Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega(kulia) akimueleza jambo Balozi wa Tanzania nchini Korea, Balozi Togolani Mavura walipokutana ofisini kwake jijini Dodoma mapema leo Machi 8, 2023. lengo ni kujadiliana kuhusu fursa za ushirikiano baina ya nchi hizo mbili kwenye kukuza na kuimarisha uchumi wa buluu nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe. Balozi Togolani Mavura (kushoto) akiongea na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega walipokutana ofisini kwa Waziri huyo jijini Dodoma Machi 8, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Korea, Mhe. Balozi Togolani Mavura (kulia kwake) muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo yao mapema leo Machi 8, 2023. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Bi. Agness Meena. Wengine katika picha ni Wataalam kutoka Wizarani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni