Na. Stanley Brayton
Wataalamu Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamekutana kwa ajili ya kupitia na kufanyia Maboresho Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 kwa kufanya uchambuzi na kuandaa Rasimu ya mapendekezo ya Kanuni mpya kwa kukusanya maoni ya wadau wa uvuvi ikiwa ni njia mojawapo ya kubaini mapungufu na changamoto zilizopo katika utekelezaji wake.
Akizungumza, leo Novemba 18, 2024, mkoani Morogoro katika kikao cha kupitia Kanuni hiyo ili kubaini mapungufu na changamoto zake, Mkurugenzi Msaidizi wa Uthibiti Ubora, Viwango na Masoko ya Uvuvi - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Christian Nzowa, amesema kutokana na changamoto zinazojitokeza katika usimamizi wa rasilimali za uvuvi nchini, Wizara imekuwa ikifanya marekebisho ya Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 mara kwa mara ili kuingiza masuala yanayohitaji mabadiliko na kukabiliana na changamoto za kipindi husika.
"kutokana na kukua kwa teknolojia na mabadiliko yanayojitokeza katika njia za mbinu za Uvuvi nchini, Imeonekana kwamba Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 zinahitaji kufanyiwa mapitio upya ili kuendana na hali halisi ya shughuli za uvuvi kwa sasa " amesema Bw. Nzowa
Aidha, Bw. Nzowa amesema, lengo kuu la mapitio ya kanuni hizi na marekebisho yake, ni kuboresha usimamizi endelevu wa rasilimali za Uvuvi, kulinda mfumo wa ekolojia, na ustawi wa jumla wa jamii inayotegemea sekta ya Uvuvi, kuimarisha udhibiti wa uvuvi na biashara haramu za mazao ya uvuvi, kujumuisha matumizi ya teknolojia katika ufuatiliaji, udhibiti na usimamizi wa shughuli za uvuvi nchini, pamoja na kuboresha utoaji wa Huduma kwa wadau wa Uvuvi na kuhakikisha usimamizi wa mazalia ya samaki.
Vilevile, Bw. Nzowa ametoa shukrani za dhati kwa Shirika la Umoja wa Kimataifa wa Kulinda Uasilia (IUCN) kwa kuwa bega kwa bega na Wizara katika kuhakikisha kwamba rasilimali za Uvuvi nchini zinasimamiwa, kuendelezwa na kutumiwa kwa njia endelevu hususani katika suala zima la kuwa na mfumo wa Kisheria unaofanya kazi vizuri.
Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Neema Mwanda, amesema mapitio haya ya Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 yanafanyika kwani Kanuni hii ni ya muda mrefu na ina miaka 15, kiasi kwamba sasa zinapitiwa ili kuboresha zaidi na inafanyika kwa kuwashirikisha Maafisa Uvuvi, wanasheria pamoja na wadau wote wa Uvuvi
Bi. Mwanda amesema baada ya mchakato mzima kufanyika, Kanuni mpya itasaidia kurahisisha utendaji kazi kwa sababu karne hii ni ya sayansi na teknolojia na italeta mabadiliko kwa Sekta ya Uvuvi kiujumla.
Kwa upande wake Afisa Ushirikiano wa Jamii wa Shirika la Umoja wa Kimataifa wa Kulinda Uasilia (IUCN), Bw. Innocent Edward Kilewo amesema wao kama IUCN, wapo bega kwa bega na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuhakikisha mchakato wa mapitio ya Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 unafanyika vizuri ili kuweza kuleta matokeo mazuri kwa serikali na wavuvi.
Pia Bw. Kilewo ameiomba Wizara kuzingatia mambo matatu wakati wa mapitio ya kanuni hizo ikiwa ni pamoja na Kuimarisha usimamizi wa ushirikiano wa uvuvi nchini Tanzania kupitia Kanuni za Uvuvi, Kuunganisha Suluhu zinazozingatia Mazingira ili kuimarisha ustahimilivu wa hali ya hewa kupitia Kanuni za Uvuvi na Kusaidia ushirikishwaji wa kijinsia kupitia Kanuni za Uvuvi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uvuvi ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uthibiti Ubora, Viwango na Masoko ya Uvuvi - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Christian A. Nzowa, akizungumza na Maafisa walioshiriki katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 juu ya kuzingatia mambo sita katika maboresho ya kanuni hiyo, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Neema Mwanda, akitoa utangulizi juu ya upitiaji wa kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 ili kubaini changamoto na mapungufu, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni hiyo ya Uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Afisa Uvuvi Mkuu - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Owen M. Kibona, akielezea baadhi ya kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 na kukaribisha wajumbe kutoa mapendekezo ili kuboresha kanuni hiyo, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni hiyo ya Uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Afisa Ushirikiano wa Jamii - Shirika la Umoja wa Kimataifa wa Kulinda Uasilia (IUCN), Ndg. Innocent Edward, akitoa salamu kutoka IUCN na kuishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuanzisha mchakato wa mapitio ya kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 na kuwaomba wazingatie mambo matatu na katika mapitio hayo, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni hiyo ya Uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Afisa Uvuvi Mkuu - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Emanuela Mawoko, akitoa mapendekezo ya Tozo katika uboreshwaji wa kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni hiyo ya Uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Afisa Mfawidhi Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi - Tanga, Bw. Jacob Nalaila, akielezea na kuonesha kwa kutumia Projekta (haipo pichani) sehemu za kufanya uchambuzi, utambuzi wa mapungufu ya maeneo yaliyopendekezwa kwa kuboresha, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni hiyo ya Uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Mteknolojia wa Samaki Mwandamizi - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Masui Munda, akitoa mapendekezo ya kuboresha Kanuni, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni hiyo ya Uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Afisa Sheria Mwandamizi - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Mariam Mgendwa, akitoa mapendekezo ya kuboresha Kanuni, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni hiyo ya Uvuvi, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Afisa Sheria - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Zulu Gama, akitoa mapendekezo ya kuboresha Kanuni, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Picha ni moja ya kikundi cha Maafisa wakifanya mapitio ya Kanuni za Uvuvi kimakundi, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Picha ni baadhi ya washiriki wa Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 18, 2024 Morogoro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni