Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiongea na Uongozi wa Kampuni ya Meli ya
Albacora alipokutana nao kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali
na Kampuni hiyo hususan kwenye eneo la Uvuvi wa Bahari Kuu. Mhe. Ulega
alikutana na Uongozi huo jijini Dar es Salaam Machi 14, 2023. Uongozi wa
Kampuni ya Albacora uliongozwa na Mkurugenzi wa Meli, Bw. Imanol Loinaz.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akimuonesha Mkurugenzi wa Meli za Albacora, Bw.
Imanol Loinaz maelezo yaliyopo katika Kitabu cha Ilani ya ya Uchaguzi ya Chama
cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 - 2025 yanayosisitiza kuhusu Uvuvi wa bahari kuu
wakati wa kikao chao kifupi kilichofanyika jijini Dar es Salaam Machi 14, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Meli za Albacora, Bw. Imanol Loinaz (wa pili kushoto) muda mfupi baada ya kumaliza kikao chao kifupi kilichofanyika jijini Dar es Salaam Machi 14, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA), Dkt. Emmanuel Sweke.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni