KAMBA MIFUGO NA UVUVI ZATEMBEZA VICHAPO SHIMIWI 2026

◼️Wanawake wawaburuza RAS Morogoro mivuto 2-0

◼️Wanaume waigaragaza UCSAF

Timu za mchezo wa kuvuta kamba (wanaume na wanawake) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi zimeendelea kudhihirisha matokeo ya protini inayotokana na nyama, samaki na maziwa baada ya kufanikiwa kushinda michezo yao waliyocheza Septemba 27,2026 kwenye michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Kilimanjaro.

Timu ya kamba upande wa wanawake ndo ilikuwa ya kwanza kuonesha ubabe wao baada ya kuivuta timu ya RAS Morogoro kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkali kwa pande zote mbili ambapo sekunde ya 45 walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mvuto wa kwanza kabla ya kurejea awamu ya pili na kufanikiwa kushinda sekunde ya 20 tu ya mchezo huo.

Baada ya hapo timu ya kamba upande wa wanaume iliingia dimbani kumenyana na timu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ambapo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mvuto wa kwanza katika sekunde ya 25 kabla ya kurejea awamu ya pili na kufanikiwa kushinda mvuto wa pili katika sekunde ya 20 ya mchezo huo.

Kufuatia matokeo hayo timu hizo zimejiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye hatua ya 16 bora ambapo timu ya kamba wanaume imejikusanyia alama zote sita baada ya kushinda michezo yao yote huku wanawake wakiwa na alama 4 kufuatia kushinda mchezo mmoja, kutoa sare mmoja na kupoteza mmoja.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI