DKT. KILEMILE AONGOZA KIKAO CHA KUIMARISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KIDIJITI KATIKA HUDUMA ZA AFYA YA WANYAMA

Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania, Dkt. Amani Kilemile, ameongoza kikao cha kujadili namna bora ya kuboresha ukusanyaji wa taarifa za huduma za afya ya Wanyama nchini kwa kutumia teknolojia za kidijiti kikao hicho kimefanyika Julai 15, 2026, katika Ukumbi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, jijini Dodoma.

Akiongoza majadiliano hayo, Dkt. Kilemile alisisitiza umuhimu wa matumizi ya mfumo wa kidijiti utakao endana na mifumo ya serikali kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati. 

Katika kikao hicho washiriki walijadili fursa na changamoto zilizopo katika matumizi ya mfumo uliopo sasa ili  kubaini maeneo yanayohitaji maboresho katika kuandaa uandaaji wa mfumo mpya wa kidijitali. 

Majadiliano yalijikita katika uboreshaji wa mifumo ya taarifa za afya ya wanyama, usimamizi wa taarifa za wataalamu wa mifugo, utoaji wa huduma kwa njia za kidijiti pamoja na kuimarisha uratibu na ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali zinazohusika na sekta ya afya ya wanyama.

Kikao hicho kiliwakutanisha wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Baraza la Veterinari Tanzania pamoja na wadau wa maendeleo wakiwemo Shirika la Brooke East Africa, ASPA na INADES Formation-Tanzania, ambao walitoa uzoefu na mapendekezo yatakayosaidia kuendeleza mchakato wa kidijitali katika huduma za afya ya wanyama nchini.








Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UTEKELEZAJI WA UFUGAJI SAMAKI KWA VIZIMBA WAANZA ZIWA TANGANYIKA

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI