Mfugaji kwenye mabwawa Bw.
Manoa Samson (kushoto) akielezea namna walivyoanza ufugaji wa samaki na adi
walipofikia kwa sasa pamoja na changamoto na mafanikio waliyoyapata na
kuhamasisha wafugaji wengine kutokukata tamaa wakati walipotembelewa na
watendaji kutoka wizara ya mifugo na uvuvi, Machi 14, 2023 Wilaya ya Chamwino
mkoani Dodoma .
Afisa Uvuvi kutoka Wizara
ya Mifugo na Uvuvi (uvuvi) Bw. John Mallya (wa pili kutoka kulia) akijibu
baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wafugaji wa samaki walipowatembelea wafugaji
hao kwenye wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Machi 14,2023
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Mkomanile Mahundi akiwaeleza wafugaji wa samaki
kwenye mabwawa aina ya vyakula vya kulisha samaki hao na namna ya kuwalisha
wakati walipowatembelea kwenye kijiji cha Handari halmashauri ya wilaya ya
chamwino mkoani Dodoma, Machi 14,2023
Mkurugenzi Msaidizi wa
Utafiti, mafunzo na Ugani kutoka wizara
ya mifugo na uvuvi (uvuvi) Bw. Anthony Dadu (katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na wafugaji wa samaki kwenye mabwawa
na wataalam kutoka sekta ya uvuvi mara baada ya kuwatembelea wafugaji
hao na kuona namna wanafanya ufugaji wao na changamoto zinazowakabili kwenye
wilaya ya chamwino mkoani Dodoma, Machi 14,2023
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni