DSFA, TDB, TAFIRI WAANDAA MCHAPALO KWA WANAMICHEZO SHIMIWI
Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari kuu (DSFA), Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) na Taasisi ya utafiti wa Uvuvi nchini (TAFIRI) wameandaa chakula pamoja cha usiku kwa wanamichezo wa Wizara ya Mifugo wanaoshiriki michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza kwa niaba ya Taasisi hizo zote, Mteknolojia wa chakula kutoka Bodi ya maziwa nchini Bw. Sijali Mabena amewapongeza wanamichezo hao kwa uwezo waliouonesha kwenye michezo mbalimbali mpaka sasa na kuwataka kufanya vema zaidi kwenye hatua zinazofuata.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa michezo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Sebastian Shilangalila amewashukuru viongozi hao kwa kuwezesha chakula hicho ambapo amesisitiza kinasaidia kujenga umoja wa wanamichezo hao.






Maoni
Chapisha Maoni