SERIKALI KUANDAA MWONGOZO WA ULINZI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA UVUVI NCHINI
Na. Stanley Brayton, WMUV Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza kuandaa Mwongozo wa Utendaji Kazi kwa ajili ya Shughuli za Ulinzi na Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi nchini ikiwa na lengo la kuandaa Mwongozo ambao utawezesha utekelezaji wa majukumu ya Usimamizi wa Rasilimali hizo kufanyika kwa ufanisi zaidi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali inayotumika katika Sekta ya Uvuvi. Akizungumza leo Juni 11, 2026 Mkoani Morogoro, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uvuvi Nchini, katika Kikao kazi cha Kuandaa Mwongozo huo, Mkurugenzi Msaidizi wa Uvuvi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Christian Nzowa amesema kuwa Wizara imekutana na wadau mbalimbali kutoka Halmashauri zenye Maeneo ya Uvuvi wa mwambao wa Ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa, Maji Madogo na Bahari ya Hindi, pamoja na Maafisa Wandamizi Wastaafu wa Uvuvi na Maafisa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ili kupitia Mwongozo wa kiutendaji ujulikanao kama Standard Operating Procedure SOPs, na ambao utat...