DKT. KIJAJI AKAGUA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA KAMPENI YA CHANJO ZA MIFUGO NA UTAMBUZI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametembelea na kufanya ukaguzi wa maandalizi ya Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya mifugo na utambuzi leo, Juni 13, mwaka 2025 katika Viwanja vya nane nane eneo la Nyakabindi wilayani Bariadi Mkoa wa  Simiyu.

Mhe. Dkt. Ashatu ameambatana na  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Riziki Shemdoe, Naibu Katibu Mkuu (Mifugo) Bw. Abdul Mhinte na Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa wizara hiyo  Dkt. Benezeth Lutege.

Katika Ukaguzi huo Waziri Dkt. Kijaji amekagua eneo la uzinduzi wa kampeni ya chanjo, sehemu ya itakayotumika kuwakabidhi vitendea kazi wataalam watakaotekeleza zoezi la Chanjo Kitaifa. Pia ametembelea eneo ambalo litafanyika Kongamano la Wafugaji siku ya Jumapili ya Juni 15, 2025 kabla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo na Utambuzi Kitaifa Juni 16, mwaka 2025 mkoani Simiyu.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO