KAMBA WANAUME WAENDELEZA UBABE SHIMIWI 2026

◼️Yawagaraza OR-Vijana mivuto 2-0

◼️Mpira wa Miguu waanza kwa kupoteza

◼️Kamba wanawake wanakimbiza mwizi kimya kimya

Timu ya mchezo wa kuvuta kamba (wanaume) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendeleza ubabe wake kwenye michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Kilimanjaro baada ya kuibuka na ushindi wa mivuto 2-0 dhidi ya timu ya OR-Vijana kwenye mchezo uliochezwa Septemba 26,2026 kwenye viwanja vya CCP mkoani humo.

Timu ya OR-Vijana iliingia katika mchezo huo ikiwa imeshakata tamaa ya kushinda kutoka na ubora wa timu ya Mifugo na Uvuvi hali iliyofanya mchezo huo ukamilike kwa sekunde 15 pekee za mchezo.

Baada ya mchezo huo timu ya Mifugo na Uvuvi sasa itamenyana na timu ya UCSAF kwenye mchezo utakaopigwa Septemba 28 kwenye viwanja vya CCP mkoani Kilimanjaro. 

Wakati huo huo katika hali iliyowashangaza wengi timu ya mchezo wa kuvuta kamba kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa upande wa wanawake licha ya kupoteza kwa mivuto yote miwili imeonesha ushindani mkubwa dhidi ya timu ya Mashtaka ambayo ni moja ya timu tishio kwenye mashindano hayo ya mwaka huu.

Nayo timu ya mpira wa Miguu imeanza vibaya kampeni yake ya michuano hiyo kwa kupoteza michezo miwili mfululizo wa kwanza ukiwa ni dhidi ya timu ya Ulinzi na mwingine uliopigwa leo ukiwa ni dhidi ya timu ya Ardhi licha ya kuonesha kandanda safi na la kuvutia kwenye mechi zote mbili.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI