Nav bar

Jumanne, 12 Novemba 2024

TANZANIA NA CHINA KUSHIRIKIANA KATIKA TAFITI ZA UVUVI NA UFUGAJI SAMAKI KIIKOLOJIA KUPITIA TAFIRI

 Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 11 Novemba, 2024 akiwa nchini China katika Jiji la Nanjing, Jimbo la JiangSu ametembele Taasisi ya Jiografia na Limnolojia ya Nanjing (Nanjing Institute of Geography and Limnology, Chinese Academy of Sciences, NIGLAS) ambayo inajihusisha na utafiti kwenye sayansi akua.

Akiwa NIGLAS, Prof. Shemdoe amefanya mazungumzo na Menejimenti ya Chuo hicho na kukubaliana kushirikiana na Tanzania katika kazi za Utafiti wa Mambo ya Uvuvi na ufugaji samaki kiikolojia kupitia TAFIRI. Pia, Shemdoe amezipongeza NIGLAS na TAFIRI kwa kuendeleza mashirikiano ambayo yanaendeleza mahusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China ambayo yaliasisiwa na Mwl. Nyerere na Rais Mao Zedong. 

Vilevile, Katibu Mkuu alikutana na kupokea taarifa ya mafunzo ya maabara yaliyotolewa kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa watumishi wa kada ya Mafundi Sanifu Maabara kutoka TAFIRI.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (kushoto) leo tarehe 11 Novemba, 2024 akiwa Nchini China  na Prof. Zhang Ganlin (kulia)  Mkuu wa Taasisi ya  Nanjing Istitute of Geography and Limnology Chinese Academy of Sciencies (NIGLAS) wakibadilishana mawazo mara baada ya kuwasili katika taasisi hiyo. Katikati ni Dkt. Ismael Kimirei, Mkurugenzi Mkuu wa TAFIRI.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (wa pili kutoka kulia) akiwa na Prof. Zhang Ganlin Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Nanjing Institute of Geography and Limnology Chinese Academy of Sciences (NIGLAS) kulia. Wengine katika Picha ni Prof. Zhang Lu, Mkurugenzi wa Utafiti anayeshughulikia Kanda ya Afrika na Dkt.Ismael Kimirei, Mkurugenzi Mkuu wa TAFIRI Tanzania.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (Wa tatu kutoka kulia)  leo tarehe 11 Nov. 2024  akiwa kwenye kikao cha pamoja  na Menejimenti ya NIGLAS, Nchini China.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni