TANZANIA YASITISHA VIBALI VYA KUAGIZA WANYAMA KUTOKA NAMIBIA

◼️Ni kufuatia mifugo ya nchi hiyo kukumbwa na ugonjwa wa Miguu na Midomo

Nchi ya Tanzania imesitisha kutoa vibali vya kuagiza wanyama kutoka nchini Namibia kufuatia mifugo ya nchi hiyo kukumbana na kadhia ya ugonjwa wa Miguu na Midomo au  “FMD” kama unavyotambuliwa na wafugaji wengi.

Mlipuko wa ugonjwa huo umetokea katika eneo la Karasburg ambalo hapo awali lilitangazwa kuwa huru dhidi ya ugonjwa huo kabla ya Wataalam wa Mifugo wa eneo hilo kubaini jumla ya mifugo 10 kati ya 11 iliyopimwa kuthibitika kuwa na ugonjwa huo kufuatia majibu ya vipimo yaliyotoka Septemba 23,2026.

Aidha katika kukabiliana na ugonjwa huo, Serikali ya Namibia inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha chanjo kwenye mifugo ambayo haijaathiriwa na changamoto hiyo kwenye eneo hilo.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI