WATAALAM 155 WA WANYAMA WAPATIWA USAJILI 

Na. Stanley Brayton, WMUV

◾ Vituo 69 kupewa Usajili katika Utoaji Huduma za Afya ya Wanyama.

Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) limekamilisha mapitio kwa ajili ya kusajili Wataalam wa Wanyama wenye sifa stahiki, pamoja na Vituo mbalimbali vya kutoa Huduma za Afya ya Wanyama, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Sheria ya Veterinari SURA 319.

Akizungumza katika Kikao cha 63 cha Baraza, leo Mei 23 2026 Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), ambaye  ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka amesema Baraza limepitia na kuridhia kuwapa usajili Wataalam wa Wanyama 155 na Vituo vya Utoaji Huduma za Wanyama 69, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo.

“usajili huu umefanyika kwa kuzingatia Sheria ya Veterinari SURA 319, pamoja na Kanuni mbalimbali na miongozo ambayo imeangalia uhalali na vigezo mbalimbali stahiki vya Wataalam” amesema Prof. Kusiluka

Aidha, Prof. Kusiluka amewataka Wataalam hao na Vituo hivyo kutoa Huduma hizo kwa kuzungatia Sheria, taratibu, Miongozo na Kanuni zinavyowataka.



Mwenyekiti wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka, akizungumza na Wajumbe wa Baraza juu umuhimu wa utekelezaji wa shughuli Baraza kufanyika kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya 2050, katika Kikao cha 63 cha Baraza, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Gerwill, Mei 23, 2026 Dodoma.

Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Dkt. Amani Kilemile, akielezea hatua na mchakato mzima wanaoutumia katika kusajili na kutoa leseni kwa Wataalam wa Wanyama, katika Kikao cha 63 cha Baraza, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Gerwill, Mei 23, 2026 Dodoma.

Mjumbe wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) ambaye pia ni Wakili Mwandamizi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi. Mariam Haji, akitoa ufafanuzi wa hatua stahiki za kisheria zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kufanya mapitio na kusajili Wataalam wa Wanyama, katika Kikao cha 63 cha Baraza, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Gerwill, Mei 23, 2026 Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), wakipitia Orodha ya Maombi ya Usajili na Leseni ya utoaji Huduma za Afya ya Wanyama, katika Kikao cha 63 cha Baraza, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Gerwill, Mei 23, 2026 Dodoma.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO