Nav bar

Jumanne, 19 Novemba 2024

MABORESHO YA KANUNI ZA UVUVI ZA MWAKA 2009 KUSAIDIA KATIKA UWEKEZAJI

Na. Stanley Brayton

Mkurugenzi wa Uvuvi Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Ally Sheikh amesema maboresho haya ya Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 yatasaidia sana katika shughuli za uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuwavutia wawekezaji wa nje na ndani katika tasnia ya uvuvi.

Akizungumza, leo Novemba 19, 2024, mkoani Morogoro katika kikao cha kupitia Kanuni hiyo ili kubaini mapungufu na changamoto zake, Prof. Sheikh,  amesema mabadiriko haya ya kisheria yatasaidia sana katika shughuli za uwekezaji katika Sekta ya uvuvi hasa kwa kuwavutia wawekezaji kutoka nje na wawekezaji waliopo ndani ili kuwekeza katika sekta hiyo.

"kitu tunachofanya sahivi hakiepukiki kwani ni kitu cha lazima, na ni lazima kufanya maboreaho ya hizi kanuni za Uvuvi ili kuendana na hali ya sasa" amesema Prof. Sheikh

Aidha, Prof. Sheikh amesema viongozi wa ngazi za juu ya Serikali wanafanya juhudi kubwa katika kukuza biashara na kuweka mazingira mazuri ya biashara katika Sekta ya Uvuvi na hii inapelekea katika kuboresha mazingira na Kanuni ili wawekezaji wanaokuja na walioko ndani wawe na mazingira mazuri kisheria na kikanuni.

Vilevile, Prof. Sheikh amesema kuwa kuna vikwazo vingi katika Sekta ya Uvuvi ikiwemo swala la Uvuvi haramu, kwa hiyo kanuni hii itakuwa mwarobaini katika Uvuvi huo haramu na ni lazima kuwa na mikakati ya kisheria kuhakikisha kwamba tunaongeza Sekta ya Uvuvi iweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa na maisha ya watu kiujumla.


Mkurugenzi wa Uvuvi  - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Ally Sheikh, akizungumza na Maafisa walioshiriki  katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 juu ya mambo ya kuzingatika katika kuboresha Kanuni hizo, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 19, 2024 Morogoro.


Picha ni Maafisa wakifanya mapitio ya Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, ni katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni hizo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 19, 2024 Morogoro.


Mkurugenzi wa Uvuvi  - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Ally Sheikh (aliyesimama kulia), akijadiliana na maafisa walioshiriki katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 kuhusu ushirikishwaji wa wadau katika uboreshwaji wa Kanuni hizo, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 19, 2024 Morogoro.



Mkurugenzi Msaidizi wa Uthibiti Ubora, Viwango na Masoko ya Uvuvi - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Christian A. Nzowa (aliyesimama), akijadiliana na Maafisa walioshiriki katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 kuhusu utumizi wa nyavu zinazokubalika katika shughuli za Uvuvi, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 19, 2024 Morogoro.


Mkurugenzi wa Uvuvi  - Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Mohamed Ally Sheikh (katikati mstari wa mbele), akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa walioshiriki  katika Kikao cha kupitia na kuboresha Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, ni baada ya kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Flomi, Novemba 19, 2024 Morogoro.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni