MTUPO MMOJA WAIPA MIFUGO NA UVUVI (WANAWAKE) NAFASI YA PILI TUFE

◼️ Ni kupitia kwa mshiriki wake Theodata Sallema licha ya mitupo yake miwili kukataliwa

◼️Yashika nafasi ya 4 mita 1500 upande wa riadha.

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye mchezo wa kurusha tufe kwa upande wa wanawake baada ya mshiriki wake Theodata Sallema kufanikiwa kurusha tufe hilo umbali wa mita 8.20 akizidiwa alama 0.5 pekee na mshindi wa kwanza kutoka Bunge aliyerusha umbali wa mita 8.25.

Katika mchezo huo uliofanyika Oktoba 01,2026 ikiwa ni mwendelezo wa michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Kilimanjaro Bi. Sallema amefanikiwa kuibuka na ushindi huo mbele ya washiriki wengine 20 ambapo kila mmoja alifanikiwa kurusha mitupo 3 huku mitupo miwili ya Bi. Salema ikikataliwa kufuatia kutoka nje ya duara la kurushia kinyume na utaratibu wa mchezi huo.

Wakati huo huo Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia kwa mwanariadha wake Mariam Stephen imefanikiwa kushika nafasi ya 4 kwenye mchezo wa riadha umbali wa mita 1500 zilizofanyika leo  Oktoba 01,2026 kwenye uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro.

Bi. Stephen amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kuwashinda wanariadha wenzake kutoka Mahakama, Ras Mara, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mambo ya ndani na Wizara ya Uchukuzi.

Aidha mbali na nafasi hiyo ya Bi. Stephen, Washiriki wengine Neema Jigwa na Fihiri Mbawala wameshika nafasi ya 3 na 4 kwenye hatua ya mtoano ya mbio za mita 200.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI