Mkuu wa Kikosi cha 27KJ
Makoko mkoani Mara, Lt. Col. Simon Rugaimukamu (kulia) akiwaeleza wataalam
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu
namna walivyowapokea vijana ambao wamepelekwa kwa ajili ya kupata mafunzo kwa
vitendo kuhusu ufugaji wa samaki kwenye vizimba ambapo ameiomba Wizara
kukitumia kituo hicho kama shamba darasa ili vijana na wavuvi waweze kujifunza.
(15.03.2023)
Afisa Uvuvi Mwandamizi, Bi.
Kresensia Mtweve akizungumza na vijana waliopo kwenye kituo cha 27KJ Makoko
mkoani Mara (hawapo pichani) kwa ajili ya kupata mafunzo kwa vitendo kuhusu
ufugaji wa samaki kwenye vizimba wakati wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na
Uvuvi na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu walipotembelea kituo hicho
kuona namna mafunzo hayo yanavyoendeshwa ambapo amewasihi vijana hao kutumia
elimu waliyofundishwa ili kuleta tija katika ufugaji. (15.03.2023)
Picha ya pamoja ya wataalam
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu
na vijana wanaopata mafunzo kwa vitendo kwenye kituo cha 27KJ Makoko mkoani
Mara mara baada ya kukagua na kunzungumza na vujana hao. (15.03.2023)
Baadhi ya Vizimba vilivyopo
kwenye kikosi cha 27KJ Makoko mkoni Mara vinavyotumika kufugia samaki.
(15.03.2023)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni