MIFUGO NA UVUVI YAIDUWAZA MAMBO YA NDANI

◼️Yawaburuza mivuto yote miwili

Timu ya mchezo wa kuvuta kamba (wanaume) kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeibuka na ushindi wa mivuto yote miwili dhidi ya timu ngumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwenye mchezo uliochezwa Septemba 23,2026 ukiwa ni mchezo wao wa kwanza kwenye michuano ya SHIMIWI inayofanyika mkoani Kilimanjaro.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali kwa pande zote mbili timu ya Mifugo na Uvuvi ilifanikiwa kushinda mvuto wa kwanza baada ya wapinzani wao kushindwa kuhimili presha waliyokuwa wakiwapa hali iliyowalazimu wachezaji wake kulala chini wakati wakiendelea kuvuta.

Kufuatia matokeo hayo Viongozi wa michezo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na wachezaji wengine wa Wizara hiyo walichanga na kuikabidhi timu hiyo motisha ya takribani shilingi 400,000 ili waendelee kufanya vizuri zaidi kwenye michezo inayofuata.

Kwa matokeo hayo timu ya Mifugo na Uvuvi inakuwa kinara wa kundi C linalojumuisha timu za Wizara ya Mambo ya Ndani, Ofisi ya Rais-Vijana, Tume ya Sheria na UCSAF.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI