KAMBA WANAWAKE WAFUZU 16 BORA
◼️Waiburuza Viwanda mvuto 1-0 kwenye mchezo wa maamuzi
Timu ya mchezo wa kuvuta kamba (wanawake) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya SHIMIWI baada ya kuibuka na ushindi wa mvuto 1-0 kwenye mchezo wake wa marudiano dhidi ya timu ya Wizara ya Viwanda uliochezwa mapema leo Septemba 29,2026 kwenye viwanja vya CCP mkoani Kilimanjaro.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani kwa pande zote ambao pia ulichezwa kwa raundi moja pekee uliamuliwa na ubora na utimamu wa kimwili wa wachezaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo licha ya kuonesha upinzani mkali timu ya Viwanda iliupoteza sekunde ya 20 ya mchezo.
Kwa matokeo hayo timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kumenyana na timu ya TAKUKURU kwenye hatua hiyo ya 16 bora kwa mujibu wa mchoro wa mashindano hayo.


Maoni
Chapisha Maoni