VIWANDA YAPONEA CHUPUCHUPU DHIDI YA MIFUGO
◼️Walazimisha sare ya mvuto 1-1
Timu ya mchezo wa kuvuta kamba (wanawake) Wizara ya Mifugo na Uvuvi imelazimishwa sare ya mvuto 1-1 dhidi ya timu ya Viwanda kwenye mchezo wao wa kwanza wa michuano ya SHIMIWI uliochezwa Septemba 24, 2026 kwenye viwanja vya CCP mkoani Kilimanjaro.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkali kwa pande zote mbili timu ya Viwanda iliwashangaza wengi baada ya kuibuka na ushindi wa sekunde za jiooni katika mvuto wa kwanza kabla ya kuvutwa mapema katika mvuto wa pili.
Kufuatia matokeo hayo timu hizo zimevuna alama moja kila upande huku zikisubiri kukutana na wapinzani wao kwenye michezo inayofuata ambapo Mifugo na Uvuvi watavutana na timu ya Mashtaka huku Viwanda wakipepetana na timu ya RAS Morogoro.
Michuano hiyo itaendelea tena baadae jioni ambapo Timu ya soka ya wizara ya Mifugo na Uvuvi itashuka dimbani kumenyana na timu ya Ulinzi.



Maoni
Chapisha Maoni