Nav bar

Ijumaa, 27 Juni 2025

TAKRIBAN WATANZANIA MILIONI 6 WANAJIHUSISHA NA SHUGHULI ZA UVUVI - RAIS DKT SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na uwekezaji katika sekta ya Uvuvi mazao ya uvuvi yameongezeka kutoka tani 4077.18 zenye thamani ya shilingi bilioni 2.77  mwaka 2020/2021 hadi kufikia tani  543598.9  zenye thamani ya shilingi bilioni 3.04 mwaka 2025.

Mhe. Dkt. Samia amesema hayo wakati akihutubia na kuhitimisha shughuli za Bunge la Jamhuri za Bunge Muungano wa Tanzania hafla iliyofanyika Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 27, mwaka 2025.

Aidha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan serikali amesema takriban watanzania milioni 6 wanajihusisha na shughuli za uvuvi .

Pia, amesema kuwa kukamilika kwa bandari ya uvuvi ya Kilwa Masoko kunatarajiwa kuzalisha  ajira  takriban elfu 30,000 ambapo hadi sasa ujenzi wa bandari hiyo unaogharimu shilingi bilioni  279.5 umefikia asilimia 81.9.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni