Meneja wa Shamba la kufugia
Samaki la KONGA AGRIBUSINESS FARM, Bw. Steven Satola akitoa maelezo ya utendaji
kazi wa shamba hilo ambalo limepokea vijana wahitimu waliochaguliwa kupata mafunzo ya vituo
atamizi vya uvuvi na ukuzaji Viumbe maj
kwa wataalamu wa Uvuvi waliotoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, walipoenda
kutembelea na kuona mafunzo hayo yanavyoendelea kwa vijana hao kwenye shamba
hilo lililopo Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza, Machi 15,2023.
Wataalamu wa Uvuvi kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakiongea na vijana wa mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji
viumbe maji kwa Vitendo (Atamizi) waliochaguliwa kwenye Shamba la kufugia
Samaki la KONGA AGRIBUSINESS FARM, ili kujua wanajifunza nini na changamoto
gani wanazioitia wanapokuwa kwenye mafunzo hayo, shamba hilo lipo katika Wilaya
ya Magu, Mkoani Mwanza, Machi 15,2023.
Vijana waliochaguliwa
kwenye mafunzo ya uvuvi na Ukuzaji viumbe maji (Atamizi) wakifanya zoezi la
kuhamisha vifanga vya Samaki kwenye bwawa ili waweze kusafisha bwawa hilo
ambalo wanafanyia mafunzo ya Ufugaji Samaki katika Shamba la KONGA AGRIBUSINESS
FARM Lililopo Wilaya ya Magu,Mkoani Mwanza
mbele ya Wataalamu wa uvuvi kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Machi 15,2023.
Vijana wa mafunzo ya uvuvi
na Ukuzaji viumbe maji kwa Vitendo (Atamizi) waliochaguliwa kwenye Shamba la
kufugia Samaki la KONGA AGRIBUSINESS FARM, wakiwaelezea wataalamu wa Uvuvi
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (hawapo pichani) namna ya vifaranga vya samaki
vinavyozalishwa katika Maabara ya Uzalishaji wa Vifaranga vya samaki
(Hatchery), Shamba hilo lipo katika Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza, Machi 15,2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni