Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2026

WATAALAM WA MIFUGO WANA FURSA KUBWA KUINUA SEKTA KUPITIA C-SDTP

Picha
Na Chiku Makwai; Mbeya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Fabian Madele, amesema wataalam wanaopatiwa mafunzo kupitia Mradi wa Mageuzi ya Sekta ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) wana nafasi kubwa ya kuchochea mageuzi na kuinua sekta ya mifugo nchini. Dkt. Madele ameyasema hayo leo Oktoba 5, 2026, katika Chuo cha Mafunzo ya Mifugo Uyole, mkoani Mbeya, wakati akizindua Mafunzo ya Wawezeshaji wa Mashamba Darasa ya Ng’ombe wa Maziwa yanayotekelezwa kupitia mradi wa C-SDTP, amesisitiza  kuwa wataalam wanapaswa kuhakikisha maarifa na teknolojia wanazozitoa zinaendana na mazingira uwezo wa mfugaji pamoja na rasilimali zinazopatikana katika eneo husika. “Kutibu mifugo siyo sifa nzuri pekee kwa mtaalam; sifa kubwa ni kuzuia magonjwa ya mifugo ili kuhakikisha tunapata maziwa bora na salama yenye viwango vinavyokubalika katika masoko ya ndani na nje ya nchi,” amesema Dkt. Madele. Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wataalam uwezo wa kubaini ...

MTUPO MMOJA WAIPA MIFUGO NA UVUVI (WANAWAKE) NAFASI YA PILI TUFE

Picha
◼️ Ni kupitia kwa mshiriki wake Theodata Sallema licha ya mitupo yake miwili kukataliwa ◼️Yashika nafasi ya 4 mita 1500 upande wa riadha. Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye mchezo wa kurusha tufe kwa upande wa wanawake baada ya mshiriki wake Theodata Sallema kufanikiwa kurusha tufe hilo umbali wa mita 8.20 akizidiwa alama 0.5 pekee na mshindi wa kwanza kutoka Bunge aliyerusha umbali wa mita 8.25. Katika mchezo huo uliofanyika Oktoba 01,2026 ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Kilimanjaro Bi. Sallema amefanikiwa kuibuka na ushindi huo mbele ya washiriki wengine 20 ambapo kila mmoja alifanikiwa kurusha mitupo 3 huku mitupo miwili ya Bi. Salema ikikataliwa kufuatia kutoka nje ya duara la kurushia kinyume na utaratibu wa mchezi huo. Wakati huo huo Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia kwa mwanariadha wake Mariam Stephen imefanikiwa kushika nafasi ya 4 kwenye mchezo wa riadha umbali wa mita 1500 zilizofanyika leo  Oktoba 01,2026 kw...

DKT. BASHIRU AAGIZA VIFAA VYA UGANI VITUMIKE KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZIWA NCHINI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, leo Oktoba 2, 2026, jijini Dodoma, amekabidhi rasmi magari, pikipiki na vifaa maalumu vya kiufundi vilivyonunuliwa kupitia Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) na kuagiza vifaa hivyo vitumike kuongeza tija ya uzalishaji katika tasnia ya maziwa. Makabidhiano hayo ni hatua muhimu katika kuimarisha utekelezaji wa mradi na kuhakikisha huduma za kitaalamu zinawafikia wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kwa haraka, ufanisi na kwa wakati Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Magari 6 aina ya Toyota Hilux Double Cabin; pikipiki 23,  pamoja na vifaa vya ugani. Akikabidhi vifaa hivyo, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally amesisitiza vifaa hivyo vitumike kwa lengo la kusaidia Walengwa wa mradi na kuleta matokeo chanya katika mageuzi ya Tasnia ya Maziwa nchini Tanzania huku akiwaasa viongozi wa Mikoa iliyokabidhiwa vifaa hivyo kusimamia  uangalizi  makini wa vifaa ...

DSFA, TDB, TAFIRI WAANDAA MCHAPALO KWA WANAMICHEZO SHIMIWI

Picha
Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari kuu (DSFA), Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) na Taasisi ya utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) wameandaa chakula pamoja cha usiku kwa wanamichezo wa Wizara ya Mifugo wanaoshiriki michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Kilimanjaro. Akizungumza kwa niaba ya Taasisi hizo zote, Mteknolojia wa chakula kutoka Bodi ya maziwa nchini Bw. Sijali Mabena amewapongeza wanamichezo hao kwa uwezo waliouonesha kwenye michezo mbalimbali mpaka sasa na kuwataka kufanya vema zaidi kwenye hatua zinazofuata. Kwa upande wake Mwenyekiti wa michezo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Sebastian Shilangalila amewashukuru viongozi hao kwa kuwezesha chakula hicho ambapo amesisitiza kinasaidia kujenga umoja wa wanamichezo hao.

SERIKALI: WAKULIMA NA WAFUGAJI WAMECHANGIA UHIMILIVU WA UCHUMI, USALAMA WA CHAKULA

Picha
Serikali imeeleza kuwa Wakulima na Wafugaji wamechangia kuleta  uhimilivu wa uchumi na usalama wa chakula kutokana na uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo yanayotosheleza mahitaji ya nchi hatua ambayo imetajwa kulifanya taifa kuwa na utulivu wakati huu ambao kuna vita kubwa za kiuchumi duniani. Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa  wakati wa kufungua Kongamano la Kitaifa la Wakulima Wadogo na Mkutano Mkuu wa 31 wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima  (MVIWATA) itakayofanyika kwa siku tatu kuanzia Leo 29 Septemba hadi Oktoba Mosi , 2026 Mkoani Morogoro. Balozi Dkt. Bashiru amesema nchi inajivunia kuwa na wakulima na wafugaji wanaozalisha chakula cha kutosha ambao wamekuwa nguzo muhimu katika kuimarisha usalama wa chakula na kueleza umuhimu wa kujadili changamoto zinazowakabili wakulima wadogo, ikiwemo uhakika wa ardhi, kilimo ikolojia na masoko ya mazao, katika jitihada za kuelekea uhuru wa chakula.  Aidha...

KAMBA WANAWAKE WAFUZU 16 BORA

Picha
◼️Waiburuza Viwanda mvuto 1-0 kwenye mchezo wa maamuzi Timu ya mchezo wa kuvuta kamba (wanawake) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya SHIMIWI baada ya kuibuka na ushindi wa mvuto 1-0 kwenye mchezo wake wa marudiano dhidi ya timu ya Wizara ya Viwanda uliochezwa mapema leo Septemba 29,2026 kwenye viwanja vya CCP mkoani Kilimanjaro. Mchezo huo uliokuwa na ushindani kwa pande zote ambao pia ulichezwa kwa raundi moja pekee uliamuliwa na ubora na utimamu wa kimwili wa wachezaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo licha ya kuonesha upinzani mkali timu ya Viwanda iliupoteza sekunde ya 20 ya mchezo. Kwa matokeo hayo timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kumenyana na timu ya TAKUKURU kwenye hatua hiyo ya 16 bora kwa mujibu wa mchoro wa mashindano hayo.

NZEGA YAADHIMISHA SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI KWA KISHINDO, MBWA NA PAKA 14,450 WACHANJWA

Picha
Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora imeandika historia kwa kuadhimisha kilele cha Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani kwa kishindo, ambapo jumla ya mbwa na paka 14,450 wamechanjwa.Halmashauri ya Nzega ilipewa dozi 21,500 za chanjo ili kufanikisha wiki ya maadhimisho. Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Septemba 28, 2026 katika Viwanja vya Mwanhala, Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Naitapwaki Tukai, amesema kila mwananchi ana jukumu la kujilinda na kuwalinda watoto dhidi ya madhara ya ugonjwa huo hatari unaoweza kusababisha kifo kwa binadamu. "Unapong'atwa na mbwa au kupata mkwaruzo, osha kidonda kwa maji mengi yanayotiririka na sabuni haraka na kisha nenda kituo cha afya. Jamii inapaswa kutoa taarifa mapema kuhusu wanyama wenye dalili hatarishi ili waweze kudhibitiwa," amesema Mhe. Tukai. Ameongeza kuwa jamii inapaswa kudhibiti mbwa wanaozurura na amewataka wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi, akisema kaulimbiu ya mwaka huu isemayo "Kwa pamoja tu...

FETA YAHITIMISHA MAFUNZO YA UONGOZI WA JAMII KATIKA UHIFADHI WA RASILIMALI ZA PWANI NA BAHARI

Picha
Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) Tarehe 27 Septemba, 2026 imehitimisha mafunzo ya muda mfupi ya Uongozi wa Jamii katika Uhifadhi wa Rasilimali za Pwani na Bahari (Conservation Leadership Training Programme) yaliyolenga kuwawezesha viongozi na wadau wa jamii kushiriki kikamilifu katika usimamizi na uhifadhi endelevu wa rasilimali za pwani na bahari. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Kampasi ya FETA Mbegani, Bagamoyo, kwa siku 14 kuanzia 14–27 Septemba, 2026 yakishirikisha washiriki 20 kutoka Tanga na Pemba yamefadhiliwa na  Ubalozi wa Ireland Tanzania kupitia IUCN Tanzania, huku FETA ikiwa mshirika wa utekelezaji katika kujenga uwezo wa washiriki wanaohusika na usimamizi, matumizi na uhifadhi wa rasilimali za pwani na bahari. Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa FETA, Bw. Deus J. Bwathondi, amewataka washiriki kutumia maarifa na ujuzi walioupata kuleta matokeo chanya katika jamii zao. Alisisitiza kuwa mafunzo hayo hayapaswi kuishia kwa washiriki pekee, bali yawe c...

KAMBA WANAUME YATINGA 16 BORA

Picha
◼️Wanawake waiburuza RAS Tabora, Viwanda washikilia tiketi yao ya 16 bora Timu ya mchezo wa kuvuta kamba (wanaume) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kushinda mchezo wao kwa mivuto 2-0 dhidi ya timu ya Tume ya Sheria na kufanya timu hiyo kinara wa kundi lao baada ya kushinda michezo yake yote. Katika mchezo huo timu ya Mifugo na Uvuvi ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mvuto wake wa kwanza sekunde 6 za awamu ya kwanza kabla ya kufanikiwa kushinda awamu ya pili katika sekunde ya 8 tu ya awamu hiyo. Nayo timu ya mchezo huo kutoka Wizarani hapo kwa upande wa Wanawake imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mivuto 2-0 dhidi ya timu ya RAS Tabora ambapo ilifanikiwa kushinda mvuto wake wa kwanza sekunde ya 4 tu ya awamu ya kwanza kabla ya kuibuka na ushindi wa mvuto wa pili katoka sekunde ya 6 tu ya awamu ya pili. Timu ya Wanaume imefanikiwa kuongoza kundi lake baada ya kushinda mechi zake zote dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Ofisi ya Rais-Maendeleo ya...

DC NZEGA AWAKARIBISHA WATANZANIA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA KICHAA CHA MBWA

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Naitapwaki Tukai, amewaalika wananchi wa Nzega na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani kitakachofanyika kesho Septemba 28, 2026 katika viwanja vya Mwanhala, Wilayani Nzega Mkoani Tabora. Kutokana na juhudi mbalimbali ikiwemo utoaji wa chanjo ya kichaa cha mbwa, kumekuwa na mafanikio makubwa ya kupunguza matukio ya ugonjwa huo Wilayani humo, kutoka matukio 315 mwaka 2021 hadi kufikia matukio 75 tu mwaka 2026, ameyasema hayo Leo Septemba 27, 2026 Nzega. "Niwaombe wananchi kutunza mbwa kwa kuwapa chanjo ili kuweza kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kwa binadamu. Kesho siku ya maadhimisho chanjo itatolewa sambamba na kufunga vizazi  ili kuzuia mbwa kuzaa kiholela, na elimu itatolewa kwa kina," amesema Mhe. Tukai. Aidha, Mhe. Tukai amesisitiza umuhimu wa kuwafundisha watoto namna ya kumtunza mbwa ili kupunguza idadi ya mbwa wanaozurura mitaani na kujikinga na madhara...

KAMBA MIFUGO NA UVUVI ZATEMBEZA VICHAPO SHIMIWI 2026

Picha
◼️Wanawake wawaburuza RAS Morogoro mivuto 2-0 ◼️Wanaume waigaragaza UCSAF Timu za mchezo wa kuvuta kamba (wanaume na wanawake) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi zimeendelea kudhihirisha matokeo ya protini inayotokana na nyama, samaki na maziwa baada ya kufanikiwa kushinda michezo yao waliyocheza Septemba 27,2026 kwenye michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Kilimanjaro. Timu ya kamba upande wa wanawake ndo ilikuwa ya kwanza kuonesha ubabe wao baada ya kuivuta timu ya RAS Morogoro kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkali kwa pande zote mbili ambapo sekunde ya 45 walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mvuto wa kwanza kabla ya kurejea awamu ya pili na kufanikiwa kushinda sekunde ya 20 tu ya mchezo huo. Baada ya hapo timu ya kamba upande wa wanaume iliingia dimbani kumenyana na timu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambapo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mvuto wa kwanza katika sekunde ya 25 kabla ya kurejea awamu ya pili na kufanikiwa kushinda mvuto wa pili katika sekunde ya 20 ya mc...