Nav bar

Jumanne, 17 Desemba 2024

DKT KIJAJI AIAGIZA NARCO KUZALISHA MBEGU ZA MIFUGO, MALISHO KWA WINGI

◼️Ataka visima 6  vya maji NARCO kukamilishwa Kabla ya  January 5, 2025 

Waziri wa Mifugo na  Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameiagiza Kampuni ya Ranchi za Taifa NARCO iliyopo Kongwa Jijini Dodoma Kuongeza wigo wa Uzalishaji wa Mbegu Bora za  Mifugo na Malisho itakayoongeza upatikanaji wa Nyama nchini na Kukuza uchumi wa Wafugaji.

Dkt. Kijaji ametoa maagizo hayo Leo Desemba 17, 2024 Wakati wa Ziara yake kwenye Kambuni ya Ranchi za Taifa NARCO na kuahidi kurudi Januari 5, 2025 ili kuona utekelezaji wa maagizo hayo.

" NARCO Mnajukumu la kuzalisha mbegu bora za aina Mbalimbali, Watanzania wanahitaji mifugo inayouzika kwa urahisi  hapa ndani ya nchi na  Kimataifa tunataka kila mfugaji akiuza Ng'ombe apate Milioni Nne hivyo nawataka Mzalishe mbegu Bora kwaajili wafugaji wetu" amesema Dkt. Kijaji.

Kuhusu uzalishaji wa Mbegu za Malisho Dkt Kijaji amemwagiza Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya  Masoko Stephen Michael  kushirikiana na NARCO kukamilisha malipo ya Mkandarasi wa mradi wa visima sita wenye thamani ya milioni 700 ili visima hivyo vianze kutumika kuzalishia malisho.

" Tumetembelea mradi wa Visima hapa Narco ni mradi mkubwa serikali imetoa milioni 700 lakini umekwama kwa sababu ya madai ya Mkandarasi, sasa nataka nitakaporudi hapa Januari 5, 2025 Visima na Mabirika haya ya kunyweshea Ng'ombe  niyakute yameanza  kutumika" alisema  Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Bodi ya NARCO Aziz Mrima  amesema bodi hiyo inajukumu la kuifanya kampuni hiyo kuzalisha  mbegu bora za mifugo zitakazoweza kushindana na wafugaji wengine barani afrika hivyo ameahidi kuyatekeleza  maelekezo ya Waziri Dkt. Kijaji.

Naye Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko Stephen Michael  katika kutekeleza maelekezo hayo idara yake itaendelea kufuatilia ili kukamilika mradi huo ambapo hadi sasa tayari Bilioni 3.2 zimepatikana kwaajili ya Malipo hayo.

                                                                    
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (aliyonyoosha mkono), akimuuliza Kaimu Meneja wa Ranchi za Taifa (NARCO LTD), Dkt. Nickson Mbise, juu ya aina na sifa ya ng'ombe wanaopatikana katika Ranchi ya Taifa ya Kongwa, mara alipowasili Ranchi ya Kongwa kwa ajili ya Ziara fupi ya Kikazi, Disemba 17, 2024 Kongwa - Dodoma.

 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji (wa kwanza kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ndg. Stephen Michael, mara alipowasili Ranchi ya Kongwa kwa ajili ya Ziara fupi ya Kikazi, Disemba 17, 2024 Kongwa - Dodoma.



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO LTD), Ndg. Mohammedi Zuberi Mbwana, akitoa Ripoti ya Utendaji kazi wa NARCO, mara alipowasili Ranchi ya Kongwa kwa ajili ya Ziara fupi ya Kikazi, Disemba 17, 2024 Kongwa - Dodoma.



MKurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Maliso na Rasilimali za vyakula za Mifugo. Dkt. Asimwe Rwiguza (wa tatu kulia), akimuelezea Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba (wa kwanza kushoto), sifa za malisho ya majani aina ya Juncao, mara alipowasili Ranchi ya Kongwa kwa ajili ya Ziara fupi ya Kikazi, Disemba 17, 2024 Kongwa - Dodoma.










Hakuna maoni:

Chapisha Maoni