WATAALAM WA MIFUGO WASHIRIKI MKUTANO WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA WOAH
Wataalamu wakishiriki mkutano wa kuanza utekelezaji wa Mradi wa Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH) unaolenga kuimarisha ushirikiano wa maabara katika uchunguzi, ufuatiliaji na udhibiti wa Homa ya Bonde la Ufa (Rift Valley Fever – RVF) kati ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Kituo cha Magonjwa Ambukizi na Bioteknolojia (CIDB), Huduma za Mifugo Tanzania na Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Kilimo na Maendeleo (CIRAD).
Mkutano huo umefunguliwa na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS), Dkt. Benezeth Lutege Malinda, leo Septemba 22, 2026, katika Makao Makuu ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Temeke, Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa kitaalamu na ushirikiano wa maabara katika uchunguzi, ufuatiliaji na udhibiti wa Homa ya Bonde la Ufa nchini Tanzania na katika ukanda wa Afrika Mashariki.



Maoni
Chapisha Maoni