WAZIRI OLE NASHA ALIVYOVALIA NJUGA MIGOGORO YA ARDHI RUFIJI.TANZANIA DAIMA TAREHE 9 JUMAMOSI, JANUARI,2016. UK 9
NA ASHA BAN
Uelewa mdogo wa wananchi katika swala la sheria na kanuni za utawala wa ardhi,ndiko kunasababisha na kuchochea migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya nchi.
NYAVU ZA MILIONI 41/=ZATEKETEZWA.GAZETI LA TANZANIA DAIMA,NIPASHE UK 28 YA TAREHE 11 JUMATATU, JANUARI,2016.UK 6.
NA WALTER MGULUCHUMA.
Idara ya uvuvi Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa imeteketeza kwa kuzichoma moto nyavu 52 zenye thamani za sh Milioni 41 zilizokuwa zikitumika kwa Uvuvi haramu katika ziwa Rukwa.
WAFUGAJI WAASWA KUTUMIA FURSA.GAZETI LA RAIA TANZANIA LA TAREHE 11 JUMATATU,JANUARI 2016 UK 7, GAZETI LA UHURU UK 9,NIPASHE JUMAPILITAREHE 10 UK11.
NA ISAACK MBWAGA
Wadau wa Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa,wamekumbushwa kutumia fursa zilizopo ili kuinua kipato na kupunguza umasikini.
POLI LA LOLIONDO HATARINI KUHARIBIWA.GAZETI LA HABARILEO,JUMATATU 11,2016 UK 8.
NA JOHN MHALA,LOLIONDO
Shughuli zakibinadamu zinazodaiwa kufanywa katika poli tengefu la Lolindo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha huenda zikaua pori hilo na kumaliza uoto wa asili wa misitu katika siku chache zijazo.
TANGA KUJENGA VIWANDA VYA SAMAKI,GAZETI LA UHURU JUMATATU,JANUARI 11,2016 UK 2
NA SOPHIA WAKATI,TANGA.
Sekta ya Uvuvi mkoani hapa huenda ikazidi kuimarika baada ya uongozi wa serikali mkoani tanga kujiwekea mikakati kabambe ya ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki.
MAMA LISHE KUMLALAMIKIA DC AGIZO LA KUBORESHA MAENEO YA BIASHARA.GAZETI LA NIPASHE JUMALI TAREHE 10 UK 8,uk 28 HABARI PICHA.
NA DEGE MASOLI TANGA.
Umoja wa mama lishe wa soko la samaki la DeepSea la Jiji la Tanga wamepanga kwenda kwa Mkuu wa Wilaya kulalamikia uongozi wa Halmashauri ya jiji hilo kuhusu agizo lake la kuwataka kufanya biashara katika majengo ya kisasa wakati wao hawana uwezo wa kuyajenga.
DAR TO START BREEDING NEW FISH SPECIES,SUNDAY NEWS,JANUARY 10,2016
BY MASEMBE TAMBWE
Tanzania will soon start breeding the recently discovered mtera Tilapia that can exist in both salty and fro aquaculture breeding.
WAFUGAJI VIPEPEO WAOMBA MSAADA, TANZANIA DAIMA TAREHE 29 DESEMBA 2015, MUHEZA NA HADIJA BAGASHA.
TANGA KUJENGA VIWANDA VYA SAMAKI,GAZETI LA UHURU JUMATATU,JANUARI 11,2016 UK 2
NA SOPHIA WAKATI,TANGA.
Sekta ya Uvuvi mkoani hapa huenda ikazidi kuimarika baada ya uongozi wa serikali mkoani tanga kujiwekea mikakati kabambe ya ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki.
MAMA LISHE KUMLALAMIKIA DC AGIZO LA KUBORESHA MAENEO YA BIASHARA.GAZETI LA NIPASHE JUMALI TAREHE 10 UK 8,uk 28 HABARI PICHA.
NA DEGE MASOLI TANGA.
Umoja wa mama lishe wa soko la samaki la DeepSea la Jiji la Tanga wamepanga kwenda kwa Mkuu wa Wilaya kulalamikia uongozi wa Halmashauri ya jiji hilo kuhusu agizo lake la kuwataka kufanya biashara katika majengo ya kisasa wakati wao hawana uwezo wa kuyajenga.
DAR TO START BREEDING NEW FISH SPECIES,SUNDAY NEWS,JANUARY 10,2016
BY MASEMBE TAMBWE
Tanzania will soon start breeding the recently discovered mtera Tilapia that can exist in both salty and fro aquaculture breeding.
WAFUGAJI VIPEPEO WAOMBA MSAADA, TANZANIA DAIMA TAREHE 29 DESEMBA 2015, MUHEZA NA HADIJA BAGASHA.
WAFUGAJI zaidi ya 200 wa vipepeo wanakabiliwa na uhabawa vifaa vya kufugia, hatua inayochangia kazi hiyo kuwa ngumu.
WAZIRI OLE NASHA ATOA SIKU 28 AKABIDHIWE RIPOTI YA VIWANJA,MTANZANIA TAREHE 26 DESEMBA 2015. NA FRAJA MASINDE, DAR ES SALAAM.
NAIBU Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Olenash, amewaagiza wataalamu wa Wizara hiyo kuandaa ripoti ndani ya siku 28 itakayotoa majibu juu ya nani anayehusikana utoaji wa hati za viwanja takriban 1000 vilivotolewa kinyemela kwenye eneo la Mnada wa Serikali ulioko Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
WAFUGAJI 700 WAITAHADHARISHA SERIKALI KUTIMULIWA DAKAWA NIPASHE TAREHE 20 NOV 2015, MOROGORONA ASHTON BALAIGWA.
Wafugaji zaidi ya 700 katika kijiji cha Dakawa Tarafa ya Dhuthumi mkoa ni Morogoro, wameukuzwa na kuktakiwa kuondoka ndani ya kipindii cha mwezi mmoja kuanzia sasa na uongozi wa serikali ya kijiji hicho kwa madai ya kuvamiwa eneo hilo.
WAFUGAJI 700 WAITAHADHARISHA SERIKALI KUTIMULIWA DAKAWA NIPASHE TAREHE 20 NOV 2015, MOROGORONA ASHTON BALAIGWA.
Wafugaji zaidi ya 700 katika kijiji cha Dakawa Tarafa ya Dhuthumi mkoa ni Morogoro, wameukuzwa na kuktakiwa kuondoka ndani ya kipindii cha mwezi mmoja kuanzia sasa na uongozi wa serikali ya kijiji hicho kwa madai ya kuvamiwa eneo hilo.
NARCO INATEKETEA KWA UFISADI WA WATU WACHACHE. mwananchi tarehe 6/11/2015 Na. Mhariri
Sisi wafanyakazi wa kampuni ya Ranchi za taifa (NARCO) tunaandika barua hii kwa masikitiko makubwa baada ya kubaini ranchi zinanufaisha watu wachache wanaokumbatiana ufisadi.
DAR IMPLEMENTS RIFT VALLEY FEVER PLAN, DAILY NEWS OCTOBER 5,2015 UK 24. by Iddy Mwema
Government has started to implement the 2012 National Rift Valley Emergency preparedness and response plan (NRVF - EPRP).
KUKAMATWA KWA BIDHAA ZITOKANAZO NA MIFUGO ENEO LA TABATA BIMA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA CHANNEL TEN SAA TANO KAMILI USIKU TAHERE 06/10/2015. Na Hamisi Suleiman na Dina Chahali.
Taarifa ya Habari ya saa 5:00 kamili usiku Ilionyesha
kukamatwa kwa bidhaa zitokanazo na Mifugo katika eneo la Tabata Bima. Bidhaa
hizo zikitiliwa mashaka juu ya uhalali wake wa kusafirishwa nje ya nchi ambazo
ni pembe za ng'ombe, kwato na viungo vya uzazi vya madume ya ng'ombe, ambapo
utaratibu wake wa ukaushaji wa viungo hivyo vya madume vimekutwa kwenye hali
mbaya ya uchafu na uozo.
JAMII YA WAFUGAJI YAIANGUKIA SERIKALI,GAZETI LA MWANANCHI TAREHE 05/10/2015,UK 12.Na Filbert Rweyemamu
SIMANJIRO.Viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji wa kimasai wameiomba serikali iwashirikishe katika mipango mbalimbali ya maendeleo na kuhamasisha amani.
CATTLE PRICES UP AS SUPPLY DECLINES,DAILY NEWS PAG 19,DATED 05/10/2015
Moving cattle into distance places to look for pasture and water is one of the factors that contributed to the decline of supply during September.
MUHEZA WAFUNGUA MNADA WA KISASA,GAZETI LA MWANANCHI UK 35,TAREHE 05/10/2015
MUHEZA.Mnada mpya wa ng'ombe na bidhaa zinazohusiana na mifugo wa Mkanyageni Umezinduliwa rasmi huku wafanya biashara wakitakiwa kuutumia kwa manufaa yao na ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
POLI LA BUGIRI NI MUHIMU KULIKO KURA ZA WAFUGAJI, TAREHE 26/08/2015 MWANANCHI UK 10 NA PHINIAS BASHAYA
Poli la Burigi ni muhimu kuliko kura za wafugaji “ Tunawaangalia wafugaji kwa sababu ya
uchaguzi, tunasahau Athari ya baadae itakayogharimu vizazi vyetu”.
RC: MARUFUK KUKAMATA NG'OMBE, TAREHE 26/08/2015 MWANANCHI UK 33 NA SHAABAN NDYAMUKAMA
RC: Marufuku
kukamata N’gombe hifadhini
-Baadhi ya
maofisa wanyamapori wanadaiwa kukamata mifugo na kuwatoza faini wamiliki.
ILLEGAL FISHING IN WEST OF L.VICTORIA THREATENS OVER 11,000/=, TAREHE 26/08/2015 THE GUARDIAN PAGE 7
Illegal fishing in west
of L.Victoria threatens over 11,000/= human lives (By correspondent
Beatrice Philemon, Just back from kagera)
CLIMATE CHANGE SHRINKING UGANDA'S LAKES AND FISHING, 26/08/2015 DAILY NEWS PAGE 14
-Climate change shrinking
Uganda’s lakes and fishing
INDIGENOUS Fish species
in Uganda being caught on lake Victoria have shrunk in size due to an increase
in water temperature as a result of climate change
UHARIBIFU WA MAZINGIRA ZIWA VICTORIA WATISHIA SAMAKI, TAREHE 31/08/2015 MTANZANIA UK 21 NA SHEILA KATIKULA.
-Mwanza – Uharibifu wa mazingira ziwa Victoria
watishia samaki
WANANCHI wa kata ya Nyegezi jijini
mwanza wameshauriwa kuwa walinzi na watunzaji wa mazingira ya kando ya ziwa
Victoria kutokana na uharibifu mkubwa
unaofanywa pembezoni mwa ziwa hilo .
UVUVI WA WATANZANIA KULA SAMAKI WASABABISHA TANI 315,000 KUSAFIRISHWA, TAREHE 01/09/2015, MTANZANIA (UK 10) NA ASIFIWE GEORGE.
-Uvuvi wa
Watanzania kula samaki wasababisha tani
315,000 kusafirishwa
Kwa
kipindi cha cha miaka 10 ya wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi imejitaidi
kuboresha sekta ya uvuvi ndani ya miaka
10 na kuhakikisha wanakuza viumbe kwenye maji asili na maji chumvi.
HABARI PICHA, TAREHE 02/09/2015, HABARI LEO UK 16 - 17
Vijana kutoka kijiji cha mfano
kilichotokana na sera ya maendeleo ya vijana cha green city pathfinder wilayani
sikonge mkoani tabora wakihudumia mradi wao wa kuku.
MBINU ZA UFUGAJI NA KUTIBU KWARE KWA DAWA ZA ASILI.HABARILEO,ALHAMISI 23JULAI,2015.UK 19.MAKALA
Kware ni ndege ambao kwa sasa wanafugwa majumbani na wanataga mayai kwa wingi kuliko kuku.Ndege hao ni wadogo na wanauzito kati ya gramu 280 hadi 300.Kware wanarangi ya kahawia,nyeusi na wengine wanarangi nyeupe yenye miraba na madoa ya rangi ya ugoro au kijivu.Kwa habari zaidi soma gazeti lililo tajwa hapo juu.
UTENDAJI KAZI WIZARA YA MIFUGO WAMEMKERA KIKWETE. GAZETI LA RAIA TANZANIA TAREHE 21 JULAI 2015 UK 3. NA CHRISTINA MWAGALA DAR
Rais Jakaya Kikwete ameonyesha kukerwa na Utendaji mbovu wa Watendaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, baada ya kushindwa kukamilisha ujenzi wa maabara ya uhawilishaji wa viini tete kwa ajili ya uzalishaji wa Ng'ombe.
Taarifa inayofanana na hii ipo katika magazeti yafuatayo:
JAMBO LEO UK. 5 LENYE KICHWA CHA HABARI "JK AWAKOSOA WATENDAJI WIZARA YA MIFUGO" NA EMERESIANA ATHANAS.MTANZANIA UK. 2 LENYE KICHWA CHA HABARI "JK AWA MBOGO KWA WATENDAJI WIZARA YA MIFUGO" NA GRACE SHITUNDU & ASIFIWE GEORGE DAR.
THE
GUARDIAN (TAKING A NEW LOOK AT THE NEWS) 25/08/2015
ESTABLISHED IN 1995 EDITORIAL
“This
can be Salvation for Livestock Keepers”
Tanzania is reputed for being among African countries
that have many cattle, and yet it is not using this important wealth to its
full.
For, traditionally, cattle keepers in Tanzania have only
regarded the animals as a sign of wealth and respect in communities. As such
the many herds of cattle one has the more the respect he/she gets from the
society.
Yet these animals could be put to better use than that.
For instance, the milk could be processed into pasteurized milk, butter, cheese
and cooking oil.
The hides could also be good raw materials for shoe and
garment factories; Not that the country had no such factories; it had many of
them, but they had closed shop at the time the free market policy was
introduced in early 1990s.
Unfortunately, the textile factories were turned into
other use, and the rest of the story is too well known to need repetition.
Nevertheless, the country still has a chance to put into use the wealth of
Livestock it still has.
In this connection we commend the Tanzania Domestic
Biogas Programme (TDBP) which has introducing a programme that would benefit
over 30,000 households of cattle keepers in Arusha by 2018. It is expected to
improve their Livelihood and reinforce environment conservation.
Since time immemorial, Livestock keepers have been
leading a nomadic life, shifting from place to place in search of pasture and
water for their Livestock. In Such circumstances, therefore they cannot build
permanent houses or put up tangible investments that would make their lives
better.
For fuel most of them use firewood which they collect
from nearby forests or charcoal made from wanton cutting of trees.
However, they could very well turn to their cattle and
use dung to manufacture biogas. And this is what the TDBP is all about.
The programme manager of the centre for Agricultural
Mechanisation and Rural Technology (CAMARTEC), Lehada Shila, introduced the
project in Arusha recently.
Among those he introduced to were the financial
institutions, village community banks as well saving and credit societies
(SACCOS).
Clearly, these were the appropriate institutions that
could take up this programme to members of the public, in this case Livestock
keepers.
We commend the programme for being vital not only to
cattle keepers in Arusha, but in other parts of the country as well. It should
be extended to all Livestock keepers in Tanzania.
What is required is for officials of the TDBP to
popularize it among them, and leave the rest to the financial institution.
They could use the mass media and other means to get the
programme known among members of the public. But having done so there is also
the aspect of capital as start – ups for the projects.
This is where such bodies as financial institution,
VICOBA and Saccos come in handy. They should be readily available to people who
would like to give the project a try.
All said, however; we believe that TDBP could be the
salvation for many Livestock keepers.
WAFUGAJI WALALAMIKIA VITENDO VYA KINYAMA VINAVYOFANYWA NA ASKARI WA WANYAMA PORI, WILAYA YA BUSIGA MKOA WA SIMIYU. ITV SAA 2 USIKU TAREHE 10/05/2015
Wafugaji walalamika kuwa Askari wa wanyama pori kwa kuwatoza faini kubwa Wafugaji na pia wanachkua hatua ya kuwa piga risasi.
WAFUGAJI KUJENGEWA UWEZO KWENYE UFUGAJI. ARUSHA - LONGIDO, KIPINDI CHA NIPASHE ASUBUHI RADIO ONE SAA 12:30 TAREHE 11/05/2015
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Kaika Kelele alisema serikali itaendelea kuhudumia wafugaji wanaoishi katika hifadhi ya Ngorogoro. Wafugaji hao wameshauriwa kutokujenga makazi ya kudumu katika hifadhi hiyo
NDAMA AZALIWA NA VICHWA VIWILI GAZETI LA JAMBO LEO JUMANNE TAREHE05/05/2015 UK. 11 NA FLORIDA MAREKANINi jambo la ajabu lakini kweli. Huko Marekani katika jimbo la Florida kumetokea tukio la Ajabu ambalo wataalam wa Wanyama wamesema kuwa ni nadra kutokea.
WATANZANIA 500 KUSHIRIKI MAONESHO MAKUBWA YA ITALIA.HABARILEO JUMATANO APRILI 29/04/2015.NA IKUNDA ERICK.
Watanzania 500 wanatarajia kushiriki kwenye maonesho makubwa ya dunia ya Expo Milan 2015,ya bidha,Teknolojia na maswala ya chakula yanayofanyika nchini Italia kuanzia mei mosi mwaka huu.UK 4
MVOMERO WATAKA MGOGORO BONDE LA MGONGOLA UTATULIWE.HABARI LEO,JUMANNE APRILI 28/04/2015.NA JOHN NDITI,MOROGORO.
Wananchi wa Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro wameomba Serikali kupitia wizara ya Ardhi,Maendeleo ya makazi na nyumba kumaliza mgogoro wa miaka mingi wa Ardhi katika bonde la mpunga la Mongola.
Wameomba umalizwe haraka na suluhu la kuduma lipatikane ili kukomesha matukio ya mauaji ya wakulima na wafugaji wa vijiji mbalimbali vya kata ya hembeti wilayani humo. uk 24
CATTLE SUPPLY AT DAR MARKET DOWN, PRICE UP DAILY NEWS 28/04/2015/ By Daily News.
SUPPLY of cattle at the Pugu auction market Registered down-ward trend by 7.6 percent to a weekely avearage of 2,725 from 2,950 of the week earlier.
HATUNA MGOGORO NA WAFUGAJI-NYALANDU,RAIA TANZANIA 27/04/2015.NA SHARIFA MARIDA,DAR.
Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu,amesema serikali haina migogoro na wafugaji kama ambavyo watu wengine wanadai,hivyo inaangalia namna ya kuitatua kwa kutafuta maeneo ya kufugia mifugo yao.
WAFUNZWA KUTENGENEZA BIDHAA ZA NGOZI,RAIA TANZANIA 27/04/2015.NA GIFT THADEY,BABATI.
Wajasiriamali mkoani Manyara,wamatakiwa kutumia ipasavyo rasilimali inayotokana na ngozi ili kujiinua kiuchumi kwa kusindika na kutengeneza bidha kama vile mabegi,viti na mikanda
KIBOKO AUA MVUVI AKIVUA SAMAKI ZIWANI,JAMBOLEO JUMATATU APRILI 27,2015.NA AHMED MAKONGO,BUNDA.
Mvuvi mashauri mabuba (61) amekufa baada ya kushambuliwa na mnyama aina ya Kiboko wakati akivua samaki ziwa Victoria eneo la Wilaya ya Bunda Mkoni Mara.
AFA ZIWA VICTORIA KWA KUSHAMBULIWA NA KIBOKO,HABARILEO JUMATATU APRIL 27/04/2015.NA AHMED MAKONGO,BUNDA.
Mkazi wa kijiji cha buzibwe kata ya butimba wilayani Bunda amekufa baada ya kushambuliwa na kiboko wakati akivua samaki katika ziwa Victoria.Tukio hilo ni la juzi saa 11:00 jioni katika eneo la kitongoji cha majengo,kijijijini humo.
'ASILIMIA 70 YA MAGONJWA HUTOKA KWA WANYAMA'HABARILEO JUMATATU APRIL 27/04/2015.NA LUCY LYATUU.
Serikali imesema zaidi ya asilimia 70 ya magonjwa yanayosumbua binadamu yanatoka kwa wanyama kwenda kwa bidamu,jambo ambalo wafugaji wametakiwa kutoa taarifa kwa wataalamu kutokomeza tatizo hilo.
UKOSEFU WA MALISHO,CHANZO CHA MATESO,MAUAJI KWA WAFUGAJI,MWANANCHI 24/04/2015 NA ANTHONY MAYUNGA,MWANANCHI.
Matukio ya wafugaji kujeruhiwa hata kuuawa kwa kupigwa risasi na mifugo kupotea na kuuawa,yamekuwa si mageni hasa maeneo yaliyo kandokando ya hifadhi za taifa na mapori ya akiba.
Kukithiri kwa matukio hayo yanayojatwa kufanywa na askari wa wanyamapori kunaelezwa kwenda na kasi ndogo ya kuwashughulikia watuhumiwa wa matukio,ikilinganishwa na yanavyoshulikiwa matukio ya wanyamapori kuuawa.
APEWA KUKU SITA, SASA ANAMILIKI KAMPUNI, NIPASHE 24/04/2015 NA ELISANTE JOHN,ARUSHA
Kwa baadhi ya vijana ufugaji wa kuku ni shughuli ambayo hawaichukulii kwa uzito unaostahili.Wanaiona kama ni ya kawaida kabisa inayostahili kufanywa na watu waliokwama kimaisha.
NG'OMBE,MBUZI WAIMARISHA UCHUMI WA WAFUGAJI WADOGOWADOGO,NIPASHE TAREHE 24/00/2015. Na Hussein Ahmed
Mfugaji katika wilaya ya Marsabit katika eneo kame kaskazini mwa Kenya alisafiri kwenda nchi jirani ya Ethiopia kutafuta maji na malisho kwa ajili ya ng'ombe wake kisha kuwapoteza wote alikata tamaa kuhusu maisha yake.
WANAFUNZI WA CHUO CHA MIFUGO WAANDAMANA, TANZANIA DAIMA 23/04/2015, NA RISTUTA FISOO,BABATI
Wanafunzi 150 wa chuo cha Kilimo na Mifugo cha Upendo Ebeneza,kilichopo Nyunguu Wilaya Babati, Manyara wameandamana hadi Mkuu wa Wilaya hiyo, Ciprina Meela wakipinga kitendo kilichofanywa na chuo hicho cha kuwatunuku cheti cha awali badala ya cheti.
UFUGAJI WA KUKU WA KISASA, HABARI LEO 23/04/2015.
Katika Ufugaji wa kuku wa kisasa kuna mabo mengi ambayo yanapotekelezwa kwa usahihi hufanya ufugaji uwe wa mafanikio na wenye tija. Mambo hayo yasipotekelezwa nfugaji anaweza kupata hasara kubwa sana. Kuku wake wanaweza kufa kwa wingi au ufugaji utakuwa wa gharama kubwa kutokana na ununuzi wa dawa. Gharama nyingi zinaweza kuzuilika iwapo atazingatia kanuni za ufugaji bora.
MVUA YABOMOA MABWAWA YA MIFUGO, MONDULI ARUSHA . TAREHE 21/04/2015 HABARI ITV SAA 2 USIKU
Mvua kubwa imenyesha huko monduli ARUSHA, mabwawa ya mifugo yameharibiwa na mvua, wafugaji wamekosa sehemu ya kunyweshea mifugo yao. Serikali itilie mkazo ili kurudisha hayo mabwawa katika hali ya kawaida na miundombinu iboreshewe.
MALORI 15 YANASWA YAKIVUSHA NG'OMBE 1,000 KWENDA KENYA. NIPASHE JUMATATU APRILI 20, 2015. Na Samson Chacha TARIME.
Jeshi
la Polisi Maalum ya Tarime/Rorya mkoa wa Mara, limekamata malori 15
yenye matela yakisafirisha zaid ya Ng'ombe 1,000 aina ya ankole kutoka
Tanzania kupeleka Kenya huku baadhi ya wafanyabiashara wakiwa hawana
vibali.
Ng'ombe hao walikuwa wakitoka Baridi, Shinyanga, Sumbawanga, Geita, na Tabora.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, ameagiza mifugo yote ambayo haikulipwa ushuru ilipiwe katika Kituo cha Forodha cha mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Sirari huku akiwaonya wanaopitisha mifugo na bidhaa katika njia za panya na kuonesha serikali mapato, watachukuliwa hatua kali.
Aidha, Luoga amewahimiza wafanyabiashara hao wa Mifugo kufuata sheria na kuwa waaminifu katika kutoa takwimu za mifugo yao waliyolipia ushuru na kuhakikisha "wafanyabiashara waaminifu katika biashara zao, hufuata sheria za nchi na taratibu zilizowekwa ili kufanikisha biashara zao, lakini wasio waaminifu hujaribu kukwepa kodi mara zote.
Baadhi yenu hapa mnaonyesha vibali vya ng'ombe 200 huku mkiwa na ng'ombe 280, wengine wadai vibali vipo nyuma vinakuja, lakini mifugo ipo vijiji vya mipakani kutaka kupitia njia za panya. Na mnapokamatwa na kulipa ushuru halali, mnadai nanyanyaswa msifanye biashara ya kizamani ya mbali fuateni taratibu zilizowekwa na serikali hamtapata usumbuf wowote," alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara. wameitikia wito na kulipia ushuru na hvyo kuendelea na safari lakii mengine yaliendelea kusubiri vibali na leseni za kusafirisha mifugo hiyo nje ya nchi.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime/Rorya, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kukamatwa kwa malori hayo.
Aidha, Luoga amewahimiza wafanyabiashara hao wa Mifugo kufuata sheria na kuwa waaminifu katika kutoa takwimu za mifugo yao waliyolipia ushuru na kuhakikisha "wafanyabiashara waaminifu katika biashara zao, hufuata sheria za nchi na taratibu zilizowekwa ili kufanikisha biashara zao, lakini wasio waaminifu hujaribu kukwepa kodi mara zote.
Baadhi yenu hapa mnaonyesha vibali vya ng'ombe 200 huku mkiwa na ng'ombe 280, wengine wadai vibali vipo nyuma vinakuja, lakini mifugo ipo vijiji vya mipakani kutaka kupitia njia za panya. Na mnapokamatwa na kulipa ushuru halali, mnadai nanyanyaswa msifanye biashara ya kizamani ya mbali fuateni taratibu zilizowekwa na serikali hamtapata usumbuf wowote," alisema.
Hata hivyo, baadhi ya wafanyabiashara. wameitikia wito na kulipia ushuru na hvyo kuendelea na safari lakii mengine yaliendelea kusubiri vibali na leseni za kusafirisha mifugo hiyo nje ya nchi.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime/Rorya, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kukamatwa kwa malori hayo.
WATAKA BAJETI YA SEKTA YA MIFUGO IONGEZWE, MWANANCHI, JUMATATU APRILI 20, 2015. Na Happy Lazaro ARUSHA.
Serikali imeshauriwa kuongeza bajeti na kuweka kipaumbele katika sekta ya Mifugo itakayosaidia kuondoa changamotozinazowakabili wafugaji.
Hayo yalisemwa juzi na mratibu wa shirika la Kinapa Development Programme Samwel Ole Kao.
Shirika hilo linatekeleza mradi wa utetezi wa maendeleo katika sekta ya ufugaji wa asili. Akizungumza katika uzinduzi wa ufugaji wa asili kwa maendeleo ya uchumi (PIE), Ole Kao alisema unalenga kufanya ushawishi na utetezi ili kukuza na kuendeleza Sekta ya Ufugaji wa asili nchini.
Alisema serikali hutoa vipaumbele katika maswalana sekta mbalimbali kama Madini, Kilimo, Afya, Elimu na Miundo mbinu ya barabara na kuisahau sekta ya Mifugo yenye mchango mkubwa katika kuliingizia taifa mapato.
Ofisa miradi wa shirika hilo, Dinno Selastine akizungumzia mradi huo, alisema ulianza Februari, mwaka huu na unatekelezwa nchi nzima alisema walengwa ni wafugaji wa asili walio katika mikoa yenye ufugaji wa asili ambayo ni Rukwa, Arusha, Manyara, Mara Shinyanga, Morogoro, Tanga na Pwani.
Ofisa Mifugo na Uvuvi Wa wilaya ya Mvomero, Daniel Pangani alisema Wilaya inakabiliwa na upungufu wa Maeneo ya Malisho na wataalam wa Mifugo.
Wizara
ya mifugo yabanwa Nanenane. Tanzania Daima, Alhamisi Julai 24, 2014.
Na Happiness Mtweve,
Dodoma.
Wizara ya Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi imetakiwa kuhakikisha inawapa washindi wote zawadi walizoahidi
katika kilele cha maonyesho ya nanenane 2013 kabla ya kuanza maonesho ya Kanda
ya Kati Agosti mosi mwaka huu ili kuondoa ubabaishaji.
Agizo hilo limetolewa
mjini hapa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi, wakati wa kikao
cha pili cha Maandalizi ya maonyesho na mashindano maalumu ya mifugo kitaifa na
maonyesho ya Nanenane Kanda ya Kati.
Alisema kitakuwa
kitendo cha aibu kama wataanza mashindano mengine bila kuwakabidhi zawadi zao
washindi wa mwaka jana.
Kwa upande wake wizara
hiyo ilisema juhudi zinaendelea ili kutekeleza ahadi hiyo kabla ya kuanza
maonyesho ya mwaka huu, licha ya kuwa Dr.Nchimbi aliyakataa majibu hayo na
kutaka waeleze kwa uwazi zaidi.
Baada ya Dr. Nchimbi
kupingana na majibu hayo, walieleza kuwa wanachosubiri ni fedha za matumizi ya
kawaida ya ofisi (OC ), ya Julai mwaka huu ambazo bado hazijatoka na mara tu
zitakapotoka , watawapa washindi wote zawadi zao.
Katika hatua nyingine,
Tanzania Daima ilifanya mahojiano na washindi kwa sharti la kutokutajwa majina
yao kuhusu jambo hilo, ambalo wametishia kuandamana kuhakikisha wanapewa zawadi zao kabla ya washindi wa
mwaka huu.
Viongozi watembelea jengo la Tafico
kinyemela – Tanzania Daima, Jumatatu, Juni 16,2014
Na Shehe Semtawa, Dar es Salaam.
Baadhi ya
viongozi wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wamekuwa wakitembelea kwa
siri jingo la lililokuwa Shirika la Uvuvi nchini (Tafico), kujionea athari za
maji ya bahari jinsi yanavyoweza kuliporomosha jingo hilo wakati wowote.
Viongozi hao walifanya hivyo baada ya gazeti
hili kuandika habari kuwa Wizara hiyo imeingia katika kashfa nzito ya kudaiwa
kutafuna zaidi ya shilingi milioni 200 za kujenga ukuta wa kuzuia kuanguka kwa
jingo hilo kutokana na mmomonyoko unaosababishwa na maji ya bahari.
Kwa mujibu
wa chanzo chetu, viongozi hao wamekuwa wakifika katika eneo hilo kimya kimya
huku wakikwepa kuzun gumza na wafanyakazi walioko kwenye jingo hilo.
Aidha
vuiongozi hao wamekuwa kimya kulizungumzia sakata hilo na hata waandishi
wanapokwenda ofisini kwao wanawakwepa licha ya wakati mwingine kuwataka wafanye
hivyo
Mmoja wa
wafanyakazi kwenye kitengo cha ugavi ambaye hakutaka jina lake liandikwe
gazetini aliliambia Tanzania Daima kuwa viongozi hawako tayari kuzungmzia suala
hilo kwa kuwa mchakato mzima wa matumizi ya fedha hizo hauoneshi kumbukumbu
sehemu yoyote.
Hivi
karibuni Tanzania Daima limeshuhudia jingo hilo ambalo liko kwenye ufukwe wa
Bahari ya Hindi eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, ambalo linaweza kuanguka
wakati wowote endapo litaachwa bila kujengewa ukuta haraka.
TFDA: Kati ya machinjio 900
yaliyosajiliwa ni 20 - HabariLeo, Jumanne June 3, 2014
Na Gloria Tesha, Dar es Salaam
Mamlaka ya
Chakula na Dawa TFDA imesema kati ya machinjio zaidi ya 900 yaliyopo nchini, ni
20 pekee yaliyosajiliwa jambo linalochangia huduma mbovu isiyozingatia viwango
vinavyotakiwa.
Imesema
ilitoa agizo la maboresho zaidi ya miaka mitatu iliyopita na sasa inaandaa
mikakati kuleta mapinduzi katika sekta ya nyama hasa machinjio ili kuboresha
huduma, afya ya jamii na kuhakikisha sheria na miongozo inazingatiwa.
Polisi walalamikiwa kulinda wezi wa
mifugo ‑ Nipashe, Jumatatu juni 02, 2014.
Na Samson Fridolin, Pwani
Baadhi ya
wananchi wilayani Bagamoyo Pwani, wamelilalamikia jeshi la polisi kwa
kutowasaidia kutokomeza mtandao wa kihalifu wa wezi wa mifugo.
Aidha
wamewatuhumu baadhi ya polisi kwa kushirikiana na mtandao huo wa kihalifu na
kuwakwamisha kurejeshewa ng’ombe zaidi ya 200 walioibwa katika mazizi yao kwa
nyakati tofauti kwa miezi mitatu sasa.
Wawekezaji ufukweni waombwa wasivunje
sheria - Habari Leo, Jumatatu Juni 02,
2014
Na Anna Makange, Tanga.
Wawekezaji na wadau wa shughuli za utalii karibu na maeneo ya
fukwe za badari wametakiwa kuhakikisha kuwa shughuli hizo haziathiri maisha ya
viumbe wanaotumia fukwe hizo.
Wameonywa kuacha vitendo vya uvunjifu wa sheria ya Uhifadhi
wa Mzingira ya Bahari inayoagiza kuacha kuingilia fukwe kwa umbali wa meta 60
kutoka usawa wa bahariili kuruhusus viumbe bahari akiwemo tasa kuendelea
kutaga.
Rai hiyo
imetolewa na Afisa mradi wa Sea Sense (Bahari Hai) Boniventure Mchomvu katika
mahojiano hivi karibuni na gazeti hili wakati wa mafunzo maalumu ya kuwajemngea
uwezo viongozi na watoa maamuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Tushirikiane kutokomeza uvuvi haramu
- Habari Leo,
Ijumaa Mei 30, 2014
Mhariri
Katika
gazeti hili kuna habari kutoka mkoani Mwanza, kuhusu uvuvi haramu katika ziwa
Victoria.
Habari hiyo
imeeleza kuwa uvuvi haramu umekithiri katika ziwa hilo kubwa kuliko yote
nchini. Matumizi ya dhana haramu za uvuvi, yameongezeka katika ziwa hilo katika
maeneo mengi. Wavuvi wamekuwa wakivuna samaki kwa wingi.
Huko nyuma,
ziwa huilo lilikuwa likichangia mapato makubwa katika pato la taifa. Lakini
takwimu za hivi sasa zinaonesha kuwa mqapato hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Utafiti
uliofanyika ziwa katika ziwa hilo umeonesha kuwa uvunaji wa mazao ya samaki
ulikua kilo 289 kwa mwaka 1989, kwa sasa umepungua hadi kilo 1989.
Uvuvi
haramu umesababisha kushuka kwa pato la taifa linalotokana na mazao mbalimbali
ya samaki. Ni wazi kutokana na hali ya
ziwa ilivyopo sasa.
Elimu madhara ya uvuvi haramu itaokoa
rasilimali za bahari - Mtanzania Ijumaa Mei 30, 2014
Na Amina Omari, Tanga
Elimu duni
juu ya utunzaji wa rasilimali zitokanazo na bahari umesababisha kukithiri kwa
uvuvi haramu kwenye bahari ya Hindi unaofanywa na wakazi wa kijiji cha Mwarongo
kilichopo kwenye kata ya Tangoni mkoani Tanga.
Kimsingi
huwezi kutofautisha umasikini na suala zima la uharibifu wa mazingira kwani
hali hizo husababishwa na ukosefu wa elimu sahihi ya utunzaji wa rasilimali za
nchi.
Quality milk starts from the farm - The Guardian Friday, May 30 2014
By Herry Ngoitiama.
Dairy
farming has a great potential to improve national and household economy. It
creates a wide range of economies as well as employment opportunities. The milk
provides diary farmers with regular income through out the year.
The diary
farm is the first stage before the production of milk and diary products. It
the farm that milk is produced and stored before being transferred to a
processing facility where it’s made into final products to the consumers. It is
important that the farmer does all the right things at the farm level to
produce quality raw milk.
Watanzania wahamasishwa kunywa maziwa
- Nipashe, ijumaa mei 30, 2014.
Na George Marato , Musoma.
Bodi ya
maziwa nchini kushirikiana na Sirika la Kimataifa la Heifer International
wameanzisha mpango maalumu wa kuhamasisha unywaji wa maziwa nchini.
Lengo ni
kuwawezesha watanzania wengi zaidi wakiwemo watoto kuwa na mwamko wa unywaji
maziwa ili yatumike kama lishe kuboresha afya zao.
Wavuvi waandamana kupinga uvamizi - Tanzania
Daima Ijumaa, Mei 30, 2014
Na Ashura Jumapili, Muleba
Zaidi ya
wavuvi 30 wa kisiwa cha Mazinga, kata ya Mazinga wilayani Muleba wameandamana
hadi kituo cha polisi cha wilaya kulalamikia kutokuwepo ulinzi katika ziwa
Victoria, hali inayochangia majambazi kuvamia na kuwapora zana za uvuvi zennye
thamani ya mamilioni.
Wakizungumza
na Tanzania Daima juzi katika kituo cha polisi, wavuvi hao walisema wameamua
kuandamana kutokana na kuongezeka kwa uvamizi huohuku jeshi la polisi likikaa
kimya bila kuchukua hatua za ulinzi.
Kiwanda cha ngozi cha Sak chafungwa - Habari Leo, Jumatatu, Mei 26, 2014.
Na Veronika Mheta, Arusha
Manispaa ya
Jiji la Arusha imekifunga kiwanda cha ngozi ch Sak Tanney kinachomilikiwa na
raia wa Pakistankilichopo katika kata ya Unga Limited jijini hapa kwa kosa la
kutiririsha maji machafu yenye kemikali kwenye makazi ya watu.
Kufungwa kwa
kiwanda hicho kumetokana na mmiliki wa kiwanda hicho kukaidi maelekezo yote
ambayo yamekuwa yakitolewa na maofisa wa afya wa kata na jiji juu ya
kutiririsha maji hayo kwenye makazi ya watu.
Kesi dhidi ya wachina uvuvi baharini yapigwa kalenda-Nipashe alhamisi mei 8, 2014.
Na Hellen Mwango, Dar es Salaam
Mahakama
ya hakimu Mkazi Kisutu , imeahirisha kesi inayowakabili raia wawili wa china
Hsu Tai na Zhao Hanquing, ya kufanya shughuli za uvuvi katika bahari ya
Hindi eneo la uchumi la Tanzania bila
kibali hadi Mei 20, mwaka huu baada ya upande wa Jamuhuri kudai kuwa upelelezi
wake bado haujakamilika.
Kesi
hiyo iliahirishwa jana na Hakimu Mkazi
Mkuu Waria lwande Lema. Wakili wa Serikali Ofumad Mtenga, alidai kuwa upelelezi
wa kesi hiyo bado haujakamilika na upande wa Jamuhuri uliomba tarehe ya
kutaja.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
RUZUKU KWA WAVUVI
TAARIFA KWA UMMA
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi imetenga kiasi cha fedha katika mwaka 2013/2014 kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa jamii za wavuvi. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
anawatangazia wananchi kuwa, Serikali itatoa ruzuku kwa vyama vya
ushirika wa wavuvi, vikundi vya wavuvi na Vikundi vya Usimamizi Shirikishi wa
Rasilimali za Uvuvi (BMUs) vilivyosajiliwa kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014.
Vigezo na masharti yatakayotumika kutoa ruzuku ni kama
ifuatavyo:-
1. Ruzuku
itatolewa kwa vyama vya ushirika vya wavuvi, vikundi vya wavuvi na Vikundi vya
Usimamizi Shirikishi wa Raslimali za
Uvuvi vilivyosajiliwa kisheria, na vyenye
kuzingatia jinsia;
2. Kikundi
kiwe kinafanya kazi za uvuvi kufuatana
na Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 na Kanuni za Uvuvi
za mwaka 2009 na kuzingatia miongozo mbalimbali;
3. Kikundi
kiwe na Akaunti ya Benki;
4. Mradi
wowote wa uvuvi utakaowasilishwa na kikundi
lazima ukidhi matakwa ya Sheria ya
Uvuvi
Na. 22 ya mwaka 2003 na Kanuni za Uvuvi za
mwaka 2009 na sheria nyingine
za nchi ikiwemo ya Mazingira ya mwaka 2004;
5. Miradi
itakaofadhiliwa ni pamoja na ununuzi wa boti za uvuvi, injini za kupachika,
nyavu za dagaa na nyavu za samaki wakubwa ndoana (long line);
6. Kikundi
kithibitishe kuwa kina uwezo na kipo tayari kuchangia asilimia arobaini (40%) ya gharama
ya mradi unaoombwa. Serikali itachangia asilimia sitini (60%) ya gharama za zitakazonunuliwa;
7. Maombi
yapitishwe kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa husika kwa ajili ya
kupitia maombi hayo na kuona kama yanakidhi vigezo vilivyowekwa na baada ya
hapo kuwasilishwa Wizarani;
8. Maombi
yaambatane na mchanganuo wa gharama za mradi;
Kwa tangazo hili, vikundi husika vinashauriwa
kujiandaa kwa ajili ya kutumia fursa hii kwa
kushirikiana na Halmashauri zao. Aidha,
Halmashauri zinashauriwa kufuatilia na kuwandaa
walengwa ili hatimaye vipatikane vikundi vyenye
sifa ya kupewa ruzuku.
Tangazo limetolewa na:-
Katibu Mkuu,
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo
na Uvuvi,
Sanduku La Posta 9152,
DAR ES SALAAM.
Wednesday, April 10, 2013
TAARIFA KWA UMMA
Waanzisha vipindi kupinga ukatili kwa mifugo
HABARI LEO, JUMATANO APRILI 10,2013
Na Katuna Masamba
Kutokana na tatizo la ukatili kwa mifugo kuwa kubwa, Taasisi ya ustawi wa jamii ya wanyama nchini (TAWESO) imeamua kuanzisha vipindi maalumu mashuleni ili kupinga ukatili huo.
Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi gazeti hiyo Dk Thomas Kahema,alisema wana imani kupitia mpango huo wa kutoa elimu mashuleni kwa kiasi kikubwa utafanikiwa kupunguza ukatili wa mifugo.
``Unajua watoto wanapenda sana wanyama kuliko hata sisi watu wazima,sasa tutakapowapa hao elimu naamini kabisa watakuwa ni mabalozi wazuri wa kutetea haki za wanyama''alisema Dk Kahema
Alisema tayari wameshaanzisha mpango huo katika shule mbalimbali kwa mkoa wa Dar es salaam na maeneo mengine ikiwemo wilaya ya Mpwapwa, Dodoma.
Ugonjwa watishia mifugo kutoweka Musoma - Mwananchi, Jumanne, Machi 12,2013
Na. Sheilla Sezzy, Mwananchi
Inashangaza kuona wataalamu wa mifugo wakisaini karatasi ya kuidhinisha mkandarasi kulipwa wakati kazi alizofanya haziridhishi - Mayamba Mgeta
Halmashauri ya Musoma vijijini inakabiliwa na tishio la kutoweka kwa mifugo linalotokana na Ugonjwa wa kupe unaosababisha ndama kufa ovyo.
Hayo yalisemwa juzi na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Magina Magesa,alipopkuwa akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara ya mafunzo ukaguzi wa miradi,yaliyotolewa na shirika la maendeleo la Uholanzi (SNV) kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kufufua majosho ambayo yalikuwa hayafanyi kazi.
Alisema Musoma vijijini ina majosho 33, lakini ni 13 tu yanayofanya kazi na mengine 10 ni mabovu .Mwenyekiti huyo alisema majosho mengine tisa hayafanyi kazi kwa sababu mbalimbali.
Kama majosho hayo yangefanya kazi kuogesha mifugo,ugonjwa huo wa kupe ungetokomea na idadi ya mifugo ingeongezeka na kuiwezesha halmashari kupata mapato yanayotokana na mifugo hiyo,alisema Magesa.
Mwenyekiti huyo alisema sababu nyingine ni ya watendaji wa Idara ya Kilimo na Mifugo kushindwa kuwajibika ipasavyo katika kusimamia sheria ndogo ya uogeshaji wa mifugo.
Alisema sheria hiyo inataka wafugaji wanaogoma kuogesha mifugo yao kwa madai mbalimbali yasiyokuwa na msingi,kuadhibiwa.
Kuhusu kukamilisha miradi hiyo ya majosho, Diwani wa kata ya Bikima,Mayamba Mgeta,alisema inashangaza kuona wataalam wa mifugo wakisaini makaratasi na kutoa idhini kwa mkandarasi kulipwa fedha wakati kazi alizofanya ziko chni ya kiwango.
Madudu yaibuka Mifugo na Uvuvi, Uhuru Agosti 13, 2012
Vigogo wahusishwa na uvuvi haramu
Wanamiliki zana za kisasa zikiwemo boti
Watumishi wafichua mtandao wa kutisha
Boti za doria zadaiwa kuhujumiwa
Uvuvi haramu umeendelea kutikisa maeneo mbalimbali nchini, huku baadhi ya watumishi wa ngazi ya juu natika Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakitajwa kuhusika.
Kuhusika kwa vigogo hao, kumeibuliwa na wafanyakazi ambao wameweka hadharani mbinu zote chafu zinazofanywa na viongozi wao.
Kuibuliwa kwa tuhuma hizo kumekuja ikiwa ni siku chache baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. David Mathayo, kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Wanaoingiza nyama Machinjio ya Vingunguti wawajibishwe, Tanzania Daima Alhamisi Mei 10, 2012
Na. Shehe Semtawa
Hivi karibuni Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala liliwashikilia watu wawili akiwamo Ofisa wa Afya wa Machinjio ya mbuzi Vingunguti, Walter Macha, kwa tuhuma za kuingizwa utumbo wa mbuzi kilo 640 na maini kilo 670 katika mzunguko wa biashara huku vikiwa vimeharibika.
Nyama hiyo iliingizwa katika machinjio hayo ikiwa imepakiwa katika gari lenye namba za usajili T728 BUF Toyota Pick Up, ikitokea mkoani Dodoma . Uingizwaji wa nyama hiyo ulizua tafrani katika machinjio hayo baada ya wananchi kubaini kuwa nyama hiyo ilikuwa imeharibika huku ikitoa harufu.
Wananchi hao waliokuwa wamekusanyika baada ya kutangaziwa katika kipaza sauti kilichokuwa cha Ofisa wa Afya wa machinjio hayo kuwa kulikuwa kuna nyama hiyo, aina ya utumbo na maini ikiuzwa kwa bei nafuu ya Shs.11,000 badala ya Shs.12,000.
Wananchi walishangazwa baada ya kugundua kuwa nyama hiyo imeharibika, kitendo ambacho hawakukubaliana nacho ndipo walipoanza kuhoji kulikoni kuuziwa nyama iliyooza.
Vurugu hizo ziliendelea kwa muda, wakipinga kuuziwa nyama hiyo ambapo baadhi ya wananchi walifikisha taarifa kwa Diwani wa Kata ya Vingunguti, Asia Simba, pamoja na Dk. Wa Machijio hayo Juma Nganyanga. Viongozi hao walipofika katika tukio walibaini kuwa nyama hiyo ilikuwa imeharibika na haikufaa kuliwa na binadamu, kwa kuwa ingeweza kuhatarisha afya za walaji.
Kutokana na hali hiyo, wananchi wakishirikiana na viongozi hao walifikia uamuzi wa pamoja kuifukia nyama hiyo katika ulinzi mkali ili isije ikaenda kuuzwa tena kiujanja ujanja. Baada ya hapo waliwachukua wahusika na kufikishwa kituo cha polisi Buguruni. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kisheria hakuna kibali chochote kinachoruhusu kuingiza nyama yoyote katika machinjio hayo, bali sheria inaruhusu kuingizwa mnyama akiwa hai.
Inashangaza daktari wa machinjio hayo kusikika akisema eti watu hao walikuwa na kibali cha kuingiza nyama hiyo, kitendo kinachowashangaza wananchi. Wananchi hao wamekwenda mbali kwa kudai kuwa huo umekuwa utaratibu wa watendaji wa machinjio kuingiza nyama kama hizo huku wakipokea shukrani kwa waingizaji wa nyama.
Wanadai ndani ya wiki moja kumeingizwa nyama ya ng’ombe kama hiyo mara mbili bila maelezo ni kwanini wanakiuka taratibu za machinjio hayo.
Diwani wa kata hiyo anasema haelewi ntindo huo unaofanywa na watendaji hao ambao wamesomea kazi hiyo pamoja na sheria zinazomlinda mlaji. Anaamini kulikuwa na mchezo mchafu kwani haiwezekani Ofisa wa Afya kutoa ushauri kwa mtu anayefanya biashara kinyume cha sheria, amuelekeze bei na kumpa ulinzi kwa maslahi tu binafsi bila kujali maisha ya wananchi.
Anasema suala hilo amewaachia polisi kulifanyia uchunguzi wa kina ili kukomesha vitendo hivyovya hatari kwa maisha ya binadamu. Katika hili, nadhani Ofisa wa Afya aliyekamatwa hayuko peke yake, kwa mfano kama daktari wa machinjio hayo ameonekana akiwa anamtetea mtu huyo aliyeleta nyama hiyo kuwa alikuwa na kibali halali kinachomruhusu kufanya hivyo, kidogo inatia shaka.
Kikubwa hapa wananchi wanapaswa kuambiwa ukweli kibali hicho cha uvunjaji wa sheria kimetolewa na nani na kwa masilahi ya nani ili wananchi waelewe. Haikubaliki kama sheria inapinga kuingizwa kwa nyama, leo inaingizwa huku wahusika wakikaa kimya, hii inamaanisha kuwa watendaji hao hawafai, kwani wanaweza kulisababishia taifa gharama kubwa katika kununua dawa za kutibu maradhi ambayo yamesababishwa na uzembe wao.
Kwa kuwa suala hili limegusa afya za walaji, kuna ulazima kwa kila hatua inayofanyika kuhusu watuhumiwa hao wananchi waambiwe, ikiwa ni pamoja na kutajwa mhusika na kuungnishwa na wale wanaoshikiliwa polisi kwa uchunguzi zaidi.
Serikali: Hatujasitisha uwezeshaji wafugaji – Mwananchi, Jumatatu April 16, 2012
Na. Happy Lazaro, Arusha
Serikali imesema kuwa haijasitisha mradi wa uwezeshaji wa mifugo kwa kaya za wafugaji wilayani Monduli, zilizopoteza mifugo yote kutokana na ukame uliotokea msimu wa 2008/2009 na 2009/2010.Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga alitoa ufafanuzi huo kufuatia na uvumi na taharuki zilizozuka katika baadhi ya vijiji vya Kata za Sepeko na Lepuroko kwa jamii ya wafugaji ambao waliitisha mikutano kuzungumza madai ya kusitishwa kwa mradi huo. Mradi huo uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa Wilaya ya Longido, huku mipango ikiwa mbioni kwa wilaya nyingine za Monduli na Ngorongoro ambapo kwa wilaya zote tatu mradi huo umelenga kutoa kifuta machozi cha ng’ombe 25,000 na mbuzi 14,000 kwa kaya 6, 127.“Serikali haijasitisha mradi wa uwezeshaji kaya za wafugaji wilayani Monduli, huo ni uvumi na ni jambo lisilo la kweli”. Alisema Kasunga. Wakizungumza katika mikutano yao, jamii hiyo ya wafugaji katika wilaya hizo walieleza kuwa wapo tayari kusafiri hadi jijini Dar es Salaam ili kupeleka kilio chao kutokana na kusitishwa kwa zoezi hilo.Baadhi ya wananchi waliopewa zabuni ya kununua ng’ombe kwa ajili ya mradi huo Lendinya Saitoti na Peter Lemomo walisema kuwa tayari wamenunua ng’ombe zaidi ya 2000 kwa mikopo ya benki lakini Serikali haijagawanya ng’ombe hao kwa jamii hiyo ya wafugaji.
Wabunge Kanda ya Ziwa ‘walia’ na Waziri Mathayo – Mwananchi, Jumatatu April 16, 2012
Na. Habel Chidawali, Dodoma
Wabunge wa Kanda ya Ziwa wamemweka ‘kiti moto’ Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk. David Mathayo kuwa Wizara yake haiwasaidii wafugaji na badala yake inawakandamiza.
Wakichangia muswada wa marekebisho wa sheria ya utafiti wa mifugo, wabunge hao walionyesha masikitiko yao kuwa Serikali imekuwa ikishindwa kuwasaidia wafugaji namna bora ya kuboresha mifugo yao, badala yake kila wakati inawataka kupunguza mifugo.
“Serikali inawabughudhi wafugaji na kuwaambia wapunguze mifugo yao, hivi kwa nini wafugaji ndiyo waambiwe kupunguza mifugo na siyo kuongeza? Nchi za wenzetu kama Kongo wanakula nyani kwa kwa kukosa mifugo, hapa tunabahati ya kuwa na ng’ombe” alisema Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo. Cheyo alisema Serikali kila mara inapandikiza chuki kwa wafugaji na kushindwa kuboresha mifugo yao, huku wakati mwingine inafanya kazi ya kuwapora kwa visingizio mbalimbali. Mbunge huyo alisema kuwa na kumekuwa na kasumba ya kuwaona wafugaji kuwa ni watu waliochoka na hawafai, huku wakikandamizwa na kushindwa kuwapatia mahitaji muhimu ikiwamo kuwatengea maeneo ya malisho na majosho.
Kwa upande wake, mbunge wa Viti Maalum, Magdalena Sakaya, alisema kukosekana kwa mipango thabiti ndani ya Serikali kunafanya kuwapo na usumbufu kwa wafugaji ambao wanafukuzwa kama mbwa. Sakaya alituhumu Serikali kuwa kutokana na kufanya mambo yake kwa kukurupuka bila kuwashirikisha wafugaji, ndiyo maana inashindwa kutoa takwimu za mifugo iliyokufa katika kuhamisha wafugaji Bonde la Ihefu na kiwango cha hasara kilichopatikana.
Akijibu tuhuma hizo Dk. Mathayo alisema Serikali imejipanga kuhakikisha inaboresha maisha ya wafugaji na kuwafanya wafuge kisasa zaidi. Waziri Mathayo alisema wafugaji watatengenezewa mazingia mazuri ya kuona mifugo yao kuwa ina thamani kubwa kuliko ilivyo sasa na kwamba, utaratibu mzuri unawekwa ikiwamo maabara nzuri na kisasa itakayosaidia uchunguzi wa magonjwa ya mifugo.
Akemea wafugaji wanaohamia – Mwananchi, Jumatatu Aprili 16, 2012
Na. Sanjito Msafiri, Kibaha
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani Halima Kihemba, amekemea tabia ya vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wafugaji kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa mifugo kutozingatia sheria na utaratibu unaotakiwa. Akizungumza ofisini kwake juzi, Kihemba alisema wafugaji hao wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wa mifugo kuiingiza wilayani humo kwa kisingizio cha biashara, baadaye kubadilisha matumizi na kufanya makazi.
Kihemba alitaja mikoa inayoongoa kuingiza mifugo kwa wingi wilayani humo kinyemela ni Tabora, Kigoma na Mara na kwamba, kitendo hicho ni uvunjaji wa sheria, hivyo Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wafugaji hao. Alisema kitendo cha kudanganya serikali ni koa kwa mujibu wa sheria za nchi, hivyo aliwataka wafugaji hao ambao tayari wameingia ndani ya wilaya hiyo kinyume cha sheria kuondoka mara moja.
“Nawaomba waondoke mara moja maana sisi tumeshawagundua mchezo wao wanaofanya, kama watakaidi agizo hili wasitulaumu mbele ya safari, Sheria zipo wazi kabisa na hapa ninapozungumza na wewe nimeshatuma ujumbe wa viongozi kwenda kufuatilia hilo” alisema Kihemba.
Kihemba alisema, kila mkoa unatakiwa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafugaji na wakulima na maeneo mengine ya shughuli za serikali, kwa lengo la kuondoa migogoro mbalimbali ambayo imekuwa ikijitokeza baina ya wakulima na wafugaji. “Kila kundi la jamii ni muhimu katika nchi mkulima, mfugaji, mfanyabiashara, sasa kila wilaya ina takwimu za idadi ya makundi hayo ndiyo maana uongozi huwa unaketi na kuyapanga maeneo maalumu kwa mgawanyo unaotakiwa” alisema.
Alisema Serikali haitakuwa tayari kuvurugwa na kundi lolote ambalo linataka kufanya hivyo kwa maslahi binafsi bila kufuata sheria, huku akisisitiza kuwa wafugaji hao waangalie uwezekano wa kwenda sehemu nyingine.
Wavuvi Z’bar watahadharisha wawakilishi wao – Mwananchi, Jumatatu April 16, 2012
Kamati Tendaji ya Wavuvi Mkoa wa Kaskazini Unguja (Minca) imewaomba wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wasijaribu kubadilisha sheria ya uvuvi haramu, kwa sababu imeleta maendeleo makubwa Ukanda wa Bahari Zanzibar.
Wavuvi hao waliotoa wito huo eneo la Uroa Unguja na kwamba, tangu kutungwa kwa sheria ya uvuvi haramu imepelekea kupatikana samaki wa kubwa Ukanda wa Bahari upande wa visiwani. “Kama tuna nia ya kuhifadhi samaki na kulinda utumiaji bora wa bahari, basi sheria ambayo ipo iendelee kufanya kazi.” Ali Mkame Mabaha, Katibu wa Kamati hiyo na kuongeza; “Sheria hii haikuja kwa ajili ya mtu, bali ni kwa watu wote kwa sisi wavuvi tunasema iendelee kutumika.” Mabaha alisema wapo watu wachache ambao wanaona wamebanwa kuendesha uvuvi haramu ndiyo wanaochochea kufanyiwa marekebisho sharia hiyo. Mabaha alisema kama ulinzi juu ya uvuvi haramu ukiendelea hata vizazi vijavyo vitafaidika na raslimali hiyo. Mjumbe wa kamati hiyo, Khamis Haji kutoka Tumbatu Gomani, alisema wawakilishi siyo wavuvi hawajui mambo ya bahari. “kila mtu na kazi yake, wawakilishi siyo kwa uvuvi kazi yao ni siasa wafanye kazi yao, uvuvi watuachie wenyewe,”alisema Khamisi.
Upande wa wavuvi wa kisiwa cha Pemba, waliungana na wenzao wa Unguja kwa kuwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutodharau sheria hiyo. Akizungumza kwenye kikao cha dharura cha kamati Tendaji kilichofanyika Wesha Chakechake, Katibu wa Peca, Khamis Shariff Haji, alisema wapo baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi, wamekuwa na tabia ya kubeza na kudharau sheria hiyo. Alisema wawakilishi hao wamekuwa na tabia ya kuhalalisha baadhi ya vipengele ambavyo sheria hiyo vinavyobainisha makosa kuwa vinatakiwa kurekebishwa.
Uvuvi wa kokoro Ziwa Nyasa wapamba moto – Majira , Jumatatu Aprili 16, 2012
Na. Sangalwise Abia, Njombe
Licha ya Serikali kuzuia uvuvi wa samaki kwa kutumia nyavu aina ya kokoro katika maeneo mbalimbali yanayojishughulisha na uvuvi hapa nchini jitihada hizo zimeonekana kuwa zimegonga mwamba huku maeneo mbalimbali yanayojishughulisha na uvuvi, wavuvi wakiendelea kukiuka agizo hilo, Majira limebaini. Hali hiyo imedhihirika wazi katika maeneo ya kandokando ya Ziwa Nyasa kata ya Manda wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe ambapo shughuli za uvuvi wa kutumia makokoro umekuwa ukifanyika mchana kweupe bila wasiwasi wowote.
Baadhi ya wavuvi wakizungumza na Majira mwishoni mwa wiki walidai wanafanya hivyo kwa kuwa samaki wakubwa hupatikana kwa nadra na endapo wakipatikana wakazi wa eneo hilo hushindwa kumudu gharama na hivyo kuwapelekea kukosa kitowewo. Aidha, wavuvi hao walieleza kuwa samaki wanaovuliwa kwa njia ya kokoro ni samaki ambao tayari wamekwisha komaa kwa ni hawakui zaidi ya hapo. “Ndiyo maana tangu enzi za mababu zao walikuwa wakiwavua samaki wa aina ya vitui, utapi na magoliama”. Alidai mmoja wa wavuvi hao ambaye hakuwa tayari kuandikwa jina lake gazetini. Mbali na hayo walisema iwapo serikali itaendelea kuzuia uvuvi huo itawasababishia adha kubwa ya hupatikanaji wa kitoweo na hivyo shughuli za maendeleo zitazorota kutokana na watu kukosa chakula bora.
Hata hivyo Ziwa Nyasa ni miongoni mwa maziwa yaliyobahatika kupewa boti za doria kwa ajili ya kupambana na uvuvi haramu ikiwapo uvuvi wa kokoro lakini bado mafanikio yameonekana kuwa ni hafifu kwani shughuli za uvuvi huo zimeonekana kuendelea kufanyika huku boti hizo zikiwa zimeegeshwa bila kufanya kazi. Pia gazeti hili limebaini kuwa jambo ambalo linashangaza ni hupatikanaji wa nyavu zinazotumika katika uvuvi wa kokoro ambazo zimeonekana kuwa ni nyavu mpya kabisa. Lakini ikumbukwe kuwa jitihada za kupambana na uvuvi haramu ziliimarishwa na Dkt. John Magufuli alipokuwa katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ujenzi kwa kuwa mara kadhaa alionekana akichoma moto nyavu zenye macho madogomadogo katika maeneo mbalimbali hapa nchini hasa ziele zenye urefu wan chi mbili na nusu kushuka chini hivyo mpango huo unapaswa kuendelezwa.
Wakati Dkt. Magufuli alipokuwa katika Wizara hiyo baadhi ya wananchi wilayani hapa walisema, vitendo hivyo vya uvuvi haramu vilipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na udhibiti wa utengenezaji na kuchoma moto aina zote za nyavu hizo.
“Lakini baada ya waziri huyo kuhama wizara hiyo na kupelekwa Wizara ya Ujenzi huku nyuma ndiyo kwanza shughuli za uvuvi haramu zinaonekana kupamba moto katika maeneo kadha wa kadha hapa nchini likiwepo Ziwa Nyasa pamoja na upatikanaji wa nyavu zinazosababisha uvuvi haramu. “Jambo jingine la kujiuliza ni kwamba sera ya kudhibiti shughuli za uvuvi haramu zilikuwa ni Mheshimiwa John Pombe Magufuli binafsi au ni sera za Serikali? Kila waziri anatakiwa kuwajibika kwa kuzifanyia kazi sera na kuzitilia mkazo ili taifa liendelee kupiga hatua kwa kulinda vyema rasilimali zake kwa manufaa ya vizazi vya leo na vijavyo,” alisema Bw. Thomas Emmanuel ambaye ni miongoni mwa wakazi wa Ludewa.
Balozi Kagasheki amvaa Waziri Mathayo – Mwananchi Jumanne April 10, 2012
Na. Phinas Bashaya, Bukoba
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki, ametofautiana na Waziri wa Mifugo na Uvuvu, Dkt. Mathayo David kuhusu utendaji wa Ofsa Mfawidhi Kikosi cha Doria Kanda ya kagera, Rodrick Mahimbali. Kwenye ziara yake hivi karibuni, dk. Mathayo alisifu utendaji wa kujituma wa Mahimbali baada ya kushuhudia malundo ya nyavu haramu na mitumbwi iliyokamatwa baada ya wamiliki kuhusishwa na uvuvi haramu.
Hata hivyo, juzi katika hotuba iliyorushwa na kituo cha redio cha kasibante, Balozi Kagasheki alinukuliwa akimlaumu Dk. Mathayo kuwa hakumtendea haki kwani kabla ya kufanya ziara alimweleza tuhuma zainzomkabili ofisa huyo. Katika hotuba hiyo, Balozi Kagasheki alidai Mahimbali amekuwa akiwanyanyasa wapiga kura kwa kisingizio cha kudhibiti uvuvi haramu na kwamba kusifia utendaji wake hakuwatendea haki wapiga kura wake.
“Nilizungumza na Waziri Mathayo nikamwambia mambo anayofanya Ofisa uvuvi wake hatukubaliani nayo, anavunja mitumbwi ya watu, anaweza kukamata lakini hakuna sheria inayomruhusu kuvunja mitumbwi,” alisema Balozi Kagasheki. Huku akimtaja ofisa huyo kwa jina kwenye hotuba yake kupitia redio anayomiliki, Balozi Kagasheki alisisitiza kutofautiana na Dk. Mathayo kuhusu utendaji wa Mahimbali ingawa alikiri uvuvi haramu unahatarisha rasilimali za Ziwa Victoria. Pia alisema maisha ya wananchi kwenye mialo mbalimbali yanategemea shughuli za uvuvi, huku akitaka suala la kuwatetea wananchi dhidi ya unyanyasaji na udhalilishaji aliodai unafanywa na ofisa huyo lisihusishwe na mambo ya siasa.
Hata hivyo wakati wa ziara yake katika moja ya mikutano na wananchi kwenye mwalo wa Nyamkazi, Waziri Mathayo alimshangaa ofisa huyo kutomfikisha mahakamani diwani wa kata ya Nyanga, Deus Mtakyawa (CCM) aliyetoa shutuma huku akibainika alikuwa anavunja sheria za uvuvi bila kuchukuliwa hatua. Diwani huyo ambaye alikuwa akiwaongoza mamia ya wananchi kutoa shutuma dhidi ya Mahimbali, alikiri mbele ya Waziri Mathayo kujihusisha na masuala ya uvuvi huku ikibainika kuwa alikuwa akifuga vifaranga vya samaki bila kibali.
Wanawake watano wakamatwa samaki waliopigwa marufuku – Mwananchi, Jumanne April 10 2012
Na. Omary Magongo, Same
Katika juhudi za Serikali kudhibiti uvuvi haramu, maofisa maliasili wa halmashauri ya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, wamevamia gulio la kwasakwasa na kuwakamata wafanyabiashara wa samaki waliokuwa wanauza kutoka na kupigwa marufuku. Maofisa hao waliokuwa wanatekeleza zoezi hilo chini ya Ofisa Maliasili wa wilaya hiyo, James Nshare waliwakamata wafanyabiashara wanawake watano waliokuwa wakiuza samaki hao.
Akitoa maelekezo kwa wasaidizi wake wakati wa operesheni hiyo, Nshare alisema wafanyabiashara hao wanapelekwa polisi ili sheria ichukue mkondo wake. Baadhi ya wananchi walioshuhudia kukamatwa kwa wanawake hao, walisema udhibiti wa biashara hiyo unatakiwa ufanyike na kuimarishwa maneo ya uvuvi, badala ya kusubiri samaki wavuliwe na kufikishwa sokoni.
Juma Mbaga na Naetwe Kija, walisema hatua ya samaki waliopigwa marufuku kuvuliwa kusafirishwa hadi kufikishwa sokoni kunaonyesha kuwapo kwa uzembe kwa baadhi ya watendaji wenye dhamana na sekta hiyo. Kija alisema umefika wakati sasa kwa Serikali Halmashauri za wilaya ya Mwanga na Same, kujipanga kuhakikisha uvuvi huo unadhibitiwa katika vyanzo vya uvuvi hasa bwawa la nyumba ya Mungu na mengine.
Uvuvi haramu limekuwa tatizo sugu nchini licha ya serikali kuchukua hatua kadhaa za sheria ikiwemo kuteketeza nyavu zilzoruhusiwa.
Serikali yatelekeza ‘mgodi’ wa samaki – Tanzania Daima, Jumanne April 10, 2012
Na. Japhet Josiah, Bukoba
Uvuvi katika Ziwa Victoria ni raslimali iliyotelekezwa. Wadau wa uvuvi na wenyeji wa maeneo ya kanda ya Ziwa, hasa mkoani Kagera, wanasema ziwa lao ndiyo mgodi wao na samaki ndiyo dhahabu yao. Lakini hawaoni kama serikali inafanya jitihada za kutosha kuwekeza katika uvuvi na kuinua uchumi wa watu waliozungukwa na ziwa na wanaolitegemea kwa maisha yao ya kila siku. Hata watendaji wachache wa serikali waliopo, wameachwa wakikabiliwa na changamoto nyingi, zikiwamo ukosefu wa raslimali fedha na watu wake.
Serikali imeshindwa kufanya doria za kudhibiti uvuvi haramu, kuwapiga faini, na kukusanya kodi ya kutosha kwa ajili ya maendeleo ya watu wake. Mkoani Kagera, ambako gazeti hili lilifanya uchunguzi, watendaji wa serikali na waau wa uvuvi wanakiri kwamba serikali inapoteza mabilioni ya shilingi kila siku kutokana na kushindwa kuwekeza katika rasilimali watu na fedha. Ofisa Mfawidhi, Uhifadhi Rasilimali za Uvuvi Kanda ya kagera, Rodrick Mahimbali anasema ofis yake imekuwa ikikusanya zaidi ya milioni 500 kwa mwaka wa fedha. Anaamini kwamba kama kungekuwa na miundombinu inayofaa, serikali ingekusanya pesa nyingi zaidi. Katika mwaka wa fedha wa 2010/2011, ofisi yake ilikusanya shs. Milioni 700.4 badala ya lengo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, shilingi bilioni 1.2. mahimbili anasema ukusanyaji huo mdogo ulitokana na uhaba wa watumishi katika sekta hiyo, vifaa pamoja na fedha kwa ajili ya doria katika Ziwa Victoria. Anasema ugumu wa doria unatokana na ukubwa wa eneo la ulinzi majini na nchi kavu. Ofisi yake (Kanda ya kagera) Makao Makuu ina watumishi watano, lakini mahitaji halisi ni watumishi 10.
Kanda hiyo pia ina vituo vidogo vine, vyenye watumishi wachache. Vingine vipo katika mipaka ya Tanzania na nchi jirani, hivyo kuhitaji watumishi wa kutosha. Kituo cha Rusumo kina mtumishi mmoja, Kabanga hakina mtumishi. Vituo hivi viko katika wilaya ya Ngara, mpakani mwa Tanzania na Rwanda. Kituo cha Kanyigo kina watumishi wawili, cha Mutukula hakina mtumishi hata mmoja. Hivi viwili viko katika wilaya ya Misenyi mpakani mwa Tanzania na Uganda. Kwa mujibu wa Mahimbali, kila kituo kinahitaji watumishi wasiopungua wanne. Anasema ofisi yake imekuwa inaomba kuongezewa watumishi kutoka wizarani, lakini hajafanikiwa. Kwa sababu hiyo, hata pesa inayokusanywa kutokana na doria wanayofanya ziwani na nchi kavu, ni kidogo sana isiyokidhi mahitaji ya ofisi yake kiutendaji. “Ikumbukwe kuwa kazi ni ngumu sana, ili kupambana na watu wanaokwenda kinyume cha shughuli za uvuvi ziwani na nchi kavu ambao ni wavuvi wa samaki, wachuuzi, walaji na wenye viwanda, zinahitajika fedha za kutosha”. Anasema.
Bila kutaja kiasi halisi wanchoomba serikalini na wanachopewa, anasema kwamba ofisi yake imekuwa ikipatiwa robot u ya bajeti inayoombwa serikalini. Kwa sababu ya bajeti pungufu, ansema ofisi yake inakabiliwa na ugumu katika kutekeleza majukumu yake, matokeo yake serikali inapoteza mabilioni ya fedha ambayo yangetokana na makusanyo ya faini kwa wavuvi haramu”.
“ Uvuvi haramu tunaoshughulikiwa nao katika doria zetu ni utumiaji wa nyavu zisizostahili, makokoro, uvuvi wa dagaa na samaki wachanga, uvuvi wa samaki wazalishaji, uvuvi wa mitumbwi isiyosajilijwa:, anasema.
Wafugaji watunishiana misuli na wawekezaji – Majira, Jumanne April 03, 2012
Na. Stephano Samo, Manyara
Katika hali isiyokuwa ya kawaida vurugu kubwa zimezuka kwenye mashamba ya ngano baina ya wafugaji wa Kijiji cha Gidagamuoda Kata ya Mogitu Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na wakulima wakubwa. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wafugaji wa kata ya Mogitu jana walidai kuwa vurugu hizo zilianza juzi baada ya wakulima hao kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji unaofanywa na wakulima wakubwa.
Walisema, wakulima hao walikuta mtoto wa wwafugaji hao akichunga mifugo kandokando ya mashamba na kumkamata kisha kumfungia ndani ya nyumba zao ndipo wafugaji hao wakapata taarifa ya tukio hilo na kuamua kuchukua hatua. Walisema kuwa katika vurugu hizo silaha za jadi zilitumika ikiwemo mikuki, sime na mapanga ambapo wafugaji hao walimkata na mapango mmoja wa wakulima hao na kumjerhi vibaya na kusababishia maumivu makali hiyo kupelekwa Hospital ya Tumaini wilayani humo kwa ajili ya matibabu.
Walidai kuwa wakulima hao wakubwa ambao ni watanzania wenye asili ya kiasia eneo hilo lenye aidi ya hekari 40,000 wamekuwa wakiyatumia mashamba hayo kwa ajili ya kuzalisha zao la ngano.
Akizungumzia hali hiyo Mbunge wa Jimbo la hanang, Dkt. Mary Nagu alisema hawezi kuvumilia tena kuona wawekezaji wakijichukulia sheria mikononi kwa kuwa kuna njia za kufuata ili kuepusha migogoro kama hiyo. “Hawa wahindi wanatunyanyasa .. sana, kwa kutumia fedha zao wanatufanya tuwe watumwa kwenye ardhi yetu, yaani mifugo yetu haina thamani kabisa hawataki iwepo wakati ndiyo tegemeo letu” alisema. Alisema kuwa, wakuliwa hao wakubwa wamekuwa wakiwanyanyasa wafugaji hao kwa kukamata mifugo yao kila wakati na pia kuwafikisha Kituo cha Polisi Katesh hasa vijana pindi mifugo iikiwa inakamatwa inalishwa pembeni ya mashamba hayo.
Hata hivyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Kapteni Mstaafu Winfrid Ligubi akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana alidai kuwa magazeti yamekuwa kiandika habari za vurugu badala ya kuandika za maendeleo.
Nyinyi kazi yenu ni kusubiri vurugu zitokee na kuandika habari mbona mambo mengi ya maendeleo yakifanyika huwa hamuandiki, mnasubiri wahuni wawapigie simu na kuwajulisha vurugu zimetokea ndipo mnaandika asliema Ligubi na kuongeza kwa nini hampendi kuandika mambo ya msingi nabaki kuandika mambo ya vurugu tu kila mara vurugu tu.
‘Uwekezaji sekta ya uvuvi bado’ – Majira, Jumanne Aprili 03, 2012
Serikali imekiri kuwa uwekezaji katika sekta ya uvuvi Zanzibar bado utekelezaji wake ni mdogo licha ya hatua mbalimbali zilizofanywa na Serikali kuhamasisha uwekezaji katika eneo hilo. Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Bi. Thuwaiba Edington Kisasi alilieleza Baraza la Wawakilishi jana kuwa kutokana na hali hiyo Serikali kwa sasa imekuwa ikitoa leseni za uvuvi wa bahari kuu ili kuweza kuongeza mapato yake wakati juhudi za kuwakaribisha wawekezaji katika eneo hilo zinaendelezwa. Hata hivyo alisema, ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kuhifadhia samaki na nyenzo za kisasa za kuvulia ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wavuvi wa Zanzibar ambazo Serikali inakabiliana nazo.
Alisema, Serikali kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo kupitia miradi wanayoifadhili wakiwemo MACEMP, UNDP na Join Program 5 na wengine imekuwa ikitoa vifaa mbalimbali vya kuhifadhia samaki kwa baadhi ya wavuvi wa maeneo ya Nungwi, Kizimkazi ili kuhifadhia bidhaa hiyo wakati wa dharura na kuepuka kuharibika.
Aidha, alisema kwamba kwa upande wa uwekezaji wa viwanda imebainika kuwepo kwa vivutio hafifu vya kuwavutia wawekezaji na kusema kwamba Serikali inaendelea na kuifanyia mapitio sera ya maendeleo ya viwanda kwa lengo la kuimarisha vivutio na kuweka mazingira bora zaidi ya kisera.
Awali Mwakilishi wa Jimbo la Koani Bw. Hassan Hamad Omar (CUF) alitaka kujuwa Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wavuvi kwa kuwapatia vifaa vya kuhifadhia samaki hatua itakayowasaidia wavuvi hao kutouza samaki wao kwa bei ya chini kwa kuepuka samaki wote kuharibika.
Serikali kuwasaidia wafugaji – Majira, Jumanne April 03, 2012
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar imesema inaangalia uwezekano wa kuwasaidia wafugaji wazalendo ili kuweza kuzalisha kwa ufanisi na kukabiliana vema na ushindani wa masoko ya kibiashara. Hayo yameelezwa jana na kaimu Waziri wa Wizara hiyo Bi. Fatma Abdulhabib Fereji katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi wakati akijibu swali la mwakilishi wa nafasi za wanawake Bi. Ashura Sharif Ali.
Alisema, mbali na wafugaji hao kukabiliana na ushindani lakini pia wataweza kufanya kazi na wazalishaji wao kwa ukaribu zaidi na kuwapatia taaluma ya uzalishaji bora. Bi. Fereji alisema, kwamba kuruhusiwa uingizaji wa bidhaa za kuku wa nyama katika nchi kunaweza kuwavunja moyo wafugaji wao lakini pia kutawapa hari ya uzalishaji zaidi wafugaji wao na kwa ubora zaidi.
Alisema, hatua hiyo itafikiwa na wafugaji wao hao iwapo kutajengwa mazingira ya kuwatia hari wafugaji hao na kukabiliana na ulimwengu wa ushindani hasa kibiashara wasiouweza kuepukana nao. Awali mwakilishi huyo alisema kwamba kuruhusiwa uingizaji wa bidhaa za kuku wa nyama katika nchi yao Serikali haioni kwamba ni kuwavunja moyo wafugaji wazalendo pamoja na kuwapunguzia au kuwakosesha soko la kuuza bidhaa hiyo.
Hamna utaratibu wa kuwapa watumishi maziwa – Waziri, Majira Jumanne April 03, 2012
Alisema kwamba kutokana na kutokuwepo kwa masharti hayo pia kuna baadhi ya taasisi zimeondoa utaratibu huo kutokana na kuwa si rahisi kuwapa maziwa watumishi wote wanaotumia kompyuta ambao idadi yao ni kubwa kuliko wasiotumia.
Serikali imesema kwamba haina utaratibu wa kuwapa maziwa watumishi wake ambao wanatumia kompyuta katika ofisi zao na wala hakuna sharti hilo. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Haji Omar Kheir alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa nafasi za wanawake Bil Shadya Mohammed Suleiman jana katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.
Alisema, kwamba kutokana na kutokuwepo kwa masharti hayo pia kuna baadhi ya taasisi zimeondoa utaratibu huo kutokana na kuwa si rahisi kuwapa maziwa watumishi wote wanaotumia kompyuta ambao zaidi idadi yao ni kubwa kuliko wasiotumia.
Serikali haina utaratibu huo na wala hakuna sharti hilo, ukweli ni kwamba hao wanapewa posho hiyo …hawaitumii kwa kununulia maziwa alisema.
Hata hivyo alisema kuwa maziwa si dawa ya kuzuia madhara ya kutumia kompyuta na kueleza kwamba zaidi ya hayo hakuna sheria inayoelekeza hivyo.
Large-scale indigenous chicken rearing project lauched – The Guardian, Monday April 2, 2012
By Alpha Nuhu
Tanzania is set to make indigenous poultry keeping an important economic venture that could play a key role in poverty reduction in the country. Already, the government has vowed to help small-scale chicken keepers to improve their livelihood following the successful MUVEK Development Solutions lauch of Research Into Use (RIU) Programme knowledge outputs last week …………..
At the lauch of the programme, Prime Minister Mizengo Pinda commended RIU knowledge innovations in making indigenous poultry keeping an important economic activity that could help small-scale indigenous poultry keepers play a key role in the country’s poverty eradication strategy.
“Indeed Muvek through RIU have been an eye opener, by enabling small scale farmers to keep 100 to 400 chickens MUVEK and RIU have proved that indigenous chicken farming can be used for poverty eradication,” Pinda told his audience.
Wafugaji washirikishwe kuboresha mifugo vijijini, Habarileo, Alhamisi Machi 29, 2012
Na. John Nditi
Mfugaji bora ni yole anayetoa sehemu ya shughuli mbalimbali za kuboresha miundombinu ya sekta ya ufugaji, hasa vijijini ili kuifanya iwe endelevu na itakayoleta tija katika kukuza uchumi wa mfugaji mmoja mmoja na taifa. Ni Yule anayeamua kutunza baadhi ya mifugo hasa ng’ombe wake ili kupata fedha za kuchangia shughuli za maendeleo hususani ya ujenzi wa malambo, mabwawa, uchimbaji wa visima badala ya kuitegemea serikali kwa kila kitu.
Hatua hiyo inasaidia kuboresha miundombinu ya mifugo, kwa lengo la kuhudumia mifugo yao, badala ya kila jambo kusubiri kufanyiwa na serikali yao.
Mfumo huo ndiyo unaotekelezwa kwenye sekta ya mifugo na nchi ya Botswana, na umeiwezesha mifugo yake kuwa ya kisasa. Katika nchi hiyo wao wenyewe wameondokana na dhana kuwa uwekezaji huo lazima uwe wa serikali pekee, bali ni pamoja na kuchangiwa na wafugaji. Wafugaji hao wanadiri kuuza sehemu ya mifugo yao na kuchangia asilimia kubwa katika kuboresha miundombinu ya mifugo, ambayo ni kuchimba maji ardhini na kupanda majani kwa ajili ya mifugo yao.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. Mathayo David katika makala haya, anaelezea mpango huo umefanikiwa kuufanya ufugaji wa nchi ya Botswana, kuwa wa kisasa zaidi na wenye tija kwa manufaa yao na ya serikali. Dk. Mathayo ameliweka wazi jambo hilo katika mkutano na wafugaji wa Kijiji cha Wami Sokoine wilayani Mvomero, ambao uliwakutanisha pia na wafugaji wa Kanda ya Mashariki ya Mikoa ya Pwani, Tanga na Morogoro.
Wajiendeleza kwa ufugaji kuku Mbuguani – Majira, Ijumaa Machi 30, 2012
Mradi huu wa ufugaji wa kuku wa mayai Kisiwani Pemba unaendeshwa na kikundi cha watu 10, wanawake saba na wanaume watatu. Kikundi hiki kinafuga kuku 250.
Kulingana na maelezo ya Katibu wa kikundi hiki Bi. Mariam Hamad Makame, kikundi chao kinajulikana kama kikundi cha Nuru Njema ambacho ni ushirika wa ufugaji kuku kwa maslahi ya watoto yatima wa Shehia ya Mbuguani. Mradi huo ulianza Novemba 2011 kwa ufadhili wa shilingi milioni 8.8 zilizotolewa na MACEMP kupitia TASAF. Ili kufanikisha ujenzi wa banda, wanakikundi walisafisha eneo, kuchimba msing, kubeba mawe, mchanga na matofali ili kupunguza gharama.
“Pamoja na juhudi zetu hatukuweza kukamilisha ujenzi huo kutokana na kuongezeka kwa bei za vifaa vya ujenzi, ilibidi kufanya yale ya muhimu tu na kuanza ufugaji” Anazungumza Katibu Bi. Mariam Hamad Makame. Maneno yake ni kweli tupu kwani hata hali ya banda haijakamilika kwa kiwango kinachostahili licha ya kuwemo kuku ndani. Banda la kufugia kuku lina vyumba viwli na kila chumba kina kuku 125 umri wa miaka 6. Kuku wanapata chanjo na huduma za kitaalam kutoka kwa wataalam, na wanakikundi pia wamefundishwa jinsi ya kutoa huduma kwa mifugo yao.
“Ufugaji wa kuku umekuwa na gharama kubwa kuliko matarajio yetu. Madawa na chakula ni ghali mno kiasi mara nyingine tunapata na hofu kama faida itapatikana. Kuku wanavyozidi kukua ndivyo wanavyohitaji chakula na dawa zaidi. Vikundi vingi vilivyoanza kufuga vimeshindwa kuendelea na ufugaji kutokana na gharama kuwa kubwa. Sisi bado tupo”
Pamoja na changamoto hii wanakikundi hawa hawajakata tama kwani wanasema toka waanze mradi lengo lao lilikuwa ni kufikia uzalishaji utakaowawezesha kuanzisha miradi mingine hatua kwa hatua kwa hiyo wanaendelea kujizatiti. Ama kwa hakika mvumilivu hula mbivu iko siku kikundi hiki kitafaidi matunda ya juhudi zao. Katibu wa kikundi alitanabaisha kuwa mara zote hufarijika sana wanapopata wageni kwani ule usemi wa “mgeni kawia mwenyeji apone” kwao unawapa manufaa sana.
“Kila wageni wanapotutembelea tunapata ushauri wa nini tufanye ili tusonge mbele” Kwa sasa kuku hao wameanza kuonyesha ishara njema ya kutaga mayai na hupata tray 4 za mayai kwa siku. Kwa wastani tray moja huunzwa shilling 7,000/=. Kikundi kina soko la uhakika kwani kuna mtu ambaye wanampelekea ukiacha wale ambao wanakwenda kununua hapo bandani.
Walengwa wanatilia suala la mafunzo, wanasema japo japo mwanzo wakati wanaanza kufuga walipata mafunzo hata hivyo mafunzo hayo hayajakidhi kiwango.
Ni jukumu la maafisa ugani hasa wa kilimo na mifugo kutoa utaalam kwa vikundi kama hivi ili viweze kufuga kwa tija zaidi. Endapo mafunzo yatatolewa vikundi vingi vitaweza kujiendesha vyenyewe na kupata kipato cha kuwafanya wamudu maisha bila ya kutegemea misaada kwa wasamaria wema na wafadhili.
Anufaika kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji, Majira Toleo Maalum la TASAF, Ijumaa Machi 30, 2012
Wengi tunadhani ufugaji wa kuku wa kienyeji hauhitaji utaalamu, dhana hii si sahihi na inabidi tubadilike! Hata wahenga walifuga kwa uzoefu uliozaa ujuzi. Kutokana na kuishi na kuku kwa muda mrefu waliweza kujua tabia zao, dalili za magonjwa na hata aina za vyakula ambavyo kuku alipopewa alitaga mayai mengi na kuwa na afya bora. Hivyo endapo mtu anahitaji kufuga kuku wa kienyeji basi ni vuziru akachukua muda kidogo kuuliza kwa wataalam au wafugaji wa muda mrefu njia nzuri ya kufuga kuku kwa tija.
Ali Abdalah Juma ni kijana mwenye umri wa miaka 30 ambaye ameweka lengo la kuhudumia kuku wake wa kienyeji anaofuga ili wampatie kipato cha kutosha aweze kujenga nyumba, kuoa na kuanza familia. Ali ana imani kwamba ufugaji wa kuku wa kienyeji ‘utamtoa’. Ali pamoja na wanakikundi wenzake walianza ufugaji wa kuku wa kienyeji mwaka 2011 na kila mmoja kati ay wanachama kumi alikabidhiwa kuku 39, mitetea 35 na majogoo 4. Mwaka mmoja baadae Novemba 2011 Ali ana kuku wakubwa 62 pamoja na vifaranga 52. Hawa ni waliosalia baada ya kuuza na kuchinja kuku kadhaa ukiacha wale walioibiwa au kuliwa na mwewe. Polepole ndiyo mwendo. Hakika Ali anasonga mbele.
Ali anasema kuku wake wanakula kila aina ya chakula, vya madukani pamoja na mabaki ya vyakula vya nyumbani. Kuku hawa wanafugwa bandani lakini pia huachiwa na kwenda kujitafutia kama ilivyo kawaida ya kuku wa kienyeji. Kuku hawa hawakosi chanjo, na Ali mwenyewe ndiye anayetoa chanjo hii. Utalaam wa kutoa chanjo aliupata kutoka kwa daktari wa mifugo aliyewapa mafunzo ya ufugaji kipindi ambacho walikabidhiwa kuku hao. “Daktari alikuwepo kwa muda wa wiki mfululizo akitupa mafunzo ya jinsi ya kuhudumia kuku, kuwapa chakula, chanjo na kujua dalili za magonjwa, lakini baada ya muda huo hajapita tena labda itokezee mara moja kwa ratiba za kazi zake lakini hata hivyo hakuna linalonishinda” Anasema Ali kwa kujiamini.
Mbali na kufuga kuku, Ali pia anafuga bata. Anao bata nane majike na dume mmoja. Hata hivyo anasema bata hawana soko mara nyingi yeye huwatumia kwa kitoweo tu nyumbani. Anasema hata mayai ya bata pia hayapendwi sana kama ilivyo kwa mayai ya kuku. Ali sasa ameshakuwa mtaalam wa ufugaji na mengi nayajua katika tasnia hiyo. “Ufugaji unahitaji usafi wa hali ya juu ili kuku wasishambuliwe na viroboto. Viroboto ni adui mkubwa sana wa kuku wanaweza kuangamiza banda zima katika muda mfupi. Ni vizuri kusafisha banda la kuku kila mara ili libaki kavu na lisiwe na unyevunyevu”. Nilithibitisha kauli hii nilipoingia ndani ya banda hilo wakati kuku wakiwa nje kutafuta malisho. Banda lilikuwa safi na kavu. Nikakubali kweli Ali ameiva katika ufugaji na siku moja ndoto yake itakuwa kweli. Atajenga na kuoa kutokana na mradi huo. Ali hana tabu na soko la kuuzia kuku kwani huuza hapo hapo kijijini, na kwa kwenye migahawa. Pemba kama wote tunavyofahamu ni maarufu kwa utalii hivyo hata watu wenye mahoteli hufika kwa Ali na kununua kuku kwa ajili ya kuwatayarishia wageni wao. Jogoo mmoja aliyenona vizuri huuzwa kati ya shilingi 30,000 hadi 35,000.
Ali anasema magonjwa ambayo yanamsumbua mara kwa mara kwa kuku wake ni homa ambazo yeye anadai kwa muda mrefu ambao amekuwa nafuga anaweza kujua kuwa kuku ana homa kwa kuona dalili zake na ikitokea hivyo huwapa dawa za asili kama maji ya pilipili na maji ya mwarobaini kabla ya kwenda kununua dawa za mifugo na kupata ushauri wa kitaalam.
Anasema dawa hizo ni huduma ya kwanza na mara zote zimemsaidia. Changamoto kubwa anayokumbana nayo Ali katika ufugaji ni wizi wa kuku unaofanywa na binadamu pamoja na kuku kuliwa na mwewe hasa vifaranga ambao kama hakuwa makini kudhibiti basi wangemrudisha nyuma sana kwani awali walimpa shida. “Wezi wa kuku ni wengi kupita hao mwewe. Ukiwaacha tu bila uangalizi basi hutawaona tena kwa hiyo ninachofanya wakati wa kuwatoa nje nahakikisha kuwa niko mwenyewe au nimemwachia mtu awatizame.
Wizi wa kuku umewarudisha nyuma wafugaji wengi kwani ni kitu ambacho kinatokea bila mfugaji kukitarajia. Ulinzi katika mabanda na wakati wa kuwaachia kuku kujitafutia chakula ni jambo la muhimu. Suala la kupanda kwa gharama za vyakula vya kuku hasa vile vinavyotengenezwa viwandani vimechangia sana kupandisha bei za kuku. Hii pia ni changamoto nyingine ambayo Ali anakumbana nayo. “Bei kubwa ya chakula cha viwandani inaniathiri sana. Laiti ningekuwa na pesa za kununua vyakula hivyo kwa mara moja, malengo yangu ningeyafikia haraka, ila bei za vyakula ni kubwa. Ili ninunue mfuko mmoja inabidi niuze japo kuku watatu au wanne na kwangu hii ni hasara nitamaliza kuuza kuku wote kwa kununua chakula hii siwezi. Ndo maana kuku wangu nimewazoesha kula chochote kinachopatikana.
Vijana wengi wenye malengo kama Ali ni rahisi sana kuweza kufanikiwa kwa kupata msaada kidogo hata wa kimawazo. Wakishauriwa kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na kuanzisha mfuko wa kujitegemea hatimaye wanaweza kupata mikopo ili kujikomboa. Pamoja na nia njema waliyonayo huenda hawafahamu wapi wanaweza kupata miongozo ya kufikia malengo yao. Ziko wapi taasisi zisizo za kiserikali zinazoweza kutia msukumo katika upatikanaji wa nyenzo na rasilimali kwa vijana kama hawa ambao wako tayari kujikwamua kiuchumi.
Upandaji mwani wanufaisha vikundi vya ushirika – Tumbe Majira Toleo Maalum la TASAF, Ijumaa Machi 30, 2012
Vikundi vya ushirika vya upandaji mwani vya Shehia za Tumbe Mashariki na Magharibi vimesema kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) imewafungulia njia ya kufikia mafanikio yao lakini yamekua yakirejeshwa nyuma na bei ndogo ya zao hilo inayotolewa na wamiliki wa makampuni yanayojishughulisha na ununuzi wa mwani Kisiwani Pemba. Wakizungumza na waandishi wa habari katika ziara iliandaliwa na TASAF Pemba Mwenyeviti wa vikundi hivyo walisema baada ya kukabidhiwa zaidi ya shilingi milioni 35,886,690.00 kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mabanda na kupeana taaluma hilo walifanikiwa vyema. Mwenyekiti wa kikundi cha Tumbe Mashariki Asaa kassim Shaibanwe alisema kupitia kikundi hicho wanachama wamefaidika katika Nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujipatia fedha za kutatua matatizo mbalimbali kama vile michango ya skuli kwa watoto wao.
Shaibanwe alieleza kuwa wapo baadhi ya wanachama wamejinunulia vitu vya thamani kama vile cherehani na hata simu za mkononi ukiachia mbali fedha ndogondogo wanazogawana kila baada ya kipindi. “Malengo ya kikundi hichi kama yalivyotakiwa na TASAF kwenye kikundi chetu tunasema yamefikiwa maana kila mwanakikundi amepata manufaa kwa upande wake”, alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha, aliongeza kuwa katika fedha walizopewa na TASAF kwa mwaka huo 2007/2008 ziliwawezesha kujenga banda maalum la kuanikia mwani, kununua mashua na mashine yake kwa ajili ya kusombea mwani jambo ambalo hapo mwanzoni lilikuwa kikwazo kwa wanajamii wote wanaojishughulisha na kazi hiyo. Hata hivyo alisema kuwa suala la bei ya mwani ya shilingi 400/= kwa kilo ndio changamoto inayowakabili na kutokana na hilo wameifikiria kuwa na mradi mbadala wa mashamba ya chumvi. Walisema kama fedha zao zitaruhusu au wakipatiwa ufadhili wanatarajia kuanzisha mashamba ya chumvi ambayo wanaamini yatazidi kuinua kipato chao kupitia kikundi hicho.
Nae mwenyekiti wa kikundi cha mwani cha Tumbe Magharibi Hamad Sadik Mussa, alisema TASAF kwa kiasi kikubwa imewakomboa kutokana na kuwepo kwa kikundi hicho ambapo hapo kabla kazi hiyo ikifanywa na mtu mmoja mmoja na kutopata mafanikio. “Kwa njia moja ama nyingine TASAF kupitia kikundi chetu imetukomboa maana kazi hii tulikua tukiifanya sisi zamani lakini hatukufaidika maana umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu” alieleza kwa kujiamini Mwenyekiti huyo. Kuhusu bei ya mwani ya sasa wameomba angalau ifikie shilingi 1,000/= kwa kilo moja badala ya shilingi 400/= za sasa ambapo kutokana na kazi ngumu ya zao hilo la mwani haikidhi haja. Hata hivyo alisema kupitia kikundi hicho baadhi ya wanakikundi hukopa fedha kati ya shilingi 40,000/= hadi shilingi 50,000/= pale wanapokua na dharura za kifamilia na kurejesha kwa wakati.
TASAF kupitia vikundi kama hivyo huviwezesha kwa kuwapatia fedha taslimu ambapo miongoni mwa matumizi ya fedha hizo ni pamoja na kuwapatia elimu, wanavikundi na ujenzi wa majengo maalum kwa ajili ya shughuli za wanakikundi.
Kikundi cha uvuvi chajizatiti kupamba na umaskini Uweleni – Pemba – Majira toleo maalum la TASAF, Ijumaa Machi 30, 2012
Wengi wape ni jina la kikundi cha uvuvi kutoka Shehia ya Uweleni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba chenye wanachama 20 mmoja kati yao akiwa ni mwanamke. Kikundi hicho ni miongoni mwa vikundi katika jamii vilivyowezeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamiia (TASAF) mwaka 2004 baada ya wanajamii kukubaliana kuanzisha mradi huo kwa ajili ya kujiongezea kipato. Wengi Wape walipatiwa boti moja ya mashine, nyavu zenye thamani ya shilingi milioni 21,038,340.00 paoja na kupatiwa mafunzo ya muda mfupi juu ya masuala ya uvuvi kwa wanachama wake. Wengi Wape si jina la kikundi tu pia ni jina la boti yenyewe ambayo ni maarufu katika bandari ya Mkoani.
Ali Khamis Ali ni nahodha wa boti ya Wengi Wape anaelezea maendeleo aliyoyapata katika kikundi hicho baada ya kupata msaada huo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). Kabla ya kupatiwa bodi hiyo anasema kibarua kilikuwa kigumu kwani alikuwa hana uhakika wa kupata kazi ya kwenda baharini kuvua kwa sababu alikuwa hana chombo cha uhakika. Lakini baada ya kupata chombo hicho cha kufanyia kazi ameweza kupata fedha za matumizi yake ya kila siku pamoja na kitoweo jambo ambalo lilikuwa gumu kwa hapo mwanzo. Licha ya kupata faida hiyo baadhi ya siku kazi inapokuwa nzuri hupata ziaidi ya shilingi laki mbili, kiwango hicho cha fedha ambacho si kidogo kwa mfanyabiashara. “namshukuru Mwenyezi Mungu kwani kazi hii hunipatia kipato cha halali mimi na familia yangu. Kwa upande wangu naishukuru TASAF imekuwa mkombozi wangu kwani silali njaa mimi pamoja na familia yangu” alisema. Na si hayo tu lakini kikundi pia kuna mgao ambao kwa kila wiki kila mwanachama hupata shilingi elfu 50 kama mauzo yakiwa mazuri na wakati mwingine hushuka kulingana na bamvua lilivyo. Kwa upande wake msaidizi nahodha wa boti hiyo Amour Mohamed Mjawiri akizungumza kuhusiana na faida alizopata baada ya kuanzishwa kwa mradi huo alisema umemuwezesha kupata kipato ambacho hukitumia kwa ajili ya kusomesha watoto wake. Kabla ya hapo kibarua kilikuwa kigumu kutokana na chombo alichokuwa akifanyia kazi kuwa si cha uhakika lakini sasa kazi yake imekuwa nyepesi. Suala la msingi ni kuamka mzima na kuweza kwenda kibaruani kufanya kazi, kwani boti ya uhakika ipo
Pamoja na faida hizo alizopata kutokana na kazi hiyo, alisema kuna changamoto anazokabiliana nazo katika hiyo na katika kikundi pia ambazo zinamrudisha nyuma maendeleo yao na malengo waliyojiwekea. Miongoni mwa changamoto zilizomo katika kikundi ni kuwa baadhi ya wanachama wameweka maslahi yao mbele, kitendo ambacho kinaweza kupelekea kuvunjika kwa ushirika huo. Mjawiri anaendelea kusema kuwepo kwa makundi katika ushirika huo kunaweza kuathiri maendeleo yaliyofikiwa na kuvunjika kwa jumuiya hiyo ingawa sio lengo la kuanzishwa kwa kikundi hicho. ‘Si vyema kwa ushirika kuwa na makundi. Jambo la msingi ni kushirikiana ili kuhakikisha kikundi kinasonga mbele na kuwa endelevu alisisitiza. Kwa upande wa changamoto zinazowakabili katika kazi yake hiyo ni hali ya hewa baadhi ya nyakati bahari huwa chafu ambayo inaweza kuhatarisha maisha yake na nahodha wake. Kwa mujibu wa Mawiri alisema TASAF imekuja wakati muafaka ambapo mahitaji yamekuwa mengi ikiwemo suala la ajira ambalo ni gumu kwa sasa lakini jamii kupitia imeweza kujiajiri yenyewe kwa kubuni miradi mbalimbali badala ya kusubiri ajira serikalini.
Hata hivyo alisema suala la muhimu ni kuhakikisha jamii inaimarisha miradi hiyo ya maendeleo katika maeneo yoa ili miradi hiyo iwe mkombozi wao katika kupambana na umaskini.
Wachina wanaswa na tani moja ya samaki – Mwananchi, Ijumaa Machi 30, 2012
Na. Mariam Sangoda na Dotto Kahindi
Umoja wa Waagizaji na Wasafirishaji wa Samaki nje ya nchi (DAFIE) kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi na Polisi imewakamata raia watatu wa China kwa tuhuma za kufanya uvuvi haramu katika bahari ya Hindi. Katibu wa umoja huo, Barnaba Mapunda alisema kuwa watu hao walikamatwa baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwao na hivyo kutoa taarifa kwa polisi kituo cha Kigamboni ambao walifanikisha kuwamakata watuhumiwa hao. Alisema kuwa Wachina hao ambao majina yao yamehifadhiwa ili kupicha uchunguzi zaidi, walikamatwa wakiwa na tani moja ya samaki aina ya kaa ambao walikuwa wakiwaandaa tayari kwa kuwasafirisha nje ya nchi.
“kwa ushirikiano wa Idara ya Mifugo na uvuvi leo (jana) asubuhi tumefanikiwa kuwakamata raia watatu kutoka China ambao walikuwa katika harakati za kuandaa mzigo wa samaki ili kusafirisha nje ya nchi,” alisema mapunda. Watu hao walikamatwa katika maeneo ya Kigamboni kwenye kiwanda kidogo cha samaki cha Marine food Product kinachomilikiwa na Mtanzania aliyefahamika kwa jina moja la Idrisa. Umoja huo umekuwa ukiendesha oparesheni ya kuwasaka wavuvi haramu katika bahari ya hindi ambao wamekuwa wakiingizia taifa hasara kubwa kwa kuhujumu rasilimali za taifa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Temeke, Kamishna msaidizi wa polisi Maselino Luambano alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi leo.
Wafanyabiashara watakiwa kutouza ngozi kwa magendo – Mtanzania, Ijumaa Machi 30, 2012
Na Gabriel Mushi, Dsm
Serikali imewataka wafanyabiashara wa ngozi kuachana na biashara ya magendo, kwa kuwa inasababisha sekta ya ngozi nchini kuendelea kudidimia. Angizo hili lilitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Sekta ya Ngozi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Biashara na Masoko, Anuciata Njombe alipozungumza na wadau wa ngozi.
Alisema biashara ya magendo imekuwa chanzo cha kuididimiza sekta hiyo, kwa kuwa asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa ngozi wamekuwa wakikwepa kulipa kodi.
“Wakati huo huo, wamekuwa wakipeleka bidhaa hizo nje bila hata ya kuzongezea thamani, hali hii imeendelea kuwafanya kuendelea kuuza kwa bei ya chini, wakati kama wangekuwa wameongezea thamani basi wangepata faida kubwa,” alisema Njombe.
Naye, Katibu Mkuu, wa Wizara ya Viwanda na Biashara Joyce Mapunjo alisema ili kuinua sekta hiyo nchini, kunahitajika ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda. “kwa sababu suala la kukwepa kulipa ushuru ni tatizo, pia suala la kuongezea ngozi hizi thamani nalo ni suala ambalo bado ni changamoto kubwa kwetu, hivyo kila mmoja anatakiwa kushirikian an mwenzake katika kutatuta changamoto hizi”.
“Hivyo kukiwa na usindikaji mzuri hapa hapa nchini, kila mmoja atanufaika kutokana na mapato yake, badala ya kupeana sifa kuwa Tanzania ina mifugo mingi, lakini hatufaidiki nayo, hilo si suala la kujivunia kabisa,” alisema Mapunjo. Kwa upande wa ke Mwenyekiti wa Chama cha Wadau wa Ngozi Tanzania Adam Ngawiro, alisema hivi sasa sekta hiyo inakabiliwa na uwekezaji mdogo.
Wafugaji Ulanga waanza kusomesha watoto – Habarileo, Ijumaa Machi 30, 2012
Na John Nditi
Mimi sijasoma na pia umri wangu si ufahamu ila elimu niliyoipata ya kuvuna mazao ya mifugo na fedha zake kuingiza kwenye biashara nyingine, imezaa matunda kwangu na wenzangu nina watoto 34. Hiyo ni kauli ya mfugaji na mkulima wa Kisukuma Andrew Ngiri, ana wake watatu na watoto 34 na makazi yake ni Kijiji cha Ipera kata ya Itete Njiwa Tarafa ya Mtimbira wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.
Baada ya kupata elimu juu ya kutambua kuwa mifugo, pia ni sehemu ya kuwezesha kuwa na rasilimali nyingine iwapo itapunguzwa kwa kuuzwa, inaweza kuongeza pato la uchumi kwa mfugaji na Taifa. Katika kuitikia wito huo, aliamua kuuza ng’ombe 250 na kujipatia mamilioni ya fedha, zilizomwezesha kujenga nyumba ya kisasa ya kulala wageni yenye vyumba 14. Anasema eneo hilo lina maendeleo kiuchumi. Kutokana na uzalishaji wa zao la mpunga na mahindi kata ya Mtimbira wilayani humo. Katika makala haya, mfugaji na mkulima Mbogoma, anabainisha kuwa wafugaji wengi wa Kisukuma wa kata ya Itete Njiwa na Mtimbira, wameitikia wito ho wa kupunguza mifugo yao na kuwekeza kwenye nyumba za biashara na kununua zana za kilimo, hasa matreta.
Soko la Magogoni sasa kuanza kusafishwa Mei - Nipashe, Alhamisi Machi 29, 2012
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam, inachambua zabuni za usafi ili Mei, mwaka huu wazabuni waanze kufanya usafi katika soko la Magogoni ambalo lipo katika mazingira yasiyoridhisha. Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, alitoa ufafanuzi huo jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kufuatia ziara ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuv, Dk. David Mathayo sokoni hapo hivi karibuni na kukuta soko likiwa katika mazingira machafu. Silaa alisema Waziri Mathayo hakupewa taarifa sahihi za mikakati ya soko hilo kwa sababu hakushirikisha uongozi wa manispaa hiyo katika ziara hiyo ambao ungempa taarifa sahihi ya namna ya kukabiliana na mazingira ya uchafu katika soko hilo.
"Tatizo la uchafu linatakiwa lifanyiwe utaratibu maalum na tupo kwenye mkakati wa tathimini ya zabuni za usafi ambazo hadi kufikia Mei, Mosi mwaka huu, tunatarajia kuwa tumekamalisha na kupata mzabuni atakayefanya usafi kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu," alisema.
Alisema watakapoanza utaratibu mpya, wazabuni wote watatangazwa hadharani kutakiwa kuonyesha vifaa vyao vyote muhimu kwa ajili ya kuendesha shughuli za usafi, ambapo namba zao za mawasiliano zitawekwa wazi ili kila mwananchi amjue mzabuni wake na awe na uwezo wa kuwasiliana naye anapoona kuna tatizo au huduma zinalegalega.
Meya Silaa alisema utaratibu ulio wazi kwa kiongozi yeyote wa serikali anapotaka kufanya ziara kwenye taasisi yeyote hutoa taarifa mapema ama kuwasiliana na taasisi hiyo kabla ili kuepusha migongano itakayojitokeza.
Wafugaji washirikishwe kuboresha mifugo vijijini, Habarileo, Alhamisi Machi 29, 2012
Na. John Nditi
Mfugaji bora ni yole anayetoa sehemu ya shughuli mbalimbali za kuboresha miundombinu ya sekta ya ufugaji, hasa vijijini ili kuifanya iwe endelevu na itakayoleta tija katika kukuza uchumi wa mfugaji mmoja mmoja na taifa. Ni Yule anayeamua kutunza baadhi ya mifugo hasa ng’ombe wake ili kupata fedha za kuchangia shughuli za maendeleo hususani ya ujenzi wa malambo, mabwawa, uchimbaji wa visima badala ya kuitegemea serikali kwa kila kitu.
Hatua hiyo inasaidia kuboresha miundombinu ya mifugo, kwa lengo la kuhudumia mifugo yao, badala ya kila jambo kusubiri kufanyiwa na serikali yao.
Mfumo huo ndiyo unaotekelezwa kwenye sekta ya mifugo na nchi ya Botswana, na umeiwezesha mifugo yake kuwa ya kisasa. Katika nchi hiyo wao wenyewe wameondokana na dhana kuwa uwekezaji huo lazima uwe wa serikali pekee, bali ni pamoja na kuchangiwa na wafugaji. Wafugaji hao wanadiri kuuza sehemu ya mifugo yao na kuchangia asilimia kubwa katika kuboresha miundombinu ya mifugo, ambayo ni kuchimba maji ardhini na kupanda majani kwa ajili ya mifugo yao.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. Mathayo David katika makala haya, anaelezea mpango huo umefanikiwa kuufanya ufugaji wa nchi ya Botswana, kuwa wa kisasa zaidi na wenye tija kwa manufaa yao na ya serikali. Dk. Mathayo ameliweka wazi jambo hilo katika mkutano na wafugaji wa Kijiji cha Wami Sokoine wilayani Mvomero, ambao uliwakutanisha pia na wafugaji wa Kanda ya Mashariki ya Mikoa ya Pwani, Tanga na Morogoro.
Walia hali ngumu soko la samaki - HabariLeo, Alhamisi Machi 29, 2012
Wafanyabiashara wa samaki katika soko la Manzese Manispaa ya Songea wamelalamikia hali ngumu ya biashara yao kutokana na idadi ndogo ya wateja wanaofika sokoni hapo. Wafanyabiashara hao wamesema hali hiyo inawakatisha tamaa kwa kuhofia kukatika mitaji yao ya biashara ambayo wengi wao waliipata kupitia mikopo ya benki, hali inayochangia kuongeza ugumu wa maisha yao ya kila siku.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake sokoni hapo juzi, mfanyabiashara wa samaki katika soko hilo, Beda Amour alisema hali hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kuingiliana na msimu wa mavuno hasa maharage na baadhi ya mazao ya mboga hali inayochangia kupungua kwa wateja wa biashara hiyo.
Alisema tatizo lingine la kupungua kwa wateja ni bei kubwa ya samaki ikilinganisha na siku za nyuma kutokana na kupungua kwa maji katika Bwawa la Mtera, hali inayosababisha kuwepo kwa uhaba mkubwa wa samaki hivi sasa. Beda aliongeza kuwa idadi ya wateja katika soko la Manzese inapungua siku hadi siku kutokana na umbali kutoka katikati ya mjin hadi sokoni hapo na kuiomba Manispaa ya Songea kuweka utaratibu wa kuongeza maeneo kwa wafanyabiashara wengine tofauti na wauza samaki, nyanya, nazi na vitunguu ili kuongeza mvuto katika soko hilo.
Biashara ya samaki mjini hapa imekuwa ikishuka thamani kila inapofika mwezi wa tatu na nne kutokana na kuwepo kwa msimu wa mavuno ya mazao mengi mkoani Ruvuma, hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa baadhi ya biashara.
Dar City council loses Shs2bn in abbatoir scandal - The Citizen, Thursday, 29 March 2012
By. Frank Aman
Dar es Salaam, The Dar es Salaam City Council and Ilala, Temeke as well as Kinondoni municipalities have lost over Sh 2 bilioni to the collapsed East African Meat Company, which was contracted to constructed a modern abattor. According to the chairman of the Local Authorities Accounts Parliamentary committee (LAAC), Mr. Augustine Mrema, the four authorities privided the money as shareholders in the project.
figures indicated that the Dar es Salaam City Council owned shares worth Shs.1.5 bilion, Ilala Municipality shares were worth Shs.364 milioni, Temeke Municipality Shs.224 milioniwhile Kinondoni Municipality bought shares worth Shs.223 milion. but, since the money was paid to the company, the project has yet to take off and word is that the firm has already been liquidated. He said it was clear there were some people who should be prosecuted for embezzlement fo pbulic funds. "We know that there are some people who are involved in this issue and they use municipal council to implement bogus projects. We cannot let this to continue and anyone who would be found guilty will face legal action," said.
He added that apart from misusing Shs.2bilion the culprits are aslo involved in the Usafiri Dar es Salaam (UDA) company scandal whose report is yet to be presented to the government. He said his committee would prepare a report which would, among other things, call for investgations to identify those behind the scandal to have them prosecuted.
"It is impossible for a few people to use public money for their personal gain," he said.
Wafugaji wailaumu Tanga Fresh - Mwananchi, Alhamisi Machi 29, 2012
Na. Burhani Yakub, Tanga
Kiwanda cha kusindika bidhaa za maziwa cha Tanga Fresh, kimelalamikiwa na wafugaji kwamba kinawanyonya kwa kununua maziwa kutoka kwao kwa bei ya Shs.560 kwa lita, bei inayodaiwa kutokidhi gharama za uhudumiaji wa ng'ombe. Lawama hizo zilitolewa na wafugaji wakubwa na wadogo wa ng'ombe wa maziwa wa Mkoa wa Tanga, wakati wa mkutano wa mwaka wa jukwaa la wadau wa maziwa uliofanyika mjini hapa.
Wakizungumza mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Benedict Ole Kuyan ambaye alikuwa mgeni rasmi, wafugaji hao walisema, wakati kiwanda cha Tanga Fresh kikisifika ndani na nje ya nchi kwa kusindika bidhaa za maziwa zinazopendwa na walaji hali haiko hivyo kwa wafugaji. "ukiwaeleza viongozi wa Tanga Fresh ni wabishi na wanatuona wafugaji kama hatuna maana kwa sababu wao ndiyo wenye fedha" alilalamika Grace Mhando mfugaji kutoka Chama cha Msingi kilichopo Amboni wilayani Tanga.
Huku akipigiwa makofi na washiriki, Grace alisema ni ukweli kwamba wafugaji wanahitaji kiwanda cha Tanga Fresh tena wanaombea kiendelee kufanya kazi mkoani Tanga lakini wanachotaka ni kuboreshwa bei ili wajiendeshe kwa faida.
wafugaji hao kutoka vyama vya msingi vya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa kutoka wilaya mbalimbali Mkoani Tanga walisema walitegemea kwamba, ushirika wao TDCU ungeweza kufanya hivyo badala yake wanawaweka gizani kwani hawajui chochote.
Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Julius Shoo alisema kimsingi wafugaji wa ng'ombe wa maziwa wa Tanga wanahitaji mno kiwanda cha Tanga Fresh lakini kelele nyingi zinatokana na ushirika wa TDCU kushindwa kukisimamia ili waboreshewe zaidi bei.
Akizungumza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Ole Kuyan alisema kama Mtendaji Mkuu wa Serikali, ameazimia kuhakikisha sekta ya maziwa inakuwa na kumuongezea kipato cha uhakika mfugaji.
Moshi watakiwa kuchanja mifugo, Mwananchi , Alhamisi Machi 29, 2012
Na. Josephine Sanga, Moshi
Wafugaji wa Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, wametakiwa kuchanja mifugo yao ili kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya mifugo ikiwamo kimeta. Akitoa takwimu za chanjo juzi, Mtaalamu wa mifugo wa wilaya hiyo, Sakina Mhando alisema baadhi ya changamoto zinazokumba wilaya ni wafugaji wengi kutotambua umuhimu wa kuchanja mifugo yao.
Mhando alisema, umaskini na wafugaji kuogopa gharama za ununuzi wa dawa za chanjo, nayo ni changamoto nyingine inayokabili wilaya hiyo. Alisema bei ya kuchanja mfugo ni Shs.500 lakini wafugaji wengi hawachanji mifugo yao.
Alitaja idadi ya mifugo ambayo tayari imechanjwa dhidi ya kimeta kuanzia Februari 19 hadi Machi 23 mwaka huu kuwa ni 2,276.
Alisema ng'ombe ni 1,273, mbuzi 730, kondoo 171 na nguruwe 102 walipata chanjo hiyo kipindi hicho.
Wafugaji wapewa elimu Bukoba, Tanzania Daima, Ijumaa Machi 23, 2012
Na Antidius Kalunde, Bukoba
Wafugaji wadogowadogo wamepongeza uamuzi wa Mamlaka ya Ranchi za Taifa zinazojishughulisha na ufugaji wa ng'ombe kwa kuwanufaisha kwa njia ya kutoa elimu ya ufugaji ulio bora na wa kisasa.
Wakiongea na waandishi wa habari, wafugaji hao walisema utaratibu unaoendelezwa na kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) zilizo Kagoma, Kikurula, Missenyi na Mabare ni mzuri na wenye lengo la kumuinua mfugaji na mkulima ili kuondokana na umaskini.
Mmoja wa wafugaji hao, John Muganyizi (47) mkazi wa Karagwe alisema kuwa pamoja na wafugaji wengine katika maeneo mbalimbali mkoani Kagera kuwa na ujuzi wa kujiendeleza kiufugaji lakini utaratibu wa ranchi hizi ni mzuri zaidi kwani ni njia mbadala ya kumuelimisha mwananchi atambue umuhimu wa ufugaji na kilimo.
Muganyizi alisema kuwa hali ya ufugaji kwa wakulima ilikumbwa na changamoto kubwa hususan namna mbalimbali za kukabiliana na magonjwa ya mifugo, kubaini mbegu bora za ng'ombe zinazofaa katika ufugaj. Alisema kwa kuwa NARCO imeamua kuwapatia mafunzo wafugaji, ni vema wakazi wa Mkoa wa Kagera wakachangamkia fursa hii kwani ni muhimu na kwa kuelimika juu ya ufugaji janga la umaskini litapungua kwa kiasi kikubwa sana.
Tarsis Mawala, ambaye ni meneja wa Ranchi ya Missenyi, alisema utaratibu wa kutoa elimu ya ufugaji ni mojawapo ya majukumu ya NARCO na mwendelezo wa mipango ya Kampuni Kagera.
Mbunge: Hakuna mfugaji aliyerudi Ihefu Mbarali, Mwananchi, Ijumaa Machi 23, 2012
Na. Godfrey Kahango, Mbarali
Mbunge wa Jimbo la Mbarali, mkoani Mbeya, Dickson Kilufi amesema hakuna mfugaji aliyeondolewa na Serikali kupisha Hifadhi ya Taifa (TANAPA) katika Mbuga ha Ihefu wilayani humo aliyekaidi amri hiyo na kuanza kurejea tena kwenye hifadhi hiyo.
Kilufi alisema kumekuwa na gumzo kwa baadhi ya vyombo vya habari nchini na viongozi wa serikali maeneo mbalimbali kuwa wafugaji waliohamishwa mwaka 2007 na 2008 kupisha hifadhi hiyo wameanza kurudi kinyemela jambo ambalo siyo kweli.
Alisema madai hayo kimsingi hayana ukweli wowote na kwamba wafugaji wote walioko pembezoni mwa hifadhi hiyo ni wale ambao waliachwa nje ya mpaka wa hifadhi hiyo.
"Hakuna mfugaji aliyehamishwa na Tanapa ambaye amerudi tena akiwa na mifugo yake, hizo taarifa si za kweli na wanaotoa habari wanataka kuwakandamiza wafugaji walioko kisheria na walikubaliwa mifugo yao kuifuga wilayani hapa," alisema mbunge huyo.
Aidha, Kilufi alisema tatizo lililopo baina ya wafugaji na watu wa Tanapa ni kwamba hakuna mipaka inayoeleweka iliyowekwa na Serikali hali inayosababisha wafugaji kutojua mwisho wa eneo lao.
Lake Victoria basin plan set to improve people’s welfare, The Guardian Tuesday February 28, 2012
By Lusekelo Philemon, Arusha
Members of the East African Legislative Assembly (EALA) have concluded a six-day meeting on the assessment of the Lake Victoria Water Supply and Sanitation Programme Phase II (LVWATSAN II), calling on stakeholders to increase the pace of its implementation. Chairperson of EALA Committee on Agriculture, Tourism and Natural Resources, Safina Kwekwe Tsungu is confident that, if fully implemented, LVWATSAN II will greatly improve the livehoods of the people in the 15 targeted towns in the Lake Victoria Basin.
“The fact that people do not know the cause of delays in the programme is a major concern. Most of the misunderstandings focus on the interruption of information flow,” said Tsungu at a session in Kisumu Kenya.
Uvuvi Ziwa Victoria kusitishwa, Mwananchi Jumanne Februari 28, 2012
Na. Anthony Gervans, Magu
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinazopakana na Ziwa Victoria zimependekeza kusitisha uvuvi wa samaki katika ziwa hilo kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sita ili kuruhusu ongezeko la samaki katika ziwa hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarest Ndikilo alisema hayo mwishoni mwa wiki katika mwalo wa samaki wa Kigangana katika ziara yake ya siku moja wilayani Magu ya kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo.
Ndikilo alisema kuwa mapendekezo hayo yanakwenda sambamba na kufungwa kwa viwanda vya samaki katika nchi hizo tatu ili kuruhusu ongezeko la samaki Ziwa Victoria ambao wamepungua kwa kiasi kikubwa ziwani humo.
Katika Tanzania viwanda vya samaki vitakavyofungwa kwa Mkoa wa Mwanza ni Vicfish, Nile Pech, Tanzania Fish Processors (TFP), Omega na vingine vilivyokuwa vikipokea samaki kutoka katika ziwa hilo.
Alisema kusitishwa kwa uvuvi na kufungwa kwa viwanda hivyo kutasaidia kupungua kwa kasi ya uvuvi ziwani na kuboreka kwa ongezeko la samaki linalodaiwa kupungua na kuongeza kipato cha Serikali za nchi hizo mara uvuvi huo utakaporuhusiwa rasmi kuendelea na kufuguliwa kwa viwanda vyake. Katika ziara hiyo Ofisa uvuvi wa wilaya hiyo, Wenceslaus Luhasile alisema kuwa ipo mialo sita ilyoboreshwa kwa kiwango kikubwa katika mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa.
Alitaja mialo hiyo katika Mkoa wa Mwanza kuwa ni Kigangama na Kahunda, Mkoa wa Mara ni Bwai Musoma Vijijini na Sota wilayani Rorya na Mkoa wa Kagera ni Ikumbitale Chato na Marehe Bukoba Vijijini ambayo haitafungwa na itaendelea na uvuvi kwa ajili ya wananchi wa kawaida kupata samaki. Mialo hiyo kila mmoja uligharimu kiasi cha Sh588 milioni zilizotolewa kwa msaada wa Jumuiya za Nchi za Ulaya. Ofisa Luhasile alisema kuwa ipo mialo mingine iliyoboreshwa ambayo hupeleka samaki katika viwnda hivyo vitakvyofungwa ni pamoja na Chabula, Bukome, Ihale, Nyamikoma, Kashishi na Kigangama. Alisema mialo hiyo haitafungwa itaendelea kutumika kuvua samaki kwa ajili ya walaji wa kawaida pamoja na mialo mingine midogo midogo ambayo haijaboreshwa.
Watakiwa kusoma sheria za uvuvi, Mwananchi Jumanne Februari 28, 2012
Na. Salim Mohammed, TangaWavuvi wanaoendesha shughuli zao mwambao wa Bahari ya Hindi, mkoani Tanga, wametakiwa kusoma na kujua sheria za kazi yao ikiwamo kutambua zana zinazoruhusiwa, ili kuondoa migogoro inayozuka kati yao na maofisa wa maliasili.
Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa uvuvi kilichoandaliwa na Shirika lisilo la Serikali la Tanga Together Trust (TTT) , Ofisa Mfawidhi Kikosi cha Doria Kanda ya Kaskazini Mashariki, Obadia Ngogo, alisema wavuvi wengi wamekuwa wakikwepa kujiunga na vyuo vya uvuvi, hatua inayosababisha kuendelea kuvunja sheria na kusababisha mivutano na Serikali.
Ngogo alisema licha ya Serikali kuweka sheria kali za uvuvi, inaonekana wavuvi wengi wanashindwa kuziheshimu na kuongeza kuwa, kuanzia sasa ufuatiliaji leseni na uvuvi haramu utafanywa usiku na mchana.
"Jamani naomba tuambizane mapema ili tusije kuonana wabaya wakati tunapendana, kuanzia leo uvuvi haramu wa mabomu, utupa na mwingineo uwe mwisho, vinginevyo tutapelekana mahakamani," alisema Ngogo.
Alisema operesheni hizo zitasaidia kutunza rasilimali na uhai wa viumbe vya bhahari na kwamba, utakuwa mwisho wa uvuvi haramu kwa watu wenye tabia hiyo kwa kufungwa au kutozwa faini.
Awali, Ofisa Uvuvi Mkoa wa Tanga, Hasan Juma, alisema kuna baadhi ya maofisa tarafa kwa kushirikiana na watendaji wamekuwa wakiwalinda na kuwapa ushirikiano wavuvi haramu jambo ambalo kisheria ni makosa.
Juma alisema watendaji wa vijiji na wenyeviti wa serikali za mitaa wanapaswa kutoa ushirikiano katika mapambano ya uvuvi haramu, ambao umeshamiri mwambao wa Bahari ya Hindi. Alisema imebainika viongozi wa serikali za mitaa kwa kushirikiana na maofisa tarafa wamekuwa wakiwalinda wavuvi wanaotumia zana haramu, jambo ambalo ni kosa na kuwataka kuacha tabia hiyo vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.
Naye mdau wa uvuvi Makwaya Mwalimu aliomba serikali kuondoa utaratibu uliopo wa upatikanaji leseni kwa Dola ya Marekani, linawawia vigumu kupata fedha hizo na kuomba wawe wanalipa kwa shilingi.
Shehena ya mayai yakamatwa, HabariLeo Jumanne Februari 28, 2012
Na. Stella Nyemenohi
Shehena ya mayai imekamatwa jana katika maeneo ya Kitunda yakidaiwa kuingizwa Dar es Salaam kinyemela.
Bidhaa hiyo ilikutwa kwenye lori lenye namba za usajili T423BCQ mali ya Kampuni ya Morning Fresh Farms. Lori hilo baada ya kukamatwa lilipelekwa katika ofisi za Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kabla ya Waziri Dk. Mathayo David, kuamuru lipelekwe polisi wakati uchunguzi ukiendelea.
Alipohojiwa dereva wa gari hilo ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Morning Fresh Farms alitetea kuwa mayai hayo yanazalishwa katika ghala la kampuni lililoko Mkuranga, Pwani.
Dk. Mathayo alimwagiza Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Winston Mleche aondoke mara moja na maofisa wengine wa wizara kwenda Mkuranga kuungana na Ofisa Mifugo wa Wilaya ili kwenda kujiridhisha kama kwelini kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha shehena hiyo ya mayai kila siku na kuyaingiza jijini.
"Yawezekana huyu (Morning Fresh) hana kosa, anazalisha mwenyewe. Lakini kwa kuwa tumewakuta hawana kibali chochote cha kuruhusu kusafirisha mayai haya, na yapo madai kwamba kuna mayai yanayotoka nje, tunakwenda kuhakikisha isije ikawa naye anaingiza mayai kutoka nje. Mayai yanayoingizwa kutoka nje ni ya mbegu tu na siyo ya kula," alisema Waziri.
Wavuvi wa 'samaki wa Magufuli' jela miaka 20 - HabariLeo Ijumaa Februari 24, 2012
Ni wachina waliokamatwa wakivua jodari
Korti yaamuru meli itaifishwe na Serikali
Na. Regina Kumba
Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya Sh. bilioni 21 raia wawili wa China waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ) na kuwaachia huru wengine watatu.
Aidha, samaki waliokutwa kwenye meli hiyo hawatahusika na amri yoyote ya Mahakama hiyo kwa sababu Serikali ilishawagawa bure katika taasisi mbalimbali. Pamoja na adhabu hiyo, Mahakama pia iliamuru meli ya Tawaliq I ambayo ilitumika kwa uvuvi huo haramu itaifishwe na Serikali ya Tanzania, kwa sababu ilikuwa ikifanya shughuli hiyo ya uvuvi kwa majina mbalimbali.
Baadhi ya magazeti likiwemo hili, jana yalichapisha picha ya meli hiyo ambayo inaonekana kuanza kuzama karibu na bandari ya Dar es Salaam. Akisoma hukumu hiyo jana, Jaji wa Mahakama Kuu, Augustine Mwarija alisema anawatia hatiani mshitakiwa wa kwanza ambaye ni nahodha wa meli, Hsu Chin Tai na Wa saba, Zhao Hanquing ambaye ni wakala wa meli.
Uvuvi haramu unadumaza uchumi, Habarileo Jumatano Februari 8, 2012
Na. Anna Makange
Matukio ya uvuvi haramu wa samaki katika mwambao wa Bahari ya Hindi mkoani Tanga, yanaweza kupungua ikiwa ulinzi kwenye maeneo hayo utainishwa.
Ulinzi wa maeneo hayo ukiwepo utakomesha na kupunguza uvuvi haramu, ambaozo kama uvuvi halali ungefanyka, ungeliingizia taifa pato la uchumi.
Bungara aibana serikali kuhusu vifo vya mifugo, Tanzania Daima Februari 8, 2012
Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungara, maarufu kwa jina la Bwege (CUF0 ameitaka serikali kutoa kauli bungeni kuhusu malalamiko ya wananchi wa Songosongo kuhusu vifo vya mifugo yao.
Mbunge huyo alisema serikali bado haijatoa majibu ya kuridhisha kutokana na wananchi wa Kilwa Kusini, waliodai kuwa mifugo yao imekufa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa walikunywa maji yenye mabaki yaliyotokana na uzalishaji wa gesi asilia.
wafugaji wakimbia ukame Simanjiro, Nipashe Jumatano Februari 8, 2012
Na. Woinde Shizza, Manyara
Wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro mkoani hapa, wameanza kuhama kwenye vijiji vyao kukimbia ukame uliosababishwa na kutonyesha mvua.
Hayo yalibainika katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 35 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), Februari 5, mwaka huu yaliyofanyika kimkoa katika Kijiji cha Landanai Kata ya Naberera wilayani humo.
Sekta ya uvuvi kuendelezwa nchini, Nipashe Jumanne Februari 7, 2012
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, imesema serikali imeandaa mpango mkakati wa kuendeleza sekta ya uvuvi nchini ili kuboresha uzalishaji, maisha ya wavuvi wakiwemo vijana na kuongeza pato la Taifa.
Hayo yalisemwa a Naibu Waziri wake, Benedict Ole-Nangoro wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum (CUF) Amina Mohamedi Mwidau aliyetaka kujua Serikali ina mikakati gani ya kuendeleza sekta ya uvuvi mkoani Tanga.
Wafugaji wasononeka kuhamishwa Rufiji, Mwananchi - Jumanne Februari 7, 2012
Watu wa jamii za wafugaji wilayani Rufiji, wameelezea kusikitishwa kwao juu ya kile walichokieleza kuwa ni mpango wa halmashauri ya wilaya hihyo, kutaka waondolewe na kuhamishiwa katika mikoa mingine nchini.
Wafugaji hao ni pamoja na wale waliohamishiwa kutoka katika Bonde la Ihefu mkoani Mbeya ambao walisema pamoja na mambo mengine, mpango huo unalenga katika kuzididimiza familia zao kimaendeleo.
Mikindani na uvuvi wa kijadi! Mwananchi, Alhamisi Februari 2, 2012
Na. Charles Kayoka
nilipokuwa ufukweni mwa bahari mbele ya Mji wa Mikindani, Mtwara niliona kundi la vijana wengine wamesimama kulia na kushoto mwa hao vijana wapiga mateke wakishikilia nyavu. walipokuwa wakifanya hao wapiga mateke maji na kuwafukuzia dagaa na samaki kwenye nyavu ili wanase.
niliwasubiri hapo hadi walipokamilisha kazi na kuwatoa samaki kutoka kwenye nyavu. walikuwa wamejaa kwenye mfuko mdogo wa plastiki na walipowekwa kwenye sinia hawakuweza kufikia hata robo ya ujazo.
Mkoa wa Tanga wajipanga kudhibiti wavuvi haramu, Mtanzania - Jumatano Februari 1, 2012
Na. Susan Uhinga - Muheza
Serikali mkoani Tanga imejipanga kupambana na maharamia wanaofanya shughuli za uvuvi haramu wa kutumia mabomu na vifaa vingine visivyostahili vinavyohatarisha uwapo wa viumbe wa baharini.
Akizungumza na Serikali ya Kijiji cha Kigombe kilichopo wilayani Muheza katika mkutano wa dharura, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, alisema amelazimika kufanya ziara hiyo ya dharura kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uvuvi haramu.
Samaki wa Lubengela na athari kiusalama Ziwa Tanganyika, Mwanahalisi Jumatano Februari 1-7, 2012
Umati wenye uchu na wanunuzi umemzingira Mzee Masamaki, mmoja wa wavuvi wenye mafanikio katika Ziwa Tanganyika akiishi Lubengela katika Kitongoji cha Kirando Kigoma Vijijini.
"Watu wengi hapa ni wafanyabiashara na wavuvi wa samaki, hawashiriki shughuli za kilimo," anasema Alberto Ntumbala ambaye ni Afisa Maendeleo.
Kijiji hicho chenye wakazi wanaokadiriwa kufikia 6,800 ni mchanganyiko wa makabila ya Waha, Bembe Tongwe. Shughuli kubwa hapa ni ununuzi na uuzaji wa samaki katika soko la wazi. "Kama unataka kununua samaki huyu lipa shilingi elfu sabini" ni kauli ya Mzee Masamaki kwa wateja wake. Samaki wanaouzwa hapa ni sangara ambao uzito wake ni kati ya kilo 40 na 50.
Increase fish prices to stop illegal export – call, The Citizen Friday 27 January, 2012
Serikali mkoani Tanga imejipanga kupambana na maharamia wanaofanya shughuli za uvuvi haramu wa kutumia mabomu na vifaa vingine visivyostahili vinavyohatarisha uwapo wa viumbe wa baharini.
Akizungumza na Serikali ya Kijiji cha Kigombe kilichopo wilayani Muheza katika mkutano wa dharura, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, alisema amelazimika kufanya ziara hiyo ya dharura kutokana na kukithiri kwa vitendo vya uvuvi haramu.
Samaki wa Lubengela na athari kiusalama Ziwa Tanganyika, Mwanahalisi Jumatano Februari 1-7, 2012
Umati wenye uchu na wanunuzi umemzingira Mzee Masamaki, mmoja wa wavuvi wenye mafanikio katika Ziwa Tanganyika akiishi Lubengela katika Kitongoji cha Kirando Kigoma Vijijini.
"Watu wengi hapa ni wafanyabiashara na wavuvi wa samaki, hawashiriki shughuli za kilimo," anasema Alberto Ntumbala ambaye ni Afisa Maendeleo.
Kijiji hicho chenye wakazi wanaokadiriwa kufikia 6,800 ni mchanganyiko wa makabila ya Waha, Bembe Tongwe. Shughuli kubwa hapa ni ununuzi na uuzaji wa samaki katika soko la wazi. "Kama unataka kununua samaki huyu lipa shilingi elfu sabini" ni kauli ya Mzee Masamaki kwa wateja wake. Samaki wanaouzwa hapa ni sangara ambao uzito wake ni kati ya kilo 40 na 50.
Wafugaji Morogoro wahofia operesheni ya mifugo Agosti, Mwananchi - Jumanne Januari 31, 2012
Na. Juma Mtanda, Morogoro
Umoja wa Wafugaji katika Kanda ya Mashariki (Uwakama) umeishauri Serikali kusimamia kwa kikamilifu uhakiki wa idadi ya mifugo na kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo na mifugo katika vijiji vyote vya Wilaya za Kilombero na Ulanga.
Wilaya hizo zinaendesha operesheni ya kuwaondoa wafugaji na wakulima waliovamia mabonde na maeneo ya vyanzo vya maji vya Usangu na Kilombero.
Ranchi yapata Sh220mil kutoka kwa Wajapan, Mwananchi – Jumanne Januari 31, 2012
Na Hussein Semdoe, Handeni
Serikali ya Japan imemwaga msaada wa Shs220milioni, kuisaidia Ranchi ya Mzeri, iliyopo katika Tarafa ya Sindeni wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Msaada huo ambao ni matunda ya maombi yaliyofanywa na Ranchi hiyo ambayo ipo chini ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (National Ranching Company Limited), mwaka 2008 iliomba msaada kupitia Tanzania Japani Food Aid Counterpart Fund (TJFACF).
Tanzania kuongoza mkutano wa Laprovet, Mwananchi – Jumanne Januari 31, 2012
Na. Joseph Kapinga, Kibaha
Mkutano wa kwanza wa wadau wa kampuni ya kimataifa ya dawa za mifugo ya Ufaransa, Laplovet, unatarajia kufanyika kwa mara ya kwanza Ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki ambapo Tanzania itakuwa Mwenyekiti utakapofanyika nchini Kenya.
Mkutano huo umepangwa kuanza Juni 11 – 17 jijini Nairobi, Kenya ambapo Tanzania ni Mwenyekiti kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na kwamba itawakilishwa na Ephraim Massawe.
‘Serikali isihamishe wafugaji’, Mwananchi – Jumanne Januari 31, 2012
Na. Mussa Juma, Arusha
Serikali imeombwa kusitisha operesheni ya kuwaondoa wafugaji wilayani Kilombero mkoani Morogoro mpaka pale itakapopata eneo mwafaka la kuwahamishia.
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) mkoa wa Manyara, Rose Kamili alitoa wito huo jana wakati akizungumza na Mwananchi juu ya matatizo ya jamii ya wafugaji nchini na kauli za serikali kuwaondoa wafugaji wa Wilaya ya Kilombero.
Increase fish prices to stop illegal export – call, The Citizen Friday 27 January, 2012
By. Bernard Lugongo
The government has already started taking measures on the matter, including discussing with owners of the industries to raise the buing prices of the fish.
Parliamentary Public Accounts Committee (PAC) has called on the ministry of Fisheries and Livestock Development to focus more on increasing wholesale prices of fish to processing industries to tackle illegal exportation.
This comes in the wake of revelations that fishermen illegally export large amounts of fishes to industries in enighbouring Kenya and Uganda where the prices are higher than in Tanzania.
Fahamu ugonjwa wa sotoka kwa wanyama, Tanzania Daima – Alhamisi, Januari 26, 2012
Na. Asha Bani
Moja ya changamoto inayoikabili Wizara ya Mifugo ni kuendeleza na zoezi la ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko kati ya wanyama wafugwao na wanyamapori katika mazingira ya muingiliano wa wanyamapori na mifugo.
Mwaka 1982 hadi 1984 Tanzania ilipata mlipuko wa ugonjwa wa Sotoka ambao huwambukiza wanyama na unasababishwa na virusi aina ya morbilivirus.
Carbon Dioxide inadhuru ubongo wa samaki, Tanzania Daima – Alhamisi Januari 26, 2012
Na. Canberra, Australia
Upo msemo maarufu kwa upande wa Kanda ya ziwa unasema kwamba: “Nyanja itanabhulongo,” wakimaanisha kwamba ziwa halina uchawi, yaani kila kitu unachokiweka ndani ya ziwa kinachukuliwa na maji.
Kutokana na msemo huo kumekuwa na watu wengi wanaoishi pembezoni mwa ziwa au habari wanaolalamika kwamba wenye viwanda huelekeza maji yenye taka za sumu ndani ya maji.
Ufugaji umeniepusha kukaa vijiweni: Asema kinachomtatiza ni mkopo, Tanzania Daima, Jumanne Januari, 24, 2012
Na. Julieth Mkireri, Bagamoyo
Kila siku watanzania wamekuwa wakiamka na jipya huku kila jambo likiwa na sura yake. Kwa upande wa ukosefu wa ajira, hii imekuwa kama wimbo wa taifa kwani kila unapopita neno ni ajira halikauki katika midomo ya watanzania.
Mohamed Mbakwe, Mkazi wa Kijiji cha tonga, Kata ya Msoga, anazungumzia suala la kujiari mwenyewe kupitia ufugaji wa kuku ambao kwa kiasi kikubwa umemsaidia kutatua matatizo yake badala ya kukaa vijiweni na vijana wenzake bila shughuli yeyote.
Mbakwe ambaye ameanza kufuga kuku wa kienyeji mwaka 2009 baada ya kutembelea maonyesho ya wakulima Morogoro na kuvutiwa na ufugaji huo.
Wavuvi 51 watekwa nchini Kenya, Majira, Alhamisi Januari 19, 2012
Na. Ali Kombe
Watanzania 51 ambao ni wakazi wa Kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wanashikiliwa na polisi katika kituo cha Polisi Malindi Kenya kwa tuhuma za kufanya shughuli za uvuvi nchini humo bila ya kufuata sheria za nchi hiyo na walitarajiwa kupandishwa kizimbani jana.
Miongoni mwa Watanzania hao, Bw. Massoud Mzimba Hamad ambaye alifanikiwa kuwatoroka askari hao wa Kenya wakati akizungumza na Majira jana kijijini hapo alisema, mara baada ya kushikiliwa na polisi hao walikuwa wananyanyaswa huku wakishindwa jambo la kufanya.
Fishing malpractices deplete fish stocks in Moshi dam, The Guardian , Friday January 13, 2012
Na. Ali Kombe
Watanzania 51 ambao ni wakazi wa Kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wanashikiliwa na polisi katika kituo cha Polisi Malindi Kenya kwa tuhuma za kufanya shughuli za uvuvi nchini humo bila ya kufuata sheria za nchi hiyo na walitarajiwa kupandishwa kizimbani jana.
Miongoni mwa Watanzania hao, Bw. Massoud Mzimba Hamad ambaye alifanikiwa kuwatoroka askari hao wa Kenya wakati akizungumza na Majira jana kijijini hapo alisema, mara baada ya kushikiliwa na polisi hao walikuwa wananyanyaswa huku wakishindwa jambo la kufanya.
Oparesheni kuondoa mifugo kutikisa Moro, Nipashe Jumanne Januari 17, 2012
Na. Ashton Balaigwa, Morogoro
Mkoa wa Morogoro umetangaza mpango wake wa kuendesha Operesheni ya kuondoa mifugo iliyoingizwa katika wilaya zake zote kinyume na utaratibu.
Ni baada ya kupata Baraka kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kuupa kibali cha kuendesha operesheni hiyo ili kuondoa mifugo hiyo baada ya kusababisha malalamiko kwa wakulima kutokana na wafugaji kugeuza mashamba ya malisho.
Fishing malpractices deplete fish stocks in Moshi dam, The Guardian , Friday January 13, 2012
By Guardian Reporter, Moshi
Fish catches at the Nyumba ya Mungu dam have fallen from 8,851 tonnes to 1,770 tonnes per year due to diminishing fish populations caused by bad fishing practices, including requent use of explosives and undersized fishnets.
This was said by Kilimanjaro Regional Commissioner (RC) Leonidas Gama in his opening speech at the 13th regional consultative meeting.
He said the trend was threatening the Nyumba ya Mungu ecosystem and called fro cooperation with the government.
Stiegler’s Gorge: Hirizi ya wazi ya kumaliza tatizo la umeme nchini, Rai, Alhamisi Novemba 24 – 30, 2011
Na. Joshua Mbwambo
♦ Lakini wingi wa mifugo, mabadiliko ya tabianchi vyavuta miguu ya juhudi tarajiwa
Oktoba 2006, takribani mwaka mmoja tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani, lilitokea tukio ambalo si la kawaida kwa watumiaji wa mitandao ya kompyuta katika Tanzania.
Tukio hilo ni lile la kikundi cha Watanzania kuanzisha tovuti na kuitumia kukusanya saini za wananchi za kuishinikiza Serikali ya Rais Kikwete kuutekeleza mradi wa kuzalisha umeme wa maji wa Stiegler’s Gorge, kwa imani kwamba ndio ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la mgao wa umeme nchini.
Mifugo bado yakabiliwa na matatizo mengi, Habarileo Alhamisi Novemba 24, 2011
Na. Jasmin Shamwepu
Zaidi ya asilimia 90 ya mifugo ya nyama nchini, ambayo ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku na nguruwe huzalishwa katika mifumo ya asili.
Hali hiyo inafanya ufugaji kuwa sehemu ya maisha ya wafugaji na mifugo kuwa na thamani kubwa kuliko mazao yao.
Kutokana na thamani kubwa ya mifugo, uvunaji hufanyika kwa dharura, hasa kwa kuondoa mifugo iliyodhoofu au kuzeeka ili kukidhi mahitaji ya kifedha ya familia na siyo mpangilio wa kibiashara.
Govt to divide ranches into blocs: Nangoro, The Citizen Thursday 10 Novemba, 2011
By. Daniel Msangya
Dodoma. The government has made a decision to divide national ranches into blocs with sizes of between 2,000 and 4,000 hectares and allocate them to private investors.
The investors would be required to establish modern cattle keeping projects in the blocs, the parliament heard said yesterday.
Walio eneo la ranchi waongezewa ardhi, Habarileo Alhamisi Novemba 10, 2011
Serikali imesema imeanza kushughulikia migogoro ya ardhi iliyojitokeza kwa wananchi wanaopakanana ranchi za Kitengule, Kagoma na Misenyi kwa kuviongezea vijiji vya maeneo hayo ardhi zaidi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri aliyasema hayo bungeni jana wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM) aliyetaka kufahamu hatua zilizochukuliwa na Serikali kumaliza mgogoro huo.
Nangoro: Sioni sababu za kuwanyang’anya ranchi wawekezaji, Mtanzania Alhamisi Novemba 10, 2011
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifug o na Uvuvi, Benedict Ole Nangoro amesema haoni sababu ya kuwanyang’anya wawekezaji vitalu katika Ranchi za Taifa za NARCO ambao hawajakiuka masharti ya umiliki.
Akijibu swali bungeni jana Nangoro, alisema vitalu hivyo kwa sasa vinamilikiwa halali na kisheria kwa wawekezaji na vijiji.
Kambi za uvuvi Ukerewe zimeajiri watoto – Hakimu, Majira Alhamisi Novemba 10, 2011
Na. Jovither Kaijage
Watoto walioajiriwa katika kambi za uvuvi, Wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza wanalazimika kuvuta bangi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Hakimu mkazi mfawithi wilayani humo Bw. Rouben Luhasa aliyasema hayo juzi katika semina ya siku tano iliyoshirikisha wasaidizi 15 wa sheria wilayani humo ambayo imeandaliwa na Shirika la Adilisha lenye makao yake mkoani humo.
Wafugaji Kilombero sawa na viwavijeshi, Rai Alhamisi Novemba 10-16,2011
Na. Johnson Mbwambo
Sasa wanapatikana japo kwa idadi tofauti, katika kila bonde la mito mikubwa nchini na kwenye vyanzo vikubwa vya maji vyenye nyasi za kijani.
Na kila mifugo yao inapomaliza kuzitafuna nyasi hizo za kijani, huiondoa na kuanza safari nyingine kuelekea kwenye chanzo kingine cha maji na kwenye nyasi nyingine za kijani zaidi.
Mbunge: Kenya wanafanya utalii, uvuvi haramu Pemba, Majira Jumatano Novemba 9, 2011
Mbunge wa Mfenesini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, Bw. Nassib Suleiman Omar (CCM) ameitaka Serikali kutoa kauli kama inafahamu raia wa nchi ya jirani Kenya wanafanya utalii na uvuvi haramu katika eneo la Pemba kwa kutumia mabomu na nyavu zenye matundu madogo.
Pia Bw. Omar alitaka kujua hatua zilizochukuliwa kuzuia utalii na uvuvi huo na kama ipo tayari kuliwasilisha suala hilo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kupata uamuzi.
Mkurugenzi Rufiji ashiriki kukamata ng’ombe 150, Mwananchi Jumatano Novemba 9, 2011
Na. Amin Yasin, Rufiji
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Nassoro Mwingira akiwa na maofisa wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya wamekamata ng’ombe 150 waliokuwa wakishushwa eneo la mwisho wa lami wilayani hapa, badala ya kwenda mkoani Lindi kama vibali vinavyoonyesha.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mifugo hiyo ilipofika mwisho wa lami madereva wa magari hayo walisema kulingana na makubaliano mifugo hiyo ilikuwa ishushwe eneo hilo, hivyo kama wanataka kuongeza safari yafanyike maelewano mapya.
Ferry walilia sheria kuunda bodi, Mwananchi Jumanne Novemba 8, 2011
Na.Pendo Pinda na Latifa Mgeni
Mwenyekiti wa Soko la Samaki Fery, Rajabu Mng'oi ameitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kuharakisha mchakato wa kisheria wa uundaji wa bodi ya soko hilo, vinginevyo atalifikisha suala hilo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mng'oi alisema rasimu ya mwaka 2004 ya muswada wa sheria, ililenga uundaji wa sheria ambayo ingepelekea soko kuunda bodi, hatimaye kujiendesha yenyewe bila kutegemea halmashauri.
Uvuvi haramu wa jodari wabainika Libya, HabariLeo Jumanne Novemba 8, 2011
Habari hii pia inapatikana gazeti la Mtanzania Jumanne Novemba 8, 2011
Ushahidi umebainika wa kuwapo kwa uvuvi haramu wa samaki aina ya jodari katika bahari ya Libya wakati wa mapigano yaliyokuwa yameigubika Libya.
Ishara zilizorekodiwa kutoka visanduku vyeusi vya boti zinanaonesha kuwapo kwa kiwango kikubwa ndani ya maji ya Libya cha mazalia ya jodari wenye mapezi ya bluu ambao wako hatarini kutoweka.
Washtakiwa wizi wa ngozi Arusha kukamatwa, Mwananchi Jumatatu Novemba 7, 2011
Na. Happy Lazaro, Arusha
Habari hii pia inapatikana gazeti la Majira Jumatatu Novemba 7, 2011
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imeamuru kukamatwa kwa watuhumiwa wa kesi ya wizi wa ngozi za mamilioni ya fedha, mali ya Kampuni ya Salex Limited ya jijini hapa na kuhakikisha wamefikishwa mahakamani siku ya kesi hiyo.
Tayari, hati ya kukamatwa washtakiwa hao ilishatolewa. Wanaotakiwa kukamatwa ni Patricio Icioni Raia wa Italia na Jamal Abdul Wadood, Raia wa Kenya.
Sangara wachanga 900 wakamatwa Mwanza, Mtanzania Jumatano Novemba 2, 2011
Kikosi cha doria cha Idara ya Uvuvi mkoani Mwanza kimekamata sangara wachanga zaidi ya 900 kwenye gati la kufikishia samaki katika kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Vickfish kandokando ya ufukwe wa Ziwa Victoria, jijini Mwanza.
Samaki hao ambao uzito wao haukuweza kufahamika mara moja, walikamatwa Oktoba 28, mwaka huu usiku muda mfupi baada ya boti ya wakala anayesambazia kiwanda hicho samaki kutia nanga kwenye gati hilo.
Waagizwa kuwatimua wafugaji, Mwananchi Jumatano Novemba 2, 2011
Na. Hussein Semdoe, Handeni
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, imeagiza serikali za vijiji na kata wilayani humo kuwatimua wafugaji waliovamia katika maeneo yao kinyume na taratibu zilizopo.
Mbali na amri hiyo ya kuwatimua wafugaji hao, serikali hizo pia zimetakiwa kuepuka kufanya mazungumzo yoyote na watu hao, ambao wanadaiwa kuwa hodari wa kutoa rushwa kwa viongozi mbalimbali wa vijiji na kata ili kuwatafutia makazi katika maeneo yao.Kizimbani kwa vifaa haramu vya uvuvi, Mwananchi Jumatano Novemba 2, 2011
Na. Hadija Jumanne
mfanyabiashara wa samaki Banza Khalid (30) amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam kujibu shtaka la kupatikana na vifaa vya mlipuko vya kuvulia samaki.
Banza mkazi wa Mbagala jijini anayefanya biashara soko la Feri alifikishwa katika Mahakama hiyo kujibu shtaka linalomkabili la kukutwa na vifaa hivyo, ikiwamo sumu ya kuulia samaki kinyume cha sheria.
Manispaa ya Kinondoni imewaagiza wataalamu wa mifugo kusaidia katika utungaji na usimamizi wa sheria ndongondogo kuwadhibiti watu wanaokwepa kuchanja mbwa kila mwaka.
Hayo yalisemwa na Naibu Meya wa manispaa hiyo Songoro Mnyonge, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya kichaa cha mbwa duniani, yaliyofanyika Mbezi katika Manispaa hiyo.
Wizara kukabili uvuvi haramu, Mtanzania Jumatatu Oktoba 31, 2011
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar, imejipanga upya kupambana na uvuvi haramu uliojitokeza hivi karibuni, anaripoti Salma Lusangi kutoka Zanzibar .
Uvuvu huo haramu umejitokeza katika maeneo ya hifadhi ya ghuba ya Menai, Chwaka na Kisiwa cha Mnemba na hifadhi ya Bahari ya mkondo wa pemba.
Wavuvi watishia kumburuza mahakamani DC, Nipashe Jumatatu Oktoba 31,2011
Na. Anceth Nyahore
Habari hii inapatikana gazeti la MtanzaniaDaima Jumatatu Oktoba 31, 2011
Wavuvi wadogo katika bwawa la New Sola, katika wilaya ya Maswa mkoa wa Shinyanga, wametishia kumburuza mahakamani Mkuu wa Wilaya hiyo, Kampteni Mstaafu James Yamungu kwa madai ya kuharibu na kisha kuichoma moto mitumbwi na nyavu zao.
Hatua hiyo inayoungwa mkono na wabunge wa majimbo ya Maswa Mashariki Slyvester Kasulumbai na wa Maswa Magharibi John Shibuda (wote chadema) inatokana na mkuu huyo wa wilaya kudaiwa kuchoma mitumbwi 16 ya wavuvu Oktoba 25 mwaka huu ikiwa na thamani ya jumla ya shs. Milioni 16 ambazo wanataka kulipwa fidia mahakamani.
Elimu juu ya kichaa cha mbwa ni muhimu, Habarileo Jumatatu Oktoba 31, 2011
Na. Grace Chilongola
Kampeni ya kuelimisha umma wa watanzania na dunia juu ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa, sambamba na utoaji wa chanjo bure ili kukabiliana na ugonjwa huo, hufanyika Septemba kila mwaka.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya ya Wanyama Duniani, (OIE) na Shirika la Afya Duniani (WHO) watu 55,000 hufariki kila mwaka duniani Kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa, ambapo 21,000 kati ya hao hutoka Afrika.
Muleba wanunua boti kudhibiti magendo, Nipashe Jumamosi Oktoba 29, 2011
Na. George Ramadhani, Mwanza
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera imeelezea kufurahishwa kwake na hatua ya kukamilika kwa ujenzi wa boti iendayo kasi ambayo itasaidia utoaji wa huduma za kijamii, kudhibiti magendo na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato.
Boti hiyo ambayo imewasili wilayani humo kutokea jijini Mwanza imetengenezwa na Kampuni ya Sam & Anzai Boat Builders Ltd ya jijini Dar es Salaam kwa Sh. Milioni 91 zikiwamo Sh. Milioni 60 zilizotolewa na Serikali Kuu kama msaada.
Wavuvi wajitosa kilimo cha mbogamboga, Nipashe Jumamosi Oktoba 29, 2011
Na. Said Hamdani, Mtwara
Wakazi wa Kata ya Ziwani, wameanzisha mradi wa kilimo cha mboga mboga unaotarajiwa kutumia Shs.46,920,000.
Ni baada ya kufanya shughuli za uvuvi kwa muda mrefu bila ya mafanikio. Mradi huo utahusisha vijiji saba vya kata hiyo na kunufaisha kaya 2,825 za wakazi hao wa ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi.
Vijiji Kilosa vyashauriwa kuwabana wafugaji, Mwananchi Jumamosi Oktoba 29, 2011
Na. Habiba Yahya, Morogoro
Serikali za vijiji wilayani Kilosa zimeshauriwa kutunga sheria ndogo zitakazosaidia kuwabana wafugaji wanaolisha mifugo mashambani na kuzorotesha jitihada za wakulima kuondokana na umaskini.
Rai hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego, katika hotuba yake ya kuhitimisha mradi wa kilimo uliokuwa unatekelezwa na Shirika hilo la Kiserikali la kuhifadhi Mazingira mkoani Morogoro.
Kiwanda cha maziwa chasifiwa, Jambo Leo Jumatano Oktoba 26,2011
Kamati ya Bunge Viwanda na Biashara imesifu jitihada zinazofanywa na Kiwanda cha Maziwa cha Asas Dairies Ltd cha Iringa kwa kukuza ajira kwa wakazi wa mkoa huo.
Kamati hiyo imesema sekta ya viwanda na biashara imekuwa ni moja kati ya sekta nyeti katika Taifa kwa ukuzaji wa ajira na kutaja kiwanda hicho kuwa ni chachu ya maendeleo eneo hilo .
Serikali yahofia kupungua samaki Ziwa Victoria, HabariLeo Jumatano Oktoba 26,2011
Na. Prisca Libaga, Maelezo Arusha
Habari hii pia inapatikana gazeti la Mtanzania, Oktoba 26, 2011
Serikali imewataka wanasayansi kuongeza kasi ya utafiti katika Ziwa Victoria ili kuokoa kasi ya kupungua kwa samaki katika ziwa hilo hususan aina ya Sangara.
Mwito huo wa Serikali umetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Nyamurunda alipofungua mikutano wa siku tatu wa Chama cha Wanasayansi wa Uzalishaji wa Mifugo kutoka ndani na nje ya nchi.
Kweka: Mdau wa ngozi anayeishauri serikali kuiwezesha sekta hiyo nchin, Mtanzania Jumanne Oktoba 25, 2011
“Kwa muda mrefu sasa hatuna chuo cha kufundisha na kuwaandaa wataalamu namna ya kusindika ngozi jambo ambalo limekuwa tatizo kwenye sekta nzima na pengine ni kwambie kuwa mojawapo ya malengo yangu mbeleni ni kuanzisha mafunzo hayo kwa vijana wa kitanzania”, hivyo ndivyo anavyoanza kusema Condrad Kweka mjasiliamali ambaye ameamua kuanzisha utengenezaji wa vitu mbalimbali kwa kutumia ngozi ambayo anaisindika mwenyewe kwa njia ya asili kupitia kampuni yake ya Asilia Ltd.
Tayari mjasiliamali huyo ameanzisha kampuni hiyo maeneo ya Njiro nje kidogo ya jiji la Arusha, biashara ambayo kwa maoni yake inahitaji kuwezeshwa na taasisi mbalimbali kiserikali ili kuipa nguvu sekta ya usindikaji ngozi na vifaa vyake hapa nchini ikiwa ni sehemu pia ya kuviinua viwanda vidogo hapa nchini.
Wavuvi waomba kupunguziwa kodi Majira Jumatatu Octoba 24,2011
Na Jovither Kaijage, Ukerewe
Habari hii inapatikana pia katika Nipashe 0ctoba 24, 2011.
Wavuvi katika wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza, wamemuomba mbunge wa jimbo hilo Bw. Salvatory Machemli aishawishi serikali ipunguze kodi wanazotozwa kwa mwaka ili waweze kumudu gharama za maisha na kujikomboa kiuchumi.
Ombi hilo limetolewa juzi katika mikutano wa hadhara uliofanyika eneo la Nakutunguru mjini Nansio.
Waziri Mathayo njoo Mwanza- wafanyabiashara Mtanzania Jumapili octoba 23, 2011
Na. john Maduhu Mwanza
Wafanyabiashara wa samaki aina ya sangara, wamemtaka Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Mifugo Dr. Mathayo David kuingilia kati ili kuokoa kutoweka kwa samaki aina ya sangara Kutokana na kukithiri kwa uvuvi haramu katika ziwa Victoria .
Akizungumza na Mtanzania Jumapili jiji ni Mwanza Mwenyekiti wa muungano wa wafanya biashara wa samaki Tanzania (TAFU), Benjamin Bastola alisema katika muda mfupi viwanda vya samaki vitafungwa na kuleta janga kubwa kwa wananchi wanaotegemea biashara ya minofu ya samaki ya sangara.
Zijue mbinu bora za ufugaji samaki – 2, Nipashe Ijumaa Oktoba 21, 2011
Katika iliyotangulia tuliangalia suala la ufugaji wa samki ambapo wote, wale wa maji chumvi na baridi wanafugika. Cha muhimu ni kujenga bwawa linaloendana na mazingira halisi ya samaki husika.
Hata hivyo mwandishi amesisitiza umuhimu wa ujenzi bora wa mabwawa, ambao samaki wataishi. Mahali panapofaa kujenga bwawa la samaki ni pale ambapo pana maji ya kutosha ambayo hayakauki.
Wanajamii wachangia kuhifadhi, kuongeza idadi ya Kasa, Kulikoni Ijumaa Oktoba 21, 2011
Na. Marko Gideon
Uhifadhi wa viumbe hai wa Bahari walio katika hatari ya kutoweka uliyojikita katika jamii umefanikiwa kuongeza idadi ya kasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ya Tanzania tangu mwaka 2009.
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Mradi wa Kuhifadhi Kasa wa kijiji cha Ushongo wilayani Pangani, Kikundi cha Marafiki wa Maziwe na shirika la hifadhi za viumbe wa Bahari la Seasense zinaonesha kuongezeka kwa idadi ya kasi walioanguliwa na viota tangu mwaka 2009.
Wafugaji wa Kitaturu waamua kwenda shule, Uhuru Ijumaa Oktoba 21, 2011
Na. Chibura Makorongo, Shinyanga
Katika hali isiyo ya kawaida, jamii ya wafugaji ya jamii ya Kitaturu iishiyo wilayani Kishapu mkoani hapa, imeamua kutumia utajiri iliyo nayo kupambana na adui ujinga kwa kuanza kusoma.
Aidha, wafugaji hao wameiomba serikali kusaidia katika kufanikisha azma yao hiyo.
Jamii hiyo iliyoko kando ya ziwa Kitangiri katika kijiji cha Magalata kata ya Mwamalasa wilayani hapa imeanza kuandikisha watoto wao katika shule za awali, msingi na MEMKWA.
Uelewa wa hifadhi za Bahari waongezeka Mtwara, Habarileo Ijumaa Oktoba 21, 2011
Na Kennedy Kisula
Wananchi wwilaya ya Mtwara mkoani Mtwara wameanza kuelewa sasa umuhimu wa kuhifadhi rasilimali za nchi kavu na Bahari.
Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi za Bahari (Marine Park ) Mtwara, Redfred Ngowo, anasema jamii inaelewa zaidi kuhusu masuala hayo ya hifadhi kuliko mwaka 2003. anasema miaka hiyo, ilikuwa vigumu kuhifadhi rasilimali za nchi kavu na baharini.
“Marine Park ilianza kazi ukanda mto wa Ruvuma kwenye vijiji vipatavyo 12, sasa vipo 18. vijiji vingi viliomba kwa hiari yao wenyewe kutaka kuhifadhi maeneo yao ya Bahari baada ya kuona vingine vikinufaika kwa kupewa miradi mbalimbali ya uvuvi na kijamii” anasema Ngowo.
Wafugaji waiomba kampuni iwalipe fidia ya Mifugo yao, Majira Alhamisi Oktoba 20, 2011
Na. Rehema Maigala, Kilwa
Baadhi ya wafugaji katika Kisiwa cha Songasonga Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi wameiomba Kampuni ya Ndovu Limited inayohusika na uchimbaji wa gesi asilia katika eneo hilo , kuwalipa Mifugo yao ambayo ilikufa Kutokana na kunywa maji yaenye sumu.
Maji hayo yalikuwa na sumu iliyomwagwa na kampuni hiyo wakati ikizalisha gesi asilia jirani na makazi yao .
Dar es Salaam Zoo yaja na teknolojia ya kuzalisha ng’ombe: Hutoa lita 43.5 za maziwa kwa siku, Tanzania Daima Alhamisi Oktoba 20, 2011
Na. Dina Ismail
Sekta ya ufugaji nchini meendelea kupata mafanikio baada ya kuzaliwa kwa ndama watatu waliotokana na mbegu iliyoagizwa kutoka Finland maalumu kwa kuzalisha majike tu.
Mbegu hiyo ijulikanayo kwa jina la kitaalamu la “Gender Selected Semen’ (uhamilishaji) itawezesha ng’ombe hao kuwa na uwezo wa kuzalisha lita 43.5 za maziwa kwa siku.
Mwani unavyotumika kusindika vyakula, JamboLeo Alhamisi Oktoba 20, 2011
Na. Claudia Kayombo
Mwani ni aina ya zao ambalo hustawishwa majini kwa kuwa haliwezi kuhimili nchi kavu. Hustawi katika maji chumvi ama baridi.
Mmea huu hupandwa ndani ya Bahari, maziwa, mabwawa, malambo na hata katika mito . Mwani kisayansi huitwa ‘algae’ tofauti na mimea mingine inayoishi nchi kavu, mmea huu hautegemei mizizi kufyonza maji na virutubisho vingine, wala shina lake halitumiki kusafirisha virutubisho kupeleka katika mmea husika.
Kiwango cha uvuaji samaki chaongezeka, HabariLeo Jumatano Oktoba 19, 2011
Na. Anna Makange, Tanga
Kiwango cha samaki wanaovuliwa mkoani Tanga kimeongezeka kutoka tani 7,025 mwaka 2006 hadi tani 17,212 mwaka 2010 kutokana na mafanikio ya ukuzaji na utunzaji wa viumbe na mazingira katika maji.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Benedict Ole Kuyan alisema hayo jana wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi ya mkoa kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi inayoendelea na ziara ya siku tano mkoani humo.
Wafugaji Kilosa waapa hatuporwi Mifugo tena, Mwanahalisi Jumatano Oktoba 19-25, 2011
Na Yusuf Aboud
Mfugaji mmoja wa asili ya Maasai, anayeitwa Laini Kisau ni “mali sana ” kwa serikali wilayani Kilosa. Ni chimbuko la fedha.
Ukitaka kujua zaidi, chunguza tarakimu zifuatazo, anakamatwa, anatozwa faini, analipa, anakamatwa, anatozwa faini, analipa.
Kwa ufupi anakamuliwa. Yeye anakamua ng’ombe kupata maziwa, lakini serikali inamkamua yeye kupata fedha.
Wafugaji wakubaliana kuhusu mipaka ya ardhi, Mwananchi Jumanne Oktoba 18,2011
Na. Mussa Juma, Loliondo
Habari hii inapatikana gazeti la Habari Leo Jumanne Oktoba 18, 2011
Watu wa jamii za Wasonjo na Wamasai, wanaogombea ardhi katika eneo la Kisuyaswi, linalopakana na vijiji vyao, wamefikia makubaliano kuhusu mipaka ya ardhi waliyokuwa wakigombea kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
Mgogoro wa ardhi katika eneo hilo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 15 katika kipindi hicho.
Wafugaji Manyoni wanahitaji hamasa zaidi kuthamini elimu, Mwananchi Jumanne Oktoba 18, 2011
Na. Awila Silla
Nani anasema elimu ndiyo ufunguo wa maisha? Inawezekana msemo huu ukawa Sahihi kwa watu wengine, lakini siyo watu wa jamii ya kifugaji hasa waishio wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida.
Pamoja na kuwapo kwa juhudi za Serikali na wadau kuhamasisha elimu kwa jamii hiyo inayojumuisha makabila ya Wasukuma na Wakitaturu, ikiwamo ujenzi wa shule kwa ajili ya watoto, wazazi wengi ndiyo wanaochangia watoto wao kukosa fursa za elimu.
Mifugo yatakiwa kupunguzwa, Jambo Leo Jumatatu Oktoba 17, 2011
Na. Peter Kimath, Morogoro
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imewapatia mafunzo wafugaji 50 juu ya ufugaji bora wa kisasa na kuwashauri wapunguze Mifugo.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, amiri Nondo alibainisha hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari mjini hapa juu ya Mifugo inayohitajika kuwepo katika manispaa hiyo.
Ng’ombe Lushoto wapatiwa chanjo, HabariLeo Jumatatu Oktoba 17,2011
Na. Anna Makange, Tanga
Zaidi ya ng’ombe 8090 kati ya 2,000 walioko kwenye Kata ya Ubiri wilayani Lushoto katika Mkoa wa Tanga, wamepatiwa chanjo ya kuzuia magonjwa ya kimeta na chambavu yanayohofiwa kuingia kwenye baadhi ya vijiji katika mikoa inayopakana na Tanga.
Ofisa Mifugo wa Wilaya anayeshughulikia Kata ya Ubiri, Anna Temu akizungumza jana na gazeti hili, alisema hatua hiyo inalenga kutoa kinga kwa Mifugo hasa ng’ombe ambao ni wepesi kuambukizwa na kushambuliwa kwa urahisi na magonjwa hayo.
Mnada wa samaki wa uvuvi haramu katika soko la Feri, Mwananchi Jumamosi Oktoba 15, 2011
Na. Mary Mahundi
Wiki iliyopita mwandishi Mary Mahundi aliandika katika makala katika safu hii juu ya tuhuma zinazolikabili soko la Kimataifa la Samaki, Feri dare s Salaam kwamba linatumika kuendesha mnada usiku wenye utata ambao unahusisha samaki waliovuliwa kwa baruti ambao umedaiwa pia kuwahusisha baadhi ya polisi na askari wa majini wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mnada huo unadaiwa kufanyika katika eneo liitwalo Zone Namba nane maarufu “Lebanon ” kati ya saa moja na saa tano usiku, kila siku. Leo makala haya yanaangalia pamoja na mambo mengine, hali halisi katika soko hilo .
Mfugaji auza ng’ombe kuwapa rushwa polisi, HabariLeo Ijumaa Oktoba 14, 2011
Na. abby Nkungu, Singida
Mkuu wa Kituo cha Polisi Iyumba na askari wa upelelezi katika kituo hicho, wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa mfugaji walyembambikizia kesi.
Mkuu huyo, Koplo Lukololo na askari Konstebo Joseph Pazza, wanadaiwa kuchukua fedha za mfugaji huyo, Shigela Nkonga baada ya kumpekua na kumtuhumu kumkuta akimiliki silaha kinyume cha Sheria.
Kichaa cha mbwa huua watu 55,000 kila mwaka, Tanzania Daima Alhamisi Oktoba 13, 2011
Na. Tamali Vullu
Ugonjwa wa Kichaa cha mbwa (Rabies) unasababishwa na virusi na huwapata wanyama na binadamu.
Mbali na mbwa na binadamu, viumbe wengine wanaoweza kuungua ni ng’ombe, Mbuzi, kondoo, farasi na wengineo.
Fahamu, heshimu na tekeleza haki za wanyama, HabariLeo Alhamisi Oktoba 13, 2011
Na. Ikunda Eric
Makala haya ni muendelezo wa makala ya wiki iliyopita ambayo yalifafanua na kuelezea maudhui ya Sheria ya Ustawi wa Wanyama Sura 154 pamoja na vifungu vilivyo katika sehemu za kwanza na ya pili. Katika makala mwandishi wetu Ikunda Eric anaelezea ufafanuzi wa vipengele vilivyosalia, kama alivyozungumza na Dk. Muhammed Bahari, Mkurugenzi Msaidizi , wa Ugani na Usajili kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Katika sehemu ya tatu na ya nne ya Sheria ya Ustawi wa Wanyama namba 154, inajenga taswira ya utekelezaji wa kutoa makatazo, makosa ambayo ni ukiukwaji wa Ustawi wa wanyama.
Tanga Fresh na mlolongo wa faida za maziwa, Rai, Alhamisi Oktoba 13, 2011
Na. Joseph Sabinus
Tunalojivunia ni kwamba, kupitia sekta ya maziwa, tumewawezesha wafugaji takribani 4,500 mkoani Tanga kufaidi ufugaji wao kwa kujihakikishia soko la uhakika wa asilimia 100 la maziwa yao na hili limewatia moyo sana huku pia, jijini Dar es Salaam pekee, takribani watu 100 wakiwa wamepata ajira.
Ndivyo anavyosema Afisa Masoko Uendeshaji wa Kampuni ya Maziwa ya Tanga Fresh Limited – Dar es Salaam , Charles Benjamen anapotakiwa kuzungumzia umuhimu wa jamii kutumia bidhaa za maziwa.
Samaki wanafugika – 1, Nipashe Jumatano Oktoba 12, 2011
Na. Balozi Christopher Liundi
Pius B. Ngeze ameandika vitabu vingi kuhusu kilimo. Zamu hii, kitabu chake kinahusu ufugaji wa samaki. Kitabu hicho kinaitwa, Ufugaji wa Samaki. Kimechapishwa na The Tanzania Educational Publishers Ltd, mwaka 2010. Lengo la kitabu hicho ni kuelimisha namna ya kufuga samaki.
Samaki hufugwa. Wanafungwa kama wanavyofungwa kuku, ng’ombe, Mbuzi, nguruwe, nyoka, mamba na viumbe wengine wanaofugwa. Ingawa watu wengi wangependelea kuwafuga samaki, ndege au wanyama mbalimbali tatizo lao kubwa ni namna ya kuwafuga.
Hamad: Wakulima wa mwani alipwe vizuri, JamboLeo Jumatano Oktoba 11, 2011
Na. Suleiman Omar, Pemba
Habari hii inapatikana pia gazeti la Mwananchi, HabariLeo, Jumatano Oktoba 11, 2011
Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Shariff Hamad ameonya kampuni zinazojishughulisha na ununuzi wa zao la mwani kujirekebisha na kutoa bei ya zao hilo kwa mujibu wa soko la dunia na si vinginevyo.
Hamad alisema lengo la kufanya hivyo ni kuwawezesha wakulima kuongeza kipato chao kulingana na Gharama za uzalishaji wanazotumia na endapo kampuni zitashindwa kufanya hivyo Serikali itanunua zao hilo .
Mbunge awapiga jeki wavuvi Ziwa Rukwa, Nipashe Jumanne Oktoba 11, 2011
Na. Thobias Mwanakatwe, Chunya
Mbunge wa Songwe (CCM), Philipo Mulugo amevipatia vikundi vya vijana vya Bonde la Songe vinavyojishughulisha na uvuvi katika Ziwa Rukwa nyavu 300.
Msaada huo ameukabidhi wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika jimbo lake. Mulugo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, alisema shughuli za uvuvi ni ajira tosha ambayo inaweza kubadilisha uchumi wa mtu hivyo hakuna sababu ya makundi ya vijana katika jimbo hilo kuendelea kuilalamikia Serikali kuwa imeshindwa kuwatafutia ajira vijana wakati wanafursa za kutosha, hivyo ni vema wakazitumia badala ya kukaa vijiweni na kufanya shughuli zisizo rasmi.
Ng’ombe milioni moja hatarini kufa kwa homa ya mapafu, Mwananchi Jumatatu Oktoba 10, 2011
Na. Happy Lazaro, Arusha
Zaidi ya ng’ombe milini moja katika Mkoa wa Arusha wapo katika hatari ya kufa kwa ugonjwa wa homa ya mapafu Kutokana na hofu ya ugonjwa huo kuingia nchini kupitia Wilaya za Ngorongoro na Longido zilizoko mpakani na nchi jirani ya Kenya .
Akizungumza katika uzinduzi wa chanjo ya ugonjwa huo uliofanyika Mang’ola Wilayani Karatu Mkuu wa wilaya ya Karatu Mathew Sedoyeka alisema kuwa Kutokana na tishio hilo Serikali inaendesha chanjo kwa ngo’mbe wote katika wilaya zote za Mkoa wa Arusha.
Samaki wa Ziwa Nyasa anasa Ludewa, HabariLeo Jumatatu Oktoba 10, 2011
Na. Frank Leonard, Ludewa
Matumizi ya kitoweo cha samaki kwa wakazi wa Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa inayopakana na Ziwa Nyasa yameendela kuonekana anasa Kutokana na kuongezeka kwa bei ya kitoweo hicho.
Upandaji huo wa bei umesababishwa na ukosefu wa samaki wa kutosha katika ziwa hilo unaotokana na sababu za kisayansi ikiwemo ya sehemu kubwa ya ziwa hilo kuwa kwenye kina kirefu kinachozidi meta 250.
Kiama cha wavuvi haramu chakaribia, HabariLeo Jumatatu Oktoba 10,2011
Na Nelson Goima
Tunaomba wananchi watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kukomesha tatizo la wavuvi haramu.
Watakaokamata wavuvi hao haramu, au wenye taarifa za watu hao, wapige simu polisi namba 0713 217702, 0715 468822 na 0717 643048 namba zote hizi zinafanya kazi muda wote.
Hiyo ni kauli ya Ofisa wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Majini (Navy) kilichopo kigamboni Jijini Dar es Salaam, Kombo Hassan. Alitoa namba hizo tatu hivi karibuni huko Somangira Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam kwenye mafunzo kwa wadau kuhusu athari zitokanazo na uvuvi haramu. Amesema jeshi la polisi limejizatiti na litahakikisha kuwa uvuvi haramu unatokomea na kuwa historia.
Ruzuku ya dawa za Mifugo, Habarileo Jumatatu Oktoba 10,2011
Wasemavyo wananchi
Naipongeza serikali kwa kutupia jicho sekta ya Mifugo kwani ndio tegemezi hasa kwa wakulima.
Kwa kufanya hivyo hata Gharama za matibabu ya Mifugo zitapungua hivyo wakulima wataweza kutibu Mifugo yao bila matatizo.
Kichaka cha samaki wa uvuvi haramu – wanauzwa mnadani usiku, askari watuhumiwa kuhusika, Mwananchi Jumamosi Oktoba 8, 2011
Na. Mary Mahundi
Soko la Kimataifa la samaki, Feri lililoko Dar es Salaam , linadaiwa kutumika kuendesha mnada tata wa usiku wa kuuza samaki waliovuliwa kwa baruti huku baadhi ya polisi na askari wa majini wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakidaiwa kuhusika.
Uvuvi huo wa kutumia baruti ni ule unaodaiwa kufanyika katika maeneo ya Kimburu na Shida katika Bahari ya Hindi, ambao una athari za kimazingira ikiwa ni pamoja na kuharibu mazalia na makazi ya samaki na viumbe wengine baharini.
Samaki wa ajabu akutwa amekufa ufukweni Pemba, Nipashe Jumamosi Oktoba 8, 2011
Na. Suleiman Rashid Omar, Pemba
Samaki mkubwa aina ya chongowe mwenye urefu wa zaidi ya mita nne, amekutwa akiwa amekufa bandarini Mueja katika Shehia ya Chambani.
Baadhi ya wavuvi na wananchi wa Chambani na vijiji vya jirani, wamekutwa wakikata mapande kwa ajili ya kitoweo na wengine wakigema mafuta kwa madai kwamba ni tiba ya mshipa.
Wafugaji Dar kunufaika na ufugaji wa kisasa, HabariLeo Jumamosi Oktoba 8, 2011
Wafugaji wa kuku jijini Dar es Salaam na mikoa ya Tanga, Morogoro, Arusha na Kilimanjaro watanufaika na semina ya ufugaji wa kuku kwa njia ya kisasa.
Hatua hiyo inakuja baada ya kampuni ya Euro Poultry (T) Limited kupanga kuendesha semina mbalimbali kwa wafugaji hao wa kuku.
Wabrazili kuleta neema kwa wakulima, wafugaji, HabariLeo Jumamosi Oktoba 8, 2011
Na. Joseph Kulangwa, Brasilia – Brazili
Wakulima na wafugaji wa Tanzania watalazimika kuomba Mungu ili taasisi ya utafiti wa kilimo na Mifugo ya hapa, Emrapa iweze kuruhusiwa na Wizara ya Mambo ya Nje, pamoja na taasisi ya kifedha ya ABC, kufungua tawi lake nchini humo.
Hiyo inatokana na kauli ya Mkuu wa Sekretarieti ya taasisi hiyo, Dk. Francisco Basilio Souza, kumwambia Waziri Mkuu Mizengo Pinda juzi kuwa, taasisi yake iko tayari kufanya hivyo ila kwa ruhusa ya taasisi hizo mbili.
Wawekezaji wa viwanda vya maziwa waonywa, Mwananchi Ijumaa Oktoba 7, 2011
Na. Mussa Juma, Arusha
Serikali imewaagiza wawekezaji wote waliochukua viwanda vya Maziwwa, vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kuvifufua viwanda hvyo na kuanza kusindika maziwa kabla hatua kali haijachukuliwa dhidi yao .
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Benedict Ole Nangoro, alitoa wito huo jana, alipotembelea kiwanda cha kusindika maziwa cha Arusha Daily kilichopo eneo la uwanja wa nane nane katika Manispaa ya Arusha.
Kina Mama wajane waanzisha ufugaji wa ng’ombe, Majira Ijumaa Oktoba 7,2011
Wanawake wajane wanakabiliwa na changamoto nyingi za kimaisha Kutokana na kufiwa na waume zao. Ugumu wa maisha unafuata baada ya kunyang’anywa rasilimali walizochuma na waume zao na kuachwa wakiishi maisha duni na kushindwa kusomesha watoto wao, kununua mahitaji muhimu katika familia husika na kuishi kwa kuombaomba.
Kikundi cha wajane (10) katika Kijiji cha Goha katka Kata ya Myamba, Wilaya ya Same wana kila sababu ya kuushukuru mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao umekipatia kikundi hicho kiasi cha shs. 9m kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ufugaji ng’ombe wa maziwa.
TASAF yaonyesha nuru kwa watoto yatima, Majira Ijumaa Oktoba 7, 2011
Toleo Maalum
Watoto yatima 15 katika Kijiji cha Mengeni chini ya kata ya Keni Mengeni wilayani Rombo wamenufaika na mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji baada ya kupatiwa msaada kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Katika kutekeleza mradi huo TASAF ilitoa shilingi milioni 9.1 kwa watoto hao ambao walianzisha kikundi mwaka 2010 kwa lengo la kujikwamua katika umaskini baada ya kufiwa na wazazi na waliokuwa wakiwategemea.
Ataka dawa za Mifugo zifike vijijini, Mwananchi Jumatano Oktoba 5, 2011
Na. Mussa Juma, Arusha
Wasambazaji wa dawa za Mifugo zenye ruzuku ya Serikali, wametakiwa kuhakikisha wanasambaza dawa hizo maeneo ya vijijini ambapo kuna wafugaji wengi ambao Mifugo yao bado inakufa kwa maradhi.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Benedict Ole Nangoro, alitoa wito huo juzi alipotembelea Kiwanda cha Dawa za Mifugo na Kilimo cha Bajuta International (T) Ltd mjini hapa. “Nia ya Serikali kutoa ruzuku katika dawa za Mifugo ni kuhakikisha zinawafikia wafugaji hasa wa vijijini ili Mifugo isiendelee kudhurika Kutokana na maradhi”.alisema
Wilaya ya Hai hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko ya wanyama, Mtanzania Jumatano Oktoba 5, 2011
Na. Omary Mlekwa
Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro iko hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko ya wanyama. Hiyo ni Kutokana na kuingia kwa makundi makubwa ya Mifugo wanaosadikiwa kuwa hawajapata chanjo ya kuzuia magonjwa ya Mifugo.
Imedaiwa kuwa imekuwapo kasi kubwa ya wafugaji wengi kutoka nje ya wilaya hiyo kuingiza Mifugo yao katika wilaya hiyo kufuata malisho Kutokana na ukame uliozikumba wilaya zao.
Serikali kutoa ruzuku dawa za Mifugo, HabariLeo Jumatano Oktoba 5, 2011
Na. John Mhala, Arusha
Habari hii pia inapatikana katika gezeti la Mtanzania, Jumatano Oktoba 5, 2011
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Benedict Ole Nangoro amesema Serikali itatoa ruzuku ya asilimia 40 ya bei ya dawa mbalimbali za Mifugo na vifaa vya kuogeshea ili kuboresha sekta.
Nangoro alitoa ahadi hiyo jana alipokuwa akizungumza katika ziara yake iliyolenga kukagua sekta za Wizara hiyo ikiwemo machinjio ya kisasa ya Arusha Meat yaliyopo Sakina, kiwanda cha dawa za Mifugo cha Bajuta na kiwanda cha kusindika maziwa cha New Arusha Diaries.
Ng’ombe 17 wafa kwa kula mtama mchanga, HabariLeo Jumatano Oktoba 5, 2011
Na Ahmed Makongo, Serengeti
Habari hii inapatikana gazeti la Uhuru,Nipashe, Jumatano Oktoba 5, 2011
Ng’ombe 17wamekufa papo hapo baada ya kula mtama mchanga ambao ndio kwanza ulikuwa unaanza kuota shambani katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Mganga Mkuu wa Mifugo wilayani Serengeti, Dk. Tito Kajize, alisema ng’ombe hao mali ya John Sadi, walikufa juzi mchana katika Kijiji cha Nyakitono, baada ya kula mtama huo.
Pastoralists demand probe into cattle deaths in reserve, The Citizen Wednedsday, 5 October 2011
A network of pastoralists, hunters and gatherers (Pingos Forum), has asked the government to investigate an incident in which more than 100 head of cattle were killed within the Katavi National Reserve.
The Forum has asked the government to also take stern measures against people found to be behind the killing of the cattle belonging to local pastoralists in the area.
Waziri: Wanaotesa wanyama sasa watawachukulia hatua, Majira Jumatano Oktoba 5, 2011
Na. Rachel Balama
Habari hii pia inapatikana katika gazeti la The Citizen,TanzaniaDaima, HabariLeo, Uhuru, Mwananchi, Jumatano Oktoba 5, 2011
Serikali itawachukulia hatua za kisheria wasafirishaji Mifugo na kuwalipisha faini ya Shs.20,000 hadi shs. 100,000 kama watakiuka sheria ya ustawi wa wanyama kwa kuwafanyia vitendo vya ukatili.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. David Mathayo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizindua maadhimisho ya siku ya wanyama duniani katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Mbwa 16,000 kupewa chanjo Moshi, Nipashe Jumanne Oktoba 4, 2011
Na. Charles Lyimo, Moshi
Zaidi ya mbwa 16,000 katika kata za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wanatarajiwa kupatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Daktari wa Mifugo wa Halmashauri hiyo, Walter Marandu alisema kuwa kwa kuanza wamekwisha kutoa chanjo kwa mbwa 350 katika Kata ya TPC kwa siku moja.
Wapendekeza wakuwajibishwa waliohusika kuua ng’ombe, Mwananchi Jumanne Oktoba 4, 2011
Na. Mussa Juma, Arusha
Mtandao wa wafugaji, wawindaji na wakusanya matunda asili nchini (Pingo’s Forum) umetaka Serikali kufanya uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya watu waliohusika na mauaji ya zaidi ya ng’ombe 100 wanaodaiwa kupigwa risasi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Ofisa Utawala wa mtandao huo, Emmanuel Saringe, alisema kitendo cha kuua kwa risasi ng’ombe hao ni ukiukaji wa sheria za nchi.
Wafugaji kuhamishwa tena, Mwananchi Jumanne Oktoba 4, 2011
Na. Hamida Shariff, Kilosa
Uongozi wa serikali katika Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, unakusudia kuanzisha tena operesheni ya kuwaondoa wafugaji walioingia katika eneo hilo kinyume na utaratibu.
Hatua hiyo inafuatia kukithiri kwa migogoro kati ya wafugaji na wakulima inayosababishwa na ongezeko la Mifugo, baada ya kusitishwa zoezi la awali la kuwahamisha wafugaji.
Lawamani kwa kuzuia watu wasichanje mbwa, Mwananchi Jumanne Oktoba 4, 2011
Na. Sheila Sezzy, Mwanza
Daktari wa Mifugo mkoani hapa, Dk. Mugaruka ruta amesikitishwa na kitendo cha diwani wa kupitia CCM, Hilal Bilalimini wa Kata ya Karomije iliyopo wilayani Misungwi kwa kuwazuia wananchi wa eneo lake kuwapeleka mbwa wao kupata chanjo ya kichaa cha mbwa.
Diwani huyo anadaiwa aliwakataza wananchi wake kupeleka mbwa wao na paka kupatiwa chanjo kwa madai kuwa Baraza la madiwani halijakaa na kupitisha uchanjaji wa mbwa pamoja na paka.
Wafugaji wajiandae kuhama mijini, HabariLeo Jumanne Oktoba 4, 2011
Na. Shadrack Sagati
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amewakemea wananchi waofuga Mifugo katika maeneo ya mijini.
Pamoja na kuwakemea amewataka wajiandae kuhamisha Mifugo yao kwani vitendo vyao ni vya kuvunja sheria ya Mipango miji.
Wapambana kuingiza elimu ya ustawi wa wanyama shuleni, HabariLeo Oktoba 4, 2011
Wadau wa kuzuia ukatili dhidi ya wanyama wameanza jitihada za kuingiza kwenye mitaala ya shule za msingi elimu ya ustawi wa wanyama ili kudhibiti ukatili wa wanyama hao.
Akizungumza katika semina ya uelimishaji wa sheria za wanyama, Mkurugenzi Msaidizi wa Ugani na Usajili kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk. Mohamed Bahari alisema wanataka kuwepo mitaala hiyo katika shule za msingi ili kuwafanya wanafunzi wawe na mapenzi na wanyama.
CAG kukagua samaki Ziwa Victori, HabariLeo Jumanne Oktoba 4, 2011
Na. John Mhala, Arusha
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itafanya ukaguzi wa Ziwa Victoria kubaini sababu na hatua za kuchukua Kutokana na samaki ziwani kupungua
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh alisema kazi hiyo itafanywa kwa kushirikiana na wakaguzi wengine kutoka Serikali za Kenya na Uganda .
Kichaa cha mbwa chazidi kuitesa dunia, JamboLeo Ijumaa Septemba 30, 2011
Na. Grace Sima
Kicha cha mbwa ni ugonjwa ambao unaongezeka kwa kasi nchini na Duniani kwa ujumla. Ugonjwa huo hushambulia zaidi mfumo wa mishipa ya fahamu na ubongo na huwapata zaidi wanyama jamii ya mbwa, lakini pia wanyama wafugwao na wanyamapori.
Pia kichaa cha mbwa huwapata binadamu, hivyo Kutokana na hali hiyo umekuwa ukisababisha madhara makubwa kwa jamii.
Wanaofuga mbwa watakiwa kuwapatia chanjo, JamboLeo Ijumaa Septemba 30, 2011
Na. Grace Sima
Serikali imewataka wananchi wote wanaofuga mbwa na paka kuwapatia chanjo ili kuzuia kichaa cha mbwa nchini.
Hayo yalibainishwa juzi na Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge katika maadhimisho ya Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani ambayo hufanyika Septemba 28 ya kila mwaka.
SMZ kuwapatia mafunzo wakulima wa mwani, Habarileo Ijumaa Septemba 30, 2011
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema itaendelea kuwapatia elimu na mafunzo wakulima wa zao la mwani kwa lengo la kuona wanapata ujuzi wa kuzalisha utakaokidhi mahitaji ya soko la bidhaa hiyo.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Said Ali Mbarouk wakati alipowapokea wanaushirika wa vikundi vya uzalishaji wa mwani na mazao ya Bahari waliokuwa China kwa muda wa mwezi mmojo kujifunza mbinu za kisasa za uzalishaji wa mwani na ufugaji wa samaki.
Kaa ni mali, wanafugika, wana soko, Nipashe Ijumaa Septemba 30, 2011
Na. Lulu George, Pangani
Kaa ni viumbe wa baharini wanaoliwa ambao hupatikana katika Bahari Kuu ya Hindi. Hata hivyo, viumbe hawa wana maumbile tofauti na samaki wa kawaida. Wana miguu mine na uwezo wa kukaa nchi kavu kwa zaidi ya saa 12 licha ya kuwa makazi yao ni majini.
Uhaba wa upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya kuendesha shughuli za kilimo wilayani Pangani ambapo eneo kubwa limemezwa na Bahari. Wananchi wa wilaya hiyo wamekuwa wakiitumia Bahari kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kuendesha maisha yao ya kila siku. Miongoni mwa shughuli hizo ni ufugaji wa kaa, kamba mti na kilimo cha mwani.
Tunajua hali za machinji yetu ya nyama? Nipashe Ijumaa Septemba 30, 2011
Barua za wasomaji
Licha ya kusisitiza kwa muda mrefu juu ya usafi wa machinjio yakiwemo yale ya kuku, mengi yake yamebakia kuwa machafu kiasi cha kukatisha tama. Inapasa kueleweka kuwa usafi unatakiwa siyo tu kwenye mazingira yanayotuzunguka barabarani bali hata kwenye hoteli, migahawa na maeneo ya machijio.
Tufahamu kwamba hata kama nyama hiyo mwisho wa siku itapikwa ni vizuri kuwa uandaaji wake unatakiwa kufanywa kwenye mazingira ya usafi kutoka mwanzo.
Kilio hiki kiwaendee polisi, mahakama na Dk. Mathayo, Kulikoni, Ijumaa Septemba 30, 2011
Na. Hamisi Kibari, Dar es Salaam
Jumatatu hii katika moja ya vituo vyetu vya Televisheni kulikuwa na mjadala mmoja ambao ulinivutia kuufuatilia na nimeamua kuendeleza kwa sababu nilijaribu kupiga simu ili nitoe mawazo yangu bila mafanikio.
Mjadala huo uliokuwa unazungumzia uvuvi na sheria zake ulinikuna kiasi cha kufanya hii iwe mara ya tatu kama si ya nne kuandika habari kuhusu madhara ya uvuvi haramu nchini mwetu, hususan kule kwetu Kanda ya Ziwa.
Kichaa cha mbwa chaua watu wawili, Mtanzania, Ijumaa Septemba 30, 2011
Na. Oliver Richard, Iringa
Watu wawili wafariki dunia katika Manispaa ya Iringa kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa miongoni mwa watu 689 walioumwa na mbwa hao.
Ofisa Mifugo wa Manispaa ya Iringa, Dk. Fredrick Mfikwa alikuwa akitoa takwimu ya madhara ya kichaa cha mbwa katika kongamano la wataalamu wa Mifugo na afya katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa.
Namna maziwa yanavyoweza kuwa tiba kiafya, HabariLeo Alhamisi Septemba 29, 2011
Na. Ikunda Eric
Maziwa ni chakula chenye virutubisho vingi, hutumiwa kama lishe kwa watoto wachanga na pia hutumiwa na watu wazima kama kinywaji chenye virutubisho muhimu kwa afya ya mtumiaji.
Kutokana na umuhimu wake mwilini, baadhi ya watu wanayasifu maziwa kuwa ni "Damu nyeupe" mwilini kutokana na uhumihimu wake.
Tani 80 za mwani zatumbukia baharini, HabariLeo Alhamisi Septemba 29, 2011
Tani 80 za mwani kavu zilizokuwa tayari kusafirishwa kwenda Unguja zimetumbukia baharini baada ya gari ililozibeba aina ya Mitsubishi Canter kutumbukia katika gati ya Bandari ya Mkoani kisiwani Pemba.
Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Pemba, Hamad Salim Hamad alisema gari hiyo ilitumbukia baharini ilipokuwa ikirudi nyuma kujiweka sawa tayari kushusha mzigo huo.
Wakwepaji chanjo ya mbwa Kinondoni kudhibitiwa, HabariLeo Alhamisi Septemba 29, 2011
Na. Oscar Job
Vaccination of cattle gets little cooperation, The Citizen, Wednesday Septemba 28, 2011
By Zephania Ubwani, Arusha
Little cooperation from livestock keepers and a shortage of extension staff have slowed the vaccination of cattle against Contagious Bovine Pleauropneumonia (CBPP).
This has led to failure of vaccinating all the cattle in Arusha Region against the disease, also known as lung plague, that can wipe out large herds in a short time.
Kichaa cha mbwa chaua wengi, Uhuru Jumatano Septemba 28, 2011
Habari hii pia inapatikana gazeti la Nipashe, Tanzania Daima, Mwananchi,The Guardian, Jumatano Septemba 28, 2011
Mamia ya watu wamepoteza maisha Kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Kutokana na ugonjwa huo kutokuwa na tiba, serikali imewataka watu wanaofuga mbwa na paka kuwapeleka katika chanjo katika vituo husika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David alisema ni vyema wananchi wakatumia fursa ya siku ya kudhibiti ugonjwa huo duniani inayoadhimishwa leo kuwapatia chanjo wanyama hao.
Uhaba wa maziwa watikisa Tanga Fresh, JamboLeo Jumatano Septemba 28,2011
Na. Evelyn Balozi, Tanga
Kiwanda cha uzalishaji maziwa cha Tanga Fresh Ltd kilichopo mkoani hapa kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa zao la maziwa hali inayotokana na ukosefu wa malisho kwa ng’ombe hasa msimu huu wa kiangazi.
Akizungumza na Jambo Leo kiwandani hapo hivi karibuni, Ofisa Habari wa kiwanda hicho, Charles Tumaini alisema kiwanda kinalazimika kujiendesha kwa hasara Kutokana na kushindwa kufikia asilimia 100 ya uzalishaji kulingana na nguvu ya mitambo iliyopo.
Maadhimisho ya maziwa yawadia, JamboLeo Jumamosi Septemba 24, 2011
Wafaidika na ufugaji wa Mbuzi, Majira Jumanne Septemba 27, 2011
Toleo Maalum la TASAF
Wazee wa Kijiji cha Mfereji kilichopo Kata ya Monduli juu wamefaidika na mradi wa ufugaji wa mbuzi aina ya Isiolo. Aina hii ya Mbuzi wa kisasa inaopatikana nchini Kenya katika eneo linaloitwa ISIOLO ndio maana wanajulikana kwa jina hilo .
Mbuzi hao wana sifa nyingi na nzuri zikiwemo kuzaa mapacha, ni wakubwa kwa maumbo, wanatoa maziwa mengi.
‘Vikosi vya kupambana na uvuvi haramu Victoria vivunjwe’ Nipashe Jumanne Septemba 27, 2011
Na. Kibuka Prudence, Bukoba
Jamii ya wavuvi Ziwa Victoria hususani walioko mkoani Kagera, wameomba serikali kuvunja vikosi vya kupambana na uvuvi haramu ili kulinda rasilimali zilizomo ziwani humo.
Ombi hilo limetolewa na viongozi wa wavuvi hao kwa madai kuwa watendaji wake wamekuwa wakila njama na wale wanaojihusisha na vitendo hivyo katika ziwa hilo .
Ng’ombe milioni 1 hatarini kukumbwa homa ya mapafu, Nipashe Jumanne Septemba 27, 2011
Na. Charles Ole Ngereza, Arusha
Zaidi ya ng’ombe milioni moja mkoani hapa, wako hatarini kufa kwa ugonjwa wa homa ya mapafu baada ya kuzikumba wilaya za Ngorongoro na Longido zilizoko mpakani mwa Tanzania na Kenya .
Akizungumza katika uzinduzi wa chanjo ya ugonjwa huo iliyofanyika Mang’ola, Mkuu wa Wilaya ya karatu, Mathew Sedoyeka alisema kuwa kutokana na tishio hilo Serikali inaendesha chanjo kwa ng’ombe wote katika wilaya zote za Mkoa wa Arusha.
Mradi ulioanzishwa kwa ajili ya kuwakomboa wavuvi, Mtanzania Jumanne Septemba 27, 2011
Makala ya Biashara & Uchumi
Zipo changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya uvuvi nchini, hasa kwa wavuvi wenyewe ni waathirika wakuu wa changamoto hizo.
Ni dhahili kuwa sasa dunia yetu inaongozwa na sayansi na teknolojia hii inammanisha zana nyingi zinazotumika hivi sasa katika shughuli mbalimbali kiwamo za uvuvi ni zana za kisasa.
Swiss return improperly documented aquarium consignment, Guardian September 25, 2011
By Edwin Agola
A consignment of aquarium fish originating from Tanzania exported to Hunary was barred entry in that country and brought back on Friday night onboard a Swissair flight for inappropriate documentation. The Guardian on Sunday has learnt.
Lazaro Bihole, managing director of Bihole Investment Limited, which freighted the consignment told this reporter by phone that he was still waiting for communication from Zurich and promised to give a statement by Monday.
Halmashauri zashauriwa kuwatambua wavuvi, Majira Thursday September 25, 2011
Na. Livinus Feruzi, Bukoba
Halmashauri za Wilaya Mkoani Kagera, zimetakiwa kuwa na idadi kamili ya wavuvi na mitumbwi inayofanya shughuli za uvuvi kwa mwaka katika Ziwa Victoria ili kuondoa tatizo la uvuvi holela.
Ofisa Mfawidhi wa Kikosi cha Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi Kanda ya Kagera, Bw. Rodrick Mahimbali, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na Majira.
Na. Janeth Mushi, Arusha
Maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya unywaji wa maziwa shuleni ambayo hufanyika Septemba 28 kila mwaka duniani yamepamba moto mkoani Arusha ambapo yanatarajiwa kufanyika kitaifa mjini hapa.
Kanda ya Kaskazini ambao ni wenyeji wa maadhimisho hayo ya kitaifa yatahudhuriwa na wadau wa uzalishaji maziwa viwandani wakiwemo baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa hiyo pamoja na viongozi wa kitaifa.
Wiki unywaji maziwa shuleni, Mtanzania Ijumaa Septemba 23,2011
Na. Mary Mwite, Arusha
Maandalizi ya maadhimisho ya wiki unywaji maziwa shuleni duniani yamepamba moto katika Kanda ya Kaskazini ambayo ni mwenyeji wa maadhimisho hayo kitaifa.
Maadhimisho hayo yanaelezwa yatakuwa ya aina yake kwa kuwa viongozi wa taifa wanatarajiwa kuhudhuria ikiwemo na wadau wa uzalishaji maziwa viwandani na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo.
Wafugaji epukeni migogoro asema DC, Mwananchi Ijumaa Septemba 23, 2011
Watu wa jamii za wafugaji wilayani Kisarawe, mkoani Pwani wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimiana na wenzao wa jamii ya wakulima katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kuepuka migogoro inayoweza kuhatarisha amani na utulivu miongoni mwao.
Agizo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Khanifa Karamagi, kufuatia malalamiko ya wakulima wa Kijiji cha Gatwa katika Kata ya Mafizi, kuhusu vitendo vya baadhi ya wafugaji kuruhusu makundi ya mifugo kuingia kwenye mashamba na kuharibu mazao.
Na. Mary Mwite, Arusha
Maandalizi ya maadhimisho ya wiki unywaji maziwa shuleni duniani yamepamba moto katika Kanda ya Kaskazini ambayo ni mwenyeji wa maadhimisho hayo kitaifa.
Maadhimisho hayo yanaelezwa yatakuwa ya aina yake kwa kuwa viongozi wa taifa wanatarajiwa kuhudhuria ikiwemo na wadau wa uzalishaji maziwa viwandani na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo.
Wafugaji epukeni migogoro asema DC, Mwananchi Ijumaa Septemba 23, 2011
Watu wa jamii za wafugaji wilayani Kisarawe, mkoani Pwani wametakiwa kujenga utamaduni wa kuheshimiana na wenzao wa jamii ya wakulima katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kuepuka migogoro inayoweza kuhatarisha amani na utulivu miongoni mwao.
Agizo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Khanifa Karamagi, kufuatia malalamiko ya wakulima wa Kijiji cha Gatwa katika Kata ya Mafizi, kuhusu vitendo vya baadhi ya wafugaji kuruhusu makundi ya mifugo kuingia kwenye mashamba na kuharibu mazao.
Seif akunwa na ufugaji wa kamba India, HabariLeo Jumamosi Septemba, 24 2011
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwa imevutiwa na kazi za ufugaji wa kamba wadogo inayofanywa eneo la kando ya Bahari ya mji wa Kerala nchini India na imesema kuna haja taaluma hiyo ifikishwe kwa wavuvi na wakulima wa Zanzibar ambako kuna mahitaji makubwa ya samaki wa aina hiyo hasa kwenye soko la utalii.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar , Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na viongozi wa Idara ya Uvuvi katika mji huo inayosimamia kituo cha kufugia kama alisema, Zanzibar inangaliwa iwapo watendaji waende kujifunza mbinu hizo huko Keralu au wataalamu kutoka kituo hicho waende Zanzibar kufikisha ujuzi huo wa wavuvi na wakulima.
Serikali yafidia ng'ombe waliokufa kwa ukame, Mwananchi Jumatano Septemba 21, 2011Na. Musa Juma, Ngorongoro
Serikali imetoa kiasi cha Shs.3.7 bilioni kwa wafugaji wa Wilaya ya Ngorongoro, ili waweze kununua mifugo, kufidia vifo vya maelfu ya mifugo yao iliyokufa kwa ukame mwaka 2008/09.
Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Saning'o Ole Telele akizungumza katika hafla ya kumpongeza kutokana na msimamo wake bungeni, alisema fedha hizo zitaanza kugawanywa hivi karibuni kwa wafugaji.
Uko wapi mchango wa mifugo nchini? JamboLeo Jumanne Septemba 20,2011
Serikali imetoa kiasi cha Shs.3.7 bilioni kwa wafugaji wa Wilaya ya Ngorongoro, ili waweze kununua mifugo, kufidia vifo vya maelfu ya mifugo yao iliyokufa kwa ukame mwaka 2008/09.
Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Saning'o Ole Telele akizungumza katika hafla ya kumpongeza kutokana na msimamo wake bungeni, alisema fedha hizo zitaanza kugawanywa hivi karibuni kwa wafugaji.
Uko wapi mchango wa mifugo nchini? JamboLeo Jumanne Septemba 20,2011
Na. Claudia Kayombo
Ng'ombe ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya nyama nchini, vingine ni mbuzi, kondoo, kuku, nguruwe, wanyamapori na samaki.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba asilimia 53 ya nyama inayozalishwa nchini hutokana na ng'ombe. Sehemu kubwa ya nyama hiyo hutumika kwa ajili ya soko la ndani na kiasi kidogo huuzwa nje ya nchi.
Wafugaji waharibifu mashamba waonywa, HabariLeo Jumanne Septemba 20, 2011
Serikali imewaonya wafugaji wanaondesha shughuli zao kwa kuhamahama huku wakiharibu mazao ya wakulima katika maeneo wanayohamia kuacha uharibu huo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliyasema hayo juzi alipozungumza na wakazi wa Kijiji cha Suguti katika wilaya ya Musoma Vijijini.
Wafugaji sasa watakiwa kuacha kuvamia mashamba, Mwananchi Jumanne Septemba 20, 2011
Na. Ahmed Makongo, Musoma
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka wafugaji waliohamia katika Wilaya ya Musoma Vijijini Mkoani Mara, kutovamia mashamba ya wakulima na kulisha mifugo kwenye mazao yao, kwani hali hiyo inaweza kuleta machafuko na kusababisha mapigano kati yao.
Waziri Mkuu alitoa rai hiyo juzi wilayani Musoma wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Suguti, wilayani hapa.
Ufugaji kuku kwa dawa udhibitiwe, Uhuru Jumanne Septemba 20,2011
Barua za wasomoji
Huwa naogopa sana ninaposikia simulizi kwamba kuna baadhi ya kuku wa siku hizi wamelishwa dawa, ili wakuwe kwa haraka.
Woga huo unatokana na ukweli kwamba tunawala kuku kwa wingi katika sehemu mbalimbali tunazotembelea iwe katika sherehe, starehe au mlo wa kawaida.
Tanzanian fish firm seeks to regain entry into Kenyan market, The EastAfrican September 19-25,2011
By. Rosemary Mirondo
After getting clearance to sell over 124.9 metric tonnes of mackerel imported from Japan last June, Dar es Salaam based Alphakrust Ltd which was also barred from selling the fish in Kenya, is now seeking clearance to sell their products in Nairobi.
The mackerel which was blocked from entering Kenya through Namanga border post almost simultaneously with suspension of the consignments's sale in Tanzania, was suspected of being contaminated by nucleaar radiation.
Machinjio bora ni afya kwa mlaji, Majira Jumatatu Septemba 19, 2011
By. Rosemary Mirondo
After getting clearance to sell over 124.9 metric tonnes of mackerel imported from Japan last June, Dar es Salaam based Alphakrust Ltd which was also barred from selling the fish in Kenya, is now seeking clearance to sell their products in Nairobi.
The mackerel which was blocked from entering Kenya through Namanga border post almost simultaneously with suspension of the consignments's sale in Tanzania, was suspected of being contaminated by nucleaar radiation.
Machinjio bora ni afya kwa mlaji, Majira Jumatatu Septemba 19, 2011
Kwa miaka mingi serikali imekuwa ikihimiza wananchi kuwa wajasiliamali ili kuweza kujiletea maendeleo. Kutokana na wito huo, kwa kiasi kikubwa baadhi ya watanzania wameitikia wito huo kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwakwamua kimaisha.
Bw. Shechambo Mhando ni kati ya Watanzania walioitikia wito huo na katika ubunifu wake ameweza kubuni machinjio ambayo pamoja na mambo mengine imekuwa ni sehemu ya ajira kwa wengine.
Wanawake 20 kuwania tuzo ya kilimo, ufugaji, Majira Jumanne Septemba 16, 2011
Na. Stella Aron
Wanawake 20 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanatarajia kushiriki shindano la kumtafuta mwanamke bora mwenye ujuzi wa kitaalamu katika masuala ya kilimo na ufugaji mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), mratibu wa shindano hilo Bi. Lilian Kallaghe, alisema shindano hilo linalotambulika kwa jina la Mama Shujaa linatarajia kufanyika siku ya maadhimisho ya chakula duniani.
Wavuvi wasababisha kikao cha ushuru kuvunjika Sengerema, Mtanzania Ijumaa Septemba 16, 2011
Na. Victor Bariety, Sengerema
Kikao cha kutatua mgogoro wa siku nyingi wa ushuru wa mazao ya samaki kati ya wavuvi wa mialo ya Ito na Ikuli kisiwani Kome wilayani Sengerema na wakala wa kukusanya ushuru huo, kimeshindwa kufanyika baada ya wavuvi kugoma kusaini kwenye karatasi ya mahudhurio ya kikao.
Hatua hiyo ilitokana na wavuvi hao kudai kikao hicho hakikuhudhuriwa na mwakilishi wao kwenye vikao vya halmashauri Adophina Chialo alisema tukio la kwanza lilitokea Septemba 13 usiku katika Kitongoji cha Ipopoo Kijiji cha Miembeni wilayani Kilombero likimuhusisha mpanda baiskeli
Kaa wakubwa wagoea Antarctic, Tanzania Daima Alhamisi Septemba 15, 2011
Na. Leah Peter
Mambo ambayo yamewashangaza wataalamu wa wanyama wa baharini katika kipindi hiki ni kuonekana kwa kaa wakubwa karibu na eneo la Antarctica.
Kwa kawaida, eneo hili linakuwa na baridi kali ambayo hairuhusu wanyama hawa wa majini kuishi.
Ranchi za Taifa zina mchango kukuza uchumi, HabariLeo Jumatano Septemba 14, 2011
Na. Ikunda Eric
Historia ya Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) imeanza mwaka 1947, ambapo baada ya kuundwa kwa chombo hicho baadhi ya majukumu yake ilikuwa kuendeleza na kukuza ufugaji bora na wa kisasa wa ng'ombe bora wa nyama aina ya Boran, kwa ajili ya soko la ndani na lile la nje.
Aidha, majukumu mengine ni pamoja na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na mifugo kama vile nyama, maziwa, ngozi na mazao mengine ya mifugo hiyo, kadhalika pamoja na kuwa na machinjio na uzalishaji wa bidhaa za nyama.
Wafugaji waunde vyama kujiletea maendeleo yao, Majira Jumatano Septemba 14, 2011
Migogoro ya muda mrefu ambayo baadhi ya wafugaji wamekuwa kihusika sana, imekuwa ikiiletea jamii yetu madhara makubwa ikiwemo mauji hususani kati ya wafugaji na wakulima.
Wakulima wamekuwa wakiwashutumu baadhi ya wafugaji kulisha mifugo yao kwenye mashamba yao. Wapo baadhi ya wafugaji wamekuwa wakifikishwa kwenye vyombo vya sheria kushitakiwa kwa kuhusika na makosa ya kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima.
Waliobiwa mifugo washauriwa, Mwananchi Jumatano Septemba 14, 2011
Na. Sanjito Msafiri, Kibaha
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Amina Mrisho amewaasa waathirika wa uhalifu wa mifugo na wananchi kwa ujumla mkoani hapa kusaidiana na Jeshi la Polisi katika suala la ulinzi shirikishi ili kubaini uhalifu huo unaofanywa na baadhi ya watu katika maeneo mbalimbali mkoani Pwani.
Akizungumza kwenye kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa alisema kuwa zoezi hilo lipo ndani ya kampeni ya utii wa sheria bila shuruti ambayo inaendelea kufanywa na polisi.
Maajabu ya kasa hutaga alikozaliwa, JamboLeo Jumanne Septemba 13, 2011
Na. Claudia Kayombo
Kasa ni miongoni mwa viumbe wanaoishi majini kama ilivyo kwa Nguva na Samaki aina nyingine yoyote. Viumbe wa majini wamekuwa na vivutio kwa wengi, labda ni kutokana na ukweli kwama si rahisi kuonekanakatika makazi ya watu.
Hii ni kwa sababu hawana uwezo wa kukaa kwa muda mrefu wakiwa nje ya maji kwma ilivyo kwa baadhi ya wanyama wa mwituni ambao kwa nadra hutokeza katika makazi ya watu.
Wavuvi, Wajasiliamali wa samaki kuwezeshwa, Mtanzania Jumanne Septemba 13,2011
Na. Stella Aron
Wanawake 20 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanatarajia kushiriki shindano la kumtafuta mwanamke bora mwenye ujuzi wa kitaalamu katika masuala ya kilimo na ufugaji mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), mratibu wa shindano hilo Bi. Lilian Kallaghe, alisema shindano hilo linalotambulika kwa jina la Mama Shujaa linatarajia kufanyika siku ya maadhimisho ya chakula duniani.
Wavuvi wasababisha kikao cha ushuru kuvunjika Sengerema, Mtanzania Ijumaa Septemba 16, 2011
Na. Victor Bariety, Sengerema
Kikao cha kutatua mgogoro wa siku nyingi wa ushuru wa mazao ya samaki kati ya wavuvi wa mialo ya Ito na Ikuli kisiwani Kome wilayani Sengerema na wakala wa kukusanya ushuru huo, kimeshindwa kufanyika baada ya wavuvi kugoma kusaini kwenye karatasi ya mahudhurio ya kikao.
Hatua hiyo ilitokana na wavuvi hao kudai kikao hicho hakikuhudhuriwa na mwakilishi wao kwenye vikao vya halmashauri Adophina Chialo alisema tukio la kwanza lilitokea Septemba 13 usiku katika Kitongoji cha Ipopoo Kijiji cha Miembeni wilayani Kilombero likimuhusisha mpanda baiskeli
Kaa wakubwa wagoea Antarctic, Tanzania Daima Alhamisi Septemba 15, 2011
Na. Leah Peter
Mambo ambayo yamewashangaza wataalamu wa wanyama wa baharini katika kipindi hiki ni kuonekana kwa kaa wakubwa karibu na eneo la Antarctica.
Kwa kawaida, eneo hili linakuwa na baridi kali ambayo hairuhusu wanyama hawa wa majini kuishi.
Ranchi za Taifa zina mchango kukuza uchumi, HabariLeo Jumatano Septemba 14, 2011
Na. Ikunda Eric
Historia ya Kampuni ya Ranchi ya Taifa (NARCO) imeanza mwaka 1947, ambapo baada ya kuundwa kwa chombo hicho baadhi ya majukumu yake ilikuwa kuendeleza na kukuza ufugaji bora na wa kisasa wa ng'ombe bora wa nyama aina ya Boran, kwa ajili ya soko la ndani na lile la nje.
Aidha, majukumu mengine ni pamoja na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na mifugo kama vile nyama, maziwa, ngozi na mazao mengine ya mifugo hiyo, kadhalika pamoja na kuwa na machinjio na uzalishaji wa bidhaa za nyama.
Wafugaji waunde vyama kujiletea maendeleo yao, Majira Jumatano Septemba 14, 2011
Migogoro ya muda mrefu ambayo baadhi ya wafugaji wamekuwa kihusika sana, imekuwa ikiiletea jamii yetu madhara makubwa ikiwemo mauji hususani kati ya wafugaji na wakulima.
Wakulima wamekuwa wakiwashutumu baadhi ya wafugaji kulisha mifugo yao kwenye mashamba yao. Wapo baadhi ya wafugaji wamekuwa wakifikishwa kwenye vyombo vya sheria kushitakiwa kwa kuhusika na makosa ya kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima.
Waliobiwa mifugo washauriwa, Mwananchi Jumatano Septemba 14, 2011
Na. Sanjito Msafiri, Kibaha
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Amina Mrisho amewaasa waathirika wa uhalifu wa mifugo na wananchi kwa ujumla mkoani hapa kusaidiana na Jeshi la Polisi katika suala la ulinzi shirikishi ili kubaini uhalifu huo unaofanywa na baadhi ya watu katika maeneo mbalimbali mkoani Pwani.
Akizungumza kwenye kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa alisema kuwa zoezi hilo lipo ndani ya kampeni ya utii wa sheria bila shuruti ambayo inaendelea kufanywa na polisi.
Maajabu ya kasa hutaga alikozaliwa, JamboLeo Jumanne Septemba 13, 2011
Na. Claudia Kayombo
Kasa ni miongoni mwa viumbe wanaoishi majini kama ilivyo kwa Nguva na Samaki aina nyingine yoyote. Viumbe wa majini wamekuwa na vivutio kwa wengi, labda ni kutokana na ukweli kwama si rahisi kuonekanakatika makazi ya watu.
Hii ni kwa sababu hawana uwezo wa kukaa kwa muda mrefu wakiwa nje ya maji kwma ilivyo kwa baadhi ya wanyama wa mwituni ambao kwa nadra hutokeza katika makazi ya watu.
Wavuvi, Wajasiliamali wa samaki kuwezeshwa, Mtanzania Jumanne Septemba 13,2011
Kampuni ya Alphakrust Ltd inakusudia kuwawezesha wavuvi na wajasiliamali wadogo wa samaki na hatimaye waweze kukuza na kuboresha shughuli zao.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mkuu wa AlphaGroup, ambayo ni kampuni mama ya Alphakrust Limited, Ganeshen Vedagiri.
YVK yaja na dawa ya kudhibiti uvuvi haramu Bahari ya Hindi, Tanzania Daima Jumanne Septemba 13, 2011
Na. Chalila Kibuda
Kati ya vitu vinavyorudisha nyuma maendeleo ni pamoja na kushamiri kwa uvuvi haramu katika Bahari, mito na maziwa yanayopatikana nchini.
Kwa hapa Dar es Salaam , uvuvi haramu umekithiri katika Bahari ya Hindi, hali inayotishia ustawi wa viumbe vya majini.
Wavuvi wadogo nchini washushiwa neema, Nipashe Jumanne Septemba 13, 2011
Kampuni inayojishughulisha na biashara ya samaki, Alphakrust Ltd, imetangaza mpango wa kuinua shughuli za wavuvi na wajasiliamali wadogo wa samaki nchini Tanzania .
Hii ni moja ya mikakati ya kampuni hiyo kuharakisha utekelezaji wa mikakati ya serikali yenye lengo la kuinua na kuboresha sekta ya samaki nchini Tanzania .
Wafugaji waamriwa kurejesha ardhi ekari 4,700, HabariLeo Jumapili Septemba 11, 2011
Na. John Nditi, Mvomero
Wafugaji wa jamii ya Kimang’ati waliouziwa eneo la ardhi ekari 4,700 kati ya 12,000 katika kitongoji cha Njeula Kijiji cha Mziha, Kata ya Kanga, Wilaya ya Mvomero kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa baadhi ya viongozi wa zamani wa Serikali ya Kijiji, wameamriwa kuzirejesha mara moja mikononi mwa Serikali mpya ya Kijiji hicho.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Fatma Mwassa juzi wakati wa mikutano wa hadhara wa kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kitongoji hicho na wafugaji saba wa Kimang’ati walionunua ekari hizo bila kufuata sheria na utaratibu wa uhaulishaji wa ardhi kutoka Serikali ya Kijiji kwenda kwa watu binafsi.
Wafugaji waliovamia Selous kung’olewa, HabariLeo Jumamosi Septemba 10, 2011
Na. John Nditi, Morogoro
Serikali mkoani hapa inafanya uamuzi mgumu kuwaondoa wafugaji waliovamia na maelfu ya Mifugo katika vijiji mbalimbali vya wakulima na katika Pori la Akiba la selous.
Lengo ni kunusuru uharibifu wa mazingira na kulinda hadhi ya pori hilo lenye vivutio vingi vya utalii.
Ng’ombe 400 waliongizwa kinyemela Kilombero wakamatwa, Nipashe Jumamosi Septemba 10, 2011
Na. Ashton Balaigwa, Morogoro
Serikali wilayani Kilombero imeanza operesheni ya kukamata Mifugo iliyoingia wilayani humo kinyume cha utaratibu na kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki wake.
Operesheni hiyo inatokana na agizo la Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kulitaka Jeshi la Polisi kuendesha msako wa ng’ombe hao.
Samaki wa Japan sasa ruksa kuliwa, Mwananchi Jumamosi Septemba 10, 2011
Na. Fidelis Butahe na Freddy Azzah
Habari hii inapatikana pia gazeti la Nipashe, Majira, HabariLeo,Uhuru Jumamosi Septemba 10, 2011
Wataalamu wa Afya wa Afrika Kusini wamesema samaki waliongizwa nchini kutoka Japani na baadaye kuzuiwa wasisambazwe kwa hofu ya kuwa na mionzi inayoweza kuathiri afya za watu ni salama.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na dawa (TFDA) Hiliti Sillo, jana alithibitisha kupokea ripoti ya wataalamu hao na kwamba sasa samaki hao waendelee kusambazwa ili waliwe.