Nav bar

Alhamisi, 28 Novemba 2024

WATAALAMU KUFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA KUENDELEZA SEKTA YA NGOZI

Na. Stanley Brayton

Wataalamu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Taasisi mbalimbali za kiserikali wamekutana kwa ajili ya kufanya tathimini ya utekelezaji wa mkakati wa kuendeleza Sekta ya ngozi kwa lengo la kuangalia ni namna gani utekelezaji wa Mkakati wa Tasnia hiyo umefikia ili kuweza kuuendeleza zaidi, ikiwa ni pamoja na kubaini mapungufu yake na kuangalia mambo ya kuzingatia ili kuenda katika hatua ya kuhuisha Mkakati huo uweze kuendana na wakati uliopo.

Akizungumza, leo Novemba 28, 2024, mkoani Dodoma  katika kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu cha kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Ngozi, Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Nyamizi Bundala, amesema Tasnia ya ngozi ni moja ya tasnia muhimu hapa nchini inayotoa mchango mkubwa katika upatikanaji wa ajira, fedha za kigeni kutokana na mauzo ya ngozi nje ya nchi, na kuinua pato la wananchi pamoja na kuchangia katika Pato la Taifa kwa ujumla.  

"Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliandaa Mkakati wa kuendeleza Tasnia ya Ngozi (Mkakati wa Maendeleo ya Ngozi 2016-2020) kwa lengo la kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa malighafi bora za ngozi kwa mahitaji ya viwanda na soko, na kuimarisha Sera na Mikakati ya kitaasisi kwaajili ya maendeleo ya Sekta, pamoja na kujenga ukuaji endelevu katika tasnia ya ngozi ili kuimarisha uwezo wa sekta kwa kuongeza thamani na kuendeleza Masoko." amesema Dkt. Bundala

Aidha, Dkt. Bundala amesema mkakati wa kuendeleza Tasnia ya ngozi umeainisha mpangokazi wa utekelezaji ili kufikia malengo, na mpangokazi huo umeanisha majukumu ya kila mdau na Taasisi husika ili kwa pamoja kuweza kufikia malengo yaliyowekwa katika kuendeleza Tasnia hii. 

Vilevile, Dkt. Bundala amesema serikali inaangalia ni namna gani utekelezaji wa mkakati wa Tasnia wa Maendeleo ya Tasnia ya Ngozi (Mkakati wa Maendeleo ya Ngozi 2016-2020) umefikia ili kuweza kubaini mapungufu yake kwa kuzingatia mapungufu kwa ajili ya uhusishaji wa mkakati huo na mpango kazi wake ili kuweza kufikia malengo yatakayojiwekea na hatimae kuwe na Tasnia ya ngozi shindani.


Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Nyamizi Bundala, akizungumza na washiriki wa kikao cha kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkakati wa kuendeleza Sekta ya ngozi na kuelezea lengo mahususi la kikao, kilichofanyika katika Ofisi za NBC, Novemba 28, 2024 Dodoma.


Afisa Dawati la ngozi - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Mariam Muchakila (katikati), akitoa utangulizi na kuelezea malengo ya kikao, ni katika kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu cha kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Ngozi, kilichofanyika katika Ofisi za NBC, Novemba 28, 2024 Dodoma.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) - Mwanza, Dkt. Albert Mmari, akielezea mchango wa chuo cha DIT katika kutoa kozi mbalimbali za uzalishaji mali ghafi kwa kutumia ngozi, ni katika kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu cha kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Ngozi, kilichofanyika katika Ofisi za NBC, Novemba 28, 2024 Dodoma.


Afisa Mazingira Mwandamizi - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI), Bw. Theodory Mulokori, akitoa maoni juu ya uwepo wa ushirikiano baina ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DTI) na Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) katika kuboresha zaidi uzalishaji wa ngozi kwa kutoa wataalamu wengi na elimu bora zaidi, ni katika kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu cha kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Ngozi, kilichofanyika katika Ofisi za NBC, Novemba 28, 2024 Dodoma.


Mchumi Mwandamizi - Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Bw. Gevaronge Myombe, akielezea changamoto za ufinyu wa Viwanda vya ngozi Tanzania kutokana na gharama kubwa za uzalishaji na kubainisha uwepo wa viwanda viwili tu vya ngozi Tanzania, ni katika kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu cha kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Ngozi, kilichofanyika katika Ofisi za NBC, Novemba 28, 2024 Dodoma.


Katibu Mtendaji Chama cha Wadau wa Ngozi Tanzania (LAT), Bw. Freddy Kabala, akikumbushia malengo ya kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya ngozi, ni katika kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu cha kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Ngozi, kilichofanyika katika Ofisi za NBC, Novemba 28, 2024 Dodoma.



Picha ni washiriki wa Kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu cha kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Ngozi, kilichofanyika katika Ofisi za NBC, Novemba 28, 2024 Dodoma.
 


Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Nyamizi Bundala (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kikao kazi cha Kamati ya Wataalamu cha kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Ngozi, kilichofanyika katika Ofisi za NBC, Novemba 28, 2024 Dodoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni