CHANDE AZINDUA MAADHIMISHO MIAKA 30 YA HIFADHI ZA BAHARI MAFIA, AWAITA WAWEKEZAJI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande amezindua Maadhimisho ya Miaka 30 ya Hifadhi za Bahari Mafia pamoja na Tamasha la Mafia Festival linalolenga kuchochea uchumi wa buluu kupitia uhifadhi wa rasilimali za bahari.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo Septemba 24, 2026 katika kando ya Fukwe ya Utende, Wilayani Mafia Mkoa wa Pwani, Mhe. Chande ametoa wito kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kuwekeza katika rasilimali za bahari na kutumia fursa hizo kukuza uchumi wa buluu.

Katika hotuba yake , ametoa rai kwa vijana na wanawake kutumia fursa za utalii zinazotokana na uhifadhi wa Bahari ili kuchangia utunzwaji wa rasilimali hizo kwa kizazi cha sasa na cha baadae. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Aziza Ally Mangosongo ameitaja Wilaya hiyo kuwa kituo cha Uhifadhi, Uwekezaji na utalii ambapo ameeleza kuwa kupitia Tamasha la Mafia Festival wilaya hio itaendelea kutangaza fursa za uchumi wa buluu pamoja na uhifadhi wa bahari.

Naye, Meneja wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Dkt. Emmanuel Sweke amesema kazi ya uhifadhi wa rasilimali za bahari inahitaji ushirikiano baina ya wataalam na jamii kwa ujumla ili kuwa na uendelevu, ambapo pia alitumia jukwaa hilo kuwashukuru wadhamini na washirika walioshirikiana katika kuandaa maadhimisho hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Chande akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Mafia na Maadhimisho ya Miaka 30 ya Hifadhi za Bahari Mafia leo Septemba 24, 2026 Utende, Mafia.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Mhe. Aziza Mangosongo akieleza umuhimu wa Tamasha la Mafia na fursa za uhifadhi wa Bahari wakati wa Ufunguzi wa tamasha hilo na miaka 30 ya Hifadhi za Bahari Mafia iliyofanyika leo Septemba 24, 2026 katika Eneo la Fukwe za Bahari, Utende Mafia.

Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Dkt. Emmanuel Sweke akitoa shukran kwa wadau walioshiriki katika kuandaa maadhimisho ya miaka 30 ya Hifadhi za Bahari Mafia pamoja na Tamasha la Mafia Festival  inayofanyika kuanzia leo Septemba 24 hadi 26 2026 Kisiwani Mafia.

Baadhi ya Wananchi wakifuatilia ufunguzi wa maashimisho ya Miaka 30 ya Hifadhi za Bahari Mafia na Tamasha la Mafia

Baadhi ya Watumishi wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), wakiwemo wastaafu walioanzisha Hifadhi ya Bahari Mafia, wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi baada ya Uzinduzi leo Septemba 24, 2026 uliofanyika Utende Mafia.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI

TANZANIA DAIRY BOARD

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI