Nav bar

Jumamosi, 28 Juni 2025

BI. MEENA AHIMIZA USHIRIKIANO KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

Na. Stanley Brayton  

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena amewataka Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa na Ushirikiano katika utekelezaji majukumu Wizarani hapo.

Bi. Meena amesema hayo Juni 28, 2025 wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Nyaraka za Ofisi baina yake na Mtangulizi wake Prof. Riziki Shemdoe katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya wizara hiyo yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Aidha Bi. Meena amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo ambapo ameahid kutekeleza maelekezo yote aliyopewa wakati akiapishwa.

Kwa upande wake aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe, amewashukuru Watumishi wote wa Wizara hiyo, kwa ushirikiano alioupata na kazi kubwa waliyoifanya katika kipindi chake. 

Vilevile, Prof. Shemdoe amewasihi Watumishi wote kuishi kama familia, kuombeana mema na kuheshimiana ikiwa ni pamoja na kumpa ushirikiano Katibu Mkuu wa sasa kama walivyompatia yeye.

Akitoa Shukrani kwa niaba ya Watumishi wote, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede amemshukuru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe kwa Utumishi wake uliotukuka pamoja na Uongozi ulioutumikia katika kipindi chote huku pia akimpongeza Katibu Mkuu wa sasa Bi. Agness Meena kwa imani kubwa aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena (kulia), akikabidhiwa Nyaraka za Utendaji Kazi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe (kushoto), mara baada ya kuwasili kwa ajili ya makabidhiano ya Ofisi, makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara - Mtumba, Juni 28, 2025 Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena (wa tatu kushoto), akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Mhede (wa kwanza kulia), mara baada ya kuwasili kwa ajili ya makabidhiano ya Ofisi, makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara - Mtumba, Juni 28, 2025 Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena (kulia), akimkabidhi Tuzo ya Heshima, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe (kushoto), mara baada ya kuwasili kwa ajili ya makabidhiano ya Ofisi, makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara - Mtumba, Juni 28, 2025 Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena (kushoto), akimkabidhi Tuzo ya Heshima, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Ndg. Abdul Mhinte, mara baada ya kuwasili kwa ajili ya makabidhiano ya Ofisi, makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara - Mtumba, Juni 28, 2025 Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena (katikati mstari wa mbele), akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi na Idara ya Wizara hiyo, mara baada ya makabidhiano ya Ofisi, makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara - Mtumba, Juni 28, 2025 Dodoma.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni