TANZANIA LIVESTOCK MODERNIZATION INITIATIVE
The Tanzania Livestock Modernization Initiative (TLMI) is intended to support the progressive and adaptive development of a vibrant Livestock Sector which is responsive to growing demands and emerging commercial opportunities, and which is economically, socially and environmentally sustainable.
The TLMI aims to harness the potential of meat, diary and poultry sectors for poverty alleviation through improvements across the value chains including improvements in security and access to grazing, access to markets, quality and safely of Livestock products, processing and value addition. It will identify the coordinated intervation needed across sectors to support these improvements and the necessary regulatory environment to ensure safe and healthy Livestock products.
GOALS
The overall goal of the TLMI is to increase food and nutrition security and food safety, create employment opportunities and contribute to the national economy, social and sustainable environment.
PURPOSE
The purpose of TLMI is to improve the Livelihoods of traditional an small holder Livestock farmers and contribution of the sector to the national economy.
Mhe.Prof Peter Msolla (Mb) Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya kilimo, Mifugo na Maji;
Mhe. Jb Ndugai (Mb), mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mhe. Mku wa Wilaya ya Kongwa;
Dkt. Yohaa Budeba, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi;
Waheshimiwa Madiwani,
Wakurugenzi wa Wizara,
Meneja Mkuu wa NARVCO,
Mameneja wa RANCHI za NARCO,
Wanahabari,
Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukusanyika mahali hapa siku hii ya leo tukiwa wazima wenye afya. Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya NARCO kunialika kuja kutembelea rachi ya kongwa na kufungua duka lenu la nyama katika mamlaka ya mji mdogo wa Kibaigwa ambalolinamilikiwa na ranchi ya kongwa.
Meneja Mkuu, tangu nilipoteuliwa na mheshimiwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete nimekuwa nisisitiza kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake zote kubadili fikra katika kutekelezea majukumu ili kuleta tija katika sekta za Mifugo na Uvuvi. Hii pamoja na kuwa na ubunifu katika uzalishaji na kutafuta rasilimali fedha ikizingatiwa kuwa kiasi kinachotolewa na hazina hakiwezi kutosheleza mahitaji ya taifa zima. Hivyo napenda niwapongeze kwa hatua moja mliyofikia ya kuona umuhimu wa kufungua duka hapa Kibaigwa ili kuwahakikishia wananchi walio karibu na Ranchi yenu ya Kongwa wanafaidika kwa kupata nyama iliyobora.
Meneja Mkuu, pamoja na kufungua duka katika mji mdogo wa Kibaigwa lakini bado kuhakikisha kuwa wafugaji wanaozunguka wananufaika na elimu ya ufugaji bora na kubadilisha aina ya mifugo waliyonayo ili kuwza kuongeza tija katika uzalishaji na kunufaika kwa kuweza kuuuza mifugo walio wengi huchukua muda mrefu takriban zaidi ya miaka minne hadi kufikia uzito unaokubalisokoni. Jambo hilo linawafanya wawe watumwa wa mifugo yao wenyewe. Wafugaji wanaowazunguka watafaidika zaid kwa kuwa nyie ndio mtakuwa soko kubwa la mifugo ndani na nje nchi hatimaye kuongeza kwa vitendo maelekezo ya ILani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ambayo pamoja na mambo inaelekeza;
(a) "Kuhimiza wafugaji watekeleze kanuni za ufugaji bora na kuingiakatika ufugaji endelevu wa kisiasa na kibiashara unaozingatia hifadhi ya mazingira" na
(b) "Kuendeleza elimu kwa Wafugaji ili wajue kuwa mifugo waliyonayo ni mali inayoweza kuvuniwa katika umri na uzito muafaka unaokidhi mahitaji ya soko, ili kuwaondolea umaskini wao badala ya kuridhika na wingi wa mifugo iliyo duni na maisha ya kuhamahama.
Aidha, Ilani ya uchunguzi wa CCM inaelekea kusisitiza kuwa:
"Pamoja na mafanikio mengi tuliyopata na changamoto zilizojitokeza fusra kubwa ya kuendelea kujenga uchumi wa kisasaili kumudu ushindani katika mazingira ya utandawazi na kuongea tija kwa siasa zaidi. Nchi yetu inatambua kuwa changamoto kubwa inayotukabili ni suala la Mapinduzi YA Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Viwanda.
Meneja mkuu, katika kutekeleza Ilani hii, Wizara yangu ilifanyika mkutano na bodi pamoja na Menejimetiya ya NARCO tarehe 4 Februari, 2014 na kuweka mikakati ambayo itaiwezesha NARCO kuinuka kiuchumi na kufika lengo. Wizara imekuwa ikihimiza umuhimu wa kuendeleza sekta hii ya mifugo katika mnyororo wake wote wa thamani ikianzia na kuendeleza mashamba makubwa, ya kati na madogo ya mifugo yanayoendeshwa kibiashara yaweza kuleta maendeleo ya haraka katika sekta ya ufugaji, kwa kutoa huduma mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora za mifugo na malisho, na kuzisambaza kisasa, viwanda vya nyama na maduka ya kisasa ya kuuza nyama iliyo bora.
Meneja Mkuu, Ushauri wangu kwenu ni kuwa kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) iendeee kwa kasi na mfumo wa uendeshaji unaolenga kwenye uzalishaji wa kibiashara na unaozingatia matakwa ya soko na hatimaye kuchangia katika juhudi za taifa za kupunguza umaskini (MKUKUTA).
Pia endeleeni na kutoa mafunzo na mbinu za kisiasa za kuendesha sekta hii ya mifugo kibiashara kwa kupitia wataalamu wenu walioko katika Ranchi zenu kwa wafugaji ambao ni majirani zenu. Ni muhimu kutambua kwamba katika mfumo wa soko huhru na utandawazi, anayezalisha kwa ufanisi, ubora na kwa gharama nafuu diye atakayehimili ushindani. Hivyo ni muhimu kubadili mtizamo wa uzalishaji kwa kulenga mahitaji ya soko na NARCO muendelee kueneza dhana hii.
Meneja Mkuu, Ranchi za NARCO nazihimiza ziendelee na jitihada za kuziendeleza kwa kushiikiana na sekta binafsi ili zipate mitaji mikubwa ya uzalishaji, kunenepesha na kuuza idadi kubwa ya ng'ombe bora au mazao yake ila mwaka kwa soko la ndani na nje ya nchi. Hivyo natoa agizo kwa menejimenti ya NARCO kuendelea kuweka mipango madhubuti na iliyo endelevu ya kuvutia sekta binafsi.
Meneja Mkuu, Serikali inajitahidi kuweka mazingira mazuri yakayovutiwa uwekezaji mkubwa katika viwanda vya kusindika nyama. Ninatoa wito kwa mara nyingine kwa sekta binafsi nchini ijitokeze na itumie fursa hii kuwekeza katika sekta hii ya nyama kwa kujenga machinjio za kisasa na viwanda vya nyama. Pia ranchi hizi za NARCO na ranchi ndogondogo zilizomilikishwa kwa watanzania na zile za watu binafsi nazihimiza zitilie mkazo wa kuzalisha mifugo kwa wingi yenye ubora na yenye tija kwa sababu ya kuwepo na soko la uhakika hapa nchini na nje ya nchi.
Aidha, nitumie nafasi hii kuwahimiza watanzania kuanza sasa kupenda kununua chakula kaa vile nyama itolewayo katika mazingira mazuri na salama ili kulinda afya zao. Hayo niyo maendeleo. Tunaondoana na matumizi ya nyama ambayo haikukaguliwa na kutoka kwenye maeneo machafu eti tu kwa kuwa tumezoea. Hali hiyo ndiyo tufanya tuugue magonjwa bila hata kujua yametoka wapi. Hivyo mahali lilipo duka hili ni eneo la kimkakati kwani licha ya wananchi kibaigwa, lakini pia litahudumia viongozi wengi wanaosafiri kati ya Dodoma na Dar es Salaam.
Meneja Mkuu, ninatoa wito kwa wafanya biashara wa bidhaa za mifugo hapa kibaigwa na sehemu zote nchini, kuanzisha maduka mengine yenye ubora kama hili tuliofungua leo ili kuwezesha wananchi kupata nya ma safi isiyo na magonjwa ili kuboresha afya ya walaji.
Meneja Mkuu, baada ya kusemna haya sasa nitamke kuwa duka lenu la nyamala kisasa limezinduliwa.
Mhe. Jb Ndugai (Mb), mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mhe. Mku wa Wilaya ya Kongwa;
Dkt. Yohaa Budeba, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi;
Waheshimiwa Madiwani,
Wakurugenzi wa Wizara,
Meneja Mkuu wa NARVCO,
Mameneja wa RANCHI za NARCO,
Wanahabari,
Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukusanyika mahali hapa siku hii ya leo tukiwa wazima wenye afya. Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya NARCO kunialika kuja kutembelea rachi ya kongwa na kufungua duka lenu la nyama katika mamlaka ya mji mdogo wa Kibaigwa ambalolinamilikiwa na ranchi ya kongwa.
Meneja Mkuu, tangu nilipoteuliwa na mheshimiwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete nimekuwa nisisitiza kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake zote kubadili fikra katika kutekelezea majukumu ili kuleta tija katika sekta za Mifugo na Uvuvi. Hii pamoja na kuwa na ubunifu katika uzalishaji na kutafuta rasilimali fedha ikizingatiwa kuwa kiasi kinachotolewa na hazina hakiwezi kutosheleza mahitaji ya taifa zima. Hivyo napenda niwapongeze kwa hatua moja mliyofikia ya kuona umuhimu wa kufungua duka hapa Kibaigwa ili kuwahakikishia wananchi walio karibu na Ranchi yenu ya Kongwa wanafaidika kwa kupata nyama iliyobora.
Meneja Mkuu, pamoja na kufungua duka katika mji mdogo wa Kibaigwa lakini bado kuhakikisha kuwa wafugaji wanaozunguka wananufaika na elimu ya ufugaji bora na kubadilisha aina ya mifugo waliyonayo ili kuwza kuongeza tija katika uzalishaji na kunufaika kwa kuweza kuuuza mifugo walio wengi huchukua muda mrefu takriban zaidi ya miaka minne hadi kufikia uzito unaokubalisokoni. Jambo hilo linawafanya wawe watumwa wa mifugo yao wenyewe. Wafugaji wanaowazunguka watafaidika zaid kwa kuwa nyie ndio mtakuwa soko kubwa la mifugo ndani na nje nchi hatimaye kuongeza kwa vitendo maelekezo ya ILani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ambayo pamoja na mambo inaelekeza;
(a) "Kuhimiza wafugaji watekeleze kanuni za ufugaji bora na kuingiakatika ufugaji endelevu wa kisiasa na kibiashara unaozingatia hifadhi ya mazingira" na
(b) "Kuendeleza elimu kwa Wafugaji ili wajue kuwa mifugo waliyonayo ni mali inayoweza kuvuniwa katika umri na uzito muafaka unaokidhi mahitaji ya soko, ili kuwaondolea umaskini wao badala ya kuridhika na wingi wa mifugo iliyo duni na maisha ya kuhamahama.
Aidha, Ilani ya uchunguzi wa CCM inaelekea kusisitiza kuwa:
"Pamoja na mafanikio mengi tuliyopata na changamoto zilizojitokeza fusra kubwa ya kuendelea kujenga uchumi wa kisasaili kumudu ushindani katika mazingira ya utandawazi na kuongea tija kwa siasa zaidi. Nchi yetu inatambua kuwa changamoto kubwa inayotukabili ni suala la Mapinduzi YA Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Viwanda.
Meneja mkuu, katika kutekeleza Ilani hii, Wizara yangu ilifanyika mkutano na bodi pamoja na Menejimetiya ya NARCO tarehe 4 Februari, 2014 na kuweka mikakati ambayo itaiwezesha NARCO kuinuka kiuchumi na kufika lengo. Wizara imekuwa ikihimiza umuhimu wa kuendeleza sekta hii ya mifugo katika mnyororo wake wote wa thamani ikianzia na kuendeleza mashamba makubwa, ya kati na madogo ya mifugo yanayoendeshwa kibiashara yaweza kuleta maendeleo ya haraka katika sekta ya ufugaji, kwa kutoa huduma mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora za mifugo na malisho, na kuzisambaza kisasa, viwanda vya nyama na maduka ya kisasa ya kuuza nyama iliyo bora.
Meneja Mkuu, Ushauri wangu kwenu ni kuwa kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) iendeee kwa kasi na mfumo wa uendeshaji unaolenga kwenye uzalishaji wa kibiashara na unaozingatia matakwa ya soko na hatimaye kuchangia katika juhudi za taifa za kupunguza umaskini (MKUKUTA).
Pia endeleeni na kutoa mafunzo na mbinu za kisiasa za kuendesha sekta hii ya mifugo kibiashara kwa kupitia wataalamu wenu walioko katika Ranchi zenu kwa wafugaji ambao ni majirani zenu. Ni muhimu kutambua kwamba katika mfumo wa soko huhru na utandawazi, anayezalisha kwa ufanisi, ubora na kwa gharama nafuu diye atakayehimili ushindani. Hivyo ni muhimu kubadili mtizamo wa uzalishaji kwa kulenga mahitaji ya soko na NARCO muendelee kueneza dhana hii.
Meneja Mkuu, Ranchi za NARCO nazihimiza ziendelee na jitihada za kuziendeleza kwa kushiikiana na sekta binafsi ili zipate mitaji mikubwa ya uzalishaji, kunenepesha na kuuza idadi kubwa ya ng'ombe bora au mazao yake ila mwaka kwa soko la ndani na nje ya nchi. Hivyo natoa agizo kwa menejimenti ya NARCO kuendelea kuweka mipango madhubuti na iliyo endelevu ya kuvutia sekta binafsi.
Meneja Mkuu, Serikali inajitahidi kuweka mazingira mazuri yakayovutiwa uwekezaji mkubwa katika viwanda vya kusindika nyama. Ninatoa wito kwa mara nyingine kwa sekta binafsi nchini ijitokeze na itumie fursa hii kuwekeza katika sekta hii ya nyama kwa kujenga machinjio za kisasa na viwanda vya nyama. Pia ranchi hizi za NARCO na ranchi ndogondogo zilizomilikishwa kwa watanzania na zile za watu binafsi nazihimiza zitilie mkazo wa kuzalisha mifugo kwa wingi yenye ubora na yenye tija kwa sababu ya kuwepo na soko la uhakika hapa nchini na nje ya nchi.
Aidha, nitumie nafasi hii kuwahimiza watanzania kuanza sasa kupenda kununua chakula kaa vile nyama itolewayo katika mazingira mazuri na salama ili kulinda afya zao. Hayo niyo maendeleo. Tunaondoana na matumizi ya nyama ambayo haikukaguliwa na kutoka kwenye maeneo machafu eti tu kwa kuwa tumezoea. Hali hiyo ndiyo tufanya tuugue magonjwa bila hata kujua yametoka wapi. Hivyo mahali lilipo duka hili ni eneo la kimkakati kwani licha ya wananchi kibaigwa, lakini pia litahudumia viongozi wengi wanaosafiri kati ya Dodoma na Dar es Salaam.
Meneja Mkuu, ninatoa wito kwa wafanya biashara wa bidhaa za mifugo hapa kibaigwa na sehemu zote nchini, kuanzisha maduka mengine yenye ubora kama hili tuliofungua leo ili kuwezesha wananchi kupata nya ma safi isiyo na magonjwa ili kuboresha afya ya walaji.
Meneja Mkuu, baada ya kusemna haya sasa nitamke kuwa duka lenu la nyamala kisasa limezinduliwa.
HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA
UVUVI MHESHIMIWA DKT. TITUS MLENGEYA KAMANI (MB) ALIYOITOA KUMKARIBISHA WAZIRI
MKUU – MGENI RASMI KUTOA HOTUBA YAKE KATIKA MKUTANO WA WADAU WA MIFUGO
ULIOFAYIKA MWANZA, TAREHE 5 - 7 SEPTEMBA, 2014
Mhe.
Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,
Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri,
Mhe. Injinia Evarist Welle Ndikilo, Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza,
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa
na Wilaya,
Mhe. Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza,
Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa,
Waheshimiwa Meya wa Majiji, Miji na Manispaa na
Wenyeviti wa Halmashauri,
Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri,
Wawakilishi wa Mashirika ya Serikali, yasiyo ya Serikali
na Sekta Binafsi,
Wafugaji,
Wageni waalikwa,
Mabibi na Mabwana,
Asalaam Aleykum, Tumsifu Yesu Kristu, Bwana
Asifiwe
1. Mheshimiwa Waziri Mkuu, awali ya yote napenda kuchukua
nafasi hii, kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha leo hapa Mwanza kwenye
mkutano huu wa wadau wa mifugo tukiwa na afya njema. Nitumie nafasi hii
kukushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuitisha mkutano huu na kwa
kukubali kwako kutufungulia na kisha kuwa Mwenyekiti wa mkutano huu. Aidha, nachukua
nafasi hii kuushukuru uongozi wa Mkoa na wananchi wa Mwanza kwa kukubali kuwa wenyeji
wetu na kwa mapokezi mazuri waliyotupatia. Nipende pia kuwashukuru washiriki
wote kwa kukubali wito wa kuja kwenye mkutano huu muhimu.
2.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu, Uzalishaji
wa mazao ya mifugo nchini bado ni mdogo kwani inakadiriwa kuwa kila Mtanzania anakula
wastani wa kilo 11 za nyama, lita 45 za maziwa na mayai 72 kwa mwaka. Ulaji huo, haujafikia
viwango vya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa ambavyo ni kilo 50 za nyama, lita 200 za maziwa na mayai 300
kwa mtu kwa mwaka. Inakisiwa kwamba mifugo tuliyonayo nchini inazalisha chakula
(nyama, maziwa na mayai) yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 20. Kama ingekuwa chakula
hicho kinaagizwa kutoka nje ya nchi, kiasi hicho cha fedha kisingepatikana kutoka
kwenye bajeti yetu ambayo ni shilingi trilioni
19.
3.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu, pamoja
na uchangiaji huo katika chakula, sekta ya mifugo katika mwaka 2013/2014
ilichangia asilimia 4.4 katika pato
la Taifa. Sekta hii ingeweza kuchangia zaidi kama changamoto zinazoikabili
zingetatuliwa hivyo ni vyema sekta hii ya mifugo ikasaidiwa kutatua changamoto
zilizopo ili iweze kuwa endelevu na kuchangia zaidi katika afya na kipato cha
watanzania na uchumi wa nchi kwa ujumla. Ni matumaini yangu kuwa katika mkutano
huu tutajadili kwa kina na kutoa mapendekezo kuhusu tufanye nini ili sekta ya
mifugo ichangie zaidi katika uchumi wa Taifa.
4. Mheshimiwa
Waziri Mkuu, Mkutano
huu unafanyika katika kipindi ambacho sekta ya mifugo na hasa wafugaji wa
asili, wakiwa na changamoto nyingi. Ninaamini yale yote yatakayojadiliwa hapa
yataleta ufumbuzi wa kudumu wa changamoto mbalimbali zinazokabili sekta hii
muhimu katika uchumi wa Taifa. Sekta ya mifugo ina changamoto nyingi
zinazohitaji kupatiwa ufumbuzi wa kudumu. Naomba nitaje baadhi ya changamoto zinazoikabili
sekta ya mifugo.
Nyanda
Duni za malisho
5. Mheshimiwa
Waziri Mkuu, Tatizo
la upatikanaji wa malisho hapa nchini linaendelea kuongezeka hasa wakati wa
kiangazi ambapo malisho hupungua kwa kiasi kikubwa. Tatizo hilo limesababisha
maafa makubwa hasa kwa wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi. Wafugaji wanaohama wamekuwa wakiongezeka
kutoka maeneo yenye mifugo mingi na kwenda katika mikoa ya kusini ambako maeneo
mengi yanatumika kwa kilimo. Hali hii imesababisha kuwepo kwa migogoro kati ya
wafugaji na wakulima. Kwa mfano, migogoro ya wafugaji na wakulima Mkoani
Morogoro (Kilosa na Mvomero) na Mkoa wa Pwani (Ikwiriri – Rufiji).
Uhaba
wa Maji kwa Mifugo
6. Mheshimiwa
Waziri Mkuu, Sambamba
na tatizo la malisho, upatikanaji wa maji kwa ajili ya mifugo limekuwa pia ni
tatizo kubwa. Katika kipindi cha kiangazi maji hukauka hata katika baadhi ya
mabwawa na malambo na kufanya wafugaji kuhangaika na kuhama ili kunywesha
mifugo yao. Pamoja na juhudi za Wizara za kuchimba malambo mapya na kukarabati yaliyopo,
bado malambo haya hayatoshi kutokana na wingi wa mifugo. Ujenzi na ukarabati wa
malambo nchini unahitaji rasilimali fedha nyingi ili kuipatia mifugo maji ya
kutosha.
Magonjwa ya Mifugo
7.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu,
Magonjwa ya mifugo pia ni eneo ambalo linatakiwa kutengenezewa mikakati ya
kudumu ili iendelee kuwa na afya na kuzalisha kwa tija. Magonjwa yanayoathiri
mifugo kwa kiasi kikubwa (asilimia 70) ni yale yanayoenezwa na kupe. Serikali
imejitahidi kujenga na kukarabati majosho na pia kununua dawa za kuogesha
mifugo lakini bado magonjwa hayo yanatishia ustawi wa mifugo hapa nchini. Kati
ya mwaka 2010/2011 na 2013/2014 Serikali ilitumia shilingi bilioni 4.2 kama ruzuku
kununua na kusambaza lita 252,138 za
dawa ya kuogesha mifugo.
8.
Wizara imeanza kutenga Maeneo Huru ya
Magonjwa ya Mifugo ili kuzuia ueneaji wa magonjwa katika maeneo maalumu kwa
lengo la kuimarisha biashara ya mifugo na mazao yatokanayo na mifugo. Katika
kuendeleza azma hiyo, Wizara imeimarisha miundombinu ya Kituo cha Uchunguzi wa
Magonjwa ya Mifugo cha Kanda ya Kusini na kutoa mafunzo kwa wataalamu wake.
Hata hivyo, hili ni eneo moja tu na inatakiwa kutenga maeneo ya kutosha nchini ili kuweza kuhudumia mifugo ya kutosha.
Uzalishaji na Usambazaji wa
Teknolojia za Mifugo
9. Mheshimiwa
Waziri Mkuu,
idadi ya mifugo bora hasa ng’ombe wa maziwa na wa nyama walionenepeshwa ni ndogo
sana na hivyo bidhaa za maziwa na nyama hazitoshelezi na kusababisha kuagizwa
nje ya nchi ili kutosheleza mahitaji. Idadi ya ng’ombe wa maziwa imeongezeka
kutoka 605,000 mwaka 2009 hadi 720,000 mwaka 2013 na kuchangia kiasi
cha asilimia 30 cha maziwa
yanayozalishwa nchini. Idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na nchi jirani ya
Kenya ambayo ina ng’ombe wa kisasa wa maziwa zaidi ya milioni 4. Aidha, takriban ng’ombe 175,000 walinenepeshwa katika mwaka 2013/2014, kiasi ambacho ni
kidogo sana ikilinganishwa na idadi ya ng’ombe ya milioni 22.8.
10.Mheshimiwa
Waziri Mkuu,
teknolojia ya uhimilishaji inatumika kuzalisha na kupata ng’ombe wa kisasa
wanaozalisha maziwa na nyama zaidi. Wizara imeendelea kuimarisha Kituo cha
Taifa cha Uhimilishaji (NAIC – Usa river Arusha) pamoja na vituo vya kanda vya
uhimilishaji 6 vya Kanda ya Ziwa
(Mwanza), Mashariki (Kibaha), Kati (Dodoma), Nyanda za Juu Kusini (Mbeya),
Kusini (Lindi), Kanda ya Magharibi (Mpanda) na Sao Hill. Hata hivyo, elimu ya
kutosha inahitajika kutolewa kwa wafugaji katika suala la uhimilishaji.
Upatikanaji wa Masoko ya Mifugo na
Bidhaa zake
·
Mifugo
11.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu,
masoko ya mifugo na bidhaa zake ndani na nje ya nchi ni suala muhimu kwa
maendeleo ya sekta hii ya mifugo. Idadi ya mifugo iliyouzwa minadani imeendelea
kuongezeka mwaka hadi mwaka kutoka ng’ombe 857,208,
mbuzi 682,992 na kondoo 122,035
mwaka 2009/2010 hadi ng’ombe 1,215,541,
mbuzi 960,199 na kondoo 209,292 mwaka 2013/2014. Ongezeko hilo
bado ni dogo ukilinganisha ni idadi yote ya mifugo iliyopo ambayo inatakiwa
kuvunwa kwa asilimia 25 kila mwaka. Mauzo
ya mifugo minadani yanaendelea kuongezeka kutokana na kuimarisha miundombinu ya
minada. Hata hivyo, minada mingi iko katika hali isiyo ya kuridhisha na
inahitaji kuimarishwa zaidi ili ifanye kazi kwa ufanisi. Uuzaji wa mifugo nje
ya nchi bado ni kidogo sana kwani soko linalotegemewa ni, Comoro na nchi jirani
ambazo mahitaji yao yanabadilika mara kwa mara.
·
Zao la Nyama
12.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu, mahitaji
ya nyama kwa ajili ya soko la nje yameendelea kukua lakini tumeshindwa
kuyafikia kutokana na kukosekana kwa machinjio na viwanda vya kuchakata nyama
zinazokidhi viwango vya kimataifa. Kwa mfano, katika mwaka 2012 nchi ya Misiri
na Zambia zilihitaji tani 50,000 kwa
mwaka wakati uwezo wetu ni tani 23,000. Soko la nyama linaweza kuwa la uhakika na kuliingizia
Taifa fedha nyingi za kigeni kama tungekuwa na machinjio na viwanda vikubwa vya
kusindika nyama. Hivyo, ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Ruvu ukikamilika
utaongeza mauzo ya nyama bora ndani na nje ya nchi. Aidha, ufugaji wa ngombe wa
nyama kisasa ni muhimu ili kuongeza upatikanaji wa nyama bora kwa ajili ya
masoko maalumu na kuuza nje ya nchi. Hata hivyo, ufugaji huu unahitaji
raslimali kubwa ambazo zimekuwa vigumu kupatikana kutokana na masharti magumu
ya kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha.
·
Zao la Maziwa
13.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu, uzalishaji
wa maziwa umeendelea kuongezeka kutokana na kuongezeka kwa wingi wa mifugo.
Hata hivyo, ukusanyaji wa maziwa hayo kwa ajili ya masoko ya ndani na
usindikaji umekuwa kidogo sana kutokana na miundombinu hafifu ya ukusanyaji na
usindikaji. Kwa sasa tunavyo viwanda 74
vyenye uwezo wa kusindika lita 403,000
lakini vinazalisha lita 139,800. Aidha,
unywaji wa maziwa nchini bado ni mdogo na hivyo ni muhimu kupanua soko la ndani
ili kuongeza uzalishaji, usindikaji wa maziwa na ajira. Programu inayoratibiwa
na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ya Unywaji wa Maziwa Shuleni, kupitia
Bodi ya Maziwa Tanzania inatakiwa kupanuliwa ili kuongeza wigo wa soko la
maziwa la ndani.
·
Zao la Ngozi
14.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu, Zao la ngozi ni zao la mifugo muhimu ambalo likiendelezwa
lina mchango mkubwa kwa wafugaji na uchumi wa Taifa kwa ujumla. Hata hivyo, zao
hili linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ubora hafifu na
makusanyo madogo ya ngozi kutokana na ufugaji usiozingatia kanuni bora za
ufugaji ambazo ni aina duni za mifugo, lishe duni kwa mifugo, umri mkubwa
wakati wa kuchinjwa, upigaji chapa ovyo katika maeneo muhimu ya ngozi,
mikwaruzo itokanayo na miiba au vitu vyenye ncha kali na kupiga viboko. Aidha,
elimu duni, mapungufu katika ujuzi wa utendaji kazi kwa wachunaji na wawambaji
na kukosekana kwa mbinu za ujasiriamali kwa wafanyabiashara wa ngozi na hali
mbaya ya miundo mbinu ya machinjio, makaro ya kuchinjia, mabanda ya kukaushia
na maghala ya kuhifadhia ngozi vinachangia pia katika kupunguza ubora na thamani ya ngozi kwa siku za karibuni
tatizo la utoroshwaji wa ngozi nje ya nchi, kupungua kwa uwezo wa viwanda vya
kusindika ngozi, bei isiyotabirika ya ngozi zilizosindikwa kwa kiwango cha wet
blue na ushindani usio wa haki wa bidhaa
hafifu za ngozi (plastiki na mitumba) zinazoingizwa kutoka nje zimeendelea
kudumuza tasnia ya ngozi nchini.
Usimamizi
hafifu wa Sheria za Mifugo na Kanuni
15.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu,
ubora wa mifugo, mazao yatokanayo na mifugo, pembejeo na huduma za mifugo
husimamiwa na sheria 10 za mifugo
pamoja na kanuni na miongozo mbalimbali.
Usimamizi mzuri wa sheria huongeza ubora wa bidhaa za mifugo na hivyo
kuboresha masoko ya ndani na nje ya nchi. Kutozingatiwa kwa sheria na kanuni
zake kumesababisha bidhaa na huduma nyingi za mifugo kuwa duni na hivyo
kusababisha bidhaa na mazao ya mifugo yanayozalishwa kuwa na ubora hafifu.
16.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu, sekta
hii pia inasimamiwa na sheria nyingine ambazo usimamizi na utekelezaji wake unawataka
wadau kulipa tozo na kodi mbalimbali ambazo zimeendelea kusababisha malalamiko
kutoka kwa wadau. Kwa mfano, wadau wa maziwa wanalalamikia matakwa ya sheria zaidi
ya kumi (10) ambazo zipo katika mamlaka mbalimbali kisheria na zinasimamia shughuli
zinazofanana katika tasnia ya maziwa. Changamoto iliyopo ni jinsi ya kupunguza mzigo
wa tozo na kodi zinatozwa na mamlaka mbalimbali kwenye zao lile lile.
17.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu,
ili kuleta mapinduzi katika sekta ya mifugo, changamoto hizi na zingine ambazo
hazikutajwa hapa, zinatakiwa kupatiwa ufumbuzi. Wizara kwa kushirikiana na
wadau wake wanatakiwa kushirikiana kwa karibu ili kupanga mikakati ya pamoja ya
kutatua changamoto zilizopo.
18.
Mheshimiwa
Waziri Mkuu, baada
ya kueleza changamoto hizo, napenda kukuarifu kuwa kwa sasa sekta ya mifugo
inaingia katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa – BRN. Bado
tunaendelea na maandalizi stahiki ili kuanza kutekeleza mpango huo. Ni matumaini
yangu kuwa katika mpango huo sekta hii itaendelea kwa kasi zaidi ili kuongeza
ajira, kuongeza kipato na kupunguza umasikini kwa wananchi wa Tanzania.
19. Mheshimiwa
Waziri Mkuu,
mwisho, naomba nitumie nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na
wewe Mhe. Waziri Mkuu kwa kuhimiza maendeleo katika sekta ya mifugo. Hali hiyo
ikiendelea sekta hii itakua kwa haraka na kutoa mchango mkubwa katika pato la
Taifa na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania kwani, Sekta hii imeajiri
watanzania wengi.
20. Baada ya kusema haya Mhe. Waziri Mkuu, kwa heshima sasa naomba utufungulie mkutano na
hatimaye uongoze majadiliano.
AHSANTENI
SANA KWA KUNISIKILIZA
MADA ILIYOWASILISHWA NA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAKAZI
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
MADA KUHUSU USIMAMIZI WA MIGOGORO
YA ARDHI HUSUSAN KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI ILIYOWASILISHWA KWENYE MKUTANO WA
WAKUU WA MIKOA, MAKATIBU TAWALA WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA
Iliyotolewa na Prof. Anna Tibaijuka (MB)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
DODOMA
16 NOVEMBA, 2012
TAARIFA TAJWA HAPO JUU IPO KWENYE UKURASA WA MIGOGORO YA WAFUGAJI NA WATUMIAJI WENGINE WA ARDHI
MADA ILIYOWASILISHWA NA PROF KURWIJILA
MADA ILIYOWASILISHWA NA PROF. MDOE
MADA YA TAASISI YA UTAFITI YA MIFUGO TANZANIA (TALIRI)
MADA YA SEKTA YA MAZIWA TANZANIA ILIYOWASILISHWA KWENYE MKUTANO WA WADAU WA SEKTA YA MIFUGO MWANZA
ZIARA YA WAZIRI MKOA WA TANGA
HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI YA
MHESHIMIWA DKT.TITUS MLENGEYA KAMANI (MB) KATIKA UFUNGUZI WA MAONYESHO YA
KWANZA YA BIASHARA YA MAZIWA MKOA WA TANGA YALIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA TANGA FRESH LTD,KANGE- JIJINI
TANGA –TAREHE 15/08/2014
Mheshimiwa
mkuu wa mkoa wa Tanga
Katibu
tawala wa mkoa wa Tanga
Waheshimiwa
wakuu wa wilaya ,
Waheshimiwa
madiwani,
Kaimu
mwenyekiti wa chama cha wafugaji Tanzania
Katibu
wa chama cha wafugaji Tanzania
Mwenyekiti
wa jukwaa la wadau wa maziwa Tanga
Mwenyekiti
wa jukwaa la biashara ya maziwa Tanga
Mwenyekiti
wa bodi ya kiwanda cha Tanga fresh ltd,
Mwenyekiti
wa bodi ya ushirika wa maziwa (TDCU)
Wawakilishi
wa wadau wa jukwaa la maziwa Tanga ,SNV na AGRI-PROFOCUS,
Wanahabari
,
Wageni
waalikwa ,
Mabibi
na mabwana,
Awali
ya yote napenda tumshukuru mwenyezi mungu
wa rehema kwa kutuwezesha wote kushiriki katika maonyesho haya muhimu
siku hii ya leo .ndugu wanajukwaa
,wafugaji wote , na wageni wetu napenda nianze kwa kuwasalimia kwa salamu ya
wanamaziwa.MAZIWA……..
WANAJUKWAA
NA WALIKWA WOTE ………..DHAHABU NYEUPE!!!!
Ndugu
wanajukwaa,napenda kuwashukuru wanajukwaa la maziwa –tanga kwa kunichagua kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya kwanza
ya biashara ya maziwa ya Tanga ikiwa ni
mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwangu na mhe
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania
kuiongoza wizara ya maendeleo ya
mifugo na uvuvi. Napenda kusema kuwa haya ni maonyesho ya kwanza ya kipekee yanayohusu
maziwa .
Mimi
binafsi na serikali kwa ujumla
nawapongezeni sana viongozi wa jukwaa
la wadau wa maziwa Tanga na
uongozi wa mkoa wa tanga kwa umahiri wenu
wa kuratibu shughuli za maziwa.wakati nakagua mabanda ya maonyesho wiki ya unywaji wa maziwa kitaifa mjini musoma , niliahidi kuja Tanga
ili nijionee hali halisi. kinachonipa moyo zaidi ni kwamba kabla hata sijafika
tayari mmebuni kitu kingine kizuri yaani JUKWAA LA BIASHARA LA WADAU WA MAZIWA, hongereni sana.
Ndugu
wanajukwaa faida kubwa ya maonesho haya
ni kukutanisha wadau, kutathimini mafanikio yaliyofikiwa na kutatua kero za
wafugaji hususani zile zinazohusu kuongeza uzalishaji wa maziwa. Kutokana na
umuhimu huo nachukua fursa hii kuagiza maonesho haya yafanyike kila mwaka ili kuendeleza kazi hii nzuri mliyoanza.
Tanga mmeanza muongozez njia.
Nimebaini
kuwa tunaohusika pia na maonesho ya Wiki ya Maziwa na Nane Nane ni walewale,
hivyo ninashauri maonesho haya yafanyike mwezi wa Septemba ili wadau wengi
waweze kushiriki. Aidha nawapongeza sana kwa kushiriki maadhimisho ya Wiki ya
Maziwa na Nanenane na pia kuandaa maonesho haya muhimu katika ngazi ya mkoa
yaliyowezesha wadau kujionea , kukutana na kufanya biashara.
Ili
kuboresha tasnia ya maziwa sekta ya mifugo kwa ujumla, serikali inabidi ishiriki
kikamilifu kupitia wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya zote, Maafisa Mifugo,
Kilimo na Ushirika wanapaswa watoe mwongozo kwa wadau wengine wa maendeleo. Hii
ni muhimumsana ikizingatiwa kuwa tupo katika mfumo ambao ni shirikishi wa sekta
ya umma na sekta binafsi maarufu kama ‘DDP’ katika kutekeleza shughuli za
kiuchumi na maendeleo kiujumla.
Ndugu
wanajukwaa, napenda pia kumshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Katibu Tawala wa
Mkoa kwa kujitoa kikamilifu kufanikisha pamoja na malezi yao mazuri kwa Jukwaa
hili la kihistoria la Wadau wa Maziwa Mkoa wa Tanga ambalo lina mchango mkubwa
katika sekta. Katika Maad himisho ya Wiki ya Maziwa Kitaifa Mkoani Mara ni
Jukwaa pekee la Tanga lililoweza kuleta washiriki zaidi ya 40. Nawapongeza sana
Viongozi wa Jukwaa, Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh Ltd, Chama kikuu cha
Ushirika cha Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU), Shirika la Maendeleo la Uholanzi –SNV
Mtandao wa Kilimo na Biashara wa AGRI-HUB TANZANIA na wafugaji wote wa Mkoa wa
Tanga kwa ubunifu wa kuanzisha Jukwaa la Mkoa la Biashara la Maziwa ambalo ni
msaada mkubwa katika kutatua kero zao, lakini muhimu zaidi kukutana ili kufanya
biashara na kubadilishana ujuzi na elimu.
Ndugu
wanajukwaa, nichukue nafasi hii kuwapongeza jukwaa la Tanga kwa jinsi
wanavyoratibu masuala yote ya kupunguza kero na kuongeza tija kwa wafugaji na
haswa sauti ya mfugaji ngazi ya Mkoa na hivyo kuweka mazingira bora ya ufugaji.
Nimepokea kwa furaha kubwa ombi la kuwa Mgeni Rasmi katika Maonesho haya ya Kwanza ya Biashara ya
maziwa kwa kuwa tangu kuteuliwa kwangu kuiongoza Wizara ya Maendeleo ya Mifugo
na Uvuvi haya ni maoneso ya KWANZA
yaliyosimamiwa na JUKWAA la Maziwa ngazi ya Mkoa. Binafsi pamoja na
Serikali nawapongeza sana kwa ubunifu na uthubutu wenu .ni kweli ulio wazi
kwamba ukitaka kujifunza shughuli nzuri
katika mnyororo wa thamani wa maziwa
njoo Tanga.
Ndugu
wanajukwaa,nawakumbusha kuwa maonyesho haya yanalengo la kuunganisha wafugaji
na watoa huduma waliopo katika mnyororo
wa thamani wa maziwa na pia yanazingatia changamoto zilizopo kama
ambavyo wadau na watafiti walivyobaini
na huku watoa huduma wataonyesha wafugaji huduma wanazotoa .ni matarajio yangu
kuwa maonesho yatahamasisha wafugaji kuwaelewa watakao ingia nao
mikataba katika vituo vya kukusanyia
maziwa na hivyo kuleta huduma za uhakika karibu na shughuli zao za ufugaji
yaani “DIARY BUSINESS HUBS” ni mategemeo yangu
pia kuwa mtayaendeleza maonyesho
haya muhimu kwa kila mdau wa jukwaa kushiriki kikamilifu kila mwaka ili
kuendelea kutatua kero na kuleta tija katika kuongeza uzalishaji wa maziwa na
kuboresha ng’ombe waliopo.
Ndugu
wanajukwaa,nimefurahi kusikia kuwa jukwaa la wadau wa maziwa Tanga linaundwa na wadau wa sekta
ya maziwa mkoani Tanga na kwamba jukwaa linajitegemea na kufanya kuhudhuria
vikao mara nne kila mwaka . hili ni
jambo la kuigwa kwani wngine bila posho hawawezi kukutana . nawapongeza sana na
nawaomba mdumishe suala hili ili jukwaa liwe endelevu .
Ni
muhimu sana jukwaa likaendelezwa na kujitegemea
bila kutegemea wafadhili kwa asilimia kubwa na hivyo kuendelea kupata sauti kubwa zaidi ,
huku dhana ya PPP ikizingatiwa. Kupitia jukwaa matatizo ya kimfumo huonekana na
kupata ufumbuzi kwa wepesi zaidi kwa wahusika wote .
Ndugu
wanajukwaa,licha ya maonyesho lengo la mkusanyiko huu ni pamoja na :
• Kukutanisha wafugaji na watoa huduma
bora za kisasa za ufugaji
• Kufungua njia ya wafugaji kuingia mikataba na watoa huduma ili wafanye ufugaji endelevu wa ,kisiasa na
wakibiashara
• Kujifunza kutoka kwa wataalam na
wafugaji waliofanikiwa
• Kuwatambulisha watoa huduma fursa za
biashara zilizopo katika mkoa wa Tanga na hivyo wavutiwe kuwekeza kwa wafugaji
na wafugaji nao wapate kuendelea zaidi
• Kuwakutanisha wadau na watafiti
,halikadhlika washarika wa maendeleo na
mashirika yasiyo yakiserikali.
Ndugu
wanajukwaa, changamoto za wafugaji ni nyingi n azote haziwezi kutatuliwa na
serikali peke yake .jukwaa ni sehemu pekee ambayo wadau wote pamoja na serikali
wanakutana kujadili changamoto za sekta na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja .
maonyesho haya yamewakutanisha wauzaji wa
dawa za mifugo , wauzaji wa vyakula
vya mifugo, madaktari wa mifugo, watoa huduma za uhamilishaji, watafiti,
watoa huduma wa uzalishaji wa ng’ombe, Wafugaji wa mfano, Taasisi mbalimbali za
kifedha, Wauzaji wa Mitambo ya Biogesi, Watoa taarifa kama vile vituo vya radio
na mitandao ya simu, Wafanyabiashara wa bidhaa za umemejua na wafanyabiashara
wa bidhaa nyinginezo.
Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa, ili kufanikiwa katika tasnia ya maziwa nchini , serikali imegawa
maeneo ya kipaumbele kwa Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Mashariki,
Kaskazini na Kanda ya Ziwa. Aidha, Serikali inaendelea kuhamasisha wafugaji
kutumia zaidi teknolojia ya uhimilishaji na huku ikiongeza na kuimarisha vituo
vya uhimilishaji nchini. Mathalani, ujenzi wa kituo cha kitaifa cha
uhimilishaji kinajengwa Sao Hill-Iringa wakati vituo vya kanda vya Kibaha,
Dodoma, Katavi, Mwanza na Mbeya vinazidi kuimarishwa ili kukidhi mahitaji ya
mbegu bora yanayotarajiwa kuongezeka.
Serikali vilevile, inakamilisha ujenzi wa kituo kipya cha uhawilishaji
viini tete (embryo transfer) kwenye taasisi ya utafiti wa mifugo Mpwapwa.
Teknolojia hii inategemewa kuleta suluhisho la haraka katika ubora wa ng’ombe
wa maziwa na hivyo tija kwa mfugaji. Napenda kutumia fursa hiikuwahamasisha
wafugaji wa Tanzania kuwa muda wa kuanza kutajirika kutokana na mifugo ni sasa,
karibisha maarifa mapya na teknolojia, chukua hatua sasa.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, mifugo ni biashara, mifugo ni
uchumi. Natamani kuona wafugaji wanatambulika kwa utajiri wao na sio kwa mateso wanayoyapata kutokana na mifugo yao . kukiwa
na uwekezaji mzuri katika mifugo, Taifa litafaidika mikoa na zitafaidika
na mfugaji ataneemeka . Hivyo
niwaombe mamlaka zote za mkoa , wilaya na vijiji zitenge maeneo mahususi kwa
maendeleo ya ufugaji , siyo uchungaji . serikali kwa upande itaendelea kuangalia maeneo ya hifadhi
yaliyopoteza sifa , mashamba ya serikali
yasiyotumika vyema zikiwemo baadhi ya ranchi ya Taifa ili zitumike kwa ufugaji . viwanda vyetu vyote
74 vya maziwa nchini kikiwemo hiki chenu
cha Tanga Fresh LTD vinasindika
kwa wastani wa asilimia 35 tu ya uwezo wake. Hivyo ni muhimu sana kuongeza idadi na ubora wang’ombe wa maziwa.
Ndugu
wanajukwaa, katika kuongeza idadi ya ng’ombe
wa maziwa uzalishaji wa mitamba
hauwezi kuachiwa serikali peke yake ambayo kimsingi inasimamia sera .
Hivyo ni vyema mkaongeza ushirikiano na sekta binafsi kama hao MZUAZI
HEIFER BREEDING UNIT-HALE , MANGARA
DAIRY BREEDING –PONGWE, LAILA DAIRY AND AGRO CO LTD, na wengineo ili wajiapnue
zaidi kuzalisha mitamba bora ya kutosha kukidhi mahitaji ya Mkoa na maeneo
mengine ya nchi. Mahitaji ya Mitamba bora nchini inakadiriwa kuwa zaidi ya
60,000 kila mwaka wakati uwezo wa mashamba ya Serikali ni takribani mitamba
1,200 tu kwa mwaka. Hivyo tunahitaji
uwekezaji mkubwa katika eneo hili.
Ni
muhimu Jukwaa la Maziwa Tanga likawaalika wenzetu kutoka taasisi za fedha kama
vile TIB Development Bank, NMB n.k katika majukwaa na maonesho kama haya ili
waweze kuona fursa hizi za uwekezaji na kutoa mikopo nafuu ili wadau waweze
kujipanua kiuzalishaji kukidhi mahitaji.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, yapo mabo mengi yamsingi
yanayopaswa kuzingatiwa na mfugaji ili kuwa na ufanisi. Upatikanaji wa malisho
ya kutosha wakati wa malisho wakati wa kiangazi na maji ni muhimu katika
uzalishaji wa maziwa. Aidha, vyakula vya ziada ni vya lazima wakati wote na sio
wakati wakati wa kuamua tu. Hivyo wenzetu wa TARILI, LITA Buhuri, Shamba la
Mbegu za Malisho la Vikuge, Mruazi, Ofisi ya Mkoa wa Tanga na NAIC Usa river
Arusha washirikiane ili mbegu za malisho pamoja na kuwajengea uwezo wafugaji kwa
kuwapa mafunzo ya ujasiriamaji na ufugaji wa kisasa ili kuwa na ufugaji
endelevu na kiwanda kupata maziwa ya kutosha. Kiwanda chenu kinahitaji kuwekeza
karibu bilioni 10 ili kuongeza usindikaji pamoja na aina ya maziwa yanayokaa
muda mrefu bila kuharibika (UHT). Hili litakuwa namanufaa tu iwapo iwapo kuna
maziwa ya kutosha. Hata hivyo nipende kuwaahidi watu wa Tanga Fresh kuwa Wizara
yangu itashirikiana nanyi dhidi ya changamoto zenye nia ovu.
Ndugu
wanajukwaa, napenda kuchukua fursa hii kuzungumzia programu ya Unywaji Maziwa
Shuleni hapa Tanga. Ipo mikoa ambayo wazazi na wakuu wa shule wanatamani
kuwapatia wanafunzi angalau pakiti ya maziwa ya robo lita ya maziwa kila siku
lakini wanashindwa kwa kuwa hawana uhakika wa kupata maziwa kila siku. Naomba
wananchi wa Tanga mtambue neema ya kuwa na kiwanda ni kubwa nay a kipekee
katika nchi yetu. Hivyo boresheni mpango wa Unywaji wa Maziwa Shuleni na
kuhakikisha ni wa kudumu.
Ni
vyema kufanya mashindano baina ya shule na vyuo ili kutoa hamasa ya unywaji
Maziwa Shuleni. Vilevile wakuu wa shule za sekondari na msingi pamoja na vyuo
hakikisheni mnatumia mikutano ya baraza na wazazi kuendelea kuwahimiza wazazi
kulipa fedha kwa ajili ya watoto wao kupata maziwa kila siku. Uchangiaji wa
wazazi wa gharama za kununua maziwa utafanya mpango huu kuwa endelevu,.
Ninaamini kila mtu hapa anajua faida za maziwa mwilini na hasa kwa watoto na
vijana. Maziwa ni lishe timilifu, ni muhimu sana katika makuzi ya motto.
Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa, ufugaji ndio dawaya hakika na haraka dhidi ya umasikini katika
Taifa letu. Hivyo nawaomba viongozi na wadau wote tushirikiane tuweke maono ya
pamoja mbele, tukaze nia na mwendo, hakika tutashinda!
Mwisho
niwakumbushe kauli mbiu ya maonesho haya isemayo:
‘TUMIA
PEMBEJEO NA HUDUMA ZA KISASA KUONGEZA TIJA KATIKA UFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA’
Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa na Ndugu Wanajukwaa, kwa kumalizia napenda sasa kutamka rasmi
kwamba maonesho ya kwanza ya biashara ya maziwa yamefunguliwa rasmi!
AHSANTENI
KWA KUNISIKILIZA.
TAARIFA FUPI YA
SHAMBA LA LAILA AGRO&DAIRY COMPANY LTD
KWA MHESHIMIWA WAZIRI
WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI 15/08/2014
Mheshimiwa mgeni Rasmi, Waziri wa mifugo na uvuvi Dr.Kamani, ninayofuraha
kubwa kukukaribisha kwenye shamba letu
la mifugo lijulikanalo kwa jina la Laila
Agro &Dairy company LTD lililopo
kata ya pongwe halimashauri ya jiji la Tanga .
Mheshimiwa mgeni rasmi, mimi binafsi mkurugenzi na kwaniaba ya wakurugenzi wenzangu na
wafanyakazi wote tunatoa shukrani zetu za dhati kwako wewe binafsi na kwa uongozi mkoa wa Tanga
Na
kwa wilaya Tanga kwa kutambua juhudi zetu na kuzithamini na kuziletea ugeni huu
mzito shambani kwetu.
Mheshimiwa mgeni rasmi, nitakua
mwizi wa fadhila endapo sitatoa shukrani zangu za dhati kwa ugeni nilioletewa
miaka miwili iliyopita ambapo tulitembelewa na muheshimiwa Waziri mkuu Mizengo Pinda.
Ujio
huo ulitupunguzia baadhi ya changamoto
ambazo tulikua nazo tunasema ,
Ahsanteni sana.
Mheshimiwa mgeni rasmi shamba
letu linaeneo kama ifuatavvyo:-
v Hekta 350
v Ng’ombe 380
v Tunakamua ng’ombe 80
v Tumekausha ng’ombe 45
v Tunamitambo 80
v Mitamba ya kati 65
v Madume 75
v Ndama 35
v Tunazalisha lita za maziwa 880 kwa siku
Aina ya
ng’ombe tulio nao:-
v Friesian,Ashier na Brown swiss
v Tunao wafanyakazi 15 wanaume 8na wanawake 7 hesabu ya vibarua hufuatana na
hali ya msimu.
v Kwa upande wa malisho tumepanda majani aina ya
sirinkra,sirialisna roddes kwa shamba lote.
Uhusiano na
majirani zetu.
Mheshimiwa
mgeni rasmi,tunamshukuru mungu
sana kwamba tu nauhusiano mzuri na majirani zetu na tunashirikiana nao vizuri.
Mheshimiwa
mgeni rasmi, malengo yetu
ifikapio mwishoni mwa mwaka 2016 tunakusudia tuwe na uwezo wa kuzakisha lita
5000 za maziwa kwa siku na tuwe na mitambo bora 100 ya kuuza kwa mwaka .
Mheshimiwa
mgeni rasmi, changamoto tulizo nazo hivi kwa sasa ni hizi
zifuatazo:- kipindi cha kiangazi kinapokua mda mrefu utatuzi wake ni umwagiliaji .Miaka miwili
iliyopita tulichukua wataalam wa maji ardhini kupima maji majibu yalionyesha maji yapo mengi na salama
.Tulifuatilia kitengo cha umwagiliaji
gharama za michoro na vifaa ilikua kubwa sana , ilikua ni zaidi ya
milioni mia mbili na hamsini (250,000,000/=) tulihairisha.
Mheshimiwa
mgeni rasmi, ombi, Mheshimiwa Waziri
kama kwenye wizara yako au serikali kwa ujumla kuna msaada wowote wa
umwagiliaji tukipata malengo yetu
yatakua yamefanikiwa kwa asilimia tisini (90%)
Mheshimiwa
mgeni rasmi ,changamoto
nyingine ni upande wa ufugaji ni hizi:-
1. Maradhi;kulitokea tatizo la ugonjwa ng,ombe 18
walitupa mimba za miezi mitano hadi nane
ambapo ni hasara kubwa sana .
2. Madawa yasiyo ya viwango yamekua ni kikwazo
kikubwa sana kwetu.
3. Wafugaji kuwa na thamani duni kwa kupangiwa bei za mazao yao bila
kushirikishwa kwa kisingizio cha soko huru.
4. Upatikanaji wa miji na makazi hautambui uwepo
wa wafugaji
HITIMSHO :-
Mheshimiwa
mgeni rasmi, ninayasema haya
kutokana na kauli yako uluyoitoa bungeni
kuhusu kuchangia mifugo iliyokua inauawa
kabla hujawa waziri ulisema “Mbali na wenye mali kupata hasara hata haki
za wanyama hazikuangaliwa “HONGERA SANA
.
Mheshimiwa mgeni rasmi ,mwisho kwA maoni
yangu Wizara imepata JEMBE-CHAPAKAZI.
Mheshimiwa mgeni rasmi kwa pamoja tutajenga nchi kila mmoja akitimiza wajibu
wake.
Daudi A.Nkya
Mkurugenzi Mtendaji
TAARIFA YA USHIRIKA WA WAFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA
(UWAKO)
KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI TAREHE
16-08-2014.
Mheshimiwa
Waziri wa Maendeleo ya mifugo na Uvuvi,
Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa wa Tanga ,
Mheshimiwa
katibu tawala wa Mkoa wa Tanga,
Mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya,
Waheshimiwa
madiwani ,
Mheshimiwa
mkurugenzi,
Mheshimiwa
Mwenyekiti wa bodi ya TDCU,
Mwenyekiti
wa jukwaa la wadau wa maziwa Tanga ,
Waheshimiwa
wanaushirika,
Waheshimiwa
wageni waalikwa mabibi na mabwana,
Itifaki
imezingatiwa, ndugu wanaushirika,wafugaji wote wan g.ombe wa Maziwa na wageni
wetu napenda sasa nianze kwa kuwasalimia kwa salamu ya ushirika
USHIRIKA- PAMOJA TUJENGE UCHUMI
UTANGULIZI
Ushirika
wa wafugaji wan g,ombe wa maziwa hapa Korogwe ulianzishwa mwaka 1994 kwa lengo
la kuunganisha nguvu na sauti moja ya wafugaji ili waweze kukusanya maziwa na
kupata soko la uhakika la mazao ya maziwa na kujikwamua kiuchumi.
Ushirika
ulisajiliwa tarehe 18/02/1994 na kupewa namba ya TAR 246 ukiwa na wanachama 68
wanaume 40 wanawake 28. Kwa sasa wanaushirika tupo 77, wanaume 45 na wanawake
32. Ushirika umenunua hisa 19(kumi) kutoka kiwanda cha maziwa Tanga fresh ltd
na pia ni mwanachama katika chama kikuu cha ushirika cha Tanga Daires
co-operation union ltd (TDCU) ambacho ndicho chama kikuu kinachotokana na muungano wa vyama vya msingi 12(kumi na
mbili)vinavyojishughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa wa mkoani
Tanga.
Ushirika
huu ulipata mfadhili kutoka Netherlands(uholanzi)mwaka 1994 ambaye kwa kushirikiana
na serikali waliweza kutafuta eneo hili la viwanda na kutujengea kituo hiki cha
kutukusanyia maziwa .
HALI YA CHAMA
Ndugu
mgeni rasmi,
Jumla
ya wafugaji wanaoleta maziwa kituoni ni 144 kati ya hao wanachama ni 80 na
vijana wanao nunua maziwa vijijini na kuleta kituoni(Bicycle Boys).64.
UKUSANYAJI WA MAZIWA
ushirika
unauwezo wa kukusanya maziwa kiasi cha lita 800 kwa siku. Pia kuyahifadhi
katika tanki lenye ujazo wa lita 3350.
MTAJI WA CHAMA
Uwako
una mali za aina mbili
I.
Mali za kudumu zisizo
hamishika
·
Jengo
·
Shamba ekari 82
lipo eneo la mandela
II.
Mali
zinazohamishika
·
Tank lenye ujazo
wa lita 3350
·
Jokofu
·
Jenereta na n.k
SHUGHULI ZA CHAMA
kupokea
,kuhifadhi na kupeleka maziwa kiwandani
kuuza
maziwa yaliyo sindikwa
MAFANIKIO
Mafanikio
tuliyo yapata
1)
Uwako imeweza
kununua hisa katika banki ya ushirika zenye thamani ya TSHS.milioni tatu
(3,000,000/=)
2)
Kujiunga na
saccos ya mkoa (TDCU SACCOS)
3)
kununua hisa
kwenye kiwanda cha Tanga fresh ltd
4)
Kujiunga na mfuko
ya kijamii kama GEPF na NSSF
5)
Ufadhili toka
Land “o”lakes
Chama
kimepata ufadhili toka land “o” lakes na kupatiwa vifaa vifuatavyo:-
-computer-1
-vifaa
vya kubebea maziwa-75
-pikipiki-1
-mwanachama
kupelekwa kusomea uhamasishaji na kupatiwa vifaa vifuatavyo kwa ajili ya chama
:-mtungi mkubwa wa lita 35,mtungi mdogo wa lita 3,hewa baridi lita 38 na mbegu
20.
-tumefanikiwa
kupandisha ng’ombe 152 mpaka sasa kwa miezi mitano ambao ni wastani wa ng’ombe
25 kwa mwezi.
-wanachama
wamewezeshwa kwa kupatiwa mafunzo mbalimbali ya ;- ufugaji bora ,ujasiliamali,
Uwekaji kumbukumbu na ufugaji wa kisasa na kibiashara.
CHANGAMOTO
Ndugu
mgeni rasmi
1)
Uvamizi wa eneo la chama .
E neo la chama limekua na mgogoro tangu mwaka
2011 na tangu Josiah William ambae alifungua kesi.APPLICATION NO OF 2011 Katika
Baraza la Ardhi-korogwe ili atuhamasishe katika eneo hili na kutupa eneo hewa .
kwenye kesi hiyo katika baradha la ardhi korogwe tulishindwa na wanachama kwa kauli moja tuliamua kukata rufaa kwa mahakama moja kuu ya Tanga
ili wapate haki yao.katika rufaa hiyo, ushirika wa wafugaji tulipata haki
yetu(tulishinda kesi) ili kinachosumbua ndugu Josiah wiliam akato pingamizi
kuwa :-
·
Uwako isiendelee
na kesi ya madai
·
Kesi isikilizwe
upya
Mahakama
ilikubali kusikiliza pingamizi basi
itasikilizwa tena terehe 15/10/2014.
2) Upangaji wa
bei
Vyama vya msingi havihusishwi katika kupanga bei ya maziwa.
3)
Bei ya maziwa
Bei ya maziwa ni ndogo ukilinganisha na
gharama za uendeshaji kwa mfugaji.
Ufuatao ni uchanganuo wa mapato na matumizi kwa ng’ombe anaetoa lita saba (7)
kwa siku.
Mtumishi
mkata majani sh 2000
Kg
2 za pumba
sh 500
Ununuzi
wa maji
sh 600
Madini sh
300
Chakula
cha mtumishi sh
1000
Ushuru
wa chama
sh 28
Jumla
ya gharama za uendeshaji sh 4628
Maziwa
lita 7@ sh.678= sh 4746
Garama
za uendeshaji sh 4628
Faida Sh 118
4)
Magozwa ya mlipuko
Kwa sasa magonjwa ya mlipuko ni tatizo
kubwa katika wilaya yetu, na tunapouliza tunaelezwa na idara husika kuwa
serikali imejitoa /haina fedha , lakini kwa upande wa kilimo kuna nguvu kubwa
ya kuwasidia wakulima katika pembe jeio. Magonjwa kama homa ya mapafu,
FMD,ugonjwa wa ngozi, ni tatizo kubwa na linapunguza nguvu za uzalishaji. hivyo
tunaiomba wizara yako iangalie kwa mapana
ili kuweza kumsaidia mfugaji chanjo nyingine. Wafugaji wenyewe wanaweza
kumudu/ kugharamia chanjo kama:-E.C.F.
MATARAJIO AU MALENGO YA BAADAE
malengo
ya badae ya uwako ni kufanya yafuatayo:-
1.
kujenga kantini
kwa ajili ya kuuza mazao ya maziwa yaliyo sindikwa
2.
kujenga COLD
ROOM kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya
maziwa
3.
kujenga ghala kwa
ajili ya malisho/vya kula vya ziada
4.
kujenga duka la
pembe jeo
MALENGO YA
MDA MREFU
-K upatiwa gari yetu yenye pozeo kwa ajili ya kubebea maziwa yetu
-kupanda malisho kwenye shamba letu ili
kuondoa changamoto wakati wa kiangazi ambapo ni tatizo kwa wafugaji wa
ndani.(zero grazing).
MAPENDEKEZO
Ndugu mgeni rasmi
i.
Tunaomba idara ya
Ardhi halmashuri ya mji korogwe itupimie eneo letu na kutumilikisha kwani kesi
ya msingi ya ardhi imekwisha na nakala ya hukumu ya kesi tumepewa na kivuli
chake tumekipeleka kwenye ofisi ya idara ya Ardhi.
HITIMISHO
Ndugu mgeni rasmi,
Tunashukuru kwa
kutembelea kwenye ofisi yetu.
Naomba
kuwasilisha.
USHIRIKA KWA PAMOJA TUJENGE UCHUMI
TAARIFA YA TAASISI KWA
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI, MHESHIMIWA DR.TITUS M. KAMANI (MB) ALIPOTEMBELEA
TVLA-VVBD TANGA, 15/08/2014
1.UTANGULIZI
Taasisi
ilianzishwa mwaka 1971 kama mradi wa
utafiti wa kutokomeza ndorobo
(Tsetse
research project-TRP) Kwa kutumia
tekinolojia ya kutaasisi ndorobo madume (sterile insect technique-SIT) MWAKA
1981 ilibadilishwa na kuwa taasisi ya utafiti wa ndorobo na malale
(Tsetse&Trypanosomiasis Research institute –TTRI) Chini ya shirika la
TALIRO . kutokana na kuundwa kwa wakalaza maabara za mifugo Tanzania (Tanzania veritunary
laboratory agency –TVLA) Taasisi ilipewa majukumu mapya na jina jipya na kuitwa vector & vector –borne diseases
Research institute –VVBD) mwaka 2012
.hivi sasa wajibu wetu umeongezeka kutoka kushuhulikia mbung’o
peke ya ke na kuwa taasisi inayoshughulikia wadudu na magonjwa waenezayo yanayoathiri mifugo.
2.JUKUMU LA TAASISI
• kutafiti, kubuni na kusambaza mbinu rafiki ,rahisi na nafuu za
kudhibiti wadudu na magonjwa yaenezayo kwenye mifugo nchini kwa kutumia mbinu zinazoweza kutumika
kirahisi na jan=mii nchini.
• Kutoa mafunzo yanayohusiana na
wadudu namagonjwa waenezayo kwenye
mifugo kwa wanafunzi na wafugaji.
• Kutoa ushauri wa kitaalam kwa watunga
sera juu ya wadudu na magonjwa waenezayo
3.UKUBWA WA TAASISI
Wafanyakazi
wa taasisi
Taasisi
inajumla ya wafanyakazi 42(watafiti12, maafisa ndorobo /mifugo wasaidizi11,
watumishi wengine 20.
Eneo la taasisi
• Taasisi inaeneo la hekta 38
zilizomegwa kwenye eneo kubwa la kituo cha utafiti wa mifugo (Tanzania
livestock Research institute –TALIRI Tanga )
• Taasisi inaeneo lngine lenye ukubwa wa
hekta 5,320 lililokuwa Livestock Multiplication Unit-LMU mivumoni ilayani
pangani.
Shamba
hili lilikuwa ni shamba la kuzalisha mitamba (livestock multiplication unit
) kuanzia mwaka 1982 chini ya kurugenzi
uzalishaji mifugo .Hata hivyo mpango huo ulipofutwa shamba liliachwa bila
msimamizi na uvamizi ukaanza kujitokeza kwa shughuli zenye athari kwa mazingira
na miundo mbinu ya shamba kwa kuona uhitaji wa kuwa na shamba la kufanyia
utafiti wa magonjwa ya mifugo ,Taasisi ya utafiti wa ndorobo namalale ililiomba
shaqmba hilo kutoka kurugenzi ya
uzalishaji wa mifugo mwaka 2003 shamba hilo lilikabidhiwa kwa taasisi hii Tangu
wakati huo shamba hili limekua likitumika kama shamba darasa kwa ajili ya
wanafunzi wanao somea Tasnia ya mbung,o(astashahada ,stashahada).hadi sasa
Taasisi imekua ikipoea wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya mifugovya serikali
na vya binafsi .pia linatumika kama shamba la dara sa kwa wakulima na wafugaji
kutoka sehemu mbalimbali hasa kutoka mikoa yenye wafugaji asilia ili kujifunza
mbinu mbalimbali za kudhibiti mbung’o katika mbuga za malisho.
Malengo
makubwa ya sasa ya shamba hilo ni uzalishaji wa mitamba iliyo bora na mbuzi wa
kisasa ili kuboresha ufugaji kwa maeneo yanayozunguka shamba na mengineyo
ichini.
Majengo
ya Taasisi
• Maabara 5
2.Nyumba
za wafanyakazi
Grade
A-2, Grade B-1,gRADEc-2,Rest house -1, Nyumba ya mkurugenzi -1(iliyoko mwambani
Tanga ).
Shamba
la mivumoni Pangani
Ofisi na majengo mengine 8,Nyumba za wafanyakazi
14, malambo 9, majosho 2, tanki la maji 1(bovu )kisima kimoja kilichochimbwa
siku za karibuni .
Magari
ya taasisi
• Yanayotembea -3
• Mabovu yanayohitaji matengenezo
makubwa -3
• Magari chakavu -3(yanayotakiwa
kuondolewa –disposed)
• Trecta moja ,tela na jembe lake
Ushirikiano
Taasisi
ina ushirikiano mkubwa na mashirika yafuatayo
• Shirika la kimataifa la nguva la
atomiki la Vienna (IAEA-Viena Austria)
• Shirika la afya la duniani (who)
• Bill and Melinda Gates foundation
• Mtandao wa kutokomeza malale Afrika
mashariki na kati(EANETT)
• Pan African Tsetse %Trypanomiasis Eradication campaign (PATTEC)
• pamoja na vyuo vikuu vya ndani na
nje ya nchi.
TAFITI ZILIZOKWISHA FANYIKA KATIKA
TAASISI PAMOJA NA MAFANIKIO
• KUtokomeza mbung’o kwa kutumia
tekinolojia ya kutaasisi madume (SIT) 1994-1997,Zanzibar
• Kudhibiti mbung’o (tsetse control) kwa utumia tekinolojia ya mitego na
vitambaa vyenye dawa(targets)(Serengeti,selous,mikumi,sadaani, ngongoro n.k)
• Tafiti za mitego ya mbungo na vivutio
vimefanyika kwa ajili ya aina tofauti za mbung’o kwenye maeneo tofauti nchini mfano Tanga
scoop
• Uchunguzi wa madawa ya kuua mbung’o
kabla ya kusajiliwa nchini(Dominex,Decatix,ectopor,grenade,ectomin.Amitraz)
• Kushiriki katika kutafiti njia ya
haraka na nyepesi ya kutambua vimelea vya malale katika wadudu (xenomonitoring)
ili itumike kubaini mlipuko wa ugonjwa wa malale kabla haujalipuka (early
warning tool)
KAZI ZINAZOENDELEA
• Matokeo ya utafiti hasa yavitambaa
vyenye dawa hivi sasa yanatumika kuondoa mbung,o katika hifadhi zataifa nchini
(Serengeti ,Ngorongoro,mikumi katavi,selous,tarangire n.k) na katika baadhi ya
almashauri nchini kama vile rufiji ,Handeni ,chunya monduli,kilindi
liwale,kilwa,lindi,Kigoma,tabora n.k
• Kutoa mafunzo kwa wakulima na
wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi
Ufugaji
a ng’ombe ,mbuzi na kondookwenye shamba la mivunoni:mkakati wa kuzalisha
ng,ombe aina ya Mpwapwa breed kwa wingi kwa ajili ya wafugaji wa ,maeneo
yaliyoko Tanga na mikoa ya jiani inaendelea ,Hivi sasa tuna ng’ombe 201, mbuzi
na kondooo 76,mpango wa kuongeza ng’ombe
aina ya mpwap[wa kwa ajili ya
kuzalisha na kusambaza kwa wafugaji uanendelea (tayari jumla ya shilingi
milioni 10 zimeshalopwa kwa ajioli ya kuongeza ng.ombe zaidi) pia mpa ngo wa
kuzalisha zaidi mbuzi zaidi unaendelea kwaq kutumia madume bora ya aina Tonge
nburgn and saanen.
• Kutoa mafunzo darasa kuhusu ufugaji
bora wa mifugo kwa wanafunzi kutoka vyuo vyetu hapa nchini kwa kutumia shamba
la mivumoni na kwa wafugaji wanaoplizunguka shamba.
• Uchunguzi wa magonjwa wa mifugo pamoja
na kutoa ushauri wa kitaalam ili kudhibiti magonjwa ya mifugo.
• Uzaji wa jumla na rejareja wa chanzo
za kideri /mdondo
• Ulimaji na uvunaji wa hey kwenye hektari 1000 kwa ajili ya
kuwauzia wafugaji.
MATARAJIO YA BAADAE
• Kuanza ufugaji wa ng’ombe wa maziwa
oili kutumia fursa iliyopo wa kiwanda cha maziwa Tanga fresh
• Kuongeza uzalishaji wa mitamba bora (
Mpwampwa breed) ambayo imekua ikiulizia Sna na wafugaji.
• Ufugaji wa nyuki wasiouma pembezoni
mwa shamba ili kuvuna asali na kuongeza kipato.
• Kuongeza ekari 500 za eneo la kuvuna
na kufuga hay ili kufikia ekari 1500
• Uwezekano wa kufuga fruit flies kwa
ajili ya kudhibiti wadudu waharibifu na matunda kwa kutumia tekunolojia ya
kutaasisi madume.mchakato huo unaendelea.
• Kutokomeza mbung’o wilayani kilosa na
Serengeti kwa kutumia SIT
• Kuwa na mtambo wa liquid nitrojen
plant kwa ajili ya ukanda wa Pwani mchakato wake unaemdelea .
CHANGAMOTO
• Upungufu mkubwa wa vitendea kazi ili
kufanikisha shughuli za utafiti
• Upungufu wa wawafanyakazi (wanao
staafu ni wengi kuliko wanaoajiriwa )no technical succession)
• Uvamizi wa shamba la mivumoni (karibu
ekari 1000 zimevamiwa na wakulima )
• Taasisi haina uzio hivyo kuhatarisha
usalama wa mali za taasisi.
• Uchakavu wa majengo ya Taasisi
Nawasilisha
Dr. Imma Malale,
KAIMU MENEJA ,
TVLA-VVBD
TAARIFA YA KITUO
KUTOKA: KITUO CHA
UTHIBITI UBORA WA MAZAO YA UVUVI NA MASOKO
KANDA YA KASKAZINI TANGA
KWENDA: WAZIRI WA
WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
UTANGULIZI;
Kituo
cha uzibiti ubora wa mazao ya Uvuvi na Masoko kanda ya kaskazini kilichopo
mkoani Tanga kilianzishwa mnamo ,mwaka 2000 kikiwa na mtumishi mmoja .Baada ya
muda wa mwaka mmoja akaongezwa mtumishi wa pili na kufika hadi hivi leo kitengo
kina jumla ya watumishi wanne.
Kanda
ya kaskazini inajumla ya mikoa mine ambayo ni Tanga ,Kilimanjaro,Arusha,na
Manyara.kitengo kina jukumu la kulinda ,kusimamia na kudhibiti ubora wa mazao
ya uvuvi yanayosafirishwa ndani na nnje
ya nchi pamoja na kusimamia ukusanyaji wa maduhuli kwa kushirikiana na kituo
cha Doria uvuvi katika kanda hii ya
kaskazini.Kituo kina gari moja (01) aina ya Nissan Quaqui na pikipiki moja
(01)DT250.
KAZI ZA KITUO
Lengo
kuu la kituo ni kuthibiti ubora na usalama wa mazao ya uvuvi kwa watumiaji
/walaji ndani na n je ya nchi na kusimamia masoko ya mazao ya uvuvi kwa
kutekeleza sera ya mwaka 1997, sharia ya mwaka 2003 na kanuni ya mwaka 2009 na
uvuvi. Ili kufanikisha lengo hili kituo kinafanya malengo mahsusi kwa:
·
kwa kufanya
ukaguzi katika viwanda vya uchakataji /usindikaji wa mazao ya uvuvi,mialo na
masoko ya uvuvi.
·
Kisimamia na
kufanya kaguzi katika mipaka iliyopo kwenye kanda ya kaskazini .
·
Kutoa vibali vya
usafirishaji mazao ya uvuvi ndani na nnje ya nchi.
·
Kutoa elimu kwa
wavuvi ,wauzaji wa mazao ya uvuvi na wasindikizaji/wachakataji wa mazao ya
uvuvi viwandani .
·
Kusimamia
makusanyo ya maduhuli yatokanayo na usafirishaji wa mazao ya uvuvi ndani nan je
ya nchi.
VYANZO VYA
MAPATO
Kituo kinakusanya maduhuli kutokana na
ukusanyaji wa ushuru wa mazao ya uvuvi yanayosafirishwa nje ya nchi yakitokea
hapa jijini Tanga ,faini ya makosa yanayofanywa na wavuvi(compoundment)kama
vile kuvua kwa kutumia vyombo visivyosajiliwa,kusafirisha mazao ya uvuvi bila
kibali,kuvua bila kuwepo na leseni halali ya uvuvi.
MAFANIKIO
Kitengo kimefanikiwa kusimamia ukusanyaji wa
maduhuli jumla ya shilingi milioni 28,113,318.15 ambazo ni asilimia 28%
Kituo kimeweza kuwabadili wavuvi hasa wa pweza
kuvua pweza wenye uzito wa gram 500 na kuendelea.pia kituo kimeweza kuwapa
elimu ya kuhifadhi mazao ya uvuvi kwa ubora na usalama kwa kutumia cool box.
Kilimo kimesaidia kupatikana kwa soko la
kudumu kwa wavuvi wadogowadogo kwa kuhamasisha uongozi wa k8iwanda cha
kusindika mazao ya uvuvi kununua mazao ya uvuvi ya wavuvi hao.
CHANGAMOTO
1.Kituo kinakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi
2. Kituo kina gari 1 linahitajika lingine
3.Ofisi ya kituo inahitaji matengenezo
Nawasilisha,
Neema I. Respickius
Kny.Kaimu
Afisa Mfawidhi,
Kituo cha
Uthibiti ubora wa masoko na uvuvi-Tanga
KUTOKA; KITUO CHA UZALISHAJI VIFARANGA NA UKUZAJI SAMAKI (MACHUI-TANGA)
KWENDA: WAZIRI WA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA
MAENDELEO
YA UVUVI
TAARIFA YA KITUO CHA KUTOTOLESHEA VIFARANGA WA SAMAKI MACHUI- TANGA
UTANGULIZI
Ujenzi
wa kituo cha kituo cha kutotoleshea
vifaranga wa samaki Machui ni
moja kati ya mipango ya muda mrefu wa wizara ya mifugo na maendeleo ya uvuvi ikitekelezwa na idara ya ufugaji wa
viumbe vya majini(Department of Aquaculture) Baada ya idara kugundua kuwa
ufugaji wa samaki hauendi sambamba na
mahitaji ya viafranga vya samaki,
wizara iliagiza idara ya ufugaji viumbe kwenye maji ikishirikiana na
Halimashauri ya jiji la Tanga kuanzia ujenzi wa kituo mwezi agost mwaka 2013. Eneo la machui linaukubwa
war obo hekta lilinunuliwa katika kijiji cha
Machui kupitia Afisa Mtendaji kwa
kiasi cha 1,500,00/=
HATUA YA UTEKELEZAJI
Wizara
ya maendeleo ya Mifugo na uvuvi inatekeleza kazi ya ujenzi wa kituo cha kutotolesha vifaranga vya samaki
machui-Tanga kulingana na upatikanaji wa fedha za maendeleo.Mpaka sasa kituo kimejenga matanki sita (6) matanki
matatu yalijengwa kwa fedha za maendeleo 2012-2013 na matanki mengine matatu
pamoja na kingo za hatchery zilijengwa katika fedha za maendeleo za mwaka 2013-2014.Matanki matano (5)tu ndio
amabyo tayari yamepandwa vifaranga wapatao 698 wa aina ya perege(tilapia)
mwatiko (milk fish) na mkizi. Tanki
moja ado halijawekwa maji kutokana na kupata
nyufa . Samaki walipopandwa ndio watakao tumiwa kuzalisha vifaranga wapya wa samaki(BROODSTOCK) samaki hao wanakula chakula cha asili
kinachozalishwa kwenye bwawa kwa kutumia mwanga wajua (PHOTOSYNTHESIS)
1. UJENZI
WA MAABARA ,OFISI NA NYUMBA ZA WATUMISHI
Kazi
hii inatarajiwa kutekelezwa katika eneo la Kivindana na ndipo itakapokua ofisi
kuu ya kituo.
2. KUVUTA
UMEME
Kazi
ya kuuta umeme inatarajiwa kutekelezwa
haraka iwezekanavyo,umeme utavutwa kutoka njia kuu ya umeme baada ya
wataalam wa Tanesko kufanya soroveya
kuelekea maeneo ya ofisi za kituo na
matanki ya kuzalisha (kivindani na
machui)
3. WATUMISHI
Kituo
kinawatumishi wawili(2) wenye elimu ya
shahada na stashahada ambao wanasimamia
na kuendeleza shughuli za kituo .Ikiwa ni pamoja na kutoa ugani kwa wafuga
samaki na wakulima wa mwani.
4. MIPANGO
YA BAADAE
I. Kuongeza upatikanaji na uzalishaji wa
vifaranga vinavyo faa kufugwa kwenye
maji bahari kwa ajili ya wafugaji
waliopo mkoa wa Tanga .
II. Kutafuta maeneo yenye majangwa ya
chumvi ili kupanua mashamba (mabwawa) ya
kufugia samaki .
III. Kuchukua vifaranga vya oreochromis
urolepis kutoka kituo cha utafiti cha pangani (IMS-KIMU) Nakuanza kuwazalisha
hapa kituoni kwa ajili ya wafugajui
waliopo mwambao wa bahari ya Hindi.
IV. Kutafuta eneo ili kushirikiana na
wazalishaji wa chumvi kukuza
‘artemia’
V. Kukamilisha makubaliano ya idara ya ukuzaji viumbe na kijiji cha kivindani kwa ajili ya kupata eneo kubwa
zaidi la kujenga ofisi,hatchery pamoja na mabwawa,hii itasaidia kuweka
mazingira yanayofaa kwa ajili ya samaki
wa mapambo na michezo.
5. CHANGAMOTO
I. Mpaka sasa kituo hakina gari wala
pikipiki kwa ajili ya watumishi kwenda kituoni
machui na kwenda kutoa elimu ya
ugani kwa wafugaji samaki waliopo mkoa wa Tanga .
II. Kupitiwa ofisi kwenye jengo la coastal
zone pamoja na vifaa vya ofisi .
III. Vifaa vya kupimia maji (Techinical
equipments)
IV. Upungufu wa watumishi (mlinzi wa
kituo)
V. Pump ya kusukuma maji kuingia kwenye
matanki.
VI. Kumalizia ujenzi wa ‘hatchery’
HITIMISHO
Wizara
ya maendeleo ya mifugo na uvuvvi kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la
Tanga inahakikisha mwendelezo wa ujenzi na ufanisi wa kituo cha machui kwa ustawi wa wananchi wa
Tanga na kanda yote yay a kaskazini kwani kuitafungua ajira ,kuongeza kipato na
uhakiki wa chakula bora na salama .
Nawasilisha.
OMARY ALLY MOHAMED
AFISA
MFAWIDHI
KITUO CHA KUTOTOLESHEA VIFARANGA
MACHUI
TANGA
KUTOKA; KITUO CHA DORIA UVUVI TANGA
KWENDA; WAZIRI WA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
TAARIFA YA KITUO CHA DORIA UVUVI KANDA YA KASKAZINI-TANGA
UTANGULIZI;
Kituo
cha Doria Uvuvi- kanda ya kaskazini chenye makao yake makuu katika jiji la
tanga, kilianzishwa tarehe 14/12/2005,kikiwa na jumla ya wafanyakazi watano(05).
Kituo kinafanya kazi katika mikoa ya Tanga Kilimanjaro,Arusha na manyara pamoja
na mipaka yote inayopakana nan chi jirani ya Kenya katika suala zima la ulinzi
wa rasilimali za uvuvi na ukusanyaji wa maduhuli. Aidha vipo vituo vidogovidogo
vya horohoro na namanga vilivyo katika mipaka ya nchi jirani ya Kenya ambayo
jukumu lake kubwa ni kukusanya maduhuli yanayotokana na usafirishaji mdogo wa
mazao ya dagaa wakavu kwenda nchi jirani ya Kenya pamoja na kuhakiki uhalali wa
mazao mengine yote ya uvuvi yanayosafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia katika
mipaka hiyo na kudhibiti utoroshaji kupitia njia zisizo halali.
Kituo
kina gari moja (01) aina ya Toyota land cruiser,pikipiki moja (01)xl250,boti
nne mbili zikiwa inboard engine na mbili aina ya outboard engine.
KAZI ZA KITUO
Kituo
cha doria uvuvi-kanda ya kaskazini kina jukumu la kulinda na kusimamia
rasilimali za uvuvi pamoja na kukusanya maduhuli katika kanda hii ya kaskazini
.
Kituo
kilipewa lengo la kukusanya maduhuli yasiyopungua jumla shilingi 100,000,000/= milioni mia moja
katika mwaka wa fedha 2013-2014,ikiwa pamoja na kufanya doria 144 za majini nan
chi kavu zenye kujumuisha watendaji (mandays)1440.
VYANZO VYA MAPATO
kituo
kinategemea kukusanya maduhuli kutokana na ukusanyaji wa ushuru wa mazao tya baharini yanayosafirishwa nje ya
nchi yakitokea hapa jijini Tanga ,faini ya makosa yanayofanywa na
wavuvi(compoundment) kama vile kuvua kwa kutumia vyombo visinyo sajiliwa, kuvua
bila kuwa na leseni halali za uvuvi pamoja na ada ya leseni za uvuvi wa samaki
wa mawindo/michezo.
MAFANIKIO
kituo
kimeweza kuunganisha wilaya zote za pwani Tanga mjini, Pangani, Mkinga na Muheza)
na kufanya doria shirikishi katika maeneo yote ya mwabao mwa Bahari ya Tanga
kabla ya hapo kila wilaya ilikua ikifanya doria yake katika eneo lake na
kupeleka baadhi ya maeneo ya wilaya husika kutofanya doria kwa mda mrefu.
Kupunguza
kwa kiasi kikubwa uvuvi haramu wa
kutumia baruti,makokoro(beach senie)sumu, nyavu za utale(mohofilament)na
mikuki.
UKUSANYAJI MADUHULI
katika
mwaka wa fedha 2013-2014 kituo kilipewa lengo la kukusanya jumla ya shilingi
milioni mia moja (100,000,000/=) kwa kufanya doria 144 zenye
watendaji(mandays)1440.lakini kituo kiliweza kukusanya jumla ya shilingi
28,113,318.15 ambazo ni sawa na asilimia 28% tu ya lengo ya kiasi
kilichotakiwa kukusanywa .kiasi hicho kilikusanywa kutokana na doria 46 zilizofanywa zikiwa na nguvu kazi (mandays)460 sawa na asilimia
32%tu ya doria zilizotakiwa kufanyika na
idadi ya watu waliotakiwa kufanikisha Doria zote.
CHANGAMOTO
1. Kituo kinakabiliwa na uhaba wa vitendea
kazi, na matengenezo ya boti.
Nawasilisha,
Hassan M. Kufuku,
Kny. Afisa Mfawidhi,
Kituo cha Doria Uvuvi-kanda ya kaskazini,
Tanga.
TAARIFA YA KAMPASI YA BUHURI KWA MHE. DKT.TITUS KAMANI WAZIRI WA MAENDELEO YA
MIFUGO NA UVUVI.TAR. 16 AUGUST 2014.
Ndugu,
• Mheshimiwa Waziri
• Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa
• Mheshimiwa Katibu Tawala Mkoa
• Waheshimiwa Viongozi mbalimbali wa
Serikali
• Watumishi wa LITA
• Mabibi na Mabwana.
Mheshimiwa Waziri
Napenda
kuchukua nafasi hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuwa na
afya njema lakini pia kukufikisha salama katika kampasi yetu ya Buhuri na hivyo
kupata nafasi ya kuwa pamoja asubuhi hii ya leo.
Mheshimiwa
Waziri nichukue nafasi hii kukukaribisha pamoja na viongozi wengine
ulioambatana nao katika kampasi yetu ya LITA Buhuri na napenda kusema kuwa
tunafarijika sana kwa kuwa pamoja nanyi nasi tutajitahidi mjisikie mko nyumbani.
Mheshimiwa Waziri
Kampasi
ya LITA Buhuri ilianzishwa kama Chuo cha Mafunzo ya Mifugo mwaka 1980 kwa
ushirikiano kati ya serikali ya Uholanzi na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania. Madhumuni ya makubaliano yalikuwa ni:
• Kutoa mafunzo na stadi mbalimbali kwa
wafugaji vijijini katika fani ya ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa.
• Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa
mashamba makubwa ya ng’ombe wa maziwa.
• Kutoa mafunzo ya rejea kwa maafisa
ugani.
• Kituo cha mfano kwa ajili ya
uzalishaji maziwa
• Kituo cha mafunzo kwa vitendo. (Field
Practical Attachment) kwa awanafunzi wa vyuo vya kilimo/Mifugo.
Mheshimiwa Waziri
Kumekuwepo
mafanikio makubwa kwa ujumla kulingana na madhumuni ya kuanzishwa kwa chuo kwa
wakati huo kwani
• Wafugaji 8,335 kati yao 2,881 wakiwa
wanawake (34.6%) na wanaume 5,454 (65.4%) walipata mafunzo.
• Maafisa Ugani 537 walipata mafunzo ya
rejea.
• Jumla ya wafanyakazi 215 wa mashamba
makubwa ya ng’ombe wa maziwa walipata mafunzo.
Mheshimiwa Waziri.
Mwaka
2007, Kampasi ilianza kutoa mafunzo ya muda mrefu na stashahada ya uzalishaji
wa wanyama (Diploma in Animal Production), ambapo Juni 2011 jumla ya wahitimu
289 walimaliza mafunzo hayo na wengi wameajiriwa katika sekta mbalimbali za
mifugo na wengine kujiajiri.
Mwaka
2012 kampasi ilianza kutoa mafunzo ya Astashahada ya Afya na Uzalishaji Mifugo
baada ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuhuisha mitaala katika vyuo
vya mafunzo ya mifugo. Ambapo wanachuo 103 (wasichana 31 na wavulana 72)
walihitimu mafunzo yao mwezi Juni 2014 na wengine 101 (wasichana 32 na wavulana
69)wapo mwaka wa pili.
Mheshimiwa Waziri
Katika
mwaka wa masomo utakaoanza mwezi Septemba 2014 kampasi inatarajia kudahili
wanafunzi 135 wa mwaka wa kwanza na hivyo kuwa na jumla ya wanafunzi 236
ongezeko la wanafunzi 32.
Mheshimiwa Waziri
Mwezi
Septemba 2011 Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi iliunda wakala wa Vyuo vya
Mfunzo ya Mifugo –Livestock Training Agency (LITA) ili kuongeza ufanisi wa
kiutendaji ambapo kila kimoja ya vyuo hivyo LITIs imekuwa Kkampasi ya LITA,
hadi sasa LITA ina kampasi 6 na vyuo 2.
Mheshimiwa Waziri
Kampasi
ya Buhuri ina jumla ya watumishi wa kudumu wa kudumu 42 kati ya hao wakufunzi
15 na watumishi watendaji 27 pamoja na watumishi wengine wa maktaba 31 ambao kwa
pamoja tunasaidiana katika shughuli za kiutendaji na utawala.
Mheshimiwa Waziri
Kampasi
ina eneo lenye ukubwa wa hekta 885 ambapo ndani yake kuna maeneo ya malisho,
majengo ya makazi na ofisi pamoja na vitengo mbalimbali vya uzalishaji. Ambapo
idadi ya mifugo ni kama ifuatavyo:
Jedwali
2. Idadi ya Mifugo Kampasi ya Buhuri
Aina
ya Mifugo Idadi
Ng’ombe
majike 224
Ng’ombe
madume 70
Jumla
294
Mbuzi 57
Kondoo 26
Nguruwe 12
Pia
kampasi imekuwa ikizalisha na kusambaza ng’ombe wa maziwa kwa wahitaji mbalimbali.
kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali na. 3.
Mheshimiwa Waziri
Malengo
ya wakala kuhusiana na kuendeleza kampasi kuwa kituo mahili katika utoaji wa
taaluma na uzalishaji ni pamoja na:
Upanuzi
wa kampasi ili kuongeza udahili wa wanachuo.
Kwa
sasa Kampasi ina wanafunzi 204. Kampasi hii ina mpango wa kuongeza idadi ya
wanafunzi wa Astashahada hadi hadi kufikia 300 ifikapo mwaka 2016. Pia tuna
mpango wa kuhamisha kozi ya uendeshaji wa nyanda za malisho na uthibiti wa
Ndorobo inayoendeshwa katiak Kampasi ya Morogoro baada ya kukosa eneo la
kufundishia kutokana na Dakawa Pilot Unit (DPU) iliyotengwa kwa malengo hayo ya
serikali kubinafsishwa.
Kuanzisha
Ranchi
Kitengo
hiki kitakuwa kielelezo cha mafunzo kwa vitendo na kitatumika kwa uzalishaji.
Eneo lililotengwa kwa ajili hiyo ni hekari 370 likiwemo eneo linalotumiwa na
Holland Diaries Ltd, ambao unatarajiwa kuanza mwaka 2016 na inakadiriwa mradi
huu utagharimu Tsh. bilioni 1.3.
Uzalishaji wa mitamba bora wa ng’ombe wa
maziwa 50 kwa mwaka kwa ajili nya kampasi na wafugaji.
Uendelezaji
wa nyanda za malisho kila mwaka hekta 45 kwa ajili ya ng’ombe wa maziwa,
hifadhi na uvunaji mbegu kwa ajili ya wafugaji. Kazi hii itafanya kwa
kushirikiana na wanafunzi wetu, wafanyakazi wa maktabana wafanyakazi wa kudumu.
Kuanzisha
kituo kidogo cha usindikaji maziwa (min processing plant) ili kuongeza thamani
ya maziwa tutakayozalisha katika kampasi yetu. Makadirio ya thamani ya mradi
huu ni shilingi milioni 108.
Upanuzi
wa kitengo cha nguruwe kufikia idadi ya nguruwe 120 na ufugaji wa kuku wa mayai
kufikia 1,000 utekelezaji wa mradi huu unaanza mwaka huu wa fedha 2014/2015.
Kuongeza
uzalishaji wa mifugo na mazao yake mbalimbali kwa ajili ya kuongeza pato ambalo
litatumika katika shughuli za uendeshaji mafunzo hivyo kupunguza utegemezi wa
chuo kwenye bajeti ya serikali.
Kwa
siku za usoni tunafikiria ufugaji wa ngamia na nyati.
Mheshimiwa Waziri
Pamoja
na mafanikio tuliyoyapata Kampasi imekuwa na changamoto mbalimbali ambapo kwa kushirikiana
na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi pamoja na uongozi wa mkoa na wadau
wengine wa maendeleo tunaendelea kuzitafutia ufumbuzi.
• Kampasi ina mgogoro na Holland Dairies
Ltd ambao walipeleka shitaka mahakamani kuhusu kuondoka katika eneo la hekari
205 ambalo waliazimwa na Wizara kwa mkataba toka mwaka 2004. Madai ya awali ya
kuwa eneo hilo wamilikishwe, yalikwishatolewa hukumu na mahakama kuu tarehe
15/7/2011 ya kwamba eneo hilo ni la kampasi na hivyo wanatakiwa kuondoka.
• Upimaji wa eneo la Kampasi umekamilika
hatua inayofuata sasa ni kupata Namba ya eneo (Plot Number) kutoka Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kuwezesha kutengeneza hati. Vielelezo
mbalimbali vilikwishapelekwa wizarani kwa ajili hiyo kwa sasa kinachosubiriwa ni
Wizara kutoa anamba ya eneo ili masuala ya hati yaweze kufuatiliwa.
Kuwa
na wafanyakazi wengi ambao ni vibarua (mishahara milioni 3.4 kwa mwezi)
Uhaba
wa majengo:-
·
Madarasa 2 bwalo
la chakula na jiko
·
Maabara na
maktaba
·
Mabweni ya
wanafunzi
·
Ufinyu wa mtaji
wa kuendeleza shamba na kutekeleza miradi iliyopangwa.
·
Vyombo vya
usafiri havitoshi (hard top- pikipiki -2 Lorry-1 Mini Bus 1)
·
Uchakavu wa
miundombinu kama mashine ya kukamulia, mabomba ya maji na nyumba za
wafanyakazi.
Mheshimiwa Waziri
Tunapenda
kutoa shukrani kwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa jitihada
inazozifanya kutuwezesha kwani imeendelea kulipa mishahara kwa watumishi
japokuwa tumekua LITA. Tunaishukuru Wizara kwa kutuwezesha kuanzisha kituo cha
Artifical Insemination (AI) kwenye Kampasi yetu hii itakuwa chachu kwetu
kuongeza idadi ya ng’ombe waliobora zaidi. Pia naishukuru Serikali kwa
kuendelea kuwafadhili wanafunzi wetu katika masomo yao.
Napenda
kuchukua nafasi hii kushukuru uongozi wa Mkoa na Wilaya ya Tanga kwa jinsi
tunavyoshirikiana nao katika shughuli mbalimbali za kiutendaji.
Napenda
kutoa shukrani zangu kwa LITA makao makuu kwa kushirikiana vyema na uongozi wz
Kampasi katika kuhakikisha kuwa tunapata mafanikio tunayotazamia.
Natoa
shukrani zangu kwa taasisi za mifugo zilizopo jijini Tanga hususani TARILI na
TVLA kwa kutupa ushirikano mkubwa ambao umechangia sana katika mafanikio yetu.
Nawashukuru
pia wadau wetu wa cmaendeleo SNV, TDBP, Land O’Lakes na jamii inayotuzunguka
katika ushirikiano wao na kampasi yetu.
Ahsanteni
Naomba
kuwasilisha
Paul Kidangaking’we Shempemba
KAIMU MKURUGENZI WA KAMPASI.
TAARIFA FUPI YA UVUVI - KATA YA KIGOMBE KWA MHESHIMIWA
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI.
UTANGULIZI.
Mheshimiwa Waziri, Kata ya Kigombe ina jumla ya wafanyakazi
wapatao 5,675 jwa sense ya mwaka 2012.idadi kubwa ya wavuvi inatoka katika kijiji cha kigombe ambao wanafikia
255,hata hivyo eneo la kigombe hupata
wavuvi wageni kutoka pemba na unguja wapatao150 kwa mwaka. Eneo la uvuvi katika
kata ya kigombe ni kilomita 15 kuanzia eneo la gawani hadi dahali (coatal
line).
Mheshimiwa Waziri,Katika kata ya kigombe kuna bandari ya uvuvi
na soko la samaki ambalo moja ya shughuli zake ni uthibiti wa mazao ya uvuvi,
uwepo wa soko hili hupelekea upatikanajio wa twakimu halisi ya mazao ya uvuvi,
kuwepo uwiano wa bei kati ya mvuvi na mlaji na urahisi wa ukusanyaji wa
madhuhuli yanayotokana na uvuvi(leseni na ushuru wa samaki).
Mheshimiwa Waziri,Katika kiasi cha samaki kinachovunwa kwa mwaka
ni wastani wa tani 49.72 ambazo thamani yake ni Tsh.159,104,000/= makusanyo ya
halimashauri kutokana na leseni pamoja na ushuru ni wastani wa tsh .6,955,200/=
kw a mwaka.
Mheshimiwa Waziri, juhudi za serikali katika kipindi cha mwaka wa
fedha 2008/2009 halmashauri ilipokea jumla ya shilingi 118,262,037.50(macemp)
kwa ajili ya kuwezesha vikundi vitano
vya wavuvi kigombe na vingine vitano vya
wafugaji kuku wa asili, lengo lilikua kuwajengea uwezo wa kiuchumi wavuvi na
wananchi wanaoishi mwambao wa pwani ya
bahari ya hindi.
CHANGAMOTO.
Mheshimiwa waziri,changamoto kubwa iliyopo ni pamoja na :-
·
Uvuvi haramu wa
kutumia baruti na nyavu zenye macho madogo(majuya)
·
Ufinyu wa bajeti
kwa ajili ya kuendesha shughuli za doria na elimu kwa wavuvi juu ya uvuvi
endelevu.
·
Uhaba wa
wataalamu na vitendea kazi katika sekta ya uvuvi(halmashauri ina mtumishi
mmoja)
Mheshimiwa waziri,pamoja na changamoto zinazo tukabili wilaya inaendelea na shughuli za kutoa elimu
kwa wavuvi ili kuwa na uvuvi endelevu na
kufanya doria za mara kwa mara za udhibiti wa wavuvi haramu kwa kushirikiana na
uhifadhi wa bahari(marine park).
MAPENDEKEZO .
Mheshimiwa
waziri,baadhi ya mapendekezo ambayo tunazani yatasaid8ia kuwa na uvuvi endelevu
ni pamoja na:-
·
Kuendelea kutoa
elimu ya matumizi endelevu ya rasilimali.
·
Kuanzisha
shughuli mbadala za kiuchumi kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa bahari.
·
Serikali kuu na
halmashauri iongeze bajeti kwa ajili ya kusaidia shughuli za uhifadhi za
rasilimali za pwani na bahari.
·
Serikali kutoa
ruzuku kwa wavuvi kama ilivyo kwa wakulima na wafugaji ili kuwa na uvuvi wenye
tija.
Naomba kuwasilisha.
TAARIFA FUPI YA MAENDELEO YA
UTAFITI WA MIFUGO KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
MH.DKT.TITUS MLENGEYA KAMANI (MB) TAREHE 15/8/2014
UTANGULIZI
Mheshimiwa Waziri
Kwanza
tunapenda kukukaribisha katika Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) –Tanga
ikiwa ni mara yako ya kwanza kufika hapa toka kuteuliwa kwako kuwa Waziri wa
maendeleo ya mifugo na uvuvi.Tunapenda kukupongeza pia kwa kuteuliwa na
muheshimiwa Raisi wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete kuwa waziri wa
Maendeleo ya Mifugo na uvuvi . Tunaamini na tunamatumaini kuwa utasimamia vema
sekta hii ya mifugo kwani uanataaluma ya
uendelezaji mifugo hasa katika masuala
ya kuzuia na kutibu magonjwa yasumbuayo upatikanaji wa tija katika sekta ya
mifugo.
Mheshimiwa Waziri,
Taasisi
ya utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) ilianzishwa chini ya sheria NO.4 YA 2012
na taasisi yetu ni miongoni mwa Taasisi (7)zinazounda TALIRI.Tunapenda
kuipongeza serikali yetu kwa kupitisha sheria ya uundwaji wa Taasisi hii ambayo itasimamia kikamilifu utafiti wa mifugo Tanzania ili kuongeza
uzalishaji na kipato kwa wananchi na uchumi wa Taifa kwa ujumla wake.
Mheshimiwa Waziri,
Dira
ya TALIRI ni kuwa Taasisi ya mifugo ya mfano inayochangia kuboresha hali ya
maisha ya wafugaji na wadau wengine (To be model livestock Research Insititute
that contributes towards improved
livelihood of famers and other stake holder) na dhimaya TALIRI ni kutengeneza , kusambaza na kuhamasisisha
matumizi ya tekinolojia sahihi kwa wadau wote wa mifugo ili kuboresha
uzalishaji endelevu wa mifugo (To develop ,disseminate and promote use of
appropriate techinologies to stake holders inorder to improve live stock
productivity sustainably).
Mheshimiwa Waziri ,
Jukumu
kubwa la Taasisi hii ni kufanya utafiti wa uendelezaji Mifugo hasa katika kanda
ya Mashariki yenye mikoa ya Tanga,Dar-es-salaam,Pwani na Morogoro.utafiti
umeelezwa kwenye kutathimini aina za mifugo na vyakula ,malisho, na huduma kwa
mifugo ambazo zinaleta uzalishaji bora na wenye tija katika kanda hii. Mkazo
mkubwa unawekwa katika kuzalisha ng’ombe chotara kwa ajili ya maziwa
,kuku,mbuzi,na ng’ombe wa asili wanaotunzwa kwenye nyanda za majani na
mbuga.pia taasisi imeteuliwa kuwa mojawapo ya Taasisi mahiri katika utafiti wa
uzalishaji maziwa (Diary centre of exelllence) chini ya mradi wa EAAPP (Eastern
Africa A gricultural productivity projeck).
Mheshimiwa Waziri
Historia fupi ya taasisi utafiti wa
mifugo-Tanga
Kihistoria
eneo la Taasisi lilikua linamilikiwa na wakazi /wenyeji mpaka kipindi cha vita
kuu ya pili ya dunia (1939) wanajeshi wa anga walipofanya kambi yao.Baada ya
vita (1946),eneo likawa ni la shamba la ng’ombe wa maziwa.mwaka 1950,shamba
likabadilishwaq na kuwa kituo cha uchunguzi wa mifugo likiwa na lengo la
kuzaliha nyama walioendelezwa na kuwagawanya
kwa wafugaji. Mpango wa uzalishaji ulianzishwa ,uliousisha chotara wa ng’ombe aina ya Boran na Friesian,Guarnsey
na jersey.mpango huu ulikatishwa mwaka 1965 nakazi nyingi za utafiti
ziliendelezwa kwenye kutatua matatizo ya matunzo ya wanyama .mnamo mwaka 1969 kituo
kilitambulika kama Taasisi ya utafiti na mafunzo.
Mpango
wa uboreshaji ng’ombe ulianzishwa ambapo ng’ombe aina ya Boran wenye damu 100%
na wale wenye damu pungufu ya 25%ya ng’ombe wa kisasa walipandishwa na ng’ombe
aina ya sahiwal. Lengo hasa lilikua ni kuzalisha na kusambaza majike ya sahiwal
yenye damu kati ya 82.5-100%katika kipindi hiki kulianzishwa pia ufugwaji wa
nguruwe uliohusisha majike 17 aina ya large White na dume 1 aina ya land race.
Kuanzia
mwaka 1973 jina la kituo likabadilishwa na kuwa kituo cha utafiti wa Mifugo na
kupewa jukumu la kufanya kazi za utafiti juu ya uzazi, lishe,na matunzo ya
ng’ombe wa maziwa katika ukanda wa mashariki.jukumu hili liliendelea pamoja na
kutokea kwa mabadiliko katika mfumo wa utawala mwaka 1081-1989 ambapo kituo
kiliwekwa chini ya shirika la utafiti wa Mifugo Tanzania(Tanzania Livestock
Research Organization-TALIRO).Mwaka 1989 kituo kilirudishwa chini ya wizara ya
kilimo na maendeleo ya mifugo . kwa sasa kituo kimekua mojawapo ya Taasisi za
utafiti kwenye Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa mifugo (TALIRI) chini yaWizara
ya Maendeleo ya mifugo na Uvuvi.
Mheshimiwa Waziri,
Rasilimali
na muundo wa taasisi ni kama ifuatavyo
1.
Rasilimali watu
Mheshimiwa Waziri taasisi inawafanyakazi 40 ambapo 11
kati yao ni watafiti na 11 watafiti wasaidizi wa wafanyakazi wa kada nyingine 18.vilevile taasisi
inawafanyakazi wa muda 29 wakati wote kwa shughuli za shamba.
2. Rasilimali
Ardhi
Mheshimiwa Waziri,shamba kuu la Taasisi
lilikua na ukubwa wa hektari 800 mwaka 1973,lakini eneo hilo limezidi kupungua kufikia hektari 386 kufuatia kukua
kwa jiji la Tanga.Taasisi ina shamba linguine lenye ukubwa wa hekta 753
lililopo eneo la Buhuri wa kilometa sita kutoka kituoni.
3. Muundo mbinu
ya Taasisi
Mheshimiwa Waziri,Taasisi inamajengo ya ofisi
2 jengo la maabara moja na jingo la kantini ,pia inamajengo mawili (2) ya
karakana na stoo eneo la ofisi ,majengo haya ni ya muda mrefu ambayo yanahitaji
ukarabati .kwa eneo la makazi ,kuna nyumba za watumishi zipatazo 31 ambazo pamoja na majengo mengine
yanahitaji ukarabati mkubwa .pia kunajengo kubwa kwa shyghuli za ukamuaji,stoo
ya vyakula vya ziada,banda la utunzaji ndama na chumba cha kuhifadhi
baridi(cold room)ambavyo vilifanyiwa ukarabati katika mwaka wa fedha
2011/2012.
4.
Mifugo
Mheshimiwa
Waziri,shamba lina ng’ombe 254 na mbuzi 47.
Ng.ombe waliopo kituoni ni chotara wanaotokana na ng,ombe wa kisasa aina ya
Friesian na jersey na ng’ombe wa kiasili
aina ya Boran za zebu.pia wapo ng’ombe 19 aina ya maasai kwa ajili ya
mradi wa kuboresha vinasaba vya ng’ombe wa asili unaofadhiliwa COSTECH.
5. Muundo wa
taasisi.
Mheshiiwa Waziri,Taasisi ina idara ya utafiti
5 na idara saidizi 4 hizi ni:Utafiti wa malisho(pasture and forages Research),
Utafiti wa ng’ombe wa maziwa (diary cattle Research) utafiti wa wanyama
wadogowadogo wanaocheua (small ruminants Research),utafiti wa wanyama
wadogowadogo wanaocheua (Non-ruminants Research) na utafiti wa sayansi
jamii(socio-economics)idara saidizi ni idara ya shamba (farm)Afya ya
mifugo(Animal health)utawala (administration)na uhasibu(financial,accounts and
procurement).idara hizi zitabadilika kufuatia kutokubalika kwa muundo wa
Taliri.Taasisi pia inakamati mbalimbali:menejiment,utafiti na taaluma
,ukarabati,zabuni na tathmini(quality assuarance) na wakuu wa idara (hods) pia
kuna chama cha wafanyakazi(RAAWU).
MIRADI YA
UTAFITI
Mheshimiwa waziri, taasisi inatafiti mbalimbali zinazosimamia
ikishirikiana pia na Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa ILRI,CIAT,IRISH,AID,IFAD,ASARECA,COSTECH,SNV,SUA,EGERTON
UNIVERSITY,KARI na EIAR.
mheshimiwa waziri,kwa ushirikiano huu taasisi imeweza kufanya yafuatayo,
·
Kutengeneza
b”FEAST Tool”. Inayoweza kubainisha matatizo ya upatikanaji wa malisho katika
mwaka
·
Kutengeneza
“Techfit tool”inayoweza kuweka vipao mbele nanamna yakutatua matatizo yaliyo
inishwa na FEAST Tool.Hii imejaribiwa nchini India na Ethiopia na sasa uipo kwenye hatua za mwisho za
majaribio nchini Tanzania na Kenya kwa kupitia wanafunzi wa ngazi za uzamili na
uzamivu.
·
Kupitia mradi wa EAAPP, Taasisi yetu
tumeshiriki kwenye kusimamia maboresho ya sera za maziwa na mazao yake kwenye
nchi za afrika mashariki na kati (Reginal Dairy policies harmonization) ambapo
Tanzania inaratibu taratibu za uingizaji
na usafirishaji wa vyakula vya
ziada na malisho (import and export
procedures for compounded feeds and forages) Kenya inaratibu utoaji wa mitamba
na uwekaji kumbukumbu(movement of heifers and diary records) Uganda na Ethiopia
inaratibu usindikaji wa maziwa (processing)
·
Mheshimiwa
Waziri, kwa kupitia mradi huu pia , Taasisi imeshiriki kwenye mchakato wa
upatikanaji wa mbegu za malisho katika soko (pasture and release) kwa
ushirikiana na taasisi ya kuidhinisha
utoaji wa mbegu Tanzania (TOSCI) pamoja na wadau wengine.lengo ni kuhakikisha
mbegu za malisho zinaidhinishwa kisheria na kuweza kupatikana katiaka
masoko ili kuwafikia wafugaji na wadau
wengine.
Usambazaji wa tekinolojia (Technolojia
dissemination)
Mheshimiwa Waziri,Taasisi yetu inashiriki sana katika usambazaji
wa tekinolojia zilizotokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika hapa nchini na na nje ya nchi
.mbinu mbalimbali zilizotumika kufikisha tekinolojia hizo kwa wadau mbalimbali
ni pamoja na :
·
Kutoa mafunzo na
ziara za mafunzo
·
Vipeperushi na
vijarida
·
Vitini
·
Mikutano ya
kimataifa ,kitaifa na maonyesho ya kilimo ya kila mwaka
·
Kuunda vikundi
vya wafugaji na majukumu bunifu
·
Kutumia mashamba
darasa
Mheshi
miwa Waziri,
Miradi inayoendeshwa ndani ya Taasisi (on
station projecks)ni hii ifuatayo
I.
Breeding for optimum Diary in the humid
coastal belt of Tanzania (Uzalishaji wa ng’ombe chotara anayeweza kutoa maziwa
ya kutosha kutokana na mazingira ya
ukanda wa mashariki wa Tanzania)
Mradi huu unalenga kuwa na nucleus herd kwa ng,ombe
chotara ambao walifanyiwa utafiti
nakuonekana kwamba wanaweza kufanya vizuri katika ukanda wa pwani (coastal humid belt).
Kwa mwaka huu madume 40 na majike 10 waliuzwa kwa wafugaji katika wilaya ya
Tanga ,Muheza na Mkinga.
II.
Improvement of local Goats and milk production
by cross breeding with dual purpose bucks in small holder farming systems of
North-Eastern Tanzania.
Mradi
huu unawanufaisha wafugaji ambao hawana uwezo wa kufuga ng’ombe wa kisasa wa
maziwa lakini wanapenda kupata maziwa .lengo ni kuongeza utoaji wa maziwa kwa
mbuzi wa kwa mbuzi wa asili kupitia chotara ambao hupatikana kwa kupandisha
jike la asili kwa dume la mbuzi wa
kisasa . kwa mwaka huu jumla ya mbuzi 14(madume9,majike 5,)yaliuzwa kwa wafugaji
katika mkoa ya Tanga (10) na pwani(4)
III.
Identification and improving existing
indigenous lines of chickern in traditional production systems in north-eastern
Tanzania .
Mradi
huu unapata pesa toka serikalini .utafiti wa awali kuhusu kuku wa asili
ulionyesha kuwa miongoni mwa kuku wa asili wenye umbo dogo wanataga mayai mengi
wakati wale wenye umbo kubwa wanataga mayai kidogo .mradi unalenga kupata
kuku wa asili mwenye umbi kubwa na
anayetaga mayai mengi kwa kuwachanganya
wenye umbo kubwa na dogo (blending)aina zilizopo kwenye taasisi kwa sasa ni
kishingo,kinyavu,bukini,kuchi,multicolor feathered,black australop(ex-malawi)na
bovine brown.
IV.
Pasture and forage germplasm evaluation for
improvement of ruminant feeding in the eastern zone of Tanzania.
Mradi
huu hupata fedha serikalini lakini kwa kiasi Fulani EAAPP na MILKIT kwa lengo la kuwa na benki ya aina mbalimbali
ya malisho ikiwemo miti malisho ,nyasi, mikunde,na mikunde miti,hii husaidia
kuwapatia mbegu wafugaji pale ambapo huitaji kuendeleza mashamba ya malisho au
nyanda za malisho.
V.
Establishment of cenchrus for hay and seed
production to meet demands of animal feeds for sustainable livestock
productivity.
Malisho
aina ya cenchrus ciliaris ndiyo yanayofanya vizuri kwenye ukanda wa pwani hivyo mradii huu unalenga kuzalisha
aina hiyo kwa wingi ili wafugaji waweze kupata mbegu kwa kuendeleza mashamba
yao na nyanda za malisho. Taasisi imeweza kuanzisha ekari 160 kwa shamba la
buhari na ekari 30 kwa shamba kuu ,aidha tani 40 zilisambazwa kwa wafugaji na
mikate 2500ilivunwa.
Mheshimiwa Waziri,
Miradi
inayoendeshwqa mashambani (on farm project) nii hii ifuatayo
i.
The use of FI cross bred bulls on zebu cows
for production of cross bred with quarter exotic blood for production at
farmers level.
Mradi huu unapata fedha kutoka serikalini lengo
likiwa ni kuwa na midume chotara ambayo yanastahimili ukanda wa pwani kwa ajili
ya kuboresha ng’ombe wa asili na
kuwezesha kupata maziwa mengi kwa wafugaji ambao hawawezi kupata ng’ombe wa kisasa . kwa mwaka jana madume chotara 36
yalipelekwa kwa wafugaji wa wilaya ya tanga muheza na mkinga .
Mheshimiwa Waziri,
Mirdi
inayofadhiliwa na taasisi /mashirika mbalimbali ni kama ifuatavyo
MIRADI INAYOFADHILIWA NA EAAPP
Taasisi
inashiriki katika miradi mitatu kati ya miradi mitano chini ya uhifadhi wa EAAPP
a)
Improving value addition and marketing of milk
for small holders (VAMMS) in EAAPP and ASARECA countries.
Mradi
huu unafanyika katika nchi ta Tanzania ,Kenya na Ethiopia. Lengo kuu ni
kusaidia wafugaji wadogowadogo na ngombe wa maziwa kuongeza thamani Ya maziwa.kwa
Tanzania mradi unafanyika kanda ya mashariki
katika wilaya ya Bagamoyo na muheza .Watafiti kwa Tanzania ni
Taliri-Tanga na Sua.
b)
Enhancing adoption of appropriate policies and
safety standards of feeds and milk for improved livelihood in the ECA
Countries.
Mradi
huu unafanyika katika nchi ya Tanzania ,Kenya na Ethiopia . lengo kuu ni
kubaini sera na “standards”za vyakula na mazao yatokanayo na maziwa ili kuleta
ushindikani katika soko la ndani nan je ya nchi za Afrika Mashariki
.TALIRI-Tanga na SUA ndio wasimamizi wakuu.
c)
Improving indigenous cattle for diary
production through targeted selection and cross breeding in the EAC contries
Mradi huu unafanyika katika nchi ya Kenya na
Tanzania .lengo ni kutumia ng’ombe wetu wa asili kupata chotara watakaotoa
maziwa mengi na wanaoweza kuhimili mazingira ya kitropiki.mpaka sasa madume
32ya ng’ombe yamesambazwa kwenye vijiji 7 vya kanda ya mashariki na nyanda za
juu za kusini.
d)
MIRADI INAYOHIFADHIWA NA NFAST-COASTECH
1. Enhancing
availability and productivity of dairy cattle through genetic stabilizationin
in Tanzania .
Mradi huu unalenga kuongeza maziwa kwa chotara
wa ng’ombe wretu wa asili(majike)na wale wakigeni. Mradi unatekelezwa nyanda za
juu kusini(majike aina ya iringa red) na wale wa kigeni. Mradi unatekelezwa
nyanda za juu kusini (majike aina ya iringa red)na kanda ya mashariki (majike
aina ya maasai) .TALIRI-uyole ndio wasimamizi wakuu.
2.Developing
and promoting a stratified model ta transform traditional beef cattle
production into commercial oriented beef cattle industry in Tanzania
Mradi huu unalenga kumwezesha mfugaji wan
g,ombe wa nyama kupata soko la ndani nan je kwa kuwaweka wafugaji katika
makundi ya wazalishaji,wakuzaji na wanaofanya feed lot.mradi unafanyika kanda
ya mashariki ,kanda ya kati na kanda ya ziwa lengo likiwa pia kutumia vizuri
machinjio zetu za kisasa zilizokwu=isha jengwa na ambazo zinzkaribia kumalizika
usoni . TALIRI-Tanga ,TALIRI-M PWAPWA na
TALIRI –mabuki ndio wasimamizi wakuu.
3.ILRI-LED
COLLABORATIVE PROJECTS
1.Milk
project
Enhancing
dairy-based live hoods in Indian and
Tanzania through feed innovation and valie chain development approaches
Mradi huu unatumia majukwaa bunifu(innovation
platform) na mnyororo wa thamani (value chain) ili kuweza kupata chakula cha
ziada na malisho na malisho kwa kipindi cha mwaka mzima . mradi unafadhiliwa
na I FAD na unatekelezwa India na Tanzania . kwa Tanzania mradi unafanyika katika mkoa wa Tanga (lushoto na handeni) na
mkoa wa morogoro (kilosa na mvomero).wasimamizi wa kuu ni ILRI,
CIAT,TALIRI-Tanga na Sua .
2.more
milk in Tanzania
A dapting
dairy market hubs for pro-poor small holder value chains in Tanzania.
Mradi huu unatumia njia ya “market hubs” ili
kuboresha uzalishaji wa maziwa kwa wingi na uwezekano wa kupata pembe jeo na masoko kwa urahisi
.madi unatekelezwa moa wa Tanga na morogoro kwenye vijiji 30(Tanga 14 na
morogoro 16) wahusika wakuu ni ILRI,CIAT,Heifer,TALIRI-Tanga na SUA.
IV.
MIRADI INAYOFADHILIWA NA ASARECA
1.Intergrated productivity enhancing
technology packages in small holder dairy helds in the ECA sub –region
mradi
unatekelezwa katika nchi za AS ARECA na kwa Tanzania TALIRI –Tanga na SUA ndio
wasimamizi wakuu wa mradi ambapo morogoro (wilaya ya mvomero) na T anga (wilaya
ya Tanga na Muheza) ndipo mradi unapofanyika . lengo ni kumsaidia mkulima
ambaye pia ni mfugaji kutumia fursa zilizopo kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao na maziwa.
V.MIRADI INAYOFADHILIWA NA USAID
1.Sustainable intensification in the
sub-humid maize based cropping systems of Babati .
Mradi
huu upo chini ya Africa rising(Africa –Research in sustainable intensification
for next Generation) na unalenga kutumia malisho yaliyo endelezwa kwenye mfumo
wa kilimo cha mahindi ili kuongeza upatikanaji wa lishe endelevu kwa mifugo na
kuongeza matumizi bora ya ardhi . mradi unatekelezwa katika mkoa ya Manyara
(wilaya ya Babati).
Mheshimiwa Waziri ,
Changamoto za kiutumishi na nyinginezo
ni kama zifuatazo
§ Utumishi
Mheshimiwa
Waziri, tunapenda kuipongeza serikali kwa kutambua umuhimu wa utafiti wa mara
kwa mara kuajiri watumishi wa ngzi mbalimbali kulingana na uwezo wake .Hata
hivyo Muheshimiwa Waziri ,Taasisi bado imekua na upungufu wa wafanyakazi katika
ngazi zote yaani watafiti, watafitiwasaidizi,sapporting staff hasa walinzi,
wachungaji na wakauaji ambao ni vibarua .baada ya serikali kuondoa ajira za watumishi wa kada mbalimbali Taasisi
imelazimika kuajiri vibarua wapatao 29 ili kufanikisha kazi za kuchunga
,kukamua na uklinzi.Hali hiyo imefanya Taasisi kutumia fedha nyingi kuwalipa kila mwezi. Tunaomba serikali
kupitia bodi Ya TALIRI NA wizara ya maendeleo ya mifugo na
uvuvi iwaajiri watumishi wa kada hizi
ambazo ni muhimu sana katika shughuli za kila siku za Taasisi.
Idara ya wafanyakazi TALIRI Tanga
Aina
|
Elimu
|
Aina ya
Ya kudumu
|
Ajira
Ya muda mfupi
|
Idadi waliopo kazini
|
Idadi waliopo masomoni
|
Gap
|
Researchers
|
Phd
Msc
Bsc
|
1
6
10
|
0
0
0
|
1
6
8
|
0
1
2
|
7
9
18
|
Field officers
|
Diploma
certificate
|
4
1
|
0
0
|
4
1
|
0
0
|
20
10
|
others
|
Field
Auxiliary
Watchman
supporting
|
7
3
8
|
16
9
4
|
23
12
12
|
0
0
0
|
15
6
8
|
total
|
40
|
29
|
67
|
3
|
92
|
§ Usafiri
Mheshimiwa
waziri, tunaishukuru pia serikali kwa kuendelea kutatua matatizo ya uhaba wa
vyombo vya usafiri kwenye idara na taasisi zake ili kufanikisha shughuli
mbalimbali zikiwemi za utafiti. Pamoja na jitihada hizo hapa kwetu bado tuna
uhaba wa wa vyombo hivyo , tunalogari moja ambalo ndilo zima mengine yote ni
mabovu na ugharimi pesa nyingi kwa matengenezo ya mara kwa mara na pia
kukwamisha shughuli za utafiti.
§ Fedha za
kufanyia utafiti
Mheshimiwa waziri ,serikali imeendelea kutoa
fedha kwa ajili ya shughuli za kawaida za maendeleo ya na zautafiti kila mara ingawa wakati mwingine
fedha zinazotolewa zimekua hazitoshelezi hivyo kurudisha nyuma shughuli za
utafiti na maendeleo ili kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya taasisi.
§ Uchakavu wa
majengo
Uchakavu
wa majengo na nyumba za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na mabanda ya kufanyia utafiti limeendelea kuwa tatizo kwa ufanisi na
wafanyakazi kwenye taasisi
§ Maabara
Uhaba
wa maabara ya utafiti wa lishe ya mifugo ,kuongeza thamani ya maziwa na
uzalishaji mifugo.
Mheshimiwa waziri,
Mtazamo wa baadae wa Taasisi (future
plans )ni kama ifuatavyo
§ Kuongeza idadi ya mifugo (ng’ombe wa mazaiwa
na nyama )ndani ya taasisi na kwa wafugaji kwa kutumia MOET(Multiple ovaluation
embryo transfer)kwa kuwa na maabara (in vitro laboratory) kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali (INDICUS,SCF,na COSTECH,KARI).
§ kufanya utafiti za kuongeza ubora wa maziwa na
maziwa yatokanayo maziwa (milk handling,processing and value addition) kwa kuwa
na maabara (milk processing laboratory)innovation platforms na hub business
model.
§ Kuendelea kushirikiana na wadau m,balimbali
zikiwemo taasisi za kitaifa na kimataifa kufanya tafiti mbalimbali kwa
maendeleo ya mifugo.
Mheshimiwa waziri,
Hitimisho
Utafiti
ni sehemu muhimu sana katika kuzidi kuinua sekta hii ya mifugo. Kupitia kwako muheshimiwa Waziri tunaomba
serikali ishughulikie changamoto tulizo nazo ili kuongeza ufanisi na kufikia
malengo ya taasisi.
Mheshimiwa
Waziri,Tunapenda kukukaribisha tena
kwenye Taasisi yetu mara upatapo nafasi.
Nawasilisha
RISALA YA WANANCHI WA KIJIJI CHA MSOMERA HANDENI KWA MHESHIMIWA
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI DRT. TITUS MLENGEYA KAMANI (MB) TAREHE
18/08/2014.
Mheshimiwa
waziri wa mifugo na uvuvi kwanza sisi wananchi wa kijiji cha Msomera, tunatoa
shukrani zetu kwa Mwenyezi Mungu aliyekuongoza wewe pamoja na wote ulioambatana
nao katika msafara wako kutembelea kijiji chetu.
Mheshimiwa
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kijiji cha Msomera kilianishwa rasmi
mwaka 1922 baada ya viongozi wa tarafa ya Sindeni ambayo ndipo kilipo na tarafa
ya Mswaki ambayo sasa ipo Wilaya ya Kilindi walipofanya kikao cha pamoja na
kuona haja ya kuanzishwa kwa vijiji viwili vya wafugaji ambavyo ni Msomera
tarafa ya Sindeni na Lengusero tarafa ya Mswaki ambacho kwa sasa kipo Wilaya ya
Kilindi baada ya mgawanyo wa Wilaya hizi.
Kijiji kimefanya jitihada kubwa ya kupata haki yake na cheti chake na
ulipofika tarehe 2 januari mwaka huu, kijiji kilikabidhiwa cheti chake na Mkuu
wa Wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu. Tunashukuru kwa wote walioweka jitihada
zao katika kufanikisha hili.
Kijiji
hiki nkina jumla ya watu 4900, wanaume
2150 na wanawake 2750. Kuna jumla ya mifugo 59,362 ikiwa ni pamoja na
ng’ombe 23,500, mbuzi 16,000, kondoo 19,500na punda 362. Kijiji kina josho
ambalo kwa sasa huduma imesimama kutokana na uhaba wa maji. Aidha hali ya maji
itakapotengemaa huduma itaendelea kama kawaida.
Hapo
awali kulikuwa na mabwawa mawili ambayo ni Msomera na Mlunduzi lakini kwa
bahati mbaya mabwawa yote yamebomolewa kwa mvua na hivyo kufanya maisha ya
wakazi wa kijiji hiki kuwa ya adha kubwa kwa binadamu na mifugo. Na kwaajili ya
adha hiyo ndiyo sababu maifugo mingi haipo kijijini hapa na imetawanyika sehemu
mbalimbali ndani nan je ya Wilaya ya Handeni.
Mnamo
tarehe 23.3.2014 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ngugu Jakaya Mrisho
Kikwete alitembelea kijiji chetu na kutoa ahadi ya kutujengea mabwawa mawili,
visima virefu vitatu, kuboresha mifugo yetu kwa kuhalimisha majike zaidi ya 200 kutupa zawadi ya ng’ombe toka ranchi yake na
madume 2, kuwapeleka wafugaji watano wa kijiji hiki kwenye mafunzo Afrika Kusini, uanzishwaji wa Ranchio
ndogondogo za wananchi kupitia Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na mwisho
kina mama wawili kwenda kumkabidhi Mama Salma Kikwete vazi la kimasai. Kwa
ajili hiyo Mheshimiwa Waziri tunakuomba
kwa heshima kubwa umkumbushe Mhe. Rais hadi alizotoa ili ikiwezekana
zitekelezwe ili kuwaondolea wananchi wa kijiji hiki matatizo yaliyopo.
Mheshimiwa
waziri, kijiji hiki kimepimwa kisheria na kina ukubwa wa hekta za mraba 50,971.
Kwa sasa kijiji kipo kwenye mchakato wa kutengeneza mpango bora wa ardhi ambao
utabainisha mipaka ya kijiji hiki na vijiji vya jirani kwa kutengeneza barabara
za kuonyesha mipaka. Na mipaka ya ndani itakayotenganisha maeneo ya makazi,
malisho, kilimo, vyanzo vya maji na hifadhi kwa lengo la kuboresha utunzaji wa
mazingira na kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji.
Vilevile
kijiji kitakosa fadhila endapo hakitamshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya
Handeni ndugu Muhingo Rweyemamu ambaye juhudi zake kubwa zimeweza kufanikisha
mambo mbalimbali ya maendeleo ya kijiji hiki.
Mwisho
Mhe. Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi tunakutakia safari njema wewe na
msafara wako na Mwenyezi Mungu akubariki sana.
Naomba kuwasilisha
Imeandaliwa na Wananchi wa kijiji cha
Msomera.
Ahsante.
.
KUTOKA : KITUO CHA UDHIBITI UBORA WA MAZAO YA UVUVI NA
MASOKO KANDA YA KASKAZINI –TANGA
KWENDA: WAZIRI WA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
UTANGULIZI
Kituo
cha uthibiti ubora wa mazao ya Uvuvi na masoko kanda ya kaskazini kilichopo
mkoani Tanga kilianzishwa mnamo mwaka 2000 kikiwa na mtumishi mmoja .baada ya
mda wa mwaka mmoja akaongezwa mtumishi wa pili na kufikia hadi hivi sasa
kitengo kina idadi ya watumishi wane.
Kanda
ya kaskazini ina jumla ya mikoa mine ambayo ni Tanga ,Kilimanjaro ,Arusha na
Manyara,kitengo kinamajukumu ya kulinda ,kusimamia na kidhibiti ubora wa mazao
ya uvuvi yanayosafirishwa ndani na nnje ya nchi pamoja na kusimamia ukusanyaji
wa maduhuli kwa kushirikiana na kituo
cha Doria Uvuvi katika kanda hii ya kaskazini , kituo kina gari moja aina ya
Nissan quaqui na pikipiki moja DT 250
KAZI ZA KITUO
Lengo
kuu la kituo ni kudhibiti ubora na usalama wa mazao ya Uvuvi kwa
watumiaji/walaji ndani na nnje ya nchi na kusimamia masoko ya mazaop ya Uvuvi
kwa kutekeleza sera za mwaka 1997,sheria ya mwaka 2003 na kanuni ya mwaka 2009
za Uvuvi.ili kufanikisha lengo hili kituo kinafanya malengo mahususi kwa
• Kufanya kaguzi katika viwanda vya
uchakataji /usindikaji wa mazao ya uvuvimialo na masoko ya Uvuvi.
• Kusimamia na kufanya kaguzi katika
mipaka iliyopo kwenye kanda ya kaskazini
• Kutoa vibali vya usafirishaji mazao ya
Uvuvi ndani na nnje ya nchi
• Kutoa elimu kwa wavuvi ,wauzaji wa
mazao ya Uvuvi na wasindikaji /wachakataji wa mazao ya Uvuvi viwandani
• Kusimamia makusanyo ya maduhuli
yatokanayo na usafirishaji wa mazao ya Uvuvi ndani na nnje ya nchi’
VYANZO VYA MAPATO
Kituo
kinakusanya maduhuli kutokana na ukusanyaji wa ushuru wa mazao ya Uvuvi
yanayosafirishwa nje ya nchi yakitokea hapa jijini Tanga ,faini ya makosa
yanayofanywa na wavuvi (compoundment) kama vile
kuvua kwa kutumia vyombo visivyo sajilia ,kusafirisha mazao ya Uvuvi
bila kibali,kuvua bila kuwa na leseni halali ya Uvuvi.
MAFANIKIO
Kituo
kimefanikiwa kusimamia ukusanyaji wa
maduhuli jumla ya shilingi milioni
28,113’318.15 ambazo ni asilimia 28%
Kituo
kimeweza kuwabadili wavuvi hasa wa pweza kuvua pweza wenye uzito wa gram 500 na
kuendelea ‘pia kituo kimeweza kuwapa elimu ya kuhifadhi mazao ya uvuvikwa ubora
na usalama kwa kutumia cool box
Kituo
kimesaidia kupatikana kwa soko la kudumu
kwa wavuvi wadogowadogo kwa kuhamasisha
ongozi wa kiwanda kwa kusindika mazao ya Uvuvi kununua mazao ya Uvuvi kwa
wavuvi hao.
Nawasilisha.
KAMPUNI YA RACHI ZA TAIFA LTD
RANCHI YA MZERI HILL
TAARIFA FUPI YA RANCHI YA MZERI HILI KWA WAZIRI WA
MAENDELEO
MIFUGO NA UVUVI DKT .TITUS KAM ANI ( MB)
TAREHE 18 AUGUST 2014
MH. WAZIRI
Tunayo
furaha ya pekee kukukaribisha kwenye
Ranchi hii ya mzeri
Hii
haswa kwa kuwa ziara hii ni yakwanza kutembelea kutoka
Mheshimia
.Rais Jakaya Mrisho kikwete akuteua
kwenye wadhifa
Wako
huu.A idha kwa niaba ya wafanyakazi wote wa mzeri hii ni Ranchi
Naomba
kuchukua nafasi hii kutoa taarifa fupi ya Ranchi.
1.1
HISTORIA YA
RANCHI YA MZERIHILL
Ranchi ya mzeri hill ilianzishwa mwaka 1968 chini ya awamu ya kwanza ya program Ya Taifa ya kuendeleza Mifugo (NATIONAL LIVE STOCK DEVELOPMENT PROGRAMME - Phase 1 1968 -1971) Mradi huo ulikua unahifadhiwa na Benki ya Dunia kwa mkopo ambapo serikali serikali ya Tanzania ilitoa asilimia 30 ya gharama zote. Aidha , awamu ya pili ya mpango (1978- 1982) kulikua na uwekezaji na uimarishaji wa Ranchi .
Ranchi ya mzeri hill ilianzishwa mwaka 1968 chini ya awamu ya kwanza ya program Ya Taifa ya kuendeleza Mifugo (NATIONAL LIVE STOCK DEVELOPMENT PROGRAMME - Phase 1 1968 -1971) Mradi huo ulikua unahifadhiwa na Benki ya Dunia kwa mkopo ambapo serikali serikali ya Tanzania ilitoa asilimia 30 ya gharama zote. Aidha , awamu ya pili ya mpango (1978- 1982) kulikua na uwekezaji na uimarishaji wa Ranchi .
1.2
Ranchi hii iko km.35 kaskazini
mwa mji wa Handeni km. 47 kusini mwa mji
wa
Mombo na km 45 kusini magharibi wa mji wa korogwe , Ranchi
ipo mkoa wa Tanga
Wilaya ya Handeni na Korogwe. Ina msambao wa mchanganyiko wa
nyasi ,kundekunde
Udongo mweusi na wakichanga sehemu ndogo na
inapata mvua kiasi cha mm 760 -800 kwa
mwaka.kutokana na kuwa na udongo na mvua
kiasi cha kutosha shughuli za ufugaji zimefanyika kwa ufanisi mkubwa.
Joto la hapa ni 18c-32c. na mvua ni za misimu miwili ya kiasi ya milimita
760-800.
1.3 Mandhari ya Ranchi hii ni mazuri kwa
ufugaji na nyasi zake zenye virutubisho
vya
Kutosha kwa uboreshaji wa
mifugo.Ranchi inaukubwa wa hekta 41,246.11, lakini kufuatia
Uamuzi wa serikali wa kugawa RANCHI
ndogondogo ambazo zimemilikishwa kwa
Wawekezaji wa kitanzania ,sasa
Ranchi mama (Core Ranch) imebaki na
eneo la
Ha 21,236 ambayo inauwezo wa kuweka ng’ombe 7,000. Kwa sasa Ranch ina ng’ombe
2367,kondoo 206 mbuzi 62 na farasi
2.
2 LENGO LA KUANZISHWA
Ranchi ya mzeri hill imepewa majukumu
makubwa kama ifuatavyo:-
I.
Kuzalisha na
kusambaza ng’ombe bora kwa wafugaji.
II.
Kuzalisha na
kunenepesha ng’ombe wa nyama kwa soko la ndani kwa sasa.
III.
Kuwaelekeza
wafugaji kuhusu muelekeo wa ufugaji bora bna matumizi ya ng’ombe katika kilimo
cha kutumia maksai ambayo na teknolojia rahisi ns sahihi na uyinzaji wa
mazingira .
3 IDADI
YA WAFANYAKAZI
Ranch inajumla ya wafanyakazi 40
(wakudumu 8,mikataba 22.idadi hii huongezeka na kupungua kutokana na idadi ya
mifugo iliyopo.
4. MIFUGO
4.1.Ranch
ina ng’ombe wanakua wa nyama aina ya boran wenye asili ya kaskazini mwa Kenya,
(Ambao nao walitoka Ethiopia na Sudan) ng’ombe
wa boran wanaumbile kubwa wanakua haraka na wanamudu mazingira yetu vizuri kuliko aina nyingine za kigeni.Aidha nyama
yake inaladha nzuri kwa kula na kuweka mafuta ndani ya nyama badala ya juu ya
nyama.
Kutokana
na borani ,Ranchi pia huzalisha mtambo wa maziwa kwa njia ya uhimilishaji kwa kupandisha na mbegu za Friesians chotara
wanao zalishwa na kuuzwa kwa wafugaji wadogo wadogo kwa ajili ya uzalishaji wa
maziwa.
4.2 kondoo
Ranchi inakondoo wa nyama aina ya Black headed Persian( BHP) wenye asili
ya afrika kusini
Uzito wake hufika kilo 150. Pia chotara
kati ya BHD na Doppers hutoa machotara yenye uzito
Kilo
80 mpaka 120. Aina hii ya kondoo inanyaama nzuri ambayo haitoi shombo wakati wa
kupika na kwa wakaji pia.
4.3 Mbuzi
Ranch pia inafuga mbuzi kwa ajili ya
nyama ambao majike ya kienyeji
wamezalishwa na aina
Anglonubian na kupata mbuzi chotara
wakubwa na wenye nyama nzuri ambao hutoa kilo
60
mpaka 80.
4.4 Farasi
Ranch hufuga farasi kwa ajili ya
doria na hivyo kurahisisha shughuli za
ufuatiliaji za ufuatiliaji wakiwa malishoni.
5. UZALISHAJI
5.1
katika msimu huu wa mwaka 2013/2014
Ranchi ya mzeri imezalisha ndama 660 idadi ambayo ni sawa na asilimia 73 ya
lengo la uzalishaji.
Aidha
uzalishaji kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2008/2009 hadi 2013/2014
Unaonyeshwa
kwenye jedwali lililo ambatanishwa.
Uzalishaji
wa kipindi cha miaka 5 kuanzia 2008/2009 -2013/2014
2008
|
2009
|
2009
|
2010
|
2010
|
2011
|
2011
|
2012
|
2012
|
2013
|
2013
|
2014
|
|
Wastani
majike
|
1200
|
1302
|
1300
|
1378
|
950
|
900
|
||||||
Idadi
ya ndama
|
960
|
80%
|
1041
|
80%
|
1105
|
85%
|
797
|
70%
|
686
|
72%
|
660
|
73%
|
Vifo
vya ndama
|
20
|
2%
|
20
|
1.9%
|
20
|
1.8%
|
13
|
1%
|
20
|
1.7%
|
12
|
0.1%
|
Vifo
wakubwa
|
173
|
1.7%
|
57
|
1.3%
|
39
|
1.1%
|
106
|
3%
|
106
|
4%
|
48
|
2%
|
Jumla vifo
|
193
|
1.7%
|
77
|
1.4%
|
59
|
1.3%
|
116
|
3.5%
|
126
|
3%
|
60
|
1.4
|
6. MIUNDO
MBINU
Hali ya
miundo mbinu ni nzuri kiasi na baadhi inafanya kazi na nyingine mbovu.
Miundo mbinu inayo fanya kazi ni kama ifuatayo:-
·
Mitambo ya
kunyunyizia dawa -2 (spray race)
·
Matanki ya maji
makubwa -5
·
Matanki ya maji
madogo -6
·
Kisima kirefu
lita 10000 kwa saa 1
·
Vibanio -2
·
Feedlot-1
·
Mabwawa-5
·
Malambo-8
·
Mabanda ya mbuzi
/kondoo 2
·
Band la hei 1
·
Gereji/kapenta1
·
Banda la magari
1banda la ngozi 1
·
Duka la kuuza
/kuchinja nyama 1
·
Gari Toyota Hilux
su 36877 1
·
Lori fuso su
37223 1
·
Pikipiki tairi 3
su 35951 1
·
Trecta new
Holland su 35939 1
·
Treila la Hei su
37128 1
·
Bailar ya kufunga
hei 1 Mbovu
·
Mower ya kukata
majani 1
·
Jembe la plau 1
·
Mizani ya mifugo
2
·
Kompyuta 3
·
Over head
projecta 1
·
Laminaton/Binding/cutter
3
·
Photocopy/fax 1
·
Printer 2
·
Generator KVA
15 1
·
GeneratorKVA 7.5
1
·
Mashine za maji/
pump 2/2
·
Sola nyumba 8
7.0 MAFANIKIO
Baadhi ya mafanikio ni pamoja na ;
I.
Ranchi
inajiendesha yenyewe kwa sasa kwa kutumia rasilimali zilizopo japo hazitoshi.
II.
Ranchi imekua
ikiuza ng’ombe kwa ajili ya kuchinja kwa wafanya biashara wa nyama na kwa sasa Ranchi inachinja kiasi kikubwa
kwa ajili ya duka lake lililopo korogwe
III.
Ranchi inanunua
ng’ombe wa kunenepesha kutoka kwa wafugaji wadogowadogo wa asili (zebu) .Mpango huu unawapatia wafugaji
wadogowadogo soko la uhakika kwa ajili ya mifugo yao (mwaka 2010 hadi 1792
walinunuliwa)
IV.
Ranchi inafunga
wastani wa robota15,000 za hei kwa mwakla kutoka shamba la majani lenye thamani
ya tsh milioni 60 na hivyo kuongezea shamba mapato.
V.
Ranchi imefungua
duka la kisasa mjini korogwe ambalo huuza ng’ombe wawili kwa siku na wateja ni
korogwe ,Lushoto, na Mombo.
8.0 CHANGAMOTO
I.
Kama ilivyo kwa
Ranchi nyingine za NARCO , zipo
changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo katika uendeshaji. miongoni mwa
changamoto hizo ni pamoja na;
8.1 kukosa mtaji kumesababisha
yafuatayo;
II.
Kasi ndogo ya
ununuzi wa mifugo ya kunenepesha kutoka kwa wafugaji wadogowadogo
III.
Mifugo michache
kulinganisha na ukubwa wa eneo hvyo kuongeza gharama za uzalishaji.
IV.
Kasi ya kupunguza
vichaka imekua ndogo hivyo kupunguza uzalishaji wa malisho na kuongeza kazi ya upotevu wa mifugo mara
kwa mara.
V.
Ranchi imekua
ikiuza mashamba kila mwaka kwa muda mrefu ili kugharamia shughuli za uzalishaji
nah ii imechangia kwa majike wazazi .
8.2
Matatizo mengine.
I.
Uharibifu wa
mazingira unatokana na uchomaji miti ovyo ukataji wa miti kwa ajili ya mbao na
uchomaji mkaa.
II.
Kupanda kwa
gharama za uendeshaji hasa bei za madawa , vipuli na mafuta
III.
Milipuko ya
magonjwa mara kwa mara CBPP,FMD.
9 MIPANGO YA BAADAE :
I.
Kuongeza idadi ya
mifugo kwa kuongeza uzalishaji na ununuzi wa ng’ombe wa kunenepesha kutoka kwa
wafugaji wa ng’ombe wa asili kutokana na
fedha za mikopo kutoka kwenye taasisi za
fedha
II.
Kuendelea
kuzalisha mitambo chotara F1 wa maziwa kwa uhamilishaji kulingana na mahitaji
III.
Kuendeleza nyanda
za malisho kwaz kupandsa majani na
mikundekunde yenye ubora ili kupambana ya ukame ya dhamira ya kupunguza madhara
ya vifo hasa wakati wa kiangazi
IV.
Upunguzaji wa
vichaka kwa njia mbalimbali ili kuboresha
malisho ya mifugo kwa kuzingatia utaalam utokanao na matokeo ya
mradi uliofadhiliwa na tume ya sayansi9
COSTECH)
V.
kuendelea kutoa
elimu kwa Ranchi ndogondogo, wafugaji
wadogowadogo ili kuwepo ufugaji endelevu na wenye tija na wafanyakazi ili
kuwepo ufugaji endelevu na wenye tija
VI.
kuongeza maduka
mawili ya nyama katika eneo la Tanga mjini,Mombo, ili kupanua wigo wa
masoko
10. VITALU RANCHI NDOGONDOGO.
Ranchi inajumla ya vitalu kumi ikiwemo Ranchi mama. Vitalu hivyo
Ha,2127.22 hadi Ha, 4164.64. ifuatayo ni taarifa ya vitalu hivyo kwa
kuzi
Ngatia
miundo mbinu , mifugo pamoja na ukubwa wake kama ifuatavyo:-
I.
STAGE FARM LTD 645/1-AREA 2231.74 HA
Mifugo
Ng’ombe
400,mbuzi na kondoo 250
Miundo
mbinu:-
Mazizi
2,nyumba 2 za tofali,spray race
Wafanyakazi-
7
Maji
mto –pangani
Usafiri
pikipiki 1 .
II.
KLUB AFRIKO 645/2-AREA 2127.22 HA
Mifugo:-Ng’ombe
81, kondoo na mbuzi 227
Miundo
mbinu:-
Mazizi
2, Mabanda ya mbuzi 2
Nyumba
za tofali 2 Maji mto pangani
Usafiri
–pick up moja na trekta
wafanyakazi
5
III.
SADO FARM
645/4 –AREA 3733.12 HA
Mifugo
:- ng’ombe 90, mbuzi 210 na kondoo 340
Miundo
mbinu :-
Nyumba
2 za tofali
Zizi
moja
Mabanda
ya mbuzi 2
Spray
race 1
Wafanyakazi
6
IV.
OLOSIPA RANCH 645/5- AREA 3676.177 HA
Mifugo
ng’ombe:- 1300, mbuzi 210 na kondoo 400
Miundo
mbinu:-
Nyumba
3 za tofali, nyumba za kawaida 6 za mabati
Feedlot
1
Mabwawa
2 usafiri pickup 1, trecta 2 na pikipiki
2
Wafanyakazi
21
Umeme
– solar + generator
V.
MAJOR ONE 645/6 AREA 4164.64 HA
Mifugo:-
ng’ombe 150 , kondoo 350 na mbuzi 120
Miundo
mbinu :-
Nyumba
3 za tofali na nyingine 3 zinaendelea
kujengwa
Usafiri
pick up 1 na pikipiki 2
Bwawa
1
Wafanyakazi
5
VI.
SHALOM
FARMING AND PLANTATION 645/7 –AREA 3231. 00 HA
MIFUGO
:- ngombe 520,
Miundo
mbinu:-
Mabwawa
2
Borehole
1 Lambo 1
Nyumba
za bati 2
Mazizi
2
Usafiri
– gari 1 pick –up
VII.
GOOD CHANCE 645/8-AREA 3012.12 HA
Mifugo:-
ng’ombe 60
Kondoo
na mbuzi 25
Miundo
mbinu :-
Nyumba
2 za tofali
Wafanyakazi
7
Usafiri
pick up 1, trekta 1 na pikipiki 2
Maji
mto pangani
VIII.
LEIMBA RANCHI 645/9- AREA 3144.14 HA
Mifugo
:- Ng’ombe 800
Miundo
mbinu:-
IX.
Nyumba 2 za bati
Maji
mto pangani
Usafiri
pikipiki 2
X.
KWEISEWA VILLAGE 654/10 AREA
3065.78 HA
Eneo
hili wamepewa wanakijiji waendelee kwa shughuli za kilimo na ufugaji.
10.1 CHANGAMOTO ZA VITALU
Changamoto za vitalu zimo katika maeneo haya
makuu yafuatayo:-
a.
Kasi ya
uendelezaji ni ndogo ambao wameendeleza vizuri ni vitalu vine.
b.
Ukosefu wa maji .
10.2
MAFANIKIO
Wenye vitalu wanauhusiano mzuri na Ranch ya mzeri hill imekua shamba darasa na wamekua wakifuatilia kwa karibu matokeo ya
mradi unao fadhiliwa na COSTECH hapa
shambani na wamehaidi kutekeleza matokeo haya kwa vitendo.
11. MRADI UNAO FADHILIWA NA TUME YA SAYANSI(COSTECH)
Mwaka 2012 ya sayansi
kampuni ilibuni mradi na kupata ufadhili wa tume
ya
sayansi ( COSTECH) NARCO I;lishirikiana na chuo kikuu cha
SOKOINE
na huu mradi ni wa miaka 3.
Mradi huu ulilenga
kufanya tafiti mbalimbali hasa katika
maeneo makubwa matatu ambayo ni :-
I.
Uboreshaji wa
malisho na nyanda za malisho ambayo
majibu ya mwisho yameonyesha kuwepo kwa mafanikio mazuri na yenye tija kwa kutumia gharama nafuu , lakini pia
teknolojia iliyotumika ni rahisi na hvyo kumuwezesha kila mfugaji kumudu
kuboresha kila eneo lake la malisho ,
kwa mfano uzalishaji umeongezeka kutoka
tani 2.5 mpaka tani 9 kwa hekta.
II.
Uboreshaji
wa kosafu kwa kutumia njia ya uhamilishaji ambapo mbegu bora ya borani ilitumika kupandisha majike borani
wanapopatikana ndanim ya Ranch hii . katika zoezi hili jumla ya ng’ombe 547
walihimilishwa na ng’ombe 364 walipata mimba ambao ni sawa na asilimia
66.5% na kufaulu kuzalisha jumla ya
ndama 359. Ndama hao wamezaliwa wakiwa
na uzito kati ya kilo 35 hadi 40 ukilinganisha na ndama waliozaliwa kutokana na upandishaji wa asili (madume )
wenye uzito kati ya kilo 25 hadi 30
III.
Unenepeshaji
ulilenga na kuzingatia aina ya mifugo inayonenepeshwa, wakati wa kunenepesha na
kiwango wa uzalishaji wa chakula ili kuangalia uwiano wa ongezeko la uzito baina ya makundi hayo yanayonenepeshwa na kwa wakati gani .
Katika zoezi hili imeonekana kuwa ng’ombe wa kienyeji akinenepeshwa
huongezeka gram 500 kwa siku tofauti na ng’ombe wa nyama wa kisasa (borani)
waliongezeka gramu 1000-1500 kwa siku , hata hvyo imegundulika wakati
mzuri wa kunenepesha mifugo kwa gharama
nafuu ni kipindi cha mvua na chenye malisho yakytosha.
12 SHUKRANI.
12.1
Nashukuru uongozi wa wilwya za Handeni
na Korogwe na Mkoa wa Tanga kwa
Namna ambavyo wamekua
wakishirikiana nasi kwa shughuli mbalimbali kwa nia ya
Kuendeleza Ranchi hii na
wananchi.
12.2
Tunashukuru wizara yetu ya maendeleo
ya mifugo na uvuvi na bodi ya narco na
uongozi mzima wa kampuni kwa juhudi
zinazoendelea za kuiboresha kampuni.
12.3
TUnaipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa kuimilikisha baadhi ya maeneo kwa
Wawekezaji wa kitanzania
pamoja na kufungua milango ya
kukaribisha wawekezaji
wakubwa kwa ranchi za mfano .Tunaomba serikali iendelee na juhudi za
kuitafutia
kampuni mtaji wa kutosha , kama mkaguzi na
mzibiti mkuu wa fedha serikali alivyo
pendekeza katika ripoti zake za miaka mitatu
iliyopita.
13.
HITIMISHO
Mh: Waziri,
Tunaomba kuihakilisha serikali kwamba uwezo wa kufanya kazi tunao ,
Utaalam tunao
Nia ya kujifunza zaidi tunayo Juhudi na maarifa tunayo na nia ya
kuendeleza Ranchi tu
Nayo hivyo tunaomba tupate MTAJI na
tuongezewe mifugo ili tuendeshe Ranchi kwa u
Fanisi zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.
NAWASILISHA
EUZEBIUS RWIZA
MUTAYABARWA
MENEJA WA
RANCHI
ZIARA YA WAZIRI MKOA WA MTWARA
HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI MHE. DKT . TITUS
MLENGEYA KAMANI (MB) WAKATI WA UZINDUZI WA JENGO LA OFISI YA TAASISI YA UTAFITI
WA MIFUGO TANZANIA (TALIRI) NALIENDELE, MTWARA TAREHE 2 AGOSTI, 2014.
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara;
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Lindi;
Makaibu Wakuu wa Wizara ;
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu COSTECH;
Wakurugenzi wa Taasisi za Utafiti wa Mifugo na Uvuvi;
Wataalamu wa mifugo na Uvuvi;
Viongozi na Wananchi wa Nalindele.
Waandishi wa Habari.
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana
Napenda kuchukua fursa hii
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kuweza kukutana leo
katika hafla hii fupi na muhimu ya kufanya uzinduzi wa jingo la Taasisi ya
Taifa ya Utafiti wa Mifugo Kituo cha Naliendele hapa Mtwara. Aidha, nachukua fursa
hii kuwashukuru ninyi nyote mliotenga muda wenu wa kuja kujumuika nasi hapa
leo.
Ndugu Mkuu wa Mkoa ,Wageni waalikwa na Wananchi; Sekta za Mifugo na
Uvuvi ni muhimu kutokana na mchango wake
katiak kuwapatia wananchi lishe bora, ajira na hivyo kuchangia kuondoa au
kupunguza umasikini pamoja na kukuza uchumi wa Taifa. Kwa mwaka 2013/2014Sekta
ya Mifugo ilikua kwa asilimia 3.8 na
kuchangia katika pato la Taifa kwa
asilimia 4.4. Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe milioni 22.8, mbuzi milioni
15.6 na kondoo milioni 7.0.
vilevile wapo kuku wa asili 35.5,
kuku wa kisasa milioni 24.5 na
nguruwe milioni 2.01. ulaji wa mazao
ya mifugo kulingana na viwango vya mataifa (FAO, 2011) ni kilo 50 za nyama, lita 200 za maziwa na mayai 300
kwa mtu kwa mwaka. Kwa upande wa nchio yetu viwango vya ulaji wa mazao hayo kwa
sasa nui wastani wa kilo 12 za
nyama, lita 45 za maziwa na mayai 75 kwa mtu kwa mwaka. Viwango hivi ni
vidogo sana ukilinganishwa na mapendekezo ya FAO. Jitihada za makusudi zinatakiwa
kuwekwa katika kuhakikisha kuwa wananchi wanahamasishwa kutumia mazao ya mifugo
kwa lengo la kuboresha afya zao ili hatimaye tuweze kukaribia viwango
vinavyopendekezwa kimataifa.
Ndugu Mkuu wa Mkoa ; Serikali inajizatiti katika kufikia Azimio la Maputo
la kutenga karibu asilimia 10 ya GDP
yake kwa utafiti ambapo tathimini ya mwaka 2012/2013 inaonesha tunafikia karibu asilimia 8 ukichanganya fedha zote zinazotolewa
na Serikali na Wadau wa Maendeleo.
Katika kuimairisha na kuendeleza
utafiti Serikali imeweka na inaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuendeleza
utafiti ikiwemo kuwepo kwa Sera, sharia , kanuni na miundo ya Asasi
zinazosimamia na kuendesha utafiti kote nchini kupitia chombo kikuu
kinachoratibu cha COSTECH kwa kushirikiana na Wizara husika. TALIRI ambayo
imeanzishwa chini ya sharia namba 4 ya
mwaka 2012 kuanziaq mwaka huu 2014/2015 itakuwa ianjiendesha chini ya usimamizi
na ushauri wa bodi yake ambayo nimeiteua hivi karibuni. Hivyo naiagiza bodi ya
TALIRI kuanza kazi mara moja kusimamia na kuelekeza Taasisi hii itekeleze
majukumu yaliyokusudiwa na kuweza kujiendesha kisasa na kuleta tija. Mnatakiwa
kuhakikisha kuwa mnatumia fursa zote zilizopo na kuacha kufanya kazi kwa
mazoea.
Ndugu wananchi; napenda pia kusisitiza na kuelekeaza vityuo vyote vya
utafiti chini ya mwavuli wa TALIRI ambavyo vimetamkwa kwa majina katika sharia
na vinginevyo vitakavyoanzishwa kutokana na sharia hii vifanye kazi kwa ubunifu
wa gharama nafuu lakini wenye matokeo ya haraka ili kufanya secta ya mifugo iwe
kiongozi wa uchumi hapa nchini katika muda mfupi ujao. Bodi inayosimamia
TALIRI lazima kuhakikisha inaimarika,
inakua haraka na kutoa matokeo mazuri ya kiutafiti katika viwango vya
kiamtaifa. Mikakati ya kuboresha miundombinu ya kusomesha wataalamu waliobobea wenye shahada za juu za PHD waongezeke na
miundo mbinu na maabara kuwa za kisasa hadi zifikie viwango vya kushiriki katika mafunzo ya postgraduate
MSc na PhD zikiwa kama Deemed
universities ‘’
Ndugu mkuu wa mkoa ,Wageni waalikwa na wananchi ; Kazi ya ujenzi wa ofisi ya TALIRI
Naliendele ambayo leo nina lizindua ni katika mwendelezo wa utekelezaji wa
Ilani ya uchunguzi wa CCM ya 2010-2015 kama ilivyoainishwa katika ibara ya 38 katika vifungu (e) na(h)
vya ilani hiyo kama ifuatavyo:
1. Kuendeleza
elimu kwa wafugaji ili wajue kuwa mifugo waliyonayo ni mali ambayo inaweza
kuvunwa katika umri na uzito muafaka unaokidhi mahitaji ya soko , ili
kuwaondolea umaskini wao badala ya
kuridhika na wingi wa mifugo iliyo duni na maisha ya kuhamahama .
2. Kuimarisha
utafiti wa mifugo kwa kuboresha na kuhifadhi kosaafu za mifugo ya mifugo ili
kuongeza uzalishaji na tija
Serikali imeendelea kudhihirisha
utashi wa kisiasa (political will) kwa vitendo kwa kuimarisha utafiti wa mifugo
na tafiti nyingine .Kupitia mpango huu serikali imegharimia ujenzi wa jingo
hili la TALIRI Naliendelee ambapo limegharimu shilingi 470,821,600/=. Aidha serikali inaendelea naku gharamia ukarabati wa
maabara ya Uhawilishaji wa viini tete (embryos) kutumia teknolojia za “embyo
transfer” zinazojumuisha (MOET/OPIVF-Multiple ovulation and Embryo Transfer;
Ovum Pick-up InVitro fertilization) katika vituo vyake kuanzia na TALIRI
Mpwapwa. Nichukue fursa hii kuwapongeza TALIRI kwa kubuni na kuanza kutekeleza
ujenzi wa miundombinu ya kutumia teknolojia hii ambayo imeanza kuenea na
kutumika duniani kama njia za kusambaza”genomes” zenye sifa kwa wingi na
haraka. Matumizi ya teknolojia hizipamoja na nyingine kama “Clonining” zinaweza
kupunguza urefu wa muda wa kuzaliana kwa mifugo- “Generation Interval” ambayo
ni kubwa kuliko ilivyo ka mazao ya kilimo ya muda mfupi. TALIRI lazima mjipange
kujenga uwezo wa wataalamu wenu kuweza kufanya utafiti na kutumia teknolojia
hizi na kuwafundisha ndani nan je ya nchi na kuzieneza kwa wafugaji nchini
badala ya kuendelea kuzisikia tu kila siku kwenye taarifa na matarajio yenu.
Ndugu Mkuu wa Mkoa; nimetaarifiwa kuwa taliri mnaendelea na ujenzi
wa mtambo wa kuchakata maziwa katika kituo cha TALIRI Uyole na inaendelea kukamilisha ujenzi wa
maabara ya utafiti wa nyama ya ng’ombe katika kituo cha TALIRI Mabuki. Napenda
kuwapongeza kwa juhudi hizo na kuwaagiza mzikamilishe mapema ili ziweze
kutumika na kutoa matunda yaliyokusudiwa. Tafutebni fedha kutoka vituo vingine
nje ya vituo vya kawaida kwa kuandika na kuwasilisha maandiko ya miradi maeneo
mbalimbali hususani katika mifuko ya kimataifa inayotoa fedha kwa tafiti
mbalimbali. Kwa upande wa serikali Wizara yangu itaendelea kuwaombea na
kusisitiza Serikali iendelee kugharamia mafunzo ya watafiti wa mifugo katika
ngazi mbalimbali kwa lengo la kupata wataalamu mahiri katika sekt6a pana ya
utafiti, uzalishaji na afya ya mifugo na samaki.
Ndugu Mkuu wa Mkoa; kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto ya kuwepo
uunganisho mdogo baina ya utafiti, mafunzo na ugani. Napenda kuchukua fursa hii
kuiagiza TALIRI kuanzisha na kuendesha kitengo imara cha usamabazaji teknlojia
(technology transfer) katika vituo vyenu kwa kuwa na “Communication and
Documentation Center” mbele tu za ofisi zenu ambazo zimekuwa chanzo cha
kupata taarifa zote za teknolojia zilizokuwa zimekwisha iva na tayari kwenda kwa watumiaji. Nchini
India chini ya mwavuli wa India
Agriculture Research Institute (ICAR) KILA Taasisi ya Utafiti ina
kitengo imara cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma (Communication and Technology
Transfer) mbali na taratibu mlizozizoea za siku ya Wakulima/Wafugaji katika
vituo vyenu na tafiti za nje nza kushirikisha wadau.
Kwa upande wa wananchi wa Mkoa
Mtwara na Mikoa yote nchini natoa wito
wajenge taratibu na tabia za kufika au kuwasiliana mara kwa mara na vituo vya
Taasisi ya Utafiti wa Mifugo na Uvuvi
nchini ili waweze kujifunzza, kuona na kuchukua teknolojia bora zinazoweza
kuboresha ufugaji na uvuvi/ ufugaji viumbe kwenye maji ili waweze kuongeza tija
na kipato kinachotokana na matumizi ya teknolojia zinazozalishwa kwenye vituo
vyetu vya utafiti. Elimu hutafutwa, hivyo nawaomba wananci nao waongeze udadisi
ili ufugaji wao uwe na tija.
Ndugu Mkuu wa Mkoa; pamoja na mafanikio ya utafiti na jitihada za
Serikali kuumarisha utafiti wa mifugo bado unakabiliwa na changamoto
mbalimbali. Mojawapo ya cha changamoto hizi ni pamoja na wananchi wanaozunguka
mashamba na vituo vya utafiti kuvamia ardhi iliyotengwa kwa ajili ya shughuli
za utafiti. Wananchi katika maeneo yanayozunguka vituo kama vile TALIRI Kongwa
, Mpwapwa, Mabuki, Tanga na kituo kidogo cha Mnima Wilayani Newala wamekuwa na
tabia ya kuingia kinyume na utaratibu kwenye mashamba haya kwa nia ya kutaka
kulima, kuchunga na hata kujenga na hivyo kusababisha uharibifu wa miundombinu
na mazingira. Napenda kuchukua fursa hii kuagiza wananchi wote waliopo jirani
na vituo vyetu vya utafiti kuheshimu sharia na taratibu zilizowekwa wanapotaka
kutumia maeneo yaliyotengwa na Serikali
kwa ajili ya shughuli za utafiti.
Ndugu Mkuu wa Mkoa ; napenda kuhutimisha hotuba yangu kwa kutoa
shukrani zangu za dhati na za Wizara
yangu kwa ushirikiano uliopo na unaoendelea na Tume ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) ambayo Serikali iltoa fedha kupitia
kwao na yenyewe kutoa fedha kugharamia uimarishaji wa miundombinu ya uatafiti,
ujenzi wa miundombinu mipya ya utafiti pamoja na kusomesha watyafiti kwa lengo
la kuimarisha na kuboresha utafiti nchini. Pamoja na Taasisis hizo wizara yangu
inashauri na kuomba COSTECH kujumuisha Wakala zetu za mafunzo FETA na LITA
kuimarisha uwezo na miundombinu ya utafiti ili nazo ziweze kufanya utafiti
kutumia wataalamu waliobobea ambao wanazidi kuongezeka kadri Serikali
inavyozidi kusomesha.
Nimalize kwa kuwasihi tena
wananchi wa Mikoa hii ya Mtwara la Lindi waendelee kushirikiana kna vituo vya
utafiti vilivyopo katika ukanda huu wa Kusini ikiwemo TALIRI Naliendele ili wajipatie maarifa na ujuzi
unaotokana na jitihada zinazofanywa na wataalamu wetu. Ninawathibitishia tena
kwa Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi itaendelea
kuimariosha shughuli za utafiti kwa lengo kuhakikisha kuwa ufugaji na uvuvi
unakuwa wa tija na unamkomboa mfugaji na mvuvi kutoka katiak lindi la
umasikini.
Maada ya maelezo haya napenda
kutamka kuwa “jingo la ofisi ya TALIRI Naliendele limezinduliwa rasmi”
AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA.
HOTUBA ILIYOTOLEWA NA KAIMU MKURUGENZI
MKUU WA TALIRI DKT. RASHID MSANGI, TAREHE 02/08/2014 WAKATI WA UFUNGUZI WA
JENGO LA UTAFITI WA MIFUGO MTWARA NALIENDELE
Mheshimiwa
Mgeni Rasmi,
Jengo
hili la ofisi ya taasisi ya utafiti wa mifugo Naliendele unalozindua
leolimegharimu jumla ya shillingi 470,500,000 kati hizo Tume ya Sayasi na teknolojia (COSTECH) ilichangia
jumula ya shilingi 370,500,000 na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
ilichangia jumla ya shilingi 100 milioni.Tunapenda kuishukuru serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia COSTECH kwa kutoa fedha hizi ambazo zimewezesha
ujenzi wa jengo hili. Jengohili ambalo unalizindua leo litaongeza na kuimarisha
kazi za utafiti katika kituo hiki.
Mheshimiwa
Mgeni Rasmi,
Mpaka
sasa serikali kupitia COSTECH inaendelea kufadhili miradi mitano ya utafiti
ikiwemo utafiti wa kuku,malisho, nguruwe na ng’ombe wa nyama iliyopo
TALIRI Mpwampwa , Kongwa na Uyole. Aidha
COSTECH inaendelea kugharamia ukarabati wa miundombinu ya utafit ikiwemo ukarbati
wa maabara ya baiteknolojia (biotecknology) nalishe ya mifugo, Kwa upande
mwingine maabara za lishe ya mifugo (animal nutrition laboratory) na
baitecknolojia zilizokarabatiwa bado zinahitaji vifaa kuziwezwsha kufanya kazi
zilizokusudiwa. Vilevile COSTECH inagharamia mafunzo ya watafiti walioajiriwa
na TALIRI waliopo masomoni katikachuo kikuucha Sokoine cha kilimo (SUA) .Tunaishukuru
serikali na Tume ya Taifa ya Sayansi na Tecknolojia kwa uwezehaji huo. Aidha
tunaomba COSTECH iwezeshe kupata vifaa vya maabara illi ziweze kufanya kazi
zilizokusudiwa.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi,
Taasisi inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
upungufuwa vitendea kazi na rasilimali watu na fedha. Watafiti wamekuwa
wanaandika miradi mbalimbali kwa wadau wa maendeleo ya ndani na nje ili kuweza
kuongeza fedha za utafiti na ununuzi wa vitendea kazi. Aidha Taasisi inakubaliwa na uhaba wa nyumba za
watumishi ,lakini pia hata ambazo zipo ni chakavu na zinahitaji kukarabatiwa
,taasisi imekuwa ikitenga fedha zamaendeleo kwa ajili ya ukarabati wa nyumba
zake, ingawa fedha hazitoshi.
Moja
ya changamoto kubwa zinazoikabili Taasisi ya utafiti wa MifugoTanzania kwa ujumla
wake ni uvamizi wa maeneo ya aridhi ambapo wananchi wanaoishi karibu na
mashamba ya Taasisi wanakwenda kinyume cha sharia kwa ajili ya kulima,
kuchunga, hata kujenga. Hali hii, inasababisha watafiti kushidwa kutekeeza
majukumu yao ya kitaaluma ikiwemo kusimamia mipango ya udhabiti wa magonjwa ya
mifugo na tafiti za uendelezaji wa malisho bora. Aidha, usalama wa watumishi wa
taasisi unahatarishwa zaidi pale ambapo migogoro imepelekea ugomvi. Naomba
wananchi walio karibu na mashamba ya taasisi kuwa ni vema kutii sheria na
utaratibu zinazohusu matumizi ya rasilimali za umma yakiwemo mashamba ya TALIRI,
kwani faida zinazipatikana ni Kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote. Aidha,
taasisi inawaomb waheshimiwa wabunge na madiwani, kuendelea kuwaelimisha
wananchi juu ya kuheshimu mipaka halali ya mashamba ya serikali na taasisi
zake.
Mheshimiwa
Mgeni Rasmi,
Baada
yakusema hayo machache, napenda kukushukuru tena Kwa kukubali kufika Kwa ajili
ya shughuli hii.nawatakia wageni wetu wote hafla njema
Ahsanteni
sana.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
|
|||
|
|||
02/08/2014
Kumb.
Na.
ADM.20/ZVC/MT/VOL.lll/450
TAARIFA FUPI YA KITUO CHA HUDUMA ZA
MIFUGO CHA KANDA YA KUSINI (ZVC MTWARA): KWA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA
UVUVI, MH. DR. TITUS MLENGEYA KAMANI (MB)
Salaam
Mh.
Waziri,
Naomba
kwa niaba ya idara ya huduma za mifugo na watumishi wote wa kituo cha huduma za
mifugo kanda ya kusini; ninakushukuru kwa kuweza kufika katika kituo na
kuahirisha majukumu mengine uliyonayo kitaifa.
Utangulizi
Kituo cha huduma za mifugo cha kanda ya kusini
(ZVC Mtwara) kimeanzishwa mwaka 2012 kutokana kugawanywa kwa kituo cha
uchunguzi wa magonjwa ya mifugo cha kanda ya kusini (VIC Mtwara) kufuatia
kuundwa kwa wakala wa maabara ya mifugo Tanzania (TVLA). Hivyo kituo hiki kwa
sasa kinafanya kazi zote zilizokuwa zikifanya na VIC Mtawra isipokuwa utambuzi
wa magonjwa ya wanyama ambayo kwa sasa inafanywa na wakala.
Mh.
Waziri, kihistoria VIC Mtwara ilizinduliwa mwaka 1982 na Hayati Baba wa Taifa,
Mwl, Julius Kambarge Nyerere ikiwa ni mpango wa serikali wa kuingiza na
uendelezaji wa mifugo kanda ya kusini. Kituo hiki kilikuwa kikihudumia mikoa
mitatu yaani Lindi, Mtwara na Ruvuma. Baadhi ya kazi za iliyokuwa VIC Mtwara
ni:
1. Uchunguzi
na ufuatiliaji wa magonjwa mbalimbali ya mifugo kwa ajili ya kubaini kimaabara
2. Kiusimamia
uzuiaji wa magonjwa ya mifugo kwa kushirikiana na halmashauri zote za wilaya,
miji, wafugaji binafsi, wafanyabiashara za mifugo na wadau wote wa sekta ya
mifugo kwa ujumla.
3. Kufanya
utafiti wa magonjwa ya mifugo.
4. Upimaji
wa kimaabara wa samuli za wanyama.
5. Udhibiti
wa usalama wa biashara za mifugo, wanyama porina mazao yanayotokana na wanyama.
6. Kuchunguza
na kufuatilia magonjwa ya mifugo yanayoathiri pia binadamu kama vile Kimeta,
Mafua ya ndege na Kifua Kikuu, Kichaa cha Mbwa na Ugonjwa wa Kuharibu Mimba.
7. Kusambaza
chanjo za mifugo, kufuatilia na kusimamia ufanisi wa chanjozote za magonjwa
muhimu kiuchumi na kijamii katika kanda ya kusini.
8. Kutoa
ushauri wa mafunzo ya muda mfupiya uzuiaji na udhibiti wa magonjwa ya wanyama
kwa wadau mbalimbali wa sekta ya mifugo kwa kushirikiana na wizara na wadau
mbalimbali wa sekta ya mifugo.
9. Upimaji
wa ubora wa dawa za kuogeshea mifugo.
10. Ukusanyaji
wa ushuru wa biashara ya mifugo katika masoko ya upili (hayajaanzishwa katiak
kanda yetu.).
Mh.
Waziri, baada ya kuanzishwa kituo cha huduma za mifugo cha kanda (ZVC Mtwara)
kimeendelea na majukumu yote ya iliyokuwa VIC isipokuwa upimaji wa sampuli za
maabara na ubora wa dawa za kuogesha mifugo ambazo zipo TVLA au taasisi zingine
za serikali.
Kwa
sasa kituo chetu mbali ya kufanya kazi hizo juu, chini ya idara ya huduma za
mifugo ya wizara yako, ZVC ina majukumu mengine kama vile
I.
Kusimamia kituo cha uhimilishaji wa
ng’ombe kilichopo Lindi Manispaa.
II.
Kushirikiana na taasisi za kitafiti kama
vile TALIRI, SUA, NIMRI, TVLA, TFDA, TANAPA, TAWIRI na nyingine nyingi.
III.
Kusimamia miradi iliyowekwa na wizara
katika kanda.
IV.
Kusimamia ustawi wa wanyama kwa
kushirikiana na halmashauri za wilaya na wadau wote mifugo.
Mafanikio
Mh.
Waziri kituo kimeendelea kuwa ni tegemeo na kimbilio la matatizo mengi ya
wafugaji na jamii. Kwa mfano:
I.
Tumeweza kubaini na kuweza kuudhibiti
ugonjwa wa Sotoka ya mdbuzi na kondoo kwa kuubaini kimaabara na kufuatilia
uchanjaji wa mifugo katika maeneo ambayo yalikuwa hayajaathirika.
II.
Pia ugonjwa wa mdondo/kideri kwa kuku wa
asili umeweza kupungua kwa kiwango kikubwa kutokana na uelewa wa wafugaji juu
ya matumizi ya chanjo dhidi ya mdondo ikiwa ni pamoja na I2
III.
Kupitia mradi wa wizara wa kutokomeza
kichaa cha mbwa tumefanikiwa kuzuia vifo vya wanyama na binadamu katika
halmashauri zinazopitiwa na mradi.
IV.
Tumeweza kufuatilia vifo vya ng’ombe
katika jeshi la magereza mkoani Lindi na kudhibiti.
V.
Pia tumeweza kudhibiti ugonjwa hatari wa
kuku katika banda la utafiti wa kuku TALIRI Naliendele.
VI.
Tumefanikiwa kutoa ushauri wa kiutaalamu
katiak jeshi la polisi na mahakama juu ya wafugaji au mfugaji aliposhitaki wezi
wa mifugo .
VII.
Tumeweza kufuatilia, kuchukua sampuli na
kuwasilisha maabara kwa utambuzi wa milipuko ya magonjwa ya homa ya mapafu ya
ng’ombe na ugonjwa wa kuoza miguu au midomo.
VIII.
Baadhi ya watumishi wameweza
kujiendeleza kitaaluma na kupitia mmiradi ya wizara.
IX.
Vilevile kituo kina baadhi ya watumishi
ambao wameweza kutoa machapisho ya kisayansi katika majarida ya kisayansi ya
kimataifa.
X.
Pamoja na kugawanyika VIC,ZVC Mtwara na
TVLA katika kituo hiki tumeendelea
kufanya kazi kwa pamoja na bila ya kuelezwa hakuna anayeweza kuuona mgawanyiko
katika shughuli zetu.
Pamoja
na mafanikio haya juu kituo kinakumbana na changamoto nyingi kama ifuatavyo:
I.
Uhaba wa watumishi. Kwa sasa kituo kina
jumla ya watumishi watano tu VO-2, LFO-2
na dereva mmoja. Kituo kinahitaji kuongezwa watumishi kama ifuatavyo VO-1,
LFO-2, Mhasibu 1, Mnunuzi 1, PS -1 na dereva 1.
II.
Kituo kinahitaji kuwa na ofisi nje ya
maabara na miundombinu ya kuhifadhi chanjo lakini bado hakijafanikiwa kupata
fedha za ujenzi wa ofisi ijapokuwa katika bajeti iliyopita tumeweza kuweka
katiak bajeti ya maendeleo.
III.
Gari tunalo moja la mradi wa kichaa cha mbwa
ambalo limekuwa likitumika katika ofisi zetu mbili (TVLA na ZVC Mtwara). Hivyo
likienda safari kituo kinabaki bila usafiri.
IV.
Ucheleweshwaji wa malipo ya fedha za
matumiziya ofisi unaotokana na mfumo mpya wa malipo katika hazina. Hili
husababisha kituo kushindwa kutumia fedha katika shughuli zake. Mfano OC ya
mwezi Mei haijalipwa kutokana na matatizo ya mfumo TISS ijapokuwa hazina ndogo
ilikuwa imeshaziingiza kwa malipo.
Mh.
Waziri ili kupunguza changamoto za kituo, na hususani bajeti finyu inayotolewa
ya OC kati ya milioni 16 na milioni 26 kwa mwaka; baadhi yetu watumishi tumekuwa
tukiandika miradi na kufanikisha fedha kiasi cha shilingi milioni mia moja
ishini na moja (mil. 121) katiak miaka miwili iliyopita. Pamoja na hilobado
kituo kinaomba utusaidie tuweze kufanikisha yafuatayo:
I.
Ujenzi wa ofisi kama utakavyozindua leo
hapa taliri tunakadiria shilingi milioni mia tatu sabini zinaweza kufanikisha
hilo.
II.
Kupata gari moja au mawili zaidi aina ya
landcuiser station wagon kwa kuwa shughuli zetu zinahitaji kusafiri mara kwa
mara.
III.
Wizara iendelee kuajiri watumishi wa
sekta mifugo hapa kituoni na hata katika halmashauri.
Mwisho
japo si kwa umuhimu tunaomba upokee taarifa hii na tunakukaribisha sana uzidi
kufanya ziara kama hii mara kwa mara wakati mwingine.
Wako
katika ujenzi wa Taifa letu na ninayoheshima kuwasilisha.
Dr.
Albano Oscar Mbyuzi
Afisa
Mfawidhi
Kituo
cha huduma za mifugo kanda ya kusini
ZVC
Mtwara.
HOTUBA YA WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA
UVUVI MHESHIMIWA DK. TITUS MLENGEYA KAMANI (MB) KWENYE UZINDUZI WA MFUMO WA
KITAIFA WA UTAMBUZI NA UFUATILIAJI MIFUGO ULIOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA SHULE
YA MSINGI MTONGANI, MLANDIZI WILAYA YA KIBAHA, JULAI 22, 2014.
Mheshimiwa Mwamtumu Mahiza, Mkuu wa Mkoa wa
Pwani;
Mheshimiwa Diana Templelman, Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula na Kilimo (FAO);
Mhreshimiwa Minoru Homma, Mwenyekiti wa
Development Partners - Agricultural Working Group;
Mheshimiwa Halima Kihemba , Mkuu wa Wilaya
ya Kibaha;
Mheshimiwa Abuu Juma, Mbunge wa Jimbo la
Kibaha Vijijini;
Mheshimiwa Mansuli Ally Kisebengo,
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha;
Mheshimiwa Kasongo Kirendu, Makamu
Mwenyekiti wa Hlmashauri ya Wilaya ya Kibaha;
Mheshimiwa Fatma Shari, Diwani wa
Kilangalanga;
Wakurugenzi wa Wizara na Wakurugenzi
Watendaji wa Halmashauri za Wilaya mliohudhuria;
Dr. Helmut Karb, Mkandarasi wa ADT-UBK toka
Ujerumani;
Wenyeviti wa Vyama vya Wafugaji, Asasi na
Wadau wengine wa Mifugo.
Waandishi wa Habari;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote
napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika siku ya leo tukiwa na
afya tele. Aidha, napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru waandaaji wa hafla
hiikunialika kuwa Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi wa Mfumo wa Kitaifa wa Utambuzi
na Ufuatiliaji Mifugo.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa,napenda
kuchukua fursa hii kuwapongeza shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo
(FAO) kupitia Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na Wilaya ya Kibaha kupitia Mkuu wa
Wilaya na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha pamoja na wadau wengine waliochangia
kwa namna moja au nyingine katika kuandaaa na kufanikisha shughuli hii muhimu
kwa mustakabali wa uchumi wan chi yetukupitia biashara ya mifugo.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, Tanzania
imejaliwa kuwa na rasilimali kubwa ya mifugo. Kulingana na takwimu zilizopo,
idadi bya mifugo nchini inakadiriwa kuwa na ng’ombe milioni 22.8, mbuzi milioni
15.6 na kondoo milioni 7.0.
vilevile wapo kuku wa asili 35.5,
kuku wa kisasa milioni 24.5 na
nguruwe milioni 2.01. rasilimali ya
mifugo hii tuliyonayo inatosheleza soko la ndani ya nchi na tunaweza kuuza
ziada nje ya nchi. Tanzania tunauza wastani wa tani 353 za nyama ya mbuzi na
kondoo kwa mwaka yenye thamani ya US$ 1,343,960 katika soko la Mashariki ya
kati tu na hatujaingia la Asia ya mbali na Ulaya ambako moja ya masharti ni
kuwa na mfumo wa utambuzi wa mifugo unaofanya kazi. Uchumi wa mifugo unategemea
sana upatikanaji wa soko la uhakika kwa mifugo na mazao yako. Nchi nyingi
duniani ambamo mifugo inachangia katika uchumi ni kutokana na masoko makubwa ya
mifugo. Soko zuri la
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na Ndugu Wafugaji,
mfumo wa Utambuzi na Ufuatiliaji Mifugo ni nyenzo muhimu na yalazima katika
ufugaji kwa sasa dunianikote ili kuwezesha kukubalika katika masoko ya
kimataifa. Pamoja na hayo ni nyenzo inayosaidia kukabilian na magonjwa ya
mifugo, wizi wa mifugo, uhamishaji au usafirishaji holela wa mifugo na hivyo kuepusha
migogororo baina ya wafugaji na wakulima pamoja na watumiaji wengine wa ardhi.
Mfumo wa
utambuzi na ufuatiliaji mifugo kwa tafsiri rahisi ni utaratibu unaotuwezesha
kuwa na alama katika mifugo katika mifugo na kuweka kumbukumbu za matukio
muhimu katika maisha ya mifugo yetu. Utaratibu wa kuweka kumbukumbu ndio
usajili wa mifugo, wafugaji na matukio muhimu ya mifugo yetu. Mfano kuzaliwa,
vifo, kupotea, kuhama au kusafirisha, chanjo au matibabu mengine ili kuhifadhi
kumbukumbu zote hizi nilizotaja na nyingine nyingi unahitajika mfumo wa
kompyuta uliojengwa mahsusi kwa ajili ya shughuli hiyo. Kwa bahati nzuri Tanzania
tumepata msaada wa Dola za Kimarekani 475,000 sawa na Tsh. 781,375,000/= kutoka
kwa wnzetu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ambao
walitusaidia kuujenga Mfumo kupitia wazabuni wa Kampuni za Kijerumani
zilizoitwa UBK na ADT. Nimearifiwa kwamba mfumo huu wa kompyuta umekamilika na
sasa umeanza kufanya kazi katika Wilaya za mfano za Kibaha, Bagamoyo na Mheza
ambapo jumla ya ng’ombe 5,845 wametambuliwa.
Ndugu wafugaji, Bunge la Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania lilitunga Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuattiliaji
Mifugo Na 12 ya mwaka 2010 (Sura 184) na pia Waziri waMaendeleo ya Mifugo na
Uvuvi chini ya Sheria hii alitoa kanuni zza kuwezesha utekelezaji wa sheria hii
kupitia Tangazo la Serikali namba 362 (G.N. 362)
Sharia hii na
kanuni zake zinatumika kwa pamoja na
sheria nyingine chini ya Wizara yangu ambazo nazo zinalenga kuboresha
uzalishaji wa mifugo na soko lake. Sheria hizi
ni pamoja na Sheria ya Magonjwa ya Mifugo (Animal Diseases Act 2003), Sheria ya Tasnia ya Nyama (Meat Industry
Act, 2006), Sheria ya Nyanda za malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Mifugo Na.
13 ya mwaka 2010 na Sheria ya Ngozi (Sheria Na.18,2008).
Ndugu wafugaji, utekelezaji wa Mfumo
huu baada ya kuuzindua leo hautakuwa jambo la hiyari au utashiau utashi wa mfugaji
bali ni lazima kwa mujibu wa Sheria na Kanuni. Hivyo, napenda kuchhukua fursa
hii kuwashauri na kuwaelekeza wafugaji wote katika maeneo ambayo Waziri
nitatangaza kuwa ya Utambuzi wa Mifugo(Compusory Livestock Identification Areas)
washiriki katika kutambua na kusajili mifugo yaona wawe tayari kuchangia katika
ununuzi wa vifaa vya utambuzi wa mifugo hiyo. Serikali kupitia Wizara yangu
pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa itasimamia na kuratibu utekeleza wa
Mfumo kwa faida ya wafugaji na maendeleo ya sekta kwa ujumla.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na Ndugu Wafugaji,
Ili usimamizi na utekelezaji wa mfumo huu uwe endelevu katika ngazi za Mamlaka
za Serikali za Mitaa, Wizara yangu inazishauri mamlaka hizi kufufua na kutumia
mifuko ya Maendeleo ya Mifugo (Livestock
Development Fund LDF). Mfuko huo utawezesha kuwa na fedha za mzunguko za
kununulia vifaa vya utambuzi na kuchangia gharama za nyingine za uendeshaji. Napenda nichukue nafsi hii
kuwapongeza Halmashauri za Wilaya za
Karagwe na Ngara Mkoani Kagera kwa tafsiri sahihi ya kifungu cha 24Kifungu Kidogo
cha 2 cha Sheria ya Utambuzi na Ufuatiliaji Mifugo ambacho kimetamka kwamba
wanufaika na mfumo huu wachangie gharama ambapo walitaka wafugaji wao
kuchangia. Hivyo Mamlaka za Serikali mza
Mitaa nyingine nchini hazina budi kuiga
mfano huu.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na Wananchi,
Ili ufuatiliaji wa mifugo na mazao yake katika mnyororo wa thamani wa mifugo
nuwezekane kupitia huu. Hapana budi wadau wanaohusika kuanza ufugaji,
wasafirishaji, waendesha minada, waendesha machinjio na Maafisa Ugani pamoja na
wasimamizi wa Kanzidata ya Mfumo (TANLITS Database) watimize majukumu yao kama
yale ya kutambua mifugo, kutoa taarifa ya mifugo inapozaliwa, kufa, kuchinjwa
au kusafirishwa.
Ndugu wafugaji na wananchi, mwisho
napenda nitoe shukrani zangu za dhati kwa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja
wa Kimataifa (FAO), kwa msaada wa kugharamia ujenzi wa mfumo huu. Aidha,
shukrani hizi ziwaendee Washirika wetu wa Maendeleo (Development Partners)
waliokuwa wakichangia katika Mfuko wa
ASPP Busket Fund (Irish Aid, IFAD, JAICA na Benki ya Dunia), Mradi wa EAAPP
(Benki ya Dunia) na Serikali kwa kugharamia unu nuzi wa wa vifaa vya utambuzi
na usajili wakati wa ujenzi wa mfumo huu.
Vilevile napenda
nishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Watendaji wa Wizara yangu, Wafugaji na
Wananchi wa Mlandizi kwa kuandaa hafla hii.
Napenda kutambua
nafasi na ushiriki wa taasisis mbalimbali kwenye ujenzi wa Kanzidata ya Mfumo
wa Utambuzi na Ufuatiliaji Mifugozikiwemo;
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambao wametuwezesha kupata takwimu mbalimbali
za maeneo na ramani, Mamlaka ya Vitambulisho ya Taifa na Wakala wa Serikali
Mtandao kwa ushauri na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa mawasiliano ya
mtandao. Aidha nalipongeza Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda
(TIRDO)LILILOSHIRIKI Katika hatua za awali za uanzishwaji wa mfumo kwa
kuwezesha mijadala ambayo hatimaye ilizaa mfumo huu. Pia Benki ya Rasilimali
(TIB) ambayo imeonesha nia ya kushiriki kwa kuhamasisha wale wanaotaka kuwekeza
katika ufugaji kuzingatia matakwa ya kuwa na mfumo huu.
Ndugu wananchi, natoa wito kwa Taasisi
nyingine za Kitaifa na Kimataif kuendelea kushirikiana na Wizara yangu kuimarisha
na kuboresha zaidi mfumo huu ili uweze
kukidhi mahitaji ya Nchi nzima naviwango vya Kimataifa.
Pamoja nanyi
narejea tena kusisitiza kauli mbiu ya uzinduzi wa mfumo huu; “SAJILI MIFUGO YAKO KWA UHAKIKA
WA SOKO NA UDHIBITI WA WIZI WA MIFUGO NA MIGOGORO”
Baada ya kusema
hayo napenda kutangaza kuwa Mfumo wa Kitaifa wa Utambuzi, Usajili na
Ufuatiliaji Mifugo Mifugo Umezinduliwa Rasmi.
AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA.
VIKAO VYA WAKUU WA IDARA/VITENGO NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA
Kila wiki siku ya Jumatatu ni siku ya kufanya Kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo wa wizara kuanzia saa nne kamili asubuhi. Kama unahitaji kumuona katibu Mkuu Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa Idara au Kitengo, hakikisha unamuona kabla ya saa za kikao .
BARAZA LA WAFANYAKAZI
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ilifanya Kikao cha Baraza hilo katika ukumbi wa ST Gaspar pale Dodoma mapema mwezi juni 2011 tarehe 16 na 17 /06 na kutoa Maazimio ambayo sasa yanatekelezwa . Watumishi wote walishiriki katika uchaguzi wa uongozi mpya wa TUGHE hapa Wizarani na RAAWU kwa upande wa Utafiti kule Mpwapwa ambapo ndipo ilipo Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Mifugo Mpwapwa. Wakuu wa Idara na Vitengo wamepewa dokezo la kukumbushwa utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa pale Dodoma dokezo la tarehe 11/10/2011 na Katibu wa Baraza .
HOTUBA YA BAJETI 2011/12
Hotuba ya bajeti ya wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi imechapishwa kwenye gazeti la Uhuru na Habari leo tarehe 28/07/2011, pia inapatikana kwenye mtandao wa wizara http://www.mifugo.co.go.tz/
MAANDALIZI YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA KWA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI YATAFANYIKA VIWANJA VYA SABASABA BARABARA YA KILWA - DAR-ES-SALAAM KUANZIA TAREHE 1 - 12/12/2011
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi inapenda kuwajulisha Wadau na Wananchi kuwa itashiriki kwenye maonyesho tajwa hapo juu, yatakayofanyika kuanzia tarehe 1 - 12 /12/2011. Wadau wote wanakaribishwa, ambapo baadhi ya wadau watakuwa ni sehemu ya maadhimisho hayo, kwa wale ambao hawatashiriki moja kwa moja waje waone wenzao hatua waliyopiga mbinu ,utaratibu na utendaji wao wa kazi. (KUONA NI KUAMINI) Hakuna lisilo wezekana Vilevile mtapata fursa ya kuelezewa na Wizara ni huduma gani ambazo ikiwa ni Idara au Vitengo vya Mifugo na Uvuvi hufanya katika kuendeleza Sekta hizo muhimu katika maisha ya Mtanzania, nini jukumu la Wizara katika kutekeleza Sera Mipango na Mikakati mbalimbali ambayo imeandaliwa na Wizara. Aidha Wadau watakuwepo kuonyesha matokeo ya Sera, Mipango Mikakati mbalimbali ambapo wataeleza na kuonyesha wamenufaika vipi na usimamizi na ufuatiliaji huo wa Wizara katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuendeleza sekta hizo mbili kwa ujumla.
Wote Mnakaribishwa
WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI.
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, imegawanyika kwenyeSekta kuu mbili yaani Sekta ya
- Mifugo
- Uvuvi
- zile za Mtanbuka
Sekta ya Mifugo ina Idara zifuatazo:
- Huduma za Mifugo.,
- Uzalishaji, Masoko na Matumizi ya ardhi kwa mifugo,
- Utafiti Mafunzo,Ugani Utanmbuzi na ufuatailiaji wa Mifugo.
- Maabara Kuu ya Mifugo
- Baraza ka Vetenary
- Taasisi ya Taifa ya Utafiti Mpwapwa
Sekta ya Uvuvi ina Idara zifuatazo
- Maendeleo ya Uvuvi
- Uzalishaji Viumbe kwenye Maji.
Idara za Mtambuka
- Sera na Mipango
- Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu.
Viengo Mtambuka
- Fedha
- Sheria
- Ukaguzi wa Ndani
- Manunuzi
- Mawasiliano Serikalini.
"TUSHIRIKIANE KATIKA KUENDELEZA WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI"