Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2026

SERIKALI YAONGEZA MSUKUMO KUIMARISHA MAENEO YA MALISHO

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imesema inaendelea kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu matumizi endelevu ya maeneo ya malisho, uzalishaji na uhifadhi wa malisho, afya ya mifugo pamoja na matumizi ya teknolojia za kuongeza tija katika ufugaji. Akijibu swali Bungeni leo Septemba 04, 2026 la Mbunge  wa Bububu, Mhe.Salum Khamis Salim,  aliyehoji ni lini serikali inampango gani wa kutoa elimu kwa wafugaji pamoja na kuongeza maeneo ya malisho yanayolingana na idadi ya mifugo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng'wasi Damas Kamani amesema katika bajeti ya mwaka 2026/2027, Wizara imetenga Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwapa mafunzo Maafisa Ugani kuhusu teknolojia na mbinu mpya za uzalishaji na masoko. Mhe. Kamani amesema pia Serikali imeanzisha Kituo cha Huduma kwa Mteja kitakachopokea na kutatua changamoto za wafugaji, pamoja na kutoa taarifa, ushauri na elimu kuhusu huduma mbalimbali za mifugo. Aidha,  katika mwaka 2025/2026, Wizara kwa kushirikiana na Tume ya ...

UTALII WA NYANGUMI KUFUNGUA UCHUMI WA BULUU MTWARA 2026

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya, amezindua rasmi Tamasha la Nyangumi (Nyangumi Festival 2026) katika Viwanja vya Mashujaa, Mtwara Mjini, akisema uwepo wa nyangumi katika bahari za Mtwara ni lango la kukuza uchumi wa buluu, utalii wa kiikolojia na biashara, sambamba na kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya bahari. Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo Mh. Mwaipaya ameendelea kwa kusema kuwa Nyangumi Festival imetoa nafasi kwa Mkoa wa Mtwara kuonesha utamaduni, vipaji vya vijana, bidhaa mbalimbali za wajasiria mali, Sanaa, michezo na vivutio vinavyopatikana katika Mkoa wa mtwara.  “Natoa wito kwa wananchi wote kushiriki kikamilifu katika shughuli za tamasha hili nakutumia fursa zinzotokana nalo, ili kufungua biashara na kutengeneza ajira katika sekta mbali mbali zinazohusiana na uchumi wa buluu hususan kwa vijana na wanawake”. Amesema Mh. Mwaipaya Aidha Mh. Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza umuhimu wa uhifadhi shirikishi wa rasiliamali za bahari kati ya Serikali na ja...

WABUNGE KUHAMASISHA VIJANA KUOMBA MIKOPO YA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imetoa rai kwa Wabunge wa Mikoa Nane  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwahamisha vijana kuchangamkia fursa ya kuomba mikopo ya uwezeshaji vijana kiuchumi awamu ya pili katika sekta za mifugo na uvuvi . Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Kamani kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakati akizungumza na wabunge wa Mikoa Nane ukiwemo Mkoa wa Kagera, Simiyu, Kigoma, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Njombe na Mbeya katika kikao kuhusu uhamasishaji wa vijana kuomba mikopo ya uwezeshaji kiuchumi katika sekta hizo, kikao kilichofanyika leo Septemba 03, 2026 Bungeni jijini Dodoma. Katika taarifa kuhusu mikopo hiyo, Naibu Waziri Mhe. Kamani alieleza kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ilipokea kiasi cha shilingi bilioni 23.68 ikiwa ni sehemu ya shilingi bilioni 200 za ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuwezesha vijana  na kampuni changa kujiajiri na kujiinua kiuchumi. Amesema mikopo ya uwezeshaji...

SERIKALI YATAKA TEKNOLOJIA NA UWEKEZAJI KULETA MAPINDUZI SEKTA YA MIFUGO

Picha
Serikali imetoa wito kwa wadau wa sekta ya mifugo kuongeza matumizi ya teknolojia, ubunifu na uwekezaji ili kuongeza uzalishaji, tija na thamani ya bidhaa za mifugo, hatua inayolenga kuleta mapinduzi katika sekta hiyo nchini. Wito huo umetolewa Septemba 02, 2026 na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Steven Michael, wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Chakula, Mifugo na Ufugaji wa Kuku kwa Mustakabali 2026, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ali Kakurwa, katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere, Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Bw. Michael amesisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia na ubunifu katika kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mifugo, pamoja na kuimarisha mnyororo wa thamani kuanzia uzalishaji hadi masoko.  Ameeleza kuwa sekta ya mifugo ina mchango mkubwa katika usalama wa chakula na lishe, ajira, kipato cha wananchi na ukuaji wa uchumi wa Taifa. Akizungumz...

TDB YAWEKA WAZI FURSA NA MWELEKEO WA TASNIA YA MAZIWA NCHINI

Picha
 Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imeweka wazi fursa na mwelekeo wa Tasnia ya Maziwa nchini, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wake katika Maonesho ya Chakula, Mifugo na Ufugaji wa Kuku kwa Mustakabali 2026 yanayofanyika jijini Dar es Salaam. TDB imetoa elimu hiyo Septemba 03, 2026 kupitia mkutano uliofanyika sambamba na maonesho hayo katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere, uliopo katika Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba, ambapo Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango wa TDB Bw. Cletus Shengena, akimwakilisha Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. George Msalya, aliwasilisha mada yenye kichwa “Taswira ya Tasnia ya Maziwa Tanzania”  Katika mada hiyo, TDB iliainisha hali ya Tasnia ya Maziwa nchini pamoja na fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali ikiwemo uzalishaji, ukusanyaji, uchakataji, uongezaji thamani na masoko ya bidhaa za maziwa.  Aidha, washiriki walipata fursa ya kufahamu maeneo muhimu yanayohitaji uwekezaji, ubunifu na matumizi ya teknolojia ili kuongeza tija na ushindani wa...

DKT. MADELE AFUNGUA MAFUNZO YA MFUMO WA JINSIA GALS KUCHOCHEA UZALISHAJI WA MAZIWA

Picha
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, 𝐃𝐤𝐭. 𝐅𝐚𝐛𝐢𝐚𝐧 𝐌. 𝐌𝐚𝐝𝐞𝐥𝐞,leo Septemba Mosi, 2026  amefungua rasmi mafunzo ya siku sita ya kuwajengea uwezo Wakufunzi kuhusu 𝐌𝐟𝐮𝐦𝐨 𝐰𝐚 𝐉𝐢𝐧𝐬𝐢𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐕𝐢𝐭𝐞𝐧𝐝𝐨 (𝐆𝐀𝐋𝐒), yanayoratibiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP). Mafunzo hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Edema jijini Dodoma yamelenga kuwaandaa washiriki ambao ni Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Halmashauri mbalimbali nchini kuwa Wakufunzi na Mawakala wa Mabadiliko watakaofikisha maarifa ya GALS hadi ngazi ya jamii, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na ushirikishwaji wa wanawake na wanaume katika kupanga, kuweka malengo ya kaya na biashara, kufanya maamuzi na kusimamia rasilimali kwa pamoja.⁣ Dkt. Madele amewataka washiriki kuhakikisha elimu hiyo inaleta mabadiliko ya kimtazamo, usawa na maamuzi ya pamoja katika kaya, ili ongezeko...

KAMANI AITAJA MIKAKATI KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA SAMAKI ZIWA TANGANYIKA

Picha
DODOMA: Serikali imesema wingi wa samaki katika Ziwa Tanganyika umepungua kwa asilimia 62, kutoka tani 304,500 mwaka 1998 hadi kufikia takribani tani 116,000 mwaka 2026.  Hayo yamesemwa leo Septemba Mosi 2026 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani wakati akijibu swali la Mbunge wa Kalambo, Mhe. Edifonsi Joakim Kanoni, aliyetaka kujua lini Serikali itafanya utafiti wa kubaini wingi wa samaki katika ziwa hilo. Mhe. Kamani amesema Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) hufanya tafiti za kubaini wingi na mtawanyiko wa samaki wa tabaka la juu (pelagic species) kwa kushirikiana na nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia huku kwa upande wa Tanzania, tafiti hizo zilifanyika mwaka 1998, 2022 na 2024, huku utafiti wa mwaka 2025 na 2026 ukifanyika kwa ushirikiano wa nchi hizo. "Matokeo yanaonesha mwenendo wa kupungua kwa rasilimali za samaki, hususan dagaa na migebuka, hali inayolazimu kuimaris...

TANZANIA, QATAR KUONGEZA USHIRIKIANO WA UWEKEZAJI KATIKA MIFUGO NA UVUVI

Picha
Daudi Nyingo, DAR ES SALAAM  Serikali ya Tanzania imesema iko tayari kushirikiana na wawekezaji kutoka Qatar katika kuendeleza fursa za uwekezaji katika sekta za mifugo na uvuvi, ikiwemo kuongeza uzalishaji na usindikaji wa nyama, kupanua masoko ya bidhaa za mifugo katika nchi za Mashariki ya Kati, kuendeleza sekta ya kuku na kuwekeza katika miundombinu ya uvuvi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, wakati wa mazungumzo yake na Naibu Waziri Mkuu wa zamani wa Qatar, Mhe. Dkt. Khalid bin Mohammad Al Attiyah, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Thirty-Five Investment Holding, katika ziara yake ya kikazi nchini Tanzania. Kikao hicho kilichofanyika Agosti 31, 2026 katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Bi. Agnes Kisaka Meena; Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara.  Akizungum...

KAMANI AKUTANA NA WATAALAM KUJADILI MAENDELEO YA SEKTA YA MIFUGO

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng’wasi Damas Kamani, amekutana na wataalamu kutoka Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko (DPMD) na Idara ya Huduma za Mifugo (DVS), kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa pamoja na majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na idara hizo. Vikao vyote vilivyomkutanisha Naibu Waziri Mhe. Kamani  pamoja na wataalam kutoka vitengo na idara hizo vilifanyika  leo Agosti 31, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage Tower, jijini Dodoma kwa nyakati tofauti. Katika kikao na wataalamu wa ICT, Mhe. Kamani alipokea taarifa na kushuhudia maonesho ya mfumo (demonstration) utakaotumika katika zoezi la utoaji wa mikopo kwa ajili ya kuwawezesha vijana kiuchumi, ambapo baada ya kupitia mfumo huo, alitoa mapendekezo na maelekezo mbalimbali kwa ajili ya kuuboresha kabla ya kuanza kutumika. Katika hatua nyingine, kikao na wataalamu wa Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko, Mhe. Kamani alijadiliana...

TANZANIA YAANZA KUJADILI USTAWI WA VIUMBEMAJI

Picha
Nchi ya Tanzania kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya ufadhili wa Shirika lisilo la Serikali linalohamasisha kampeni ya “AFYA MOJA” (OHD) imeanza mkutano wa siku 2 unaojadili ustawi wa samaki wanaofugwa na  viumbe maji kwa ujumla unaofanyika Agosti 31 hadi Septemba 1, 2026 jijini Dar-es-salaam. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena amesema kuwa mbali na lengo la kutoa uelewa na kuongeza ufahamu kuhusu ustawi wa samaki na wanyama wa majini mkutano huo pia unalenga kubadilishana maarifa na uzoefu kuhusu afya ya samaki,usalama wa viumbe maji na uzalishaji unaowajibika. “Tanzania pamoja na Afrika kwa ujumla suala la ukuzaji viumbe maji limeshika kasi na watu wengi wamekuwa wakiwekeza kwenye tasnia hiyo hivyo mkutano huu unaangazia fursa na changamoto zinazoikabili tasnia ya ukuzaji viumbe maji ili kuhakikisha kwamba ufugaji wa viumbe maji unafanyika kwa uadilifu na kwa kuzingatia ustawi” Amesema Bi. Meena. Aidha Bi...