KWA AJILI YA MIRADI
Serikali kupitia Wizara ya
Mifugo na Uvuvi imetenga zaidi ya Shilingi Bilioni 10.5 kwa ajili ya mitaji ya
miradi ya vijana ili kuwainua kiuchumi.
Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi amebainisha
hayo (24.05.2024) jijini Mwanza, wakati wa kuhitimisha mafunzo kwa vitendo ya
uvuvi na ukuzaji viumbe maji awamu ya pili kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyo
Bora (BBT – LIFE) ambayo imewejenga katika kujiajiri kupitia Sekta ya Uvuvi.
Mhe. Katambi amempongeza
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) pamoja na viongozi wengine
wa wizara kwa kusimamia vyema maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza ajira kwa vijana kupitia sekta za
mifugo na uvuvi.
Ameongeza kuwa ni wakati
sasa kwa vijana kutumia vyema fursa zitokanazo na sekta hizo ili kujipatia
ajira na utajiri pamoja na kufuga kisasa na kuuza mazao ya mifugo na uvuvi
yakiwa katika ubora unaotakiwa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amesema zaidi ya vijana 300
wamenufaika kupitia mafunzo hayo ya miezi mitatu kupitia vituo mbalimbali.
Prof. Shemdoe ameongeza
kuwa lango la mafunzo hayo ni kuwezesha vijana kuwa wajisiriamali na wawekezaji
kwenye shughuli za uvuvi na ukuzaji viumbe maji kwa kuwajengea ujuzi
utakaowawezesha kubuni miradi na kuanzisha vikundi au kampuni ili waweze
kujiajiri na kutoa fursa za ajira kwa wenzao.
Amebainisha kuwa awamu ya
pili ya wigo wa mafunzo hayo imeongezeka tofauti ya awamu ya kwanza ambapo
yalipokelewa maombi zaidi ya 1,200 ambapo inaashiria vijana wana ari ya
kujiunga katika mafunzo hayo ya vitendo ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi na
Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) zinahitaji kuweka
nguvu zaidi katika kuwawezesha vijana kujiajiri.
Kwa upande wake mmoja wa
wanufaika wa BBT – LIFE akisoma risala kwa niaba ya vijana wenzake Bw. Muhsin
Mussa amesema katika mafunzo hayo wamejifunza namna ya utunzaji wa fedha,
kuunda na kusajili vikundi, maandiko ya miradi na namna ya kuiendesha pamoja na
mafunzo ya vitendo kwa vijana wa Tanzania Bara na Visiwani.
Aidha, amesema mafunzo hayo
wanaamini yataenda kupunguza wingi wa vijana wasio na ajira ambapo sasa
wataweza kujishughulisha na uvuvi pamoja na ukuzaji viumbe maji kibiashara.
Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi (mwenye tai
nyekundu) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe
(kulia kwake) wakiangalia moja ya vizimba vya kufugia samaki, wakati wa
kuhitimisha mafunzo kwa vitendo ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji awamu ya pili
jijini Mwanza kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT – LIFE).
(24.05.2024)
Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi (mwenye tai
nyekundu) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe
(kulia kwake) wakiangalia moja ya vizimba vyenye uwezo wa kufuga samaki
takriban 100 na kisichogharimu zaidi ya Shilingi Laki Moja kwa ajili ya
matengenezo yake, wakati wa kuhitimisha mafunzo kwa vitendo ya uvuvi na ukuzaji
viumbe maji awamu ya pili jijini Mwanza kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyo
Bora (BBT – LIFE). (24.05.2024)
WAVUVI WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA KUKABILIANA NA UPOTEVU WA MAZAO YA UVUVI
Naibu Katibu Mkuu Sekta ya
Uvuvi Dkt. Edwin Mhede amewataka wadau wa uvuvi kuhakikisha wanatumia
teknolojia za kisasa ambazo ni rahisi zitakazowezesha kukabiliana na changamoto
ya upotevu wa mazao ya Uvuvi.
Ameyasema hayo Mei 28, 2024
wakati akifungua mkutano wa Uzinduzi wa mradi wa Asia -Africa BlueTech
Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7 (2024-2030) wenye lengo la
kusaidia juhudi za Serikali katika kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi.
Mkutano huo ambao
umezikutanisha nchi nne Afrika, Dkt. Edwin Mhede amesema wamejielekeza
kuhakikisha wanufaika wa mradi huo wanakuwa ni wavuvi wenyewe.
Pia amesema eneo ambalo
wanalifanyia kazi kwa kushirikiana na Worldfish pamoja na Taasisi za ndani ni kuhakikisha wanakabiliana na changamoto za
upotevu wa mazao ya uvuvi, pamoja na uharibifu mbalimbali unaojitokeza kwenye
mnyororo wa thamani wakati watu wakivua, wakisafirisha, wakiuza na kununua
samaki.
"Katika kutathimini
fikra mpya za nini kifanyike zaidi ya hiki, tumejielekeza kuyagusa matatizo ya
wavuvi na kujielekeza katika kufanya hivyo kuhakikisha kwamba mradi huu
wanaofaidika ni wavuvi wenyewe"
"Ni matumaini yangu baada ya siku kadhaa tutakuja kuwa na kitu kikubwa sana kuweza kutusaidia kuyafikia maisha ya wengi ambayo ndiyo maelekezo lakini pia ndiyo maono ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunaenda kuyakuta mahitaji ya watu na tunayafanyia kazi" amesema
Dkt. Mhede amesema
changamoto nyingine zinazowakabili wavuvi hao, ni pamoja na uduni wa Teknolojia
, upatikanaji masoko, upatikanaji wa mitaji ya kifedha na maarifa lakini pia
miundombinu
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Sheikh, amesema Afrika
ikiwemo Tanzania kunatatizo kubwa la upotevu wa mazao ya uvuvi ambapo inakisiwa
kati ya asilimia 30-40 ya upotevu wa mazao hayo yanatokana na mabadiliko ya
tabianchi
"Katika kipindi cha
mvua inakua ni changamoto kubwa kwa wavuvi wetu hasa wale ambao wanachataka na
wanasafirisha mfano, wavuvi wa dagaa wanavua na kuchakata, wanahitaji pia
teknolojia mpya kwa ajili ya kusafirisha mazao yao ya uvuvi" amesema Prof.
Sheikh.
Prof. Sheikh amesema
Serikali ya awamu ya sita imeendelea na jitihada za kuhakikisha wanaongeza
uzalishaji wa mazao hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuweka mbinu bora ambazo
zitawasaidia wavuvi kuweza kuhifadhi mazao yao ambayo yatakubalika ndani na nje
ya nchi.
Naye Kiongozi wa
Mawasiliano ya Kimataifa wa Taasisi ya WorldFish, Rajita Majumdar amesema kuwa
zaidi ya tani 21.3 za samaki zimepotea kutokana na changamoto ya uhifadhi wa
mazao hayo baada ya kuvuliwa ambapo wameona ni vyema kuja nchini kuungana
na Serikali na wavuvi kwa lengo la
kupunguza upotevu huo ambao unafifisha uchumi.
"Nadhani inahitajika
matumizi ya teknolojia nafuu inayoweza kufikiwa ili kuongeza umahiri katika
kushughulikia mnyororo wa usambazaji wa chakula ambapo itasaidia kuondokana na
uharibifu mkubwa"amesema
Aditya Parmar ambaye
ametoka kwenye Taasisi ya WorldFish, amesema mradi huo umejikita katika vipengele vinne ambavyo ni usambazaji wa samaki, uuzaji, utunzaji,
uhifadhi na usafirishaji ambapo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutunza thamani ya
ubora wa chakula kwa lengo la kuhakikisha lishe bora kwa jamii ya Pwani.
"Tunataka kuona
jumuiya ya Pwani jinsi gani inaweza kuongeza mapato, tunataka kushirikisha
wanawake na vijana kutekeleza mradi huu ambao tunatarajia utabadilisha maisha
yao baada ya miaka michache ijayo "amesema
Mkutano huo unafuatiwa na mkutano ambao utafanyika Tarehe 5-7 mwezi Juni mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano Mlimani city Jijini Dar es Salaam ambao unazungumzia mahsusi wavuvi wadogo wanaochangia kwa asilimia 95.
Naibu katibu Mkuu Sekta ya
Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede akiongea wakati wa kufungua mkutano wa uzinduzi wa mradi wa Asia -Africa BlueTech
Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7
wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika upotevu wa mazao ya uvuvi., Mkutano huo
umefanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Ramada jijini Dar es Salaam Mei 28,2024
Mkurugenzi wa Uvuvi kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohamed Sheikh akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Asia -Africa BlueTech
Superhighway ambao utachukua takribani miaka 7
wenye lengo la kusaidia juhudi za serikali katika upotevu wa mazao ya uvuvi., Mkutano huo
umefanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Ramada jijini Dar es Salaam Mei 28,2024
Mwakilishi kutoka kwenye
Taasisi ya WorldFish Bw. Aditya Parmar akiwasilisha mada wakati wa mkutano wa
uzinduzi wa mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway na kuelezea vipengele vinne ambavyo mradi
huo umejikita ikiwa ni pamoja na usambazaji wa samaki, uuzaji, utunzaji,
uhifadhi na usafirishaji ambapo itasaidia kwa kiasi kikubwa kutunza thamani ya
ubora wa chakula kwa lengo la kuhakikisha lishe bora kwa jamii, Mei 28,2024
jijini Dar es salaam.
Naibu katibu Mkuu Sekta ya
Uvuvi Dkt. Edwin Mhede akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wadau wa Sekta
ya Uvuvi walioudhuria mkutano wa
uzinduzi wa mradi wa Asia -Africa BlueTech Superhighway ambao utachukua
takribani miaka 7 wenye lengo la
kusaidia juhudi za serikali katika
upotevu wa mazao ya uvuvi., Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa
hotel ya Ramada jijini Dar es Salaam Mei 28,2024
VIJANA WA BBT – LIFE WAONESHWA VITALU, RAIS SAMIA ATAJWA KWA MCHANGO WAKE MKUBWA KWENYE SEKTA YA MIFUGO
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka historia ya kutafsiri ndoto
halisi ya wingi wa mifugo nchini katika kubadilisha mfumo wa maisha kwa
watanzania kupitia sekta hiyo.
Akizungumza (21.05.2024)
wakati wa hafla fupi ya kuwaonesha vijana wanaohitimu mafunzo ya unenepeshaji
mifugo kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT – LIFE), inayosimamiwa
na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, vitalu watakavyopatiwa kwa ajili ya ufugaji
katika Ranchi za Kagoma na Kitengule zinazosimamaiwa na Kampuni ya Ranchi za
Taifa (NARCO), Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe. Julius Laizer amesema Mhe. Rais
ameweza kuirasimisha rasmi biashara ya mazao ya mifugo kwa kuwa Sekta ya Mifugo
ni muhimu katika maisha ya binadamu.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa
wa Kagera, Mhe. Laizer amesema ni vigumu kutenganisha biashara yoyote inayohusu
chakula cha binadamu isifanikiwe, hivyo kuwataka vijana wa BBT – LIFE kusimamia
vyema ndoto na maono ya Mhe. Rais kwa kuwa wapo sehemu sahihi katika kujifunza
na kufuga mifugo kibiashara.
Kwa upande wake Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Daniel Mushi amesema
wizara inawaangalia vijana hao kama waleta mapinduzi kwenye Sekta ya Mifugo
hivyo imeamua kuwaunganisha na baadhi ya benki zilizopo nchini kupata fursa za
mikopo.
Ameongeza kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alianzisha programu hiyo kwa kwa kuitambua Sekta ya Mifugo kama sekta rasmi na kuwaingiza vijana kwenye ufugaji na uvuvi wa kibiashara na kwamba kila mwaka takriban vijana 1,600 wanahitimu kwenye vyuo mbalimbali vya mifugo hivyo serikali imeona haiwezi kuwaacha bila ajira bali wajifunze ufugaji kibiashara.
Aidha, amesema Mhe. Rais
katika diplomasia ya kiuchumi amekuwa akizunguka nchi mbalimbali kutafuta
masoko ya mazao ya mifugo na uvuvi ambapo kwa sasa nchi inahitaji wawekezaji
wakubwa katika sekta hizo ili kuvipatia viwanda vilivyopo nchini mifugo kwa
ajili ya kuchakatwa na kuhudumia masoko ya kimataifa, ambapo pia vijana wa BBT
- LIFE wanatakiwa kuwa wawekezaji wakubwa katika Sekta ya Mifugo.
Pia, Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Bw. Bwire Mujarubi amesema kwa mujibu wa
mwongozo kampuni hiyo imepewa majukumu ya kutenga vitalu kwa vijana wa BBT -
LIFE, kupanga vijana hao kwenye vitalu, kuwapatia mikataba wafugaji katika ranchi
za NARCO na kuwa miongoni mwa wateja wa mifugo kutoka kwa vijana wa BBT - LIFE
watakaopatiwa vitalu katika ranchi hizo.
Amesema licha ya awamu ya
kwanza ya BBT - LIFE kuelekea mwishoni ifikapo Tarehe 30 Mwezi Juni mwaka huu,
NARCO itaendelea kuwalea vijana hao 161 ambapo kila mmoja atapatiwa hekari 10
bila kulipa gharama za upangaji katika kipindi cha miaka mitano kwenye ranchi
za Kagoma hekta 311 na Kitengule hekta 2,000 zilizopo Wilaya ya Karagwe Mkoani
Kagera.
Kwa upande wake Mtendaji
Mkuu wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) Dkt. Pius Mwambene amesema
kwa kipindi cha miaka miwili ambacho vijana wa BBT – LIFE wamekuwa wakipata
mafunzo katika wakala hiyo wamepata uzoefu mkubwa wa kuandaa miundombinu ya
mifugo pamoja na biashara ya mifugo.
Ameongeza kuwa vijana hao
wakianza rasmi ufugaji hawataangaika na kwamba watakuwa wakishirikiana na
wawekezaji wakubwa waliopo kwenye ranchi za NARCO, huku akibainisha kuwa wakati
wa mafunzo vijana hao wamekuwa wakiuza mifugo ndani ya nchi pamoja na nchi za jirani.
Pia, amesema amesema lengo
la programu hiyo ni kukuza ufugaji wa mifugo wenye tija kwa kuandaa vijana kuwa
wawekezaji wakubwa kwenye sekta hiyo na kwamba programu hiyo kwa sasa
itapelekwa kwenye ngazi za serikali za mikoa ili kuwanufaisha vijana wengi
zaidi.
Mmoja wa vijana
wanaonufaika na programu ya BBT - LIFE Bw. Posper Mugalula amesema wanashukuru
kwa kupata fursa ya kushiriki mafunzo ya unenepeshaji mifugo hususan ng’ombe
baada ya kumaliza elimu ya vyuo na wapo tayari kuingia rasmi katika ufugaji wa
kisasa baada ya kupatiwa vitalu kwenye ranchi za NARCO.
Amewaomba vijana wenzake kushirikiana ili kufikia malengo ambayo serikali imekusudia na kuwa chachu ya vijana wengine kujiunga na mafunzo kwa awamu ya pili na kufuga kibiashara kwa kuwa Sekta ya Mifugo ina soko kubwa ndani na nje ya nchi.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi
imekuwa ikiendesha mafunzo ya unenepeshaji mifugo katika vituo vya Wakala ya
Mifugo nchini (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo nchini (TALIRI) kupitia
Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT – LIFE) ili kufikia maono ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwawezesha
vijana kufanya ufugaji wenye tija katika sekta za mifugo na uvuvi.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa
wa Kagera, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Ranchi ya Kagoma iliyopo
Wilaya ya Karagwe mkoani humo ya kuwaonesha vijana wanaohitimu mafunzo ya
unenepeshaji mifugo kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT – LIFE),
baadhi ya maeneo watakayopatiwa kwa ajili ya vitalu vya kufugia mifugo, Mkuu wa
Wilaya ya Karagwe Mhe. Julius Laizer amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka historia ya kutafsiri ndoto
halisi ya wingi wa mifugo nchini katika kubadilisha mfumo wa maisha kwa
watanzania kupitia sekta hiyo. (21.05.2024)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Daniel Mushi akizungumza na kuwaonesha baadhi ya
vijana wanaohitimu mafunzo ya unenepeshaji mifugo awamu ya kwanza kupitia
Programu ya Jenga kesho Iliyo Bora (BBT – LIFE), vitalu watakavyogaiwa kufanya
ufugaji katika Ranchi za Kagoma na Kitengule ambazo ziko chini ya Kampuni ya
Ranchi za Taifa (NARCO) katika Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, ambapo katika
kipindi cha miaka mitano hawatatozwa malipo ya upangaji katika ranchi hizo.
(21.05.2024)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Daniel Mushi (mwenye kofia nyeusi) akizungumza
na baadhi ya wadau na vijana wanaohitimu mafunzo ya unenepeshaji mifugo awamu
ya kwanza kupitia Programu ya Jenga kesho Iliyo Bora (BBT – LIFE), wakati
vijana hao wakioneshwa vitalu watakavyogaiwa kufanya ufugaji katika Ranchi za
Kagoma na Kitengule ambazo ziko chini ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO)
katika Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, ambapo jumla ya vijana 161 watapatiwa
vitalu ambapo kila mmoja atapatiwa hekari 10. (21.05.2024)
WAKAGUZI MIFUGO, MAZAO YAKE WAPIGWA MSASA
Serikali kupitia Wizara ya
Mifugo na Uvuvi leo Mei 22, 2024 imeanza kutoa mafunzo ya siku 3 kwa Wakaguzi
wa mifugo na mazao yake waliopo kwenye vituo mbalimbali vya ukaguzi ikiwa ni
pamoja na vile vilivyopo kwenye mipaka yote nchini zoezi litakalofanyika mkoani
Morogoro.
Akifungua Mafunzo hayo
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini Dkt. Benezeth Lutege amewataka
wataalam hao mbali na kutumia vema taaluma zao, wazingatie weledi na watende
haki wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuomba
ushauri pale wanapopata changamoto.
“Tunapokuwa kule kwenye
vituo vyetu vya ukaguzi tunapaswa kujua sisi ndio sura ya Wizara kwa hiyo
tunavyowapokea wageni, tunavyoongea nao na tunavyotoa huduma zetu kuna athari
kubwa sana kwa viongozi wetu wanaotusimamia hivyo tunaweza kuwachafua au
kuwajengea sifa njema” Ameongeza Dkt. Lutege.
Aidha Dkt. Lutege ametoa
angalizo kwa vijana hao kuacha kutanguliza mbele maslahi yao wakati
wakitekeleza majukumu vituoni ili kuendelea kujenga dhana ya uaminifu na uadilifu
jambo litakalolinda taswira ya Wizara na Serikali kwa ujumla.
“Akifika Mteja umemkamata,
unatakiwa kumueleza makossa yake kwa moyo mweupe kabisa na kwa lugha stahiki
bila kutumia nguvu au lugha chafu kisha na yeye umpe nafasi akueleze sababu
zake na baada ya hapo upime kwa taaluma yako uone kama alichofanya ni kosa la
kukusudia au la ndipo ufanye maamuzi” Amesisitiza Dkt. Lutege.
Kwa Upande wake Mratibu
wa Mradi wa Mfumo wa Usalama wa Wanyama,
Mimea na Chakula ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia, Habari na
Mawasiliano kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Baltazar Kibola amesema kuwa
mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wataalam hao kufahamu kuhusu Afya ya wanyama na mazao yake kabla hawajatoa vibali
kupitia mfumo wa utoaji vibali vya Mifugo na Mzao yake kielektroniki (MIMIS).
Naye Mratibu wa Mradi huo
kutoka Shirika la “TradeMark Africa” ambao ndio wafadhili wakuu wa Mafunzo hayo
Bi. Kezia Mbwambo ameeleza kuwa Shirika lake liliona umuhimu wa wataalam hao
kujengewa uwezo kuhusu masuala ya usalama wa mifugo na mazao yake ili kulinda
afya za Mifugo na watumiaji wa mifugo hiyo kwa ujumla.
Akizungumza kwa niaba ya
wataalam wenzake, Afisa Mfawidhi wa kituo cha Ukaguzi wa Mifugo na Mazao yake
Wilaya ya Temeke Bi. Mwajuma Chaurembo amelishukuru Shirika hilo kwa kuwajengea
uwezo kupitia mafunzo hayo ambapo ameahidi kufanyia kazi kwa vitendo yote
watakayojifunza kwa siku zote tatu.
Mafunzo hayo yanafuatia
mafunzo ya awali yaliyodhaminiwa na Shirika la “TradeMark Afrika” na kuratibiwa
na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Kitego chake cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano ambayo
yalihusu mfumo wa utoaji wa Vibali vya Mifugo na Mazao yake kielektroniki
(MIMIS).
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma
za Mifugo nchini Dkt. Benezeth Lutege (kulia) akifungua mafunzo ya wakaguzi wa
Mifugo na Mazao yake vituoni na mipakani Mei 22, 2024 mkoani Morogoro. Katikati
ni Mratibu wa Mradi unaosimamia Mafunzo hayo kutoka Shirika la "Trade
Africa" Bi. Kezia Mbwambo na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Bw. Baltazar Kibola.
Pichani ni wakaguzi wa
Mifugo na Mazao yake vituoni na mipakani wakiwa kwenye Mafunzo yanayohusu afya
ya wanyama na mazao yake Mei 22, 2024 mkoani Morogoro.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma
za Mifugo nchini Dkt. Benezeth Lutege (wa nne kutoka kulia mbele) na baadhi ya
Viongozi na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakiwa kwenye picha ya
pamoja na wakaguzi wa Mifugo na mazao yake vituoni na mipakani mara baada ya
kufungua mafunzo kwa wakaguzi hao Mei 22, 2024 mkoani Morogoro.
TUPAZE SAUTI KUOKOA PUNDA-MNYETI
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amewataka wadau wote wanaosimamia ustawi na haki za
wanyama kukemea vikali vitendo vitakavyosababisha kutoweka kwa Punda ili
wanyama hao waendelee kuwasaidia wananchi katika shughuli mbalimbali za kijamii
na kiuchumi.
Mhe. Mnyeti ametoa rai hiyo
Mei 17, 2024 alipokuwa akifunga Maadhimisho ya siku ya Punda Afrika Mashariki
ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Dodoma yakitanguliwa na shughuli mbalimbali
ikiwemo mijadala iliyolenga kuchukua hatua mbalimbali za kunusuru kutoweka kwa
mnyama huyo.
“Punda wamekuwa wakifanya
kazi kubwa na muhimu sana katika sekta za kiuchumi ambapo katika shughuli za usafiri hivi sasa wamekuwa
wakitumika mpaka kubeba vifaa vya ujenzi na siku za hivi karibuni tumeshuhudia
wakibeba madini katika migodi mbalimali nchini” Ameongeza Mhe. Mnyeti.
Aidha Mhe. Mnyeti
amebainisha kuwa kutokana na umuhimu wa ngozi na viungo vingine vya mnyama huyo
ongezeko la uchinjaji wa wanyama hao lilikuwa kubwa hali iliyosababisha tishio
la kutoweka kwao Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.
“Serikali imechukua hatua
mbalimbali ili kudhibiti kutoweka kwa wanyama hawa ikiwa ni pamoja na kusitisha
shughuli za uchinjaji wake na biashara ya ngozi zake zilizokuwa zikiendeshwa
kwa leseni ya muda ya kampuni ya Fan-Hu kutoka China na kama tungekiacha
kiwanda hiki kiendelee kufanya kazi kwa miaka miwili basi kusingekuwa na punda
hata mmoja hapa nchini” Amesisitiza Mhe. Mnyeti.
Kwa upande wake Mtaalam wa
Mifugo na mmoja wa watetezi wa haki za Punda Dkt. Bedarn Masuruli ameipongeza
Serikali kwa hatua zake mbalimbali za kuhakikisha mnyama huyo hatoweki huku pia
akitoa rai kwa Serikali kuwazingatia wanyama hao katika Sera na Mipango
inayohusiana na Mifugo.
“Wadau wamepongeza hatua ya
Serikali kuungana na Taasisi zilizo chini ya Umoja wa Afrika kuandaa mkutano wa
kwanza wa Afrika kuhusu Punda uliozaa
azimio la Dar Es Salaam ambalo linasema “Punda Afrika Sasa na katika Siku
zijazo” Amesema Dkt. Masuruli.
Kwa upande wake Mkurugenzi
msaidizi wa Huduma za ukaguzi na ustawi wa wanyama kutoka Wizara ya Mifugo na
Uvuvi Dkt. Anette Kitambi ameitaka jamii kushirikiana na Serikali kuwalinda
Punda kwani mfumo wa uzazi ni tofauti na
wanyama wengine ambapo anaweza kuzaa mara moja au asizae kabisa na muda wake wa
kubeba mimba huwa ni kati ya miezi 12 hadi 14.
“Na maajabu mengine ya
punda kama akiona mazingira sio rafiki anaweza kuahirisha kuzaa hivyo ni mnyama
mwenye sifa za tofauti kabisa ukiinganisha na wengine na ndio maana kutokana na
umuhimu huo kati ya wanyama wote ni yeye tu ndo aliandaliwa siku yake kitaifa”
Amebainisha Dkt. Kitambi.
Maadhimisho ya Siku ya
Punda duniani hufanyika Mei 08 ya kila mwaka na kwa Afrika Mashariki huwa ni
Mei 17 huku Serikali, wataalam na wadau mbalimbali wakitumia siku hiyo kujadili
hatma ya mnyama huyo na ustawi wake kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti (katikati) akikata keki kuashiria miaka 90 ya
Shirika la kutetea haki za wanyama linaloitwa "BROOKE" wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Punda Afrika Mashariki Mei 17, 2024 jijini Dodoma,
Wanaoshuhudia Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Riziki Shemdoe na
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za ukaguzi na ustawi wa wanyama Dkt. Anette
Kitambi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wanyama (ASPA)
Bw. Livingstone Masija wakati wa maadhimisho ya Afrika Mashariki ya siku ya Punda yaliyofanyika jijini Dodoma Mei
17, 2024.
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na
wataalam na wadau mbalimbali wa kutetea haki za mnyama Punda wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya mnyama huyo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mei 17, 2024
jijini Dodoma.
warsha ya kujenga uelewa kwa wadau kuhusu mkakati wa kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi,
Mkurugenzi Msaidizi
anayesimamia uthibiti wa ubora na masoko ya mazao ya Uvuvi kutoka Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Bw. Stephen Lukanga (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha
ya pamoja na wadau wa uvuvi mara baada
ya kushiriki warsha ya kujenga uelewa kwa wadau hao kuhusu mkakati wa kupunguza
upotevu wa mazao ya uvuvi (MDS STATEGY) na kupitia mkakati wa masoko wa zao la
dagaa, Warsha hiyo imefanyika kwenye ukumbi hoteli ya Flomi mkoani Morogoro
Mei16, 2024
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Upendo Hamidu akichangia hoja wakati wa warsha ya
kujenga uelewa kwa wadau kuhusu mkakati wa kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi
na kupitia mkakati wa masoko wa zao la dagaa,
Mei 16,2024 mkoani Morogoro.
Mratibu wa Mradi
unaofadhiliwa na shirika la maendeleo la Norway kupitia Shirika la chakula na
kilimo (FAO) Bw. Joseph Lomba akieleza lengo la kufanya utafiti wa kutathmini
hali ya upotevu wa rasilimali ya uvuvi
aina ya dagaa wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa wadau kuhusu mkakati wa
kupunguza upotevu wa mazao hayo, warsha hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa hoteli
ya Flomi mkoani Morogoro, Mei 16,2024
4
Mtaalam elekezi wa Mradi wa
upunguzaji wa uaribifu wa dagaa nchini Bw. Yahaya Mgawe akiongoza warsha ya
kujenga uelewa kwa wadau kuhusu mkakati wa kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi,
warsha hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Flomi mkoani Morogoro, Mei 16,2024
Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia uthibiti wa ubora na masoko ya mazao ya uvuvi, Bw. Stephen Lukanga akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi wa warsha ya kujenga uelewa kwa wadau kuhusu mkakati wa kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi na kupitia mkakati wa masoko wa zao la dagaa mkoani Morogoro Mei 16,2024.
shughuli mbalimbali zilizofanyika kwenye Wiki ya Protini iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Mkoa wa Dodoma Mei 14, 2024.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela
Mhe. Anjelina Mabula (kushoto) akipata maelezo kuhusiana na matumizi mbalimbali
ya mazao ya Uvuvi yatokanayo na Samaki aina ya Jodar kutoka Mtaalam wa Utafiti
wa mazao hayo wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Bi. Siwema Luvanda
alipotembelea Mabanda ya maonesho ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujionea
shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye Wiki ya Protini iliyofanyika kwenye
viwanja vya Bunge Mkoa wa Dodoma Mei 14, 2024.
Mbunge wa Isimani Mhe.
Wiliam Lukuvi (kulia) akikabidhiwa nyama aina ya Kongwa Beef kutoka kwa Bi.
Beatrice Mhina (kushoto) mtaalamu kutoka Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO)
mara baada ya kuridhishwa na ubora wake alipotembelea Mabanda ya maonesho ya
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye
Wiki ya Protini iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Mkoa wa Dodoma Mei 14,
2024.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.
Halima Mdee (kulia) akipata maelezo kuhusiana na matumizi sahihi ya Chanjo ya
Mdondo (Kideli) kwa kuku kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya
Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt Stella Bitanyi (kushoto) alipotembelea Mabanda
ya maonesho ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanyika kwenye Wiki ya Protini iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Mkoa
wa Dodoma Mei 14, 2024.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa pili kushoto) akipata elimu kuhusina
matumizi ya vifaa vya uokoaji majini kutoka kwa Meneja Mradi wa kampuni ya
EMEDO Bw. Arthur Mugema (wa pili kutoka kulia) alipotembelea Mabanda ya
maonesho ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujionea shughuli zinazofanyika kwenye
Wiki ya Protini iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Mkoa wa Dodoma Mei 14,
2024.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa pili kushoto) akipata huduma ya mshikaki unaotokana na mazao ya Samaki alipotembelea Mabanda ya maonesho ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye Wiki ya Protini iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Mkoa wa Dodoma Mei 14, 2024. Aliesimama kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt Edwin Mhede na aliesimama kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei.
Waziri wa Kilimo Mhe.
Hussein Bashe (wa pili kutoka kushoto) akipata elimu kuhusiana na uzalishaji
bidhaa za mazao yatakanayo na Maziwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya ASAS
Bw. Fuad Jeffer (wa tatu kutoka kushoto) alipotembelea Mabanda ya maonesho ya
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye
Wiki ya Protini iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Mkoa wa Dodoma Mei 14,
2024.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kutoka kulia) akipata elimu kuhusiana na
uzalishaji wa dawa za kuogeshea Mifugo kutoka kwa Mtaalamu wa kampuni ya
FARMBASE Dkt. Nasib Mtoi alipotembelea Mabanda ya Wizara ya Mifugo na
Uvuvi kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanyika kwenye Wiki ya Protini iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge Mkoa
wa Dodoma Mei 14, 2024. Aliesimama katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Daniel Mushi.
WAZIRI MKUU AZINDUA KITUO CHA UFUGAJI MBUZI, KONGWA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
leo Mei 13, 2024 amezindua na kushuhudia makabidhiano ya Kituo Atamizi cha
Ufugaji wa Kibiashara kwa Vijana, baina ya Taasisi ya PASS TRUST na Taasisi ya
Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)kilichopo Kongwa mkoani Dodoma.
Akizungumza baada ya
makabidhiano ya kituo hicho, ambacho kinathamani ya shilingi bilioni 1.63
ikijumuisha uwekezaji wa vifaa na mindombinu, Mheshimiwa Majaliwa ameagiza
uwekezaji utunzwe ili taifa liweze kunufaika kupitia uwezeshwaji wa vijana.
Mheshimiwa Majaliwa amesema
kuwa lengo la mradi huo ni kuwapatia vijana ujuzi kwa vitendo ikiwemo elimu ya
ujenzi wa mabanda, ulishaji, matibabu na usimamizi wa mbuzi lakini pia kutoa
mafunzo ya biashara ili vijana waweze kuwa wajasiriamali na kuendeleza biashara
ya unenepeshaji mbuzi.
Kwa upande wake, Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa hadi kufikia Aprili 2024,
ongezeko la mauzo ya nyama nje ya nchi limefikia takribani shilingi bilioni 100
ambapo nyama ya mbuzi imeendelea kuongoza kwa kuchangia asilimia 70.1 ya mauzo
yote, hivyo kituo hicho cha unenepeshaji wa mbuzi kitaendelea kuchaguza kwenye
biashara ya nyama kupitia shughuli ya unenepeshaji wa mbuzi utakaokuwa
ukifanywa na vijana hao.
Aliongeza kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imepanga
kukifanya Kituo Atamizi cha Ufugaji
kilichopo Kongwa kuwa kituo kikubwa kwa ajili ya ufugaji na unenepeshaji wa
mbuzi nchini.
Kituo hicho kilichokuwa kikisimamiwa na
Taasisi isiyo ya kiserikali ya PASS kimekabidhiwa kwa Serikali na kitakuwa chini
ya uangalizi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI).
WATUMISHI WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI WATAKIWA KUWAJIBIKA NA KUWA WAADILIFU
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amewataka watumishi wa wizara hiyo kuwa na uwajibikaji na uadilifu katika makujumu yao ya kuwatumikia wananchi.
Mhe. Mnyeti amebainisha
hayo leo (10.05.2024) jijini Dodoma, wakati alipokuwa akihutubia wajumbe wa
Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kufafanua kuwa ana imani
kubwa na watumishi wa wizara hiyo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii
na kuwa na uzalendo.
Ameongeza kuwa katika
uwajibikaji na uadilifu watumishi wa wizara hiyo wanatakiwa kutojiingiza kwenye
matukio ya matumizi mabaya ya ofisi na kuhakikisha wanazidi kuwatumikia
wananchi kwa kiwango kikubwa hususan wafugaji na wavuvi ambao wengi wao
wanaishi vijijini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe ambaye pia ni mwenyekiti wa
baraza hilo, amesema kikao hicho kimetoka na maazimio tisa ambapo pia wajumbe
wameridhia Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2023/2024 na Mpango wa
Bajeti ya Mwaka 2024/2025 kusomwa bungeni.
Aidha, Prof. Shemdoe
akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la wizara
hiyo, amesema uongozi unaendelea kutatua changamoto mbalimbali mahali pa kazi
ikiwemo kuongeza vitendea kazi.
Pia, amesema wizara
itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi na kuwajengea mazingira bora zaidi ya
kufanyia kazi kwa kuwa wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwa kazini.
Naye Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Edwin Mhede amewataka watumishi wa
wizara hiyo kuwa tayari kuwajibika na kutekeleza bajeti ya wizara mara baada ya
kusomwa na kupitishwa bungeni.
Akisoma taarifa ya hoja na
maoni ya watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mwenyekiti wa Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) – Tawi la wizara hiyo Bw.
Silas William, ameomba uongozi wa wizara kuangalia kwa ukaribu baadhi ya
changamoto zinazowapata watumishi waliopo kazini na ambao wanastaafu ili
kuondokana na usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza.
Bw. William amesema
watumishi wa wizara wataendelea kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kila siku
kwa kuwahudumia wananchi kwa miongozo ya sheria na kanuni za utumishi wa umma
ili waweze kufikia malengo ya serikali ya kukuza sekta za mifugo na uvuvi.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipata pia fursa ya kuuliza maswali na kuchangia hoja mbalimbali na wote kwa pamoja kukubaliana na maazimio tisa kwa ajili ya kufikia malengo ya baraza hilo.
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti akiwahutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la
Wizara ya Mifugo na Uvuvi na kufafanua kuwa ana imani kubwa na watumishi wa
wizara hiyo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwa na uzalendo.
Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma na kukubaliana maazimio tisa likiwemo la
kuridhia Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2023/2024 na Mpango wa
Bajeti ya Mwaka 2024/2025 kusomwa bungeni. (10.05.2024)
Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la
Wafanyakazi la wizara hiyo, akifafanua hoja mbalimbali na kutoa taarifa ya
maazimio tisa kwenye kikao cha baraza kilichofanyika jijini Dodoma.
(10.05.2024)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Edwin Mhede amewataka watumishi wa wizara hiyo
kuwa tayari kuwajibika na kutekeleza bajeti ya wizara ya mwaka 2024/2025 mara
baada ya kusomwa na kupitishwa bungeni. Dkt. Mhede amebainisha hayo jijini
Dodoma wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo. (10.05.2024)
UPUMZISHWAJI ZIWA TANGANYIKA WAUNGWA MKONO
Wananchi wanaojishughulisha na uvuvi katika ukanda wa Ziwa Tanganyika wameunga mkono hatua ya serikali ya kupumzisha shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika ili kulipa nafasi ziwa kuongeza kiwango chake cha uzalishaji wa samaki.
Wananchi hao waliunga mkono
hatua hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi vizimba vya kufugia samaki, boti za
kisasa za uvuvi na doria na pia kupata elimu na uelewa kuhusu upumzishaji wa
shughuli za Uvuvi Ziwa Tanganyika iliyofanyika katika Mwalo wa Katonga, mkoani
Kigoma Mei 9, 2024.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti wawakilishi wa wananchi, akiwemo Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Kilumbe
Ng’enda alisema kuwa muda ambao umepangwa ziwa kupumzishwa ni muafaka kwa
sababu kipindi hicho ni maarufu kwa jina la ‘kilimia’ ambapo ziwa huwa
linajifunga lenyewe na kufanya kupungua kwa Mazao ya samaki.
Aliongeza kwa kueleza kuwa,
kwa muda mrefu sasa wavuvi wamekuwa wakitumia vifaa vyao na mafuta kwenda mbali
bila mafanikio yoyote kwa sababu samaki wamepungua sana ziwani, hivyo
kupumzisha ziwa kutasaidia samaki kuongezeka na hivyo wavuvi wataweza kupata
mavuno mengi zaidi baada ya ziwa kufunguliwa.
Naye, Mbunge wa Kigoma
Kusini, Mhe. Nashon Bidyanguze alisema kuwa mwanzoni walikuwa wanapinga
kufungwa kwa ziwa kwa sababu wananchi walikuwa hawana elimu ya kufungwa kwa
ziwa lakini sasa hawawezi kuendelea kupinga kwa sababu tayari serikali
imepeleka boti na vizimba kwa ajili ya wananchi kutumia kufuga samaki katika
kipindi ambacho ziwa litakuwa limefungwa.
Wakati akikabidhi boti na vizimba kwa wanufaika wanaofanya shughuli zao katika Ziwa Tanganyika, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Boti na Vizimba hivyo ili wananchi watumie kufugia samaki kama njia mbadala ya kujipatia kipato katika kipindi ambacho ziwa litakuwa limepumzishwa.
Aidha, Waziri Ulega
amewataka wanufaika wa boti hizo na wengine wote wanaoendesha shughuli za Uvuvi
Ziwa Tanganyika na Nyasa kutumia zana hizo kwa malengo yaliyokusudiwa, huku
akiwaelekeza maafisa uvuvi wa ukanda wa ziwa Tanganyika kutotumia kipindi hicho
kuwasumbua wavuvi hususani wavuvi wadogo badala yake waendelee kuwaelimisha ili
waweze kutoa ushirikiano wa kutosha wakati wote wa zoezi hilo.
Katika hafla hiyo, Waziri
Ulega amekabidhi vizimba 29 kwa vikundi
sita na watu binafsi 16 na Boti 6 kwa ajili ya uvuvi na doria katika mikoa ya
Kigoma, Katavi na Rukwa.